Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Yanga, Simba zijipange zaidi


TIMU za Simba na Yanga, mwishoni mwa wiki zilianza kampeni ya michuano ya kimataifa ambayo ni Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho la soka Afrika (CAF).
Yanga inayoshiriki Kombe la Shirikisho, ilianzia nyumbani kibarua chake cha hatua ya awali dhidi ya Dedebit ya Ethiopia.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, timu hizo zilitoka sare ya mabao 4-4.
Wakati matokeo hayo yakiwa mwanzo mzuri kwa Dedebit kwa vile walikuwa ugenini, kwa Yanga ni mabaya kwani wameshindwa kuutumia vizuri uwenyeji.
Wakati na baada ya mechi ya Yanga na Dedebit, wengi akiwemo Kocha Msaidizi wa Yanga, Fred Felix Minziro, na beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ walisema mvutano ndani ya klabu yao, umechangia.
Kwa upande mmoja unaweza kusema ni visingizio vya baada ya timu kukosa ushindi, lakini kwa upande mwingine kauli ya Minziro na Cannavaro si za kupuuzwa.
Tanzania Daima tukiwa sehemu ya wadau wa michezo na maendeleo kwa ujumla, tunachukua nafasi hii kuwasihi viongozi na wanachama wa Yanga kujifunza kutokana na makosa.
Tunasema hili kutokana na ukweli kuwa, ingawa sare ni sehemu ya mchezo, lakini kwa vurugu ambazo zilituama takribani wiki mbili ndani ya klabu hiyo, Yanga wanapaswa kujilaumu.
Hata hivyo, kitu muhimu ambacho kinapaswa kufanywa na Yanga, ni kuweka kando misigano yao na zogo la matokeo mabaya na kujipanga vema kwa mechi ya marudiano.
Licha ya kulazimisha sare ya nyumbani ya mabao 4-4, kama Yanga watazika misigano yao kuanzia sasa na kuiandaa timu, wanaweza kushinda na kuvuka kikwazo cha Dedebit.
Hakuna ubishi, mechi ya marudiano itakayochezwa kati ya Februari 11 na 13, itakuwa ngumu kwa Yanga kwa sababu wapinzani wao Dedebid, watakuwa nyumbani.
Lakini, kama Yanga watajiandaa vizuri hakuna kisichowezekana, wataweza kushinda na kusonga mbele katika mechi hiyo ya marudiano, hivyo kukutana na Haras El Hadou ya Misri.
Ndivyo ilivyo pia kwa watani zao Simba ambao baada ya kuvuna sare ya bila kufungana dhidi ya Elan Club ya Comoro, watalazimika kushinda mechi ya marudiano wiki mbili zijazo.
Ingawa Simba wanaonekana kuwa na kazi rahisi kiasi tofauti na Yanga kwa vile vijana hao wa Msimbazi watakuwa nyumbani, lakini si mechi ya kubeza.
Tunasema haya kutokana na mazingira ya mechi ya kwanza ambayo ilichezwa juzi mjini Mitsoudje kwani Wacomoro hao walionyesha kiwango bora ambacho hakikutarajiwa.
Tunamaliza maoni haya kwa kutoa hadhari kwa Yanga na Simba kujipanga vizri kwa mechi za marudiano, vinginevyo safari yao itaishia raundi hii ya awali.
 
Ushirikiano wa Simba na Yanga ni upi ?

Makuburi Ally

DESEMBA mwaka jana, maofisa habari wa timu kongwe za soka Tanzania Bara, Simba na Yanga, walitangaza kushirikiana kwao katika michuano ya kimataifa iliyokuwa ikiwakabili.
Maofisa hao, Cliford Ndimbo wa Simba na Louis Sendeu wa Yanga, walitangaza hatua hiyo baada ya kuketi meza moja na kung'amua kwamba mwenendo wao kimataifa hauko katika mfumo ambao utazaa maendeleo katika siku za usoni hapa nchini.
Hatua hiyo iliamsha hisia kwa wapenda soka kwamba mwelekeo wa timu hizo umedhamiria kuondokana na mfumo wa kizamani wa kuwa watani wa jadi bila ya kuzingatia uzalendo.
Maofisa hao walitoa tamko kwamba ushirikiano wao utakuwa kwenye ushangiliaji pindi moja ya timu ikiiwakilisha nchi, wamshangilie mwenzake ili kumvunja nguvu mpinzani wa mtani wake ili kufikia malengo waliyodhamiria na faida ya kitaifa zaidi badala ya klabu hizo.
Kwa muono wa haraka haraka wa baadhi ya wadau nikiwemo mimi, niliona kwamba ni ujanja fulani unaotaka kufanyika ambao una sura ya maendeleo lakini ufanikishwaji wake si rahisi kama ilivyokuwa ikitamkwa.
Sababu za kueleza hivyo ni kutokana na hoja ya umoja wenyewe ambayo inajikita kwenye ushangiliaji, jambo ambalo ni jepesi, ilitakiwa wakubaliane kushirikiana kwa karibu kwa mfano katika michezo yao ya kwanza, wangepeana majukumu ambayo yangefanikisha mpangilio huo kuliko hoja ya kushangilia tu.
Niliwahi kuwauliza maofisa habari hao kwa nyakati tofauti, wakati siku zikikaribia kabla ya michezo ya juzi ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho (CAF) ambapo Simba ilicheza na Elan ya Comoro ugenini na Yanga wakimenyana na Dedebit ya Ethiopia jijini Dar es Salaam.
Sendeu alinijibu kwamba hawajapata lolote kutoka Simba pamoja na kwamba walikubaliana wawe na ushirikiano wa mashindano ya kimataifa.
Sendeu alisema pamoja na kwamba walikubaliana kuwa na ushirikiano wa mashindano ya kimataifa, makubaliano yao yaliishia kwenye ushangiliaji.
Ndimbo naye nilipata muda wa kumuuliza kuhusu ushirikiano wao na Yanga, alinieleza kwamba hawajapeana mikakati mingine zaidi ya kubaki katika hatua ileile ya kushangiliana.
Kwa hatua hiyo inaonekana, Simba na Yanga hawajakubaliana ili kufanikisha malengo stahili katika maendeleo ya soka letu.
Nilidhani kwamba ushirikiano wa Simba na Yanga katika mashindano ya kimataifa ni kupeana mikakati, ambayo mojawapo ni kama kuifuata timu pinzani ya nje kabla ya kucheza na mojawapo.
Kwa mtazamo wangu, nilidhani pia wakati michezo yao ikikaribia wangefanya hata taratibu za michezo ya kimataifa ya kirafiki ambayo wangetoka nje ya Tanzania na si kusubiri timu za nje ndio zije hapa nchini.
Inawezekana zikatolewa sababu kwamba gharama kubwa ya kusafirisha timu kutoka Tanzania kwenda nje, jambo ambalo lingefanyika kwa mtindo wa kupeana mipango ya kufanya.
Kama kweli Simba na Yanga zina nia ya dhati na kuondokana na ubabaishaji uliokithiri katika soka la Tanzania ambapo kila uchao tunabaki kuishia hapa hapa Tanzania badala ya kwenda mbali zaidi.
Tumeona mchezo kati ya Yanga na Dedebit ya Ethiopia mchezo ambao ulichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, katika mchezo ambao Yanga waliuanza vizuri lakini ukaja kubadilika.
Katika mchezo ule, Yanga walistahili kushinda lakini waliwadharau Dedebit hali ambayo ingewagharimu, kwa sababu timu ile haikutakiwa kupewa nafasi ya kushambulia.
Pamoja na kwamba bado hamjapeana mikakati hiyo, jiandaeni kwa michezo ya marudiano ambayo inatarajiwa kuchezwa kati ya Februari 11 na 13, Yanga watarudiana na Dedebit nchini Ethiopia wakati Simba watamenyana na Elan hapa jijini.
Kama kweli tunahitaji mabadiliko ya kweli kwa soka letu baada ya kujitambua, inatakiwa kuchukua hatua ambazo zitasaidia na kuondokana na soka la hapa Tanzania pekee, badala ya kufikiria kufanya vizuri katika michuano ya Afrika na wakati mwingine mashindano ya mabara.
Hatua hizo za maendeleo zitafikiwa kikamilifu na kuondokana na mwenendo mbovu, soka letu litakuwa zaidi ya timu zilizoendelea kama TP Mazembe na nyinginezo zinazotamba barani Afrika na ulimwenguni.



