Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Wanachama SHIWATA wapatiwa hati miliki


na Makuburi Ally


WANACHAMA 127 wa Taasisi ya SHIWATA wamepatiwa hati za kimila za kumiliki maeneo yao katika kijiji cha Mwanzega kwa ajili ya makazi.
Akizungumza katika mkutano wa wanachama wa SHIWATA, jana, Mwenyekiti wa Shiwata, Taalib Cassim, alisema pamoja na wanachama hao kupatiwa maeneo yao lakini awali yaliyotokea malalamiko kwamba viwanja walivyopewa ni vidogo, hivyo wamewaongezea ukubwa wa viwanja hivyo.
Cassim alisema baada ya kuongeza ukubwa wa viwanja hivyo hivi sasa, viwanja hivyo ambavyo viligawanywa kwa viwanja 30 kwa block moja ambako kwa sasa vitakuwa viwanja 26 katika block moja.
Aidha Cassim alisema baada ya kuanza kwa makabidhiano hayo, Februari 19, utafanyika uzinduzi wa ugawaji wa viwanja utakaofanyika kijijini Mwanzega.
Awali kabla ya ugawaji wa hati hizo, jana ilifanyika semina kutoka Mawakala wa Utafiti wa Majengo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHRBA) walitoa semina ya ujenzi wa nyumba za wanachama hao.
Meneja Ushauri wa HNRBA, Dk. Simona Kintingu alisema gaharama za ujenzi wa nyumba hizo kwa kiwango cha juu ni sh mil 26 na cha chini ni sh mil. 5.
Kintingu aliongozana na Injinia Dk. G.M Kawiche ambaye ni Mkurugenzi wa NHRBA ambaye naye alitoa somo kwa wanachama hao.




 
Paka Mapepe arejea TOT


na Mwandishi wetu


KUNDI mahiri la mipasho hapa nchini, TOT Taarab limemnyakua mwimbaji mahiri wa kike wa fani hiyo, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe', aliyekuwa katika kundi lingine la Five Stars Modern Taarab.
Akithibitisha habari hizo, Katibu wa TOT, Gasper Tumaini, alimweleza mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana kuwa wamemrejesha Paka Mapepe kama moja ya mikakati yao kabambe ya kulirejesha kundi hilo katika chati.
Aidha, Tumaini alisema tayari Paka Mapepe ameshaanza mazoezi na wasanii wenzie wa TOT walioko kambini hivi sasa wakijiandaa
kwa albamu yao ijayo wanayoitarajia kuifyatua baadaye mwaka huu.

Paka Mapepe ambaye mbali ya Five Stars, pia amewahi kupitia makundi ya East African Melody na Zanzibar Stars ni kati ya waimbaji wa kike wa mipasho aliyetokea kuvuta mashabiki wengi, hasa kutokana na uimbaji wake uliojaa hisia kali.
Baadhi ya vibao alivyoimba na kuchangia kumpatia mashabiki wengi zaidi ni pamoja na kile alichokiimba akiwa na kundi la Melody,
kilichompa jina hilo, ‘Paka Mapepe', ‘Huliwezi Bifu', ‘Raha ya Mapenzi' na ‘Ndo Basi Tena'.
 
KIWEWE CHA DEDEBIT: Yanga wachapana makonde
• Suluhu kusakwa kwa Mama Karume Jumanne

