Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #4,181
UPDP wamtaka Nchimbi kusimamia maadili
na Asha Bani
CHAMA cha UPDP kimemtaka Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi kusimamia maadili ya kijamii yakiwemo mavazi kwa watumishi, wasanii wanenguaji na uanzishwaji wa kumbi mbalimbali za muziki mitaani.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Felix Makuwa, ilieleza kuwa, waziri mwenye dhamana anatakiwa kuwa makini na masuala ya kijamii, kutokana na ongezeko kubwa la mmomonyoko wa maadili kwa sasa.
Alisema, suala la mavazi kwa watumishi, wacheza muziki, filamu na ujenzi wa kumbi za muziki uliokithiri mitaani, unaharibu jamii na kuleta ongezeko la mmomonyoko wa maadili, hivyo umakini katika hilo unahitajika.
Alisema mara nyingi wamekuwa wakikumbana na kero za kelele za muziki mitaani, hali inayosababishwa na usimamizi mbovu wa viongozi waliopewa dhamana hiyo.
"Tumekuwa hatulali kutokana na kero za kelele ya muziki wa disko na ngoma, huku tabia hizo zikiambatana sambamba na utumiaji wa dawa za kulevya na hili limekuwa ni jambo la kawaida, muziki kupigwa barabarani na hata mitaani tunamoishi, jambo ambalo ni hatari sana kwa jamii," alisema Makuwa.
Alisema kama waziri anatakiwa kulifanyia utafiti suala hilo, hata kwa wakati wa usiku kupita mitaani ili aweze kujionea hali ilivyokuwa mbaya kutokana na baa kupiga muziki hata wakati wa mchana, usiku kwa sauti ya juu na kuwafanya watu kukosa usingizi.
Aliongeza kuwa litakuwa jambo la fedheha kama serikali itashindwa kusimamia suala hilo la mmomonyoko wa maadili, hivyo ofisi yake inatakiwa kuonyesha mfano wa kufanya kazi ya ziada ya kupambana na uhalifu huo ambao unazidi kuonyesha kuota matawi.