Mwandishi anapatikana kupitia 0773508779, email makuburia@yahoo.com
 
SARAH KAVINA: Mshindi 10 Km Mali aliyepania kurejesha hadhi Kili Marathon

Mwandishi wetu

HIVI sasa gumzo katika medani ya mchezo wa riadha hapa nchini, Afrika Mashariki na Kati na hata nje ya hapo, ni msimu wa tisa wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon ambazo hufanyika kila mwaka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kilimanjaro Marathon mwaka huu inatarajiwa kutimua vumbi Februari 27 kuanzia viwanja vya Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushika na Stadi za Biashara (MUCCOB's), na kupita barabara mbalimbali za mjini Moshi kisha kurejea uwanjani hapo.
Homa ya mbio hizo hapa nchini imezidi kupanda kila kukicha miongoni mwa wanariadha mbalimbali mashuhuri hapa nchini, ambao hivi sasa wako kwenye mashindano mbalimbali ambayo yatawasaidia kufanya vema kwenye Kili Marathon na wengine wakiwa wanajiona chini ya makocha wao.
Kati ya nyota hao ambao homa ya Kili Marathoni ishaanza kumpanda si mwingine bali ni Sarah Kavina kutoka klabu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Arusha, ambaye ilishuhudiwa Januari 23 jijini Bamako Mali, akiipeperusha vema bendera ya Tanzania baada ya kuibuka mshindi wa mbio za kimataifa za Kilomita 10 za Bank of Africa (BOA), zilizoshirikisha nchi takriban 12.
Sarah aliibuka kidedea baada ya kutumia dakika 35.20:20 na kuwabwaga wenzake kutoka katika nchi hizo zilizoshiriki mashindano ya kimataifa ya BOA Marathon ambayo ni msimu wake wa tatu mwaka huu, huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kushiriki.
Mara baada ya kurejea nchini, jijini Dar es Salaam Januari 26 mwaka huu, Sarah anasema, katika mbio hizo alikumbana na upinzani mkali kutoka kwa washiriki wenzake achilia mbali hali ya hewa ambayo ni ya joto kali hasa ukizingatia anatokea sehemu zenye ubaridi (Arusha), lakini alikuwa amenuia kuipeperusha vema bendera ya Tanzania pia kujipima katika kuelekea katika mbio za Kilimanjaro Marathon.
"Kikubwa nilikuwa nimenuia kuiwakilisha nchi vema katika mashindanio hayo nashukuru nimefanikiwa, lakini nashukuru mbio hizi zimenisaidia kuniweka sawa kwa ajili ya Kilimanjaro. Programu iliyobaki sasa narudi Arusha kwenda kuendelea na mazoezi kwa ajili ya mbio za Kilimanjaro," anasema.
Sarah ambaye amewahi kushiriki mbio hizo za Kilimanjaro Marathon mara kadhaa hasa katika zile za Nusu Marathon na kufanya vema, mwaka huu ameamua kujitosa katika marathoni kamili km. 42.2.
Mwanariadha huyu hivi sasa anajifua kwa nguvu huko Arusha chini ya kocha wake, Norbert Kilimtali wa JKT.
Akizungumzia maendeleo ya mchezaji wake, Kocha Kilimtali anasema, jinsi anavyomsimamia kuhakikisha anatekeleza vema programu aliyompangia mchezaji wake anampa matumaini makubwa ya kufanya vema katika mbio hizo za Kili Marathon mwaka huu na kufuta ngebe za Wakenya ambao wameiteka kwa takribani misimu miwili sasa, ambako mwaka jana, Fredah Lodepa wa Kenya alishinda akitumia saa 2:40.21.
Kilimtali anasema, mchezaji wake ananendelea vema kujifua kama hatapatwa na maumivu yoyote, basi uwezekano wa kufanya kweli katika Kili Marathon mwaka huu ni mkubwa.
Basi huyo ndiye Sarah Kavina, afande wa JKT aliyeing'arisha Tanzania Mali, anayepania kurejesha hadhi ya Watanzania Kilimanjaro Marathon 2011.
HISTORIA KWA UFUPI
JINA: Sarah Kavina
KUZALIWA: 1974 Mgama, Iringa Vijijini.
KLABU: JKT Arusha.
REKODI ZAKE:
1995 Mount Meru Marathon Na. 3
2003 Kilimanjaro Half Marathon. Na. 1
2008 Majeshi (CISM Uganda), Na. 3
2008 KLM Inter. Marathon Na. 3
2009 Ngorongoro Ant Malaria Half Marathon Na. 2
2009 Kilimanjaro Inter. Half Marathon Na. 2
2010 Poland Marathon Na. 3
2010 Taifa Cup Mita 10,000 Na. 3