na Makuburi Ally


HAIYUMKINI hali ya hewa ndani ya klabu kongwe ya Yanga ya jijini Dar es Salaam bado inaendelea kuchafuka baada ya mashabiki, wachezaji na viongozi kutwangana mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Dedebit ya Ethiopia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.
Katika mechi hiyo ya awali, Yanga ililazimisha sare ya mabao 4-4 ikisawazisha dakika za majeruhi, hali ambayo iliwakera baadhi ya mashabiki na kuanza kuwavamia baadhi ya wachezaji na kuwalaumu huku wengine wakiambulia vipigo.
Kati ya wachezaji waliokumbwa na dhahama hiyo ni Nsa Job ambaye alikumbana na kichapo kutoka kwa kundi linalodaiwa kushirikiana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Klabu hiyo, Kibwana Matokeo ambapo alipasuliwa maeneo ya kichwani.
Awali inadaiwa kundi hilo lilikuwa limepanga kuwashushia kipigo Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Davis Mosha, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Juma Seif, ambao baada ya kuumwa sikio juu ya mpango huo walitumia mbinu za aina yake na kutoweka mapema uwanjani hapo, ndipo dhahama likamshukia Job.
Job baada ya kujeruhiwa, aliripoti kituo cha polisi Msimbazi na kufungua jalada kisha kwenda kupata matibabu.
Lakini suala hilo jana lilichukua sura mpya, baada ya Mosha kukutana na Kibwana Matokeo mgahawa wa Rose Garden Kinondoni ambapo makamu huyo mwenyekiti alimvaa mwanachama huyo na kumshushia vibao vya haja, kabla hajamburuza hadi Polisi Oystebay, na baadaye kupelekwa Msimbazi ambako Job alikofungua mashtaka.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mosha alisema hatua hiyo ya kumnasa makofi Matokeo ilitoka na kushirikiana na mwenzake kuwafanyia fujo baadhi ya wachezaji wa Yanga kwa madai ya kuuza mechi hiyo.
Mosha alisema, Matokeo na kundi lake walimpasua Nsa Job wakidai kwamba amehusika kucheza chini ya kiwango, huku pia wakiwapiga mashabiki wengine uwanjani wakitekeleza maagizo ya mmoja wa maofisa Yanga.
"Matokeo ndiye kiunganishi cha matatizo yote yaliyopangwa ambayo ni kwa ajili ya fujo na matatizo ambayo yanataka kuvuruga mwenendo wa Yanga na maendeleo ya soka la Tanzania kwa ujumla," alisema Mosha na kuongeza:
"Mimi nipo Yanga kwa kutetea wachezaji, hivyo nilifikia hatua ya kumnasa makofi Matokeo baada ya kupigwa wachezaji, mtindo huu wa kupiga wachezaji sijui jamaa wameutoa wapi, sasa hivi bado tuna wakati mgumu ambapo tuna mchezo wa marudiano, badala ya kujipanga na mashindano hayo, tunaendekeza migogoro," alisema Mosha.
Mosha alisema, wamejipanga kukomesha tabia iliyoanzishwa na kundi hilo ambalo linataka kuleta fujo kwani limekuwa na tabia ya kuwafanyia fujo mashabiki mbalimbali wa timu hiyo.
Katika hatua nyingine Mosha alisema, keshokutwa wana mkutano na mdhamini wao, mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mama Fatma Karume, wakiwa na Francis Kifukwe, Yusuf Manji na wazee kwa ajili kuzungumzia maendeleo na kumaliza mitafaruku inayoiandama timu hivi sasa klabu hiyo.
 
Simba kutua Dar leo


na Mwandishi wetu


WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba wanatarajiwa kuwasili jijini leo mchana wakitokea Comoro ambapo walilazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Elan ya huko katika mechi iliyopigwa juzi mjini Moroni.
Habari zilizopatikana kutoka Moroni jana zinaeleza kwamba Simba ambayo jana ilishindwa kurejea kutokana na ratiba ya ndege kutokuwepo jana inarejea ikiwa kazi ngumu ya kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam ili kusonga mbele.
Katika mechi ya juzi tofauti na wengi walivyotegemea, Simba ilikumbana na upinzani mkali kutoka kwa mabingwa hao wa Comoro, ambao walipata nafasi nyingi za kufunga lakini wakashindwa kuzitumia, jambo ambalo lilimshangaza hata Kocha Mkuu, Mzambia Patrick Phiri ambaye alikiri kutoufahamu mchezo wa timu hiyo.
Hata hivyo, Phiri alibainisha kuwa, tayari ameishaisoma timu hiyo na mara atakaporejea jijini ataifanyia kazi, ili kuhakikisha anaibuka na ushindi katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kupigwa wiki mbili zijazo.
Mshindi katika mechi hiyo ataumana na mabingwa watetezi, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), katika hatua inayofuata.
Katika mchezo wa juzi, Simba iliwakilishwa na Ally Mustafa ‘Barthez', Haruna Shamte, Juma Jabu, Meshack Abel, Juma Nyoso, Jerry Santo, Hilary Echesa/ Amri Kiemba, Rashid Gumbo/ Nicco Nyagawa, Patrick Ochan, Emmanuel Okwi na Mussa Hassan Mgosi.
 