 
Yanga SC waelekea kuvuna walichopanda

Deodatus Mkuchu

KUTOKANA uchungu wa kidonge cha Chloroquine, mtu hupaswa kutumia ujasiri kiasi chake kukimeza.
Lakini, kwa vile ni mojawapo ya tiba kulingana na ushauri wa daktari, mgonjwa hulazimika kuimeza ili apone.
Ndani ya klabu ya Yanga, kuna ugonjwa ambao kama ukiachwa bila kupatiwa tiba sahihi, unaweza kugharimu uhai wa klabu hiyo kongwe iliyoasisiwa tangu mwaka 1935.
Kwa vile ugonjwa huu umesababishwa na wanachama na viongozi wa klabu hiyo, hakuna mwingine wa kuuponya isipokuwa hao wenyewe, kwa kuketi chini na kujiuliza nini manufaa ya misigano baina yao.
Kabla ya Yanga kuingia katika kampeni ya michuano ya kimataifa ikishiriki Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), niliwahi kuandika makala iliyokuwa imezungumzia kwa kina ulazima wa Yanga na Simba kufanya maandalizi ya uhakika.
Nilizitahadharisha Yanga na Simba inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, zote zifanye maandalizi ya uhakika kabla ya kuanza kwa kampeni hizo, kwa sababu bila maandalizi ya maana, zitabaki kuishia hatua ya awali kila mwaka.
Nilijikita zaidi kwa Yanga kutokana na hali halisi iliyoigubika klabu hiyo kwa takribani wiki tatu sasa, ambako wanachama na viongozi wamekuwa katika malumbano yasiyo na tija bali anguko la klabu hiyo.
Badala ya kutumia muda wao kuiandaa timu kulingana na programu ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mserbia Kostadin Papic, wanachama wakawa wanalumbana na viongozi wao kwa upande mmoja, wakati huohuo viongozi nao wakisigana na benchi la ufundi.
Januari 20, viongozi wa matawi ya klabu hiyo kwa Mkoa wa Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake Mohamed Msumi, walikutana kujadili mambo kadha wa kadha yahusuyo klabu yao makao makuu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, mbali ya kujadili ushiriki wa timu katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, pia walijadili tuhuma kadha wa kadha.
Kati ya hayo, ni madai ya baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji kumtuhumu Mwenyekiti wao Lloyd Nchunga kupitisha baadhi ya mambo bila ya baraka za kamati hiyo.
Kwa mfano, uteuzi wa Mbunge Abbas Mtemvu kuwa Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu hiyo, akiungana na Mama Fatma Karume, Yusuf Manji na Francis Kifukwe.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji, walihoji uhalali wa uteuzi huo huku wakiungwa mkono na wanachama ambao wao walikwenda mbali zaidi wakidai Mtemvu si Yanga.
Viongozi hao wa matawi, walikwenda mbali zaidi na kumtuhumu mfadhili na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini, Yusuf Manji kuwa ndiye anayemshinikiza Nchunga kufanya maamuzi pasipo kupitia Kamati ya Utendaji.
Viongozi hao wakamtaka Manji aeleze yeye kwa sasa ni nani ndani ya klabu hiyo, kwani kama ni mfadhili, vipi kwa siku za hivi karibu amekuwa akitoa fedha kwa sharti ya kurejeshewa?
Jingine ambalo lilikuwa sehemu ya mtafuruku, ni hatua nya Nchunga kupitia barua namba YASC/0321/LPM ya Desemba 20, kumteua Kifukwe kufufua kampuni itakayoanza na wajumbe wapatao 10.
Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosainiwa na Nchunga, uteuzi wa Kifukwe ni utekelezwaji wa kikao cha Kamati ya Utendaji cha klabu hiyo kilichoketi Novemba 30, mwaka jana kwa lengo la Yanga kujiimarisha kiuchumi.
Kifukwe ndiye ahusike na suala hilo na chini ya kampuni, nembo ya klabu hiyo itumike kibishara huku klabu ikipata kiasi cha sh mil 500 kwa mwaka kwa miaka 10.
Barua hiyo inasema, kiwango hicho kwa ajili ya matumizi ya nembo, kitakuwa kikiongezeka kila mwaka kwa asilimia 10.
Aidha, kila mjumbe wa bodi ya kampuni hiyo chini ya Kifukwe, angechangia shilingi mil. 50 kupata mtaji wa kampuni na kwamba mwenyekiti wa bodi atatoka miongoni mwao.
Pia, baada ya miaka mitatu, wajumbe hao watarejeshewa fedha zao na kampuni kurudi kwa wanachama, kwa hoja kuwa tayari itakuwa imesimama kiuchumi.
Yote haya mawili yaliweza kuutikisa vilivyo uongozi wa Yanga, kwani nyuma ya hoja hizo, viongozi wa matawi walijenga hoja kuwa, Nchunga ajadiliwe kwenye Kamati ya Utendaji na ikiwezekana asimamishwe kwa kukiuka katiba.
Nchunga ambaye ni mwanasheria kitaaluma, naye akajenga hoja kuwa kilichofanywa na viongozi hao wa matawi ni batili kwa sababu mbili; mosi wao hawakuwa na ubavu wa kufanya maamuzi kama hayo dhidi yake, kwani yeye anawajibika kwa Kamati ya Utendaji si matawi.
Hoja ya pili ya Nchunga, ikawa ni ubatili wa mkutano wenyewe ambao licha ya Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako, na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mohamed Bhinda, kushiriki kwa niaba ya uongozi, kikao kile kikaonekana ni batili.
Maamuzi ya viongozi wa matawi yalionekana kuchochea mambo, kwani kundi la Wazee wa klabu hiyo chini ya Jabir Katundu na Yusuph Mzimba, liliibuka na kumtetea Manji.
Kukiwa na sarakasi hizo, Mwalusako ikaelezwa ameamua kujiuzulu kwa sababu za kiafya kwa mujibu wa barua yake kwa Kamati ya Utendaji, ingawa kumekuwa na habari kuwa ameshinikizwa.
Mambo hayakuishia kwa Mwalusako tu, pia hadi kwa Meneja wa timu, Emmanuel Mpangala ambako nafasi yake ikawekwa mtu mwingine ambaye ni Salvatory Edward.
Hilo likafanyika sambamba na kumthibitisha Fred Felix ‘Minziro' kuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo, licha ya Mserbia huyo kukataa kuchomekewa msaidizi asiye chaguo lake.
Wakati Papic akijenga hoja ya kitaalamu, baadhi ya viongozi wa Yanga wakajenga hoja kuwa Papic kama mwajiriwa hana ubavu wa kukataa uamuzi wa viongozi, hivyo kuwepo kwa msigano kati ya Papic na uongozi.
Baada ya uongozi kumthibitisha Minziro, Papic alikabidhi barua ya kuacha kazi, ingawa kuelekea mechi ya juzi dhidi ya Dedebit ya Ethiopia, kulikuwa na juhudi za kumrejesha.
Ukiyachukua madudu yanayofanyika Yanga bila kujali nani yu sahihi na nani mkosaji, pamoja na mvurugano uliopo kwenye benchi la ufundi yaani Papic kwa upande mmoja na Mpangala kwa upande mwingine, unaweza kusema Yanga dhidi ya Dedebit wamevuna walichokipanda.
Wakati Dedebit ambao ni mara ya kwanza kwao kucheza michuano ya kimataifa wakikuna vichwa namna ya kufanya vizuri katika michuano hiyo, wanachama na viongozi wa Yanga wao wanavurugana. Matokeo ya juzi yametoa jawabu kwamba kama viongozi na wanachama wa Yanga wataendelea kuvutana, Yanga ijiandae kufanya vibaya zaidi ya hapa, si katika michuano ya kimataifa tu, pia kwenye Ligi Kuu.
Yanga wakipoteza muda katika kuvutana, Dedebit wamezidi kujipanga namna na kuwang'oa Yanga na kutinga hatua inayofuata, ambako mshindi wa jumla kati yao, atakutana na Haras El Hadoud ya Misri.
Kiuchezaji, Dedebit chini ya kocha wake mpya Gebredhin Haire aliyetwaliwa wiki mbili kabla ya mechi ya kwanza dhidi ya Yanga, wanaonekana kucheza kwa ari kila idara kiasi cha kupanga mashambulizi na yakaonekana na kuzaa matunda.
Kitu pekee ambacho kiliwagharimu katika mechi ya kwanza dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ni ugeni wao katika michuano hiyo ya kimataifa, kwani ni mechi ya kwanza kwao tangu kuanzishwa kwa timu hiyo Oktoba 31, 1998.
Yanga ndio timu ya kwanza kuwakaribisha Waethiopia hao katika michuano ya kimataifa, kwani baada ya kucheza Ligi Kuu ya Ethiopia kwa mara ya kwanza msimu uliopita, walimaliza nafasi ya pili nyuma ya St. George.
Kwa ugeni wao katika michuano ya kimataifa na ugeni wao katika uwanja wa taifa, jijini Dar es Salaam, bado Dedebit wakacheza soka ile, utapima mwenyewe na kupata jawabu hali itakuwa vipi mechi ya marudiano wiki mbili zijazo mjini Addis Ababa.
Ni kweli, katika soka lolote linaweza kutokea, lakini pia matokeo ni jawabu la jumla ya namna timu ilivyojiandaa na kutumia nafasi zilizopatikana kwa ustadi wa timu husika au udhaifu wa timu pinzani, hivyo Yanga walione hilo na kujipanga.
Bila kujipanga vizuri, wakaendeleza sarakasi zao na kuacha masuala ya msingi likiwamo la kuiandaa timu kwa mechi ya marudiano, si ajabu safari ya Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho, ikaishia katika Jiji la Addis Ababa.
Kitu muhimu kwa viongozi wa Yanga, ni kuitafakari kauli ya Minziro kwamba, mbali ya dosari nyingine zilizochangia matokeo hayo, pia msigano uliopo kwenye uongozi wa klabu hiyo na benchi la ufundi, vimeshusha morari wa wachezaji.
Kama nilivyosema, kauli ya Minziro ni chungu kama Chloroquine au shubiri, lakini kama itafanyiwa kazi na viongozi wa Yanga, ndio itakuwa nafuu ya ugonjwa unaotaka kuiangamiza kuelekea mechi ya marudiano.
Kwa kutoka sare ya mabao 4-4, Yanga italazimika kwenda kusaka ushindi katika mechi hiyo ya marudiano itakayochezwa kwenye viunga vya jiji la Addis Ababa kati ya Februari 11 na 13 ambako itakuwa zamu ya Dedebit kuwa nyumbani.
Onyo la mgogoro limetolewa hata na beki wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Canavaro' aliyeweka wazi kuwa, mgogoro wa viongozi uliopo katika klabu hiyo, umechangia kwa kiasi kikubwa kushusha ari ya wachezaji.
Ndio ni mchezo, una matokeo ya aina tatu, yaani kufungwa, kushinda au sare, lakini kuna matokeo mengine ni kama ya kujitakia kwa mfano haya ya sare ya 4-4 dhidi ya Dedebit.
Naamini kama Yanga wangekuwa wametulia na kujipanga vizuri kuanzia wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama hadi wapenzi na mashabiki, pamoja na ubora wa Dedebit, wasingepata matokeo hayo.
TOFAUTI YA YANGA, DEDEBIT
Dedebit chini ya Rais wake Kanali Awel Abdurahim, ni timu iliyoanzishwa Oktoba 31, 1998 katika viunga vya jiji la Addis Ababa, ikiwa timu ya vijana wadogo, lakini kwa sasa ikiwa kati ya timu zinazotishia zama za vigogo kama St. George.
Juni 29, 2010, Dedebit ilitwaa Kombe la Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF), dhidi ya St. George katika mechi ambayo ilivunjwa kutokana na mashabiki wa wapinzani wao kuvamia uwanja wakipinga kutolewa kwa mchezaji watano kwa kadi nyekundu, wakati huo Dedebit wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kwa kukamata nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Ethiopia nyuma ya St. George, ndipo Dedebit wakajitwalia tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Shirikisho; mara ya kwanza katika historia ya timu hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Wakati Dedebit ikianzishwa mwaka 1998, Yanga ilianzishwa 1935 – miaka 63 baadaye.
Aidha, taji pekee la kitaifa kwa Dedebit, ni Kombe la FA huku Yanga wakiwa mabingwa wa Tanzania Bara mara 22, Kombe la FA mara nne na matatu ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Kwa upande wa michuano ya kimataifa inayoandaliwa na CAF, Yanga imeshiriki mara tano tangu michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika ibadilishwe jina na kuitwa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mwaka 1997, Yanga iling'oka hatua ya awali, lakini mwaka uliofuata ikiwa chini ya Kocha Tito Mwaluvanda (marehemu), ilijitahidi hadi hatua ya makundi na kuambulia kitita cha shilingi mil 90.
Yanga ilishiriki tena michuano hiyo mwaka 2001 na kuishia raundi ya pili na mwaka 2006, wakaishia hatua ya awali kabisa.
Mwaka 2007, wakafanikiwa kuvuka raundi ya awali, lakini wakachemsha raundi ya pili na mwaka 2009, wakatolewa katika raundi ya kwanza kabla ya kufungashwa virago raundi ya awali mwaka 2010.
Historia inaonyesha kuwa, kabla ya michuano hii kubadilishwa jina kutoka Klabu Bingwa ya Afrika na kuwa Ligi ya Mabingwa, ambako ilishiriki mara 11, Yanga ilikuwa ikifanya vizuri kiasi chake ikifika robo fainali mara mbili, 1969 na 1970.
Mwaka 1971, Yanga ilijitoa ikiwa raundi ya pili ya michuano hiyo na mwaka uliofuata, ikashiriki, lakini ikiaga katika raundi ya kwanza kama ilivyokuwa katika miaka miwili iliyofuata 1972 na 1973.
Lakini mwaka 1975 na 1982, Yanga walau ilifurukuta hadi raundi ya pili, hata hivyo ikiaga raundi ya kwanza katika miaka ya 1984, 1988 na 1992 kabla ya kuaga hatua ya awali mwaka 1996.
Kwa ujumla, Yanga safari hii inashiriki mara ya tatu Kombe la Shirikisho, mara ya kwanza ikiwa mwaka 2007 ambako iliaga hatua ya kati na mwaka 2008, iliaga hatua ya pili.
Kabla ya michuano hii kuitwa Kombe la Shirikisho, ilikuwa ikijulikana kwa jina la Kombe la CAF, ambako Yanga iliwahi kushiriki mara mbili, 1994 na 1999, lakini ikiaga hatua ya kwanza.
Aidha, Yanga imewahi kucheza mara mbili Kombe la Washindi ambalo kwa sasa halipo na mwaka 1995, ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, lakini mwaka 2000 wakiaga hatua ya kwanza.
Je, kwa sare ya mabao 4-4 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya kwanza, Yanga itaweza kusawazisha makosa na kujipanga vizuri, hivyo kwenda kuvuna ushindi katika mechi ya marudiano mjini Addis Ababa? Acha, tusubiri na tuone.




 
Mfumo wetu wa soka Afrika Mashariki na Kati unatuua

Kenny Mwaisabula

KARIBUNI tena wapenzi wasomaji wa ‘Kona hii ya Mwaisabula' katika Jumatatu nyingine tulivu baada ya kuzishuhudia timu zetu kongwe ndani ya nchi yetu zikiumana katika kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.
Wakati Simba wakiwa ugenini visiwani Comoro kumenyana na mabingwa wa huko Elan de Mitsoudje, Yanga wenyewe walikuwa nyumbani ndani ya dimba letu la Taifa, wakiumana na Dedebit ya Ethiopia.
Lakini nadhani tuachane na haya matukio ya kinyang'anyiro cha Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), ambayo wote tumeyashuhudia, tusubiri mechi za marudiano wiki mbili zijazo.
Katika makala ya wiki iliyopita nilimzungumzia David Jimmy Ngonya kuwa alikuwa kiongozi asiyeyumba na mwenye msimamo, niliahidi kuwa leo nitazungumzia mfumo wa soka letu na hasa katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kati.
Jumamosi iliyopita, nilikuwa mmoja wa mashabiki wachache sana waliokuwepo Uwanja wa Uhuru kushuhudia mechi tamu kabisa na ya kusisimua kati ya JKT Ruvu na Toto African ya Mwanza, ambayo iliisha kwa maafande wa JKT kuibuka na ushindi wa bao 1-0; bao lililofungwa na mshambuliaji mahiri Hussein Bunu.
Mara baada ya mechi kuisha, nilimshuhudia Katibu wa JKT, ambaye zamani alikuwa mchezaji wa timu hiyo, David Ngaga, akiwa amebaki uwanjani ameduwaa mbali ya kushinda, lakini alikuwa akisikitika jinsi vijana wake walivyokosa nafasi nyingi za wazi, nilichomwambia ni, "Mwanangu shukuru Mungu kupata pointi 3, kwani wewe shida yako nini, maana ‘Big 2' ndani ya nchi hii inajulikana, nyie wengine mnagombea msishuke daraja tu."
Wengi waliokuwepo jirani na maongezi yale, waliniunga mkono, ndio soka la ukanda wetu wa Afrika Mashariki na ya kati limefikia hapo.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholaus Musonye, ambaye ameongoza kwa kipindi kirefu, ameshindwa kabisa kutengeneza mfumo mzuri wa kututoa hapa tulipo na matokeo yake klabu zetu za ukanda huu hazifiki mbali katika mashindano ya kimataifa.
Najiuliza, Musonye anashindwa vipi kuangalizia kwa wenzetu walioendelea, jinsi wanavyoendesha ligi katika ukanda wao, amebaki na fikra mgando za toka enzi hizo.
Nilianza kumtambua Musonye anatupeleka siko, juzi alipokuwa anapingana na mashindano mazuri kabisa ya Bonde la Mto Nile, moja ya kauli yake iliyonitisha, anasema, "Wao wanataka twende kule (Misri), watuongoze sisi tumekataa. "Kama wana hela walete tuunde umoja na tuchague viongozi wetu lakini sio kila kitu kufanya wao."
Hapo ndipo nilipoanza kupata taabu na hisia za Musonye, kama mtendaji mkuu wa shirikisho hilo kubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na ya Kati.
Kama Musonye angekopi au kuangalizia pale UEFA kwa watu walioendelea, nadhani tungesogea kidogo. Hivi hadi lini tutaendelea kuwa na ‘Big 2' yaani kila nchi kutoa washindi wawili tu kuwakilisha katika michuano ya kimataifa, jambo ambalo linasababisha kwa hapa Tanzania, muda mwingi kuwakilishwa na wakongwe tu na kuacha timu zingine zote zikiwa wasindikizaji tu.
Kama na sisi tungekuwa tunatoa timu nne bora za ukanda wetu, zikashiriki Ligi ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na ya Kati na ligi ingechezwa vilevile kwa utaratibu wa nyumbani na ugenini, nadhani leo tungeona makali ya Azam FC, Mtibwa Sugar na JKT katika ligi hiyo ya mabingwa katika ukanda wetu.
Musonye bado alikuwa ana uwezo wa kutengeneza ligi ndogo ya ukanda wetu, ikacheza katika kituo kimoja, yaani zikachukuliwa timu zile zilizoshika nafasi ya tano, sita na saba katika nchi zao, zikakutana katika kituo kimoja na kumpata bingwa wao.
Kwa mashindano hayo tu, leo tungepata wachezaji walio bora na tungewaona katika mechi nyingi, tofauti na ilivyo sasa, ambapo ‘Mheshimiwa' Musonye ameshindwa kuyafanya hayo na kubaki kupiga vita hata mambo mazuri kutoka kwa wenzetu (Misri).
Sio jambo linalohitaji elimu ya chuo kikuu kuelewa kuwa ligi zetu, hususan ligi yetu ya Tanzania, zimekosa kabisa mvuto na msisimko kama ule tuliokuwa tumezoea kuuona zamani kwa timu za Mseto, Tukuyu Stars, Coastal Union, African Sports, Vita Tabora, KMKM, Small Simba, MECCO, Ushirika Moshi na zingine nyingi.
Timu za leo za Ligi Kuu, zinacheza mechi zisizozidi 30, jambo ambalo ni kinyume kabisa na taratibu za shirikisho linaloongoza soka duniani (FIFA).
Timu zinazoshiriki ligi hiyo, sasa zaidi ya asilimia 80 hazina wazo lolote la kuwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa, zenyewe akili zao ni kupigana kuwania kutokushuka daraja tu na si vinginevyo.
Hizo zinazopanda ndio kabisa hazijulikani, zaidi ya wahusika wenyewe wanaoshiriki; TFF leo imeifanya kama michezo ya bonanza ambayo mara nyingi tunacheza sisi wakongwe, maana wachezaji hawapati muda mrefu wa kushindana kwa kupangiwa ratiba fupi mno, bila sababu zotezote za msingi.
Ligi hiyo ya daraja la kwanza, ambayo itatoa wawakilishi wanne kuingia Ligi Kuu msimu ujao, yaani kuanzia Agosti, lakini katika zile timu tisa zilizoingia fainali, zimepangwa kuanza kutimua vumbi katika kituo cha Tanga kuanzia jana hadi Februari 22.
Ni ligi itakayochezwa kwa siku 24 tu, ni ajabu na kweli, timu zinacheza mchana na jioni! Huenda hadi asubuhi zikacheza, ni hatari mno!
Ndio maana leo, utaona timu zilizopanda Daraja la Kwanza msimu uliopita, yaani Ruvu Shooting na AFC ziko chini zikisota na huenda zikarudi zilikotoka, tofauti na enzi zile Tukuyu Stars inapanda daraja na moja kwa moja kuchukua ubingwa.
Mchezaji anayetarajiwa kucheza ligi Agosti, baada ya kupandisha timu yake daraja, atakaa nje ya mashindano miezi mitano. Ni kichekesho kweli, sijawahi kusikia popote duniani zaidi ya hapa kwetu tu, hata sehemu za kazi kama ilivyo mpira kuwa ni sehemu ya kazi mfanyakazi anafanya kazi miezi 11, mwezi mmoja huenda likizo kupumzika.
Lakini tofauti na hapa kwetu, mchezaji anacheza miezi sita tu, mingine yote anapumzika, unategemea nini hapo.
Kwa hali hiyo, matatizo ya mfumo wa ligi katika ukanda wetu, kuanzia ngazi ya chini hadi ile ya kwa mzee Musonye, utatutoa kabisa katika dunia ya soka ya ushindani na kwa kuzingatia hatukubali kujifunza toka kwa walioendelea na kujiona sisi ni zaidi wakati hatujui, inasikitisha mno.
Namalizia: hivi kweli Mheshimiwa' Musonye hivi anasema toka moyoni au anatania au wivu?
Tanzania tumeshika nafasi ya sita katika mashindano ya Mto Nile, tumevuta milioni 75, unataka nini tena hapo! Tumechukua ubingwa wa Tusker Challenge Cup 2010 tumepata milioni 30 za Musonye, kweli tunafanana? Hapo ndipo ninapoungana na mchambuzi maarufu swahiba yangu, Aloyce Komba, kuwa sasa iko haja kujitoa katika mashindano ya CECAFA na kujikita katika yale ya Mto Nile.
Ndio maana leo nasema kwa mfumo huu tutaendelea kuwa watazamaji miaka nenda miaka rudi.