Wanariadha mashuhuri kujitosa Kili Marathon 2011


na Mwandishi wetu


WANARIADHA nguli wa mbio za Marathon kutoka nchi mbalimbali duniani, wako katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kwenda mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, kushiriki msimu wa tisa wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon zitakazolindima Februari 27. Francis John Keppa, Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), alisema jana kutoka mkoani Arusha kwamba, wanariadha mashuhuri kama vile Patrick Nyangero, Andrea Silvini, Daudi Joseph, Sarah Majah, Sarah Kavina na Banuelia Brighton wataungana na wanariadha wengine wa hapa nchini na kutoka mataifa mbalimbali.
Patrick Nyangero alikuwa mshindi wa pili kwenye mbio hizo mwaka 2009 akitumia saa 02:15.35, Andrea Silvini mshindi wa pili 2008 baada ya kutumia 02:16.22 huku Banuelia Brighton alishinda mbio hizo kwa upande wa wanawake akimaliza katika muda wa 02:48.37.
Wanariadha wengine waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Martin Sulle ambaye ni mshindi wa nusu marathon 2006 akitumia saa 01:04.03, Peter Sulle, Samwel Shauri na Mary Naali ambaye hivi karibuni alishinda mbio ya Vienna Marathon nchini Austria.
John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema, nchi zaidi ya 35 zinatarajiwa kushiriki huku washiriki kutoka nje ya nchi wakitarajia kuwa zaidi ya 600, ukilinganisha na 500 wa mwaka jana.
Washiriki wa kigeni wanatarajiwa kutoka nchi za Afrika Kusini, Uingereza, Zimbabwe, Kenya, New Zealand, China, Canada, Marekani, Australia, Ufaransa na Italia ambako kwa ujumla, zaidi ya wakimbiaji 5,000 wanatarajiwa kushiriki mbio za mwaka huu.
"Kati ya mambo yanayotarajiwa kuleta msisimko wa aina yake kwenye mbio za mwaka huu ni uwepo wa wasanii watakaoruka kwa miavuli kutoka kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro asubuhi ya siku hiyo na kutua kwenye uwanja wa Ushirika. Na vilevile ushiriki wa timu za wafanyakazi wa makampuni mbalimbali wadhamini unatarajiwa kuleta msisimko wa aina yake. Mpaka sasa kampuni zilizothibitisha kushiriki ni TPC Sugar, Tanga Cement, DT Dobie na KK Security," alisema Addison Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mashindano hayo wakishirikiana na Executive Solutions.
Kwa upande wake Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wakuu wa mbio hizo, George Kavishe alisema Kili Marathon imeendelea kuwa kivutio na shindano kubwa la kimataifa, ikiwa na zaidi ya mataifa 35 yanayoshiriki.
Alisema, mbio hizi huvutia wanariadha mashuhuri wa kimataifa na kuwapa fursa wanariadha wa Tanzania kujipima na kupata uzoefu katika mbio ndefu.
Kilimanjaro Marathon inadhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, huku wadhamini shirikishi ni Vodacom Tanzania (5km Fun Run), CFAO DT Dobie, KK Security, Tanzanite One, TPC Sugar, Precision air, Kilimanjaro Water, Bodi ya Utalii Tanzania na Tanga Cement.