Mwandishi wa makala hii ni mfanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), anapatikana 0713 243 711 Email: kennymwaisabula@yahoo.com
 
TAMBAZA GYM: Klabu inayojivunia kuibua vichwa katika masumbwi

Mwandishi wetu

KATIKA medani ya mchezo wa ngumi ama masumbwi au ukipenda ndonga, hapa nchini jina la Tambaza Gym sio geni miongoni mwa wadau wa mchezo huo ambao una historia ya kulitangaza vema jina la Tanzania kimataifa.
Klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1987 ilianza kwa kushirikisha michezo ya ngumi za kulipwa, karate na kunyanyua vitu vizito.
Tambaza Gym maskani yake yako karibu na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, karibu na sekondari ya Tambaza.
Katika mahojiano na mwandishi wa makala hii, mwenyekiti wa Tambaza Gym, Ally Tambaza, anasema sababu ya kuanzishwa kwa klabu hiyo ni kiu ya maendeleo ya michezo hapa nchini.
Tambaza anasema walimu walioanzisha klabu hiyo ni pamoja na Chuku Dusso ambaye alikuwa kocha wa ngumi, Msakala Tambaza kocha wa karate na Hussein Okoama alikuwa kocha wa kunyanyua vitu vizito.
Anasema, klabu hiyo hadi sasa inajivunia mabondia kadhaa ambao wanaendelea kuitangaza Tanzania katika medani ya mchezo wa ngumi hapa nchini.
Tambaza anamtaja bingwa wa Mabara wa ngumi za Mateke ‘Kickboxing', Japhet Kaseba, na wengine zaidi ya 20 kwamba walifuliwa na klabu hiyo.
Aidha Tambaza anawataja wengine ambao ni zao la Tambaza Gym kuwa ni pamoja na Mbaruk Kheri, Hussein Mombwe, Shukuru Samata, Honnest Kakobe, Masudi Mkarambati na Hamis Ndundu.
Wengine ni Mohamed Msakala na Abuu Mtambo ambao wanaitangaza klabu hiyo hapa nchini katika medani ya masumbwi.
Anasema, azma ya klabu hiyo katika nyanja za michezo ni kwamba mchezo wa ngumi ni sehemu ya kutengeneza afya, kujilinda na ajira kwa wachezaji.
Tambaza anasema wao hawachukulii kwamba mchezo huo ni sehemu ya kufanyia uhalifu na uhuni na kutoa wito kwa wenye dhana hiyo kuachana na klabu hiyo kwa sababu si fani yao.
Tambaza anasema, klabu hiyo ilitaka kuvurugwa baada ya kukabiliwa na kesi mahakamani, wakidaiwa kuwa eneo ilipo si la kwao.
Anasema, kesi hiyo iliyoanza mwaka 2004 kwa kiasi kikubwa ilizorotesha maendeleo ya mchezo huo kwa baadhi ya wadau wakidai eneo hilo ni lao, kesi ambayo iliendeshwa katika mahakama ya Samora jijini Dar es Salaam.
Anaeleza kwamba kesi hiyo imemalizika hivi karibuni ambapo familia ya Tambaza imeshinda na eneo hilo linaendelea kuwa lao.
Tambaza anasema, klabu yao ni mahiri kwa kuandaa mapambano ya ngumi, ambapo pia walisimamisha taratibu hizo kutokana na kesi ambayo ilichukua miaka zaidi ya saba ambayo imewagharimu kwa kiasi kikubwa.
Anasema, baada ya kumalizika kwa kesi hiyo wanajipanga kurudisha heshima ya Tambaza Gym iliyopotea kwa kipindi kirefu na kutoa wito kwa wadau kujiandaa na mapambano ya mchezo huo.
Tambaza anasema, hivi sasa klabu hiyo inaendelezwa kupitia makocha Haroub Ally na Shah ambao wanawanoa vijana katika ngumi, wakati katika mchezo wa kickboxing vijana wananolewa na Jumbe Tambaza ‘Jebby' ambaye pia anawanoa kunyanyua vitu vizito.
Kocha mwingine anayewanoa vijana katika kunyanyua vitu vizito ni Omar Jangala.
"Kwetu ngumi ni mchezo wa kirafiki, kwa sababu hata ukienda Morogoro, Zanzibar na kwingineko, utakutana na wenzako ambao wanacheza mchezo huo, kwetu ni mchezo wa kirafiki, ingawa mkifika jukwaani mnatoana manundu," alisema Tambaza.
Tambaza anasema, hivi karibuni vifaa vya michezo hiyo vinawasili hapa nchini vikitokea Afrika Kusini kwa ajili ya kuendeleza mchezo huo.
Anatoa wito kwa serikali, kuwapa sapoti kama ilivyo michezo mingine ili kufikia malengo ambayo yataitangaza Tanzania katika dunia ya michezo.
Tambaza alitoa wito pia kwa kina dada kujitokeza kujifunza mchezo ya ngumi ambao ni mmoja wa michezo iliyoiletea sifa Tanzania.
Klabu ya Tambaza Gym inaundwa na viongozi ambao ni pamoja na yeye akiwa mwenyekiti, Mlekwa Mkiwa na Gervas D ambao wanadhamiria kuiendeleza klabu hiyo ipasavyo.
Hiyo ndio Tambaza Gym, klabu ya ngumi inayojivunia kuibua ‘vichwa' katika medani hiyo.
 
RT inavyojiandaa kuongozwa na vimeo

Tullo Chambo

NI Jumatatu nyingine tena tunakutana wadau wa Uwanja wa Kuchonga, kama kawaida kupeana changamoto za kispoti, lengo likiwa kuboresha ufanisi.
Kabla mchezo haujaanza, tuanze kwa kujuliana hali, ambako bila shaka wote mu wazima, ila kwa wale mambo hayajakaa sawa tunawaombea mabadiliko.
Kwa faida ya wale ambao kwa namna moja ama nyingine, hatukuweza kuwa wote wiki iliyopita tupeane dondoo kwa uchache.
Wiki iliyopita tuliangali jinsi hali inavyoendelea ndani ya klabu kongwe ya Yanga ya jijini Dar es Salaam hivi karibuni iligubikwa na wingu la migogoro ambayo hadi leo bado haujakaa sawa.
Tulitafakari chanzo cha mgogoro huo na athari zake, pia tuliitizama historia ya mitafaruku iliyopita, ambako kimsingi mfadhili wa klabu hiyo Yussuf Manji haepukiki kutajwa au kuzungumziwa kwa namna moja ama nyingine na wanachama, wadau na mashabiki wa timu hiyo.
Baada ya kuichambua historia ya mgogoro huo ambao bado unafukuta, suluhisho lililopatokana ni kwa baadhi ya wanachama kuwa na upeo mdogo na kutojua ajenda inayofanyiwa kazi.
Lakini mwisho wa mwisho, tuliwataka Wana Yanga wahoji hivi sasa kwanini kila tukio likitokea kuhusiana na utendaji, jina la Manji halikosekani. Hivyo tuliwataka wanachama hao kujiangalia na kuijadili hali hii kwa ufundi wa hali ya juu, ili kubaini ‘Wana Yanga jiulizeni, Kwanini iwe Manji.
Baada ya dondoo hizo, sasa turejee katika mada yetu ya leo kama inavyojieleza; ‘Riadha Tanzania inavyojiandaa kuongozwa na vimeo'.
Hivi karibuni, uongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), ulitangaza kuvitaka vyama vya Wilaya na Mikoa kuanza harakati za kufanya chaguzi zao kuelekea ule wa Taifa.
Kwa wale ambao hawana kumbukumbu vizuri, uongozi wa sasa RT ulio chini ya Rais Francis John Keppa na Katibu Mkuu, Mujaya Suleiman Nyambui uliingia madarakani Julai mwaka 2006 katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa benki kuu (BoT), jijini Mwanza.
Ni uchaguzi ambao naweza kusema ulikuwa wa kihistoria, kwani baada ya mbilinge mbilinge za muda mrefu, ambazo ziliitoa jasho na kuitesa serikali kupitia Wizara yenye dhamana na michezo, hatimaye uliweza kufanyika lakini si katika hali ya kuridhisha asilimia 100.
Wadau tunauita ni wa kihistoria, kwani ulifanyika ikiwa chama hicho kimekaa madarakani miaka tisa bila kuchaguana, hivyo kuzusha migogoro na kupoteza dira, makovu ambayo kimsingi ndo bado yanayochochea kukosekana kwa ufanisi katika baadhi ya mambo hivi sasa.
Pia uchaguzi huo wa 2006 unabaki kuwa wa kihistoria kwa kuwa ndio uliouingiza uongozi mpya wa Keppa na Nyambui chi ya RT kutoka kilichokuwa Chama cha Riadha Tanzania (TAAA), baada ya kuandaliwa na kupitishwa kwa rasimu mpya ya katiba katika ukumbi wa Maktaba jijini Arusha.
Lakini wakati Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo nchini (wakati huo), Leonard Thadeo kuipitisha rasimu na hivyo kuruhusu uchaguzi kufanyika ambako awali ulipangwa ufanyike hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro ndipo matatizo yalipoanza na kujikuta baadhi ya viongozi ambao walikuwa wamejenga kasumba ya ‘uongozi wa kibwanyenye' katika TAAA wakiipeleka serikali mahakamani bila kuwa na hoja yenye manufaa kwa mchezo husika na Taifa kwa ujumla.
Kilichowasukuma viongozi wale ambao walikuwa wamelewa na kunogewa madaraka kuukataa uchaguzi ule wa Morogoro ambao ulikuwa umegharimiwa na serikali ni hofu ya wao kukosa kile kilichokuwa kikiwanufaisha pale TAAA huku riadha ikizidi kudorora kila kukicha.
Kwa kuwa wadau, hasa viongozi wa klabu, ambao bila ubishi wao ndio uhai wa mchezo wa riadha hapa nchini kutokana na kazi yao kubwa ya kuibua, kulea na kuendeleza vipaji vya wanariadha hapa nchini, walitambua kutothaminiwa hivyo walipigana vilivyo ili wigo wa wapiga kura kuongezwa ili kupanua demokrasia jambo lililoungwa mkono hata serikali.
Jambo hilo lilifanikiwa na klabu kuingizwa katika katika rasimu hiyo mpya, lakini ulipofika uchaguzi huo wa Morogoro, aliyekuwa Mwenyekiti Elias Sulus kwa kushirikiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walikuwa na hofu ya mabadiliko, wakakimbilia mahakama ya Ilala na kuusimamisha uchaguzi huo ili hali wajumbe kutoka pande zote za nchi wakiwa wameishawasili ukumbini.
Baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, kesi iliendelea kuunguruma mahakama ya Ilala, lakini kilichokuwa kikishuhudiwa ni viongozi hao wa TAAA kukaba shida kila siku kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa na hatimaye kwa kujiona hawana hoja wakaamua kufuta kesi wenyewe.
Hapo ndipo ukafanyika uchaguzi wa Mwanza, ambao kama si subira na uanamichezo wa baadhi ya viongozi wa klabu, nao isingefanyika, kwani ile homa ya woga wa viongozi waliojipa hatimiliki za kuongoza watakavyo katika chama hicho ilizidi kupanda na hapo wakaunda zengwe na kuzizuia klabu kupiga kura huku wakibarikiwa na kitu kinachitwa Kamati ya Uchaguzi, ambayo ilikuwa ikijionyesha wazi kutumika kwa manufaa ya viongozi walioiteua.
Na kweli, baadhi ya wagombea ambao walikuwa wakionekana wana nguvu walienguliwa kwa vugezo vya ajabu ajabu katika usaili uliofanyika jijini Dar es Salaam, lakini baada ya kamati hiyo kupigiwa kelele ikawataka eti wakate rufani katika kamati hiyo hiyo na kuwataka waende hadi Mwanza kudai haki yao, ambako baadhi walijipinda na kufika huko kamati hiyo hiyo ikawarejesha tena katika ushindani ili hali uchaguzi unafanyika kesho yake na hivyo kukosa muda wa kutosha kupiga kampeni.
Hatimaye uchaguzi ulifanyika na waliochaguliwa wakachaguliwa, lakini kimsingi wadau kadha wa kadha walishangazwa na baadhi ya matokeo ambako waliokuwa wakiwategemea huenda watapewa nafasi ili kuleta mambo mapya ndani ya chama hicho, walipigwa chini na kura za ukabila, undugu, urafiki na uenzetu zikatawala na baadhi ya watu wakarejea ili hali ni mizigo muda mrefu ndani ya chama.
Matokeo ya uchaguzi huo mi nauitwa ulikuwa wa mizengwe kutokana na kufinyangwa kwa katiba na kujaa fitna kukaingiza mchele na pumba ndani ya RT mpya na matunda ndio haya tunayoiona Riadha Tanzania ya sasa, sambamba na taswira ya mchezo huo ambao ulikuwa nuru ya Tanzania miaka ya nyuma, sasa inatia aibu hadi kumchefua Rais Jakaya Kikwete ambaye hadi sasa haelewi kwanini akina Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Nyambui na nyota wengine wa zamani, hakuna angalau wa mifano yao hivi sasa.
Anayebisha, auangalie uongozi wa sasa wa RT ambao ulipata baraka ya kuongeza muda wa kukaa madaraki ili kuendana na kalenda ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), pumba na mchele vinaonekana wazi.
Hatupendi kuanza kuorodhesha udhaifu mkubwa wa kiutendaji uliofanywa na baadhi ya viongozi waliochaguliwa Mwanza, lakini ulijidhihirisha na hata sasa wadau walioshiriki kuwachagua wanajuta kwa kile walichokiamua.
Katika kudhihirisha wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi wengi wao hawakuwa makini, kuna viongozi tangu wachaguliwe hawajaonekana wakiitumikia riadha Tanzania na hakuna wa kuhoji. Hii ndio Riadha Tanzania.
Ni ajabu na kweli, hakuna mtu anyeuhoji uongozi wa sasa wa RT aliko Makamu wa kwanza wa RT tangu alipochaguliwa kule Mwanza.
Wakati kipindi hiki cha kujuta kwa baadhi ya maa muzi yaliyofanyika Mwanza 2006, RT inaibuka na kuanza kuzitaka Wilaya na Mikoa ifanye chaguzi zake, jambo ambalo kimsingi si sahihi.
Si sahihi kwa sababu RT inafahamu fika Katiba yao ina utata ambao unayakiwa utatuliwe mapema kabla ya siku za uchaguzi kukaribia, vinginevyo tunaweza kushuhudia mbio zikihamia mahakamani tena.
Pili, jeuri ya RT kujivunia mikoa sijui inaitoa wapi ili hali mikoa mingi haina vyama vya riadha vilivyo hai na kwingine haviko kabisa. Lakini inapokea mikutano hii ya uchaguzi ambayo mara nyingi huambatana na posho huibuka watu na kujidai ni viongozi wa riadha huko watokako, ili hali riadha haichezeki huko. Lkini kwa kuwa huwa kuna malengo hasa nyakati za uchaguzi hubebwa na kukirimiwa kidogo na kisha kugawa kura zao kwa uzito posho ya siku mbili ama tatu.
Hakika kwa staili hii, hakika mabadiliko ya maendeleo ya mchezo huu yatabaki ndoto hata kwa sapoti gani kutoka serikalini.
Kwa mazingira haya RT inayokwenda nayo kuelekea uchaguzi wake mkuu, hakina inajiandaa kuingiza vimeo vingine na kuvipa hatamu ya miaka minne kujinufaisha kupitia mchezo wa riadha.
La msingi, kama kweli uongozi wa sasa una nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo wa riadha na si ubinafsi, basi ipanue wigo wa wapiga kuira kwa kuhakikisha vifungu vilivyoleta mgogoro uchaguzi wa Mwanza vinafanyiwa kazi, kisha kusimamia chaguzi za vyama na klabu kabla ya kuruhusu uchaguzi, lengo likiwa kuleta ufanisi na mafanikio katika mchezo wa riadha ambao una sifa ya kipekee hapa nchini. Tofauti na hapo, RT hivi sasa inajiandaa kuongozwa na vimeo tena.
Kila la heri tukutane wiki ijayo.
 