 
Magereza kuajiri wachezaji wa magongo


na Asha Bani, Kagera


KAMISHINA Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Augustino Nanyaro, ametoa tamko la kuajiri vijana wenye sifa za kufanya vizuri katika mchezo wa mpira wa magongo.
Nanyaro aliyasema hayo juzi kwenye hafla ya kuwapongeza wanamichezo 16 waliofanikisha timu hiyo kuwa mabingwa wa Muungano yaliyomalizika hivi karibuni Kagera.
Nanyaro alisema ameyapokea maombi ya kocha na meneja wa timu hiyo ya kutaka kuongezwa wachezaji hivyo anaangalia uwezekano wa kufanya hivyo kwa wale wenye sifa.
Nanyaro alifarijika na ushidi wa timu hiyo na kuahidi pia kuwapatia uwanja pamoja na vifaa vya mchezo huo kama wanavyoomba ikiwa ni pamoja na kutoa kiasi cha mshahara wake kuchangia.
"Wale wenye vipaji pamoja na kuwa hawana elimu lakini tutawachukua kwa kuzingatia kuwa na kipaji cha mchezo huo na si vinginevyo, tunataka kila mwaka wawe wanashinda na sio kuwa mwaka huu tu," alisema Nanyaro.
Aidha Nanyaro alisema kutokana na maombi ya meneja wa timu hiyo aliyetaka kuanzishwe timu ya wanawake alisema jeshi linajaribu kutazama kama kuna uwezekano wa kuanzisha timu hiyo.
Naye meneja wa timu hiyo ASP E Kisonga alisema timu hiyo ina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uwanja wa mazoezi na mechi za majaribio.
Kisonga aliweka bayana vifaa walivyoomba kwa Nanyaro kuwa ni pamoja na jezi, mavazi kwa mlinda mlango na mipira kwa ajili ya kujiandaa na mashindano yajayo.
Naye Ofisa Michezo wa Magereza, Elisha Kitojo, alisema mafanikio ya timu hiyo yanayopatikana katika kuendesha, kuboresha na kudumisha michezo ni kutokana na msaada kutoka kwa viongozi hivyo wana wajibu wa kujituma vilivyo na kutumia nafasi hiyo ambapo uongozi wa juu unathamini na kusaidia maendeleo ya michezo pamoja na huduma stahili ili kupata mafanikio zaidi.
 
Bulembo kuibeba Villa Squad


na Makuburi Ally


UONGOZI wa timu ya Villa Squad jana ulimtangaza Alhaj Abdallah Bulembo kuwa mfadhili wa timu hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara ambayo leo inashuka dimbani kumenyana na wenyeji Coastal Union ya jijini Tanga, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.
Akimtangaza Bulembo jana, Makamu Mwenyekiti wa Villa Squad, Idd Mbonde, alisema hatua ya kupatikana kwa Bulembo imetokana na jitihada za muda mrefu ambazo mara nyingi ziligonga mwamba kutokana na Bulembo kubanwa na majukumu ya kitaifa.
Mbonde alitoa wito kwa wadau wengine wa soka wilayani Kinondoni kujitokeza kwa sababu milango iko wazi ili kufanikisha timu hiyo kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao na kuendelea kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Naye Katibu wa Kamati ya Michezo Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mrimi, alisema pamoja na kwamba Kinodnoni katika Ligi Kuu misimu mitatu iliyopita haijashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo kupitia Bulembo Villa itapanda hadi Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mrimi alitoa wito kwa viongozi wa Villa Squad kuwa na mshikamano na ushirikiano zaidi na kuachana na migogoro ambayo itaipoteza timu hiyo yenye dhamira ya dhati kwa ajili ya michuano hiyo.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mfadhili wa timu hiyo Bulembo alisema baada ya kupumzika, kuombwa na kukataa maombi kwa ajili ya maendeleo ya michezo na kukubali ambapo aliwataka wadau wengine wasikae pembeni baada ya kuingia yeye na kutoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kuisaidia timu hiyo.
Bulembo alisema pamoja na kuwa mfadhili wa timu hiyo hatobadilisha mpangilio wowote wa timu hiyo na badala yake wataiboresha zaidi timu hiyo ili isivuruge mpangilio wake.
"Nitawashirikisha madiwani, wabunge wa Kinondoni ili tufanikishe timu yetu ishiriki Ligi Kuu, kwani mtoto mwenyewe ni mmoja asiwashinde, inabidi wapigane kufa na kupona," alisema Bulembo.