RT inavyojiandaa kuongozwa na vimeo

Tullo Chambo

NI Jumatatu nyingine tena tunakutana wadau wa Uwanja wa Kuchonga, kama kawaida kupeana changamoto za kispoti, lengo likiwa kuboresha ufanisi.
Kabla mchezo haujaanza, tuanze kwa kujuliana hali, ambako bila shaka wote mu wazima, ila kwa wale mambo hayajakaa sawa tunawaombea mabadiliko.
Kwa faida ya wale ambao kwa namna moja ama nyingine, hatukuweza kuwa wote wiki iliyopita tupeane dondoo kwa uchache.
Wiki iliyopita tuliangali jinsi hali inavyoendelea ndani ya klabu kongwe ya Yanga ya jijini Dar es Salaam hivi karibuni iligubikwa na wingu la migogoro ambayo hadi leo bado haujakaa sawa.
Tulitafakari chanzo cha mgogoro huo na athari zake, pia tuliitizama historia ya mitafaruku iliyopita, ambako kimsingi mfadhili wa klabu hiyo Yussuf Manji haepukiki kutajwa au kuzungumziwa kwa namna moja ama nyingine na wanachama, wadau na mashabiki wa timu hiyo.
Baada ya kuichambua historia ya mgogoro huo ambao bado unafukuta, suluhisho lililopatokana ni kwa baadhi ya wanachama kuwa na upeo mdogo na kutojua ajenda inayofanyiwa kazi.
Lakini mwisho wa mwisho, tuliwataka Wana Yanga wahoji hivi sasa kwanini kila tukio likitokea kuhusiana na utendaji, jina la Manji halikosekani. Hivyo tuliwataka wanachama hao kujiangalia na kuijadili hali hii kwa ufundi wa hali ya juu, ili kubaini ‘Wana Yanga jiulizeni, Kwanini iwe Manji.
Baada ya dondoo hizo, sasa turejee katika mada yetu ya leo kama inavyojieleza; ‘Riadha Tanzania inavyojiandaa kuongozwa na vimeo’.
Hivi karibuni, uongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), ulitangaza kuvitaka vyama vya Wilaya na Mikoa kuanza harakati za kufanya chaguzi zao kuelekea ule wa Taifa.
Kwa wale ambao hawana kumbukumbu vizuri, uongozi wa sasa RT ulio chini ya Rais Francis John Keppa na Katibu Mkuu, Mujaya Suleiman Nyambui uliingia madarakani Julai mwaka 2006 katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa benki kuu (BoT), jijini Mwanza.
Ni uchaguzi ambao naweza kusema ulikuwa wa kihistoria, kwani baada ya mbilinge mbilinge za muda mrefu, ambazo ziliitoa jasho na kuitesa serikali kupitia Wizara yenye dhamana na michezo, hatimaye uliweza kufanyika lakini si katika hali ya kuridhisha asilimia 100.
Wadau tunauita ni wa kihistoria, kwani ulifanyika ikiwa chama hicho kimekaa madarakani miaka tisa bila kuchaguana, hivyo kuzusha migogoro na kupoteza dira, makovu ambayo kimsingi ndo bado yanayochochea kukosekana kwa ufanisi katika baadhi ya mambo hivi sasa.
Pia uchaguzi huo wa 2006 unabaki kuwa wa kihistoria kwa kuwa ndio uliouingiza uongozi mpya wa Keppa na Nyambui chi ya RT kutoka kilichokuwa Chama cha Riadha Tanzania (TAAA), baada ya kuandaliwa na kupitishwa kwa rasimu mpya ya katiba katika ukumbi wa Maktaba jijini Arusha.
Lakini wakati Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo nchini (wakati huo), Leonard Thadeo kuipitisha rasimu na hivyo kuruhusu uchaguzi kufanyika ambako awali ulipangwa ufanyike hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro ndipo matatizo yalipoanza na kujikuta baadhi ya viongozi ambao walikuwa wamejenga kasumba ya ‘uongozi wa kibwanyenye’ katika TAAA wakiipeleka serikali mahakamani bila kuwa na hoja yenye manufaa kwa mchezo husika na Taifa kwa ujumla.
Kilichowasukuma viongozi wale ambao walikuwa wamelewa na kunogewa madaraka kuukataa uchaguzi ule wa Morogoro ambao ulikuwa umegharimiwa na serikali ni hofu ya wao kukosa kile kilichokuwa kikiwanufaisha pale TAAA huku riadha ikizidi kudorora kila kukicha.
Kwa kuwa wadau, hasa viongozi wa klabu, ambao bila ubishi wao ndio uhai wa mchezo wa riadha hapa nchini kutokana na kazi yao kubwa ya kuibua, kulea na kuendeleza vipaji vya wanariadha hapa nchini, walitambua kutothaminiwa hivyo walipigana vilivyo ili wigo wa wapiga kura kuongezwa ili kupanua demokrasia jambo lililoungwa mkono hata serikali.
Jambo hilo lilifanikiwa na klabu kuingizwa katika katika rasimu hiyo mpya, lakini ulipofika uchaguzi huo wa Morogoro, aliyekuwa Mwenyekiti Elias Sulus kwa kushirikiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walikuwa na hofu ya mabadiliko, wakakimbilia mahakama ya Ilala na kuusimamisha uchaguzi huo ili hali wajumbe kutoka pande zote za nchi wakiwa wameishawasili ukumbini.
Baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, kesi iliendelea kuunguruma mahakama ya Ilala, lakini kilichokuwa kikishuhudiwa ni viongozi hao wa TAAA kukaba shida kila siku kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa na hatimaye kwa kujiona hawana hoja wakaamua kufuta kesi wenyewe.
Hapo ndipo ukafanyika uchaguzi wa Mwanza, ambao kama si subira na uanamichezo wa baadhi ya viongozi wa klabu, nao isingefanyika, kwani ile homa ya woga wa viongozi waliojipa hatimiliki za kuongoza watakavyo katika chama hicho ilizidi kupanda na hapo wakaunda zengwe na kuzizuia klabu kupiga kura huku wakibarikiwa na kitu kinachitwa Kamati ya Uchaguzi, ambayo ilikuwa ikijionyesha wazi kutumika kwa manufaa ya viongozi walioiteua.
Na kweli, baadhi ya wagombea ambao walikuwa wakionekana wana nguvu walienguliwa kwa vugezo vya ajabu ajabu katika usaili uliofanyika jijini Dar es Salaam, lakini baada ya kamati hiyo kupigiwa kelele ikawataka eti wakate rufani katika kamati hiyo hiyo na kuwataka waende hadi Mwanza kudai haki yao, ambako baadhi walijipinda na kufika huko kamati hiyo hiyo ikawarejesha tena katika ushindani ili hali uchaguzi unafanyika kesho yake na hivyo kukosa muda wa kutosha kupiga kampeni.
Hatimaye uchaguzi ulifanyika na waliochaguliwa wakachaguliwa, lakini kimsingi wadau kadha wa kadha walishangazwa na baadhi ya matokeo ambako waliokuwa wakiwategemea huenda watapewa nafasi ili kuleta mambo mapya ndani ya chama hicho, walipigwa chini na kura za ukabila, undugu, urafiki na uenzetu zikatawala na baadhi ya watu wakarejea ili hali ni mizigo muda mrefu ndani ya chama.
Matokeo ya uchaguzi huo mi nauitwa ulikuwa wa mizengwe kutokana na kufinyangwa kwa katiba na kujaa fitna kukaingiza mchele na pumba ndani ya RT mpya na matunda ndio haya tunayoiona Riadha Tanzania ya sasa, sambamba na taswira ya mchezo huo ambao ulikuwa nuru ya Tanzania miaka ya nyuma, sasa inatia aibu hadi kumchefua Rais Jakaya Kikwete ambaye hadi sasa haelewi kwanini akina Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Nyambui na nyota wengine wa zamani, hakuna angalau wa mifano yao hivi sasa.
Anayebisha, auangalie uongozi wa sasa wa RT ambao ulipata baraka ya kuongeza muda wa kukaa madaraki ili kuendana na kalenda ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), pumba na mchele vinaonekana wazi.
Hatupendi kuanza kuorodhesha udhaifu mkubwa wa kiutendaji uliofanywa na baadhi ya viongozi waliochaguliwa Mwanza, lakini ulijidhihirisha na hata sasa wadau walioshiriki kuwachagua wanajuta kwa kile walichokiamua.
Katika kudhihirisha wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi wengi wao hawakuwa makini, kuna viongozi tangu wachaguliwe hawajaonekana wakiitumikia riadha Tanzania na hakuna wa kuhoji. Hii ndio Riadha Tanzania.
Ni ajabu na kweli, hakuna mtu anyeuhoji uongozi wa sasa wa RT aliko Makamu wa kwanza wa RT tangu alipochaguliwa kule Mwanza.
Wakati kipindi hiki cha kujuta kwa baadhi ya maa muzi yaliyofanyika Mwanza 2006, RT inaibuka na kuanza kuzitaka Wilaya na Mikoa ifanye chaguzi zake, jambo ambalo kimsingi si sahihi.
Si sahihi kwa sababu RT inafahamu fika Katiba yao ina utata ambao unayakiwa utatuliwe mapema kabla ya siku za uchaguzi kukaribia, vinginevyo tunaweza kushuhudia mbio zikihamia mahakamani tena.
Pili, jeuri ya RT kujivunia mikoa sijui inaitoa wapi ili hali mikoa mingi haina vyama vya riadha vilivyo hai na kwingine haviko kabisa. Lakini inapokea mikutano hii ya uchaguzi ambayo mara nyingi huambatana na posho huibuka watu na kujidai ni viongozi wa riadha huko watokako, ili hali riadha haichezeki huko. Lkini kwa kuwa huwa kuna malengo hasa nyakati za uchaguzi hubebwa na kukirimiwa kidogo na kisha kugawa kura zao kwa uzito posho ya siku mbili ama tatu.
Hakika kwa staili hii, hakika mabadiliko ya maendeleo ya mchezo huu yatabaki ndoto hata kwa sapoti gani kutoka serikalini.
Kwa mazingira haya RT inayokwenda nayo kuelekea uchaguzi wake mkuu, hakina inajiandaa kuingiza vimeo vingine na kuvipa hatamu ya miaka minne kujinufaisha kupitia mchezo wa riadha.
La msingi, kama kweli uongozi wa sasa una nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo wa riadha na si ubinafsi, basi ipanue wigo wa wapiga kuira kwa kuhakikisha vifungu vilivyoleta mgogoro uchaguzi wa Mwanza vinafanyiwa kazi, kisha kusimamia chaguzi za vyama na klabu kabla ya kuruhusu uchaguzi, lengo likiwa kuleta ufanisi na mafanikio katika mchezo wa riadha ambao una sifa ya kipekee hapa nchini. Tofauti na hapo, RT hivi sasa inajiandaa kuongozwa na vimeo tena.
Kila la heri tukutane wiki ijayo.
 