 
RT inavyojiandaa kuongozwa na vimeo

Tullo Chambo

NI Jumatatu nyingine tena tunakutana wadau wa Uwanja wa Kuchonga, kama kawaida kupeana changamoto za kispoti, lengo likiwa kuboresha ufanisi.
Kabla mchezo haujaanza, tuanze kwa kujuliana hali, ambako bila shaka wote mu wazima, ila kwa wale mambo hayajakaa sawa tunawaombea mabadiliko.
Kwa faida ya wale ambao kwa namna moja ama nyingine, hatukuweza kuwa wote wiki iliyopita tupeane dondoo kwa uchache.
Wiki iliyopita tuliangali jinsi hali inavyoendelea ndani ya klabu kongwe ya Yanga ya jijini Dar es Salaam hivi karibuni iligubikwa na wingu la migogoro ambayo hadi leo bado haujakaa sawa.
Tulitafakari chanzo cha mgogoro huo na athari zake, pia tuliitizama historia ya mitafaruku iliyopita, ambako kimsingi mfadhili wa klabu hiyo Yussuf Manji haepukiki kutajwa au kuzungumziwa kwa namna moja ama nyingine na wanachama, wadau na mashabiki wa timu hiyo.
Baada ya kuichambua historia ya mgogoro huo ambao bado unafukuta, suluhisho lililopatokana ni kwa baadhi ya wanachama kuwa na upeo mdogo na kutojua ajenda inayofanyiwa kazi.
Lakini mwisho wa mwisho, tuliwataka Wana Yanga wahoji hivi sasa kwanini kila tukio likitokea kuhusiana na utendaji, jina la Manji halikosekani. Hivyo tuliwataka wanachama hao kujiangalia na kuijadili hali hii kwa ufundi wa hali ya juu, ili kubaini ‘Wana Yanga jiulizeni, Kwanini iwe Manji.
Baada ya dondoo hizo, sasa turejee katika mada yetu ya leo kama inavyojieleza; ‘Riadha Tanzania inavyojiandaa kuongozwa na vimeo’.
Hivi karibuni, uongozi wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), ulitangaza kuvitaka vyama vya Wilaya na Mikoa kuanza harakati za kufanya chaguzi zao kuelekea ule wa Taifa.
Kwa wale ambao hawana kumbukumbu vizuri, uongozi wa sasa RT ulio chini ya Rais Francis John Keppa na Katibu Mkuu, Mujaya Suleiman Nyambui uliingia madarakani Julai mwaka 2006 katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa benki kuu (BoT), jijini Mwanza.
Ni uchaguzi ambao naweza kusema ulikuwa wa kihistoria, kwani baada ya mbilinge mbilinge za muda mrefu, ambazo ziliitoa jasho na kuitesa serikali kupitia Wizara yenye dhamana na michezo, hatimaye uliweza kufanyika lakini si katika hali ya kuridhisha asilimia 100.
Wadau tunauita ni wa kihistoria, kwani ulifanyika ikiwa chama hicho kimekaa madarakani miaka tisa bila kuchaguana, hivyo kuzusha migogoro na kupoteza dira, makovu ambayo kimsingi ndo bado yanayochochea kukosekana kwa ufanisi katika baadhi ya mambo hivi sasa.
Pia uchaguzi huo wa 2006 unabaki kuwa wa kihistoria kwa kuwa ndio uliouingiza uongozi mpya wa Keppa na Nyambui chi ya RT kutoka kilichokuwa Chama cha Riadha Tanzania (TAAA), baada ya kuandaliwa na kupitishwa kwa rasimu mpya ya katiba katika ukumbi wa Maktaba jijini Arusha.
Lakini wakati Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo nchini (wakati huo), Leonard Thadeo kuipitisha rasimu na hivyo kuruhusu uchaguzi kufanyika ambako awali ulipangwa ufanyike hoteli ya Mount Uluguru mjini Morogoro ndipo matatizo yalipoanza na kujikuta baadhi ya viongozi ambao walikuwa wamejenga kasumba ya ‘uongozi wa kibwanyenye’ katika TAAA wakiipeleka serikali mahakamani bila kuwa na hoja yenye manufaa kwa mchezo husika na Taifa kwa ujumla.
Kilichowasukuma viongozi wale ambao walikuwa wamelewa na kunogewa madaraka kuukataa uchaguzi ule wa Morogoro ambao ulikuwa umegharimiwa na serikali ni hofu ya wao kukosa kile kilichokuwa kikiwanufaisha pale TAAA huku riadha ikizidi kudorora kila kukicha.
Kwa kuwa wadau, hasa viongozi wa klabu, ambao bila ubishi wao ndio uhai wa mchezo wa riadha hapa nchini kutokana na kazi yao kubwa ya kuibua, kulea na kuendeleza vipaji vya wanariadha hapa nchini, walitambua kutothaminiwa hivyo walipigana vilivyo ili wigo wa wapiga kura kuongezwa ili kupanua demokrasia jambo lililoungwa mkono hata serikali.
Jambo hilo lilifanikiwa na klabu kuingizwa katika katika rasimu hiyo mpya, lakini ulipofika uchaguzi huo wa Morogoro, aliyekuwa Mwenyekiti Elias Sulus kwa kushirikiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambao walikuwa na hofu ya mabadiliko, wakakimbilia mahakama ya Ilala na kuusimamisha uchaguzi huo ili hali wajumbe kutoka pande zote za nchi wakiwa wameishawasili ukumbini.
Baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, kesi iliendelea kuunguruma mahakama ya Ilala, lakini kilichokuwa kikishuhudiwa ni viongozi hao wa TAAA kukaba shida kila siku kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa na hatimaye kwa kujiona hawana hoja wakaamua kufuta kesi wenyewe.