JUMA KIPANYA MALAPA: Mtoto wa nyoka anayetesa mchangani

Abdallah Menssah

KUNA ule usemi maarufu wa wahenga usemao, ‘Mtoto wa Nyoka ni Nyoka'. Basi katika kudhihirisha ukweli wa usemi huu, basi Juma Kipanya Malapa ni kati ya wanaodhihirisha.
Juma Kipanya Malapa (miaka 17) ni mtoto wa nyota wa zamani klabu za Yanga na Singida United; Kipanya Malapa ni chipukizi anayeonekana kufuata nyayo za baba yake kwa karibu zaidi.
Kwa hivi sasa, Kipanya ni mtoto anayekipiga kwenye timu ya mchangani ya Guruwe Kids ya Buguruni Madenge; ni kati ya vijana wenye miaka chini ya 18, aliyetokea kuwa gumzo kubwa katika viunga vya wilaya ya Ilala, ambako ndiko hata baba yake alianzia kuonekana.
Hiyo inatokana na uhodari anaouonyesha katika soka awapo uwanjani, kiasi cha mashabiki wengi kumfananisha na Jerry Tegete wa Yanga ya Dar es Salaam na Nani wa Manchester United.
Aidha, baadhi ya mashabiki, wengine wamefikia kumtabiria kuja kuwa mchezaji tishio hapo baadaye, kama zilivyo ndoto zake kwani anataka kuja kukipiga kwenye moja ya klabu kubwa hapa nchini ama hata nje ya nchi.
Kinda huyo anayecheza nafasi ya ushambuliaji, ni mrefu wa wastani, mwenye misuli iliyojengeka, mwenye kasi pamoja na pumzi, huku akiwa mwepesi wa kuwatoka mabeki wa timu pinzani na kuzua balaa golini.
Kocha wa timu yake ya Guruwe Kids yenye zaidi ya wachezaji 30, Majid Jongo, amekuwa akimpanga kwenye mechi ngumu ambako mara zote amekuwa chanzo cha mabao ya ushindi kwa timu yake hiyo.
Katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni na mwandishi wa makala hii, Kipanya anasema kuwa alianza kujifunza soka tangu alipokuwa mdogo, kwa kucheza chandimu na watoto wenzake mtaani kwao.
"Unajua, wakati ule baba alipokuwa anawika nilihamasika sana, hasa nilipokuwa nasikia akitangazwa redioni pale timu yake ilipokuwa inacheza, ndipo nami nikaanza kujifunza taratibu," anasema Kipanya.
Kipanya anasema, alianza kushangaza zaidi watu alipokuwa anasoma, ambapo katika mashindano ya UMITASHUMTA, alimudu kufika ngazi ya wilaya akiongoza kwa mabao ya kufunga.
Hata hivyo, hasiti kubainisha kuwa pamoja na kujaaliwa kipaji cha soka, maendeleo yake darasani yalikuwa ni ya kusuasua ambapo katika matokeo ya mitihani yake, alikuwa akishika nafasi ya 20 hadi 50, kati ya wanafunzi 80 darasani kwao.
Baada ya kumaliza elimu ya msingi na kutobahatika kuchaguliwa kuendelea na sekondari, Kipanya alizidisha bidii kwenye soka kwa kufanya mazoezi ya nguvu uwanjani na kwenye fukwe za bahari.
"Mwaka 2008, nilijiunga na timu ya Emima Fc ambayo ni ya vijana wenye umri wa chini ya mika 14, yenye maskani yake Buguruni Sokoni, jijini Dar es Salaam," anasema Kipanya.
Mwaka 2009, akaingia Al Binjra Fc ya Buguruni kwa Ponza, jijini Dar es Salaam, kabla ya kuitwa katika kikosi cha timu ya mchanganyiko ya vijana wenye ulemavu wa kuzungumza na wasio na ulemavu huo, iliyoko Buguruni Malapa.
Aidha, Kipanya anasema kuwa mwaka jana 2010, alijiunga na timu ya Professional Fc ya Kigogo SUKITA, jijini Dar es Salaam na baadaye, mwishoni mwa mwaka huo, ndipo alipotua Guruwe Kids.
Je, katika kuhakikisha kuwa anakuza na kuendeleza kipaji hicho cha soka alichonacho, baba yake mzazi, Kipanya Malapa anamsaidiaje?
"Baba yangu ananihimiza kufanya mazoezi kwa bidii na kufuata mafundisho ya kocha, ili niweze kufika mbali zaidi na kulirudisha upya jina lake uwanjani," anasema Kipanya.
Kadhalika, Kipanya anayevutiwa na Mrisho Ngassa wa Azam Fc, Athuman Idd ‘Chuji' wa Yanga na Didier Drogba wa Chelsea anasema kuwa matarajio yake ya baadaye ni kuwa mchezaji wa kulipwa.
Unapomuuliza juu ya watu waliochangia kumfikisha hapo alipo sasa katika soka, pamoja na wote wengine, Kipanya anawataja baba yake, Malapa pamoja na makocha Pock Mosses na Majid Jongo.
Kinda huyo, anawaasa wachezaji chipukizi kama yeye, wasife moyo hata pale wanapokumbana na vikwazo hivi na vile vinavyotishia kuwakatisha tamaa na kuwafanya wajutie uamuzi wao wa kujikita katika soka.
"Kikubwa zaidi ni kuzingatia mazoezi pamoja na kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwa makocha wetu, kwa sababu wao ndio chanzo na msingi mkuu wa mafanikio yetu ya kimpira," anasema Kipanya.
Huyo ndiye Juma Kipanya Malapa, aliyezaliwa mwaka 1994, jijini Dar es Salaam na kupata elimu ya msingi katika shule za Hekima Buguruni na Mbagala Annex jijini Dar es Salaam, kati ya mwaka 2002 na 2008.
Ndiye kifungua dimba katika familia ya Kipanya Malapa, yenye watoto wanne, watatu wakiwa ni wa kiume na wote wenye vipaji vya soka, huku mmoja aitwaye Gadaffi akiwa katika kituo cha kukuza vipaji cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Karume, jijini.





Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa, au baruapepe abmenssah@yahoo.com, au simu namba 0718 102050
 
Tamasha la Pasaka laja kivingine 2011
• Kusomesha yatima, kusaidia wajane

na Mwandishi wetu


MWENYEKITI wa Kamati ya Msama Promotions waandaaji wa tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 24, Alex Msama, amesema sehemu ya fedha zitakazopatikana siku hiyo, zitasaidia makundi yenye mahitaji maalum kwenye jamii.
Msama ambaye ni mwasisi wa matamasha ya muziki wa injili nchini, alisema sehemu ya fedha hizo zitatumika kusomesha watoto yatima ili kuwajengea msingi katika maisha yao.
Alisema, mbali ya watoto yatima ambao watanufaika na tamasha hilo kwa utaratibu ambao utawekwa wazi, tamasha hilo litasaidi pia wanawake wajane.
Kwa upande wa wajane, Msama alisema kamati yake itaangalia uwezekano wa kuwafungulia miradi midogo ambayo itakuwa msaada mkubwa kwao kwa ajili ya kuendesha maisha.
Tamasha hilo la kimataifa ambalo litafanyika siku hiyo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, tayari limeanza kuwa gumzo kubwa.
Msama alisema baada ya Diamond Jubilee, tamasha hili litalakopambwa na waimbaji mahiri wa ndani na nje ya nchi, Aprili 25, litahamia Shinyanga.
Alisema kutokana ya wadau wa muziki wa injili, baada ya kushambulia Shinyanga, siku inayofuata (Aprili 26), mashambulizi yatakuwa jijini Mwanza.
Kwa mujibu wa Msama, fedha nyingine zitakazopatikana kwenye Tamasha
hilo zitatumika kwa ajili ya kununua baiskeli za walemamu wa miguu kwa lengo la kuwapa faraja.

“Hili ni Tamasha letu la tano tangu tulianzishe, hivyo mwaka huu tumepanga kutumia fedha zitakazopatikana katika tamasha hilo kwa ajili
ya kuwasomesha watoto yatima, kuwapa mitaji ya biashara wanawake wajane na kununua baskeli kwa wenye ulemavu,” amesema Msama.

Aliongeza kuwa, tayari fedha zilizotumika katika matamasha yaliyopita wameweza kununua basikeli 300 za walemavu kwa kusaidiawa pia na Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi.
“Pia tumeshawasomesha watoto yatima zaidi ya 100 Tanzania nzima kupitia fedha za matamasha yaliyopita.”
Msama pia amesema wamewasaidia wanawake wajane cherehani 30 ikiwa ni mitaji ya bishara kwa ajili ya kuendesha maisha yao.
Katika hatua nyingine, Msama amewashukuru wadau wakubwa wa tamasha la Pasaka akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete
mke wake Salma Kikwete, kwani aliweza kuchangia katika kuwasomesha
watoto 30 kupitia mfuko wake wa WAMA.

“Pia namshukuru Spika wa Bunge la Tisa, Samuel Sita, ambaye alisaidia kusomeshwa kwa watoto 15 na aliyekuwa Waziri wa Sera na Bunge, Philip Marmo.




 
Warembo Kisura waingia kambini


na Dina Ismail


WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini jana katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo, Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12.
Kambi hiyo itahusisha warembo 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini waliofanikiwa kutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.
Mchakato wa kuwapata wasichana hao, ulianza Desemba 11 mwaka jana na kumalizika mapema mwezi huu ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,
Mbeya na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo View Resort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio wa kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema warembo walioingia kambini ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezo vinavyotakiwa.
Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.
Urio aliwataja warembo walioingia kambini ni Neema Mathew na Silipa Swai (Mwanza), Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera), Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).
Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es Salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango na Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa na Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).
Alisema wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka
katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…