Hapo ndipo ukafanyika uchaguzi wa Mwanza, ambao kama si subira na uanamichezo wa baadhi ya viongozi wa klabu, nao isingefanyika, kwani ile homa ya woga wa viongozi waliojipa hatimiliki za kuongoza watakavyo katika chama hicho ilizidi kupanda na hapo wakaunda zengwe na kuzizuia klabu kupiga kura huku wakibarikiwa na kitu kinachitwa Kamati ya Uchaguzi, ambayo ilikuwa ikijionyesha wazi kutumika kwa manufaa ya viongozi walioiteua.
Na kweli, baadhi ya wagombea ambao walikuwa wakionekana wana nguvu walienguliwa kwa vugezo vya ajabu ajabu katika usaili uliofanyika jijini Dar es Salaam, lakini baada ya kamati hiyo kupigiwa kelele ikawataka eti wakate rufani katika kamati hiyo hiyo na kuwataka waende hadi Mwanza kudai haki yao, ambako baadhi walijipinda na kufika huko kamati hiyo hiyo ikawarejesha tena katika ushindani ili hali uchaguzi unafanyika kesho yake na hivyo kukosa muda wa kutosha kupiga kampeni.
Hatimaye uchaguzi ulifanyika na waliochaguliwa wakachaguliwa, lakini kimsingi wadau kadha wa kadha walishangazwa na baadhi ya matokeo ambako waliokuwa wakiwategemea huenda watapewa nafasi ili kuleta mambo mapya ndani ya chama hicho, walipigwa chini na kura za ukabila, undugu, urafiki na uenzetu zikatawala na baadhi ya watu wakarejea ili hali ni mizigo muda mrefu ndani ya chama.
Matokeo ya uchaguzi huo mi nauitwa ulikuwa wa mizengwe kutokana na kufinyangwa kwa katiba na kujaa fitna kukaingiza mchele na pumba ndani ya RT mpya na matunda ndio haya tunayoiona Riadha Tanzania ya sasa, sambamba na taswira ya mchezo huo ambao ulikuwa nuru ya Tanzania miaka ya nyuma, sasa inatia aibu hadi kumchefua Rais Jakaya Kikwete ambaye hadi sasa haelewi kwanini akina Filbert Bayi, Juma Ikangaa, Nyambui na nyota wengine wa zamani, hakuna angalau wa mifano yao hivi sasa.
Anayebisha, auangalie uongozi wa sasa wa RT ambao ulipata baraka ya kuongeza muda wa kukaa madaraki ili kuendana na kalenda ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), pumba na mchele vinaonekana wazi.
Hatupendi kuanza kuorodhesha udhaifu mkubwa wa kiutendaji uliofanywa na baadhi ya viongozi waliochaguliwa Mwanza, lakini ulijidhihirisha na hata sasa wadau walioshiriki kuwachagua wanajuta kwa kile walichokiamua.
Katika kudhihirisha wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi wengi wao hawakuwa makini, kuna viongozi tangu wachaguliwe hawajaonekana wakiitumikia riadha Tanzania na hakuna wa kuhoji. Hii ndio Riadha Tanzania.
Ni ajabu na kweli, hakuna mtu anyeuhoji uongozi wa sasa wa RT aliko Makamu wa kwanza wa RT tangu alipochaguliwa kule Mwanza.
Wakati kipindi hiki cha kujuta kwa baadhi ya maa muzi yaliyofanyika Mwanza 2006, RT inaibuka na kuanza kuzitaka Wilaya na Mikoa ifanye chaguzi zake, jambo ambalo kimsingi si sahihi.
Si sahihi kwa sababu RT inafahamu fika Katiba yao ina utata ambao unayakiwa utatuliwe mapema kabla ya siku za uchaguzi kukaribia, vinginevyo tunaweza kushuhudia mbio zikihamia mahakamani tena.
Pili, jeuri ya RT kujivunia mikoa sijui inaitoa wapi ili hali mikoa mingi haina vyama vya riadha vilivyo hai na kwingine haviko kabisa. Lakini inapokea mikutano hii ya uchaguzi ambayo mara nyingi huambatana na posho huibuka watu na kujidai ni viongozi wa riadha huko watokako, ili hali riadha haichezeki huko. Lkini kwa kuwa huwa kuna malengo hasa nyakati za uchaguzi hubebwa na kukirimiwa kidogo na kisha kugawa kura zao kwa uzito posho ya siku mbili ama tatu.
Hakika kwa staili hii, hakika mabadiliko ya maendeleo ya mchezo huu yatabaki ndoto hata kwa sapoti gani kutoka serikalini.
Kwa mazingira haya RT inayokwenda nayo kuelekea uchaguzi wake mkuu, hakina inajiandaa kuingiza vimeo vingine na kuvipa hatamu ya miaka minne kujinufaisha kupitia mchezo wa riadha.
La msingi, kama kweli uongozi wa sasa una nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo wa riadha na si ubinafsi, basi ipanue wigo wa wapiga kuira kwa kuhakikisha vifungu vilivyoleta mgogoro uchaguzi wa Mwanza vinafanyiwa kazi, kisha kusimamia chaguzi za vyama na klabu kabla ya kuruhusu uchaguzi, lengo likiwa kuleta ufanisi na mafanikio katika mchezo wa riadha ambao una sifa ya kipekee hapa nchini. Tofauti na hapo, RT hivi sasa inajiandaa kuongozwa na vimeo tena.
Kila la heri tukutane wiki ijayo.
 
'Phiri ana kazi ya ziada marudiano' Sunday, 30 January 2011 21:04
Kocha wa Simba Patrick Phiri

Andrew Kingamkono, Moroni
KOCHA wa Simba, Patrick Phiri itamlazimu kufanya kazi ya ziada kushinda mchezo wa marudiano dhidi ya Elan Club de Mitsoudje ya Comoro katika mchezo wa pili wa raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika siku 12 zijazo.

Simba na Elan Club de Mitsoudje zilipambana mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Said Mohamed Cheikh, mchezo uliomalizika kwa suluhu.

Mabingwa hao wa Tanzania, walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kusonga kwa kishindo, lakini hali haikuwa hivyo baada ya kuzidiwa maarifa na mchezo kumalizika kwa suluhu.

Phiri ambaye alisaidia Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi , kikosi chake bado kilionekana kinasumbuliwa na tatizo la umaliziaji.

Simba iliyocheza bila kipa wake namba moja, Juma Kaseja na kumwanzisha Ali Mustapha 'Barthez' ambaye aliokoa hatari nyingi lakini kosa ambalo Phiri anaweza kujilaumu ni kumwazisha Mussa Hassan Mgosi badala ya Mbwana Samatta.

Siku ya mwisho ya mazoezi Ijumaa, Mzambia huyo alitengeneza washambuliaji pacha ili kupata mbinu za kushambulia. Pacha moja ilikuwa kati ya Mgosi na Emmanuel Okwi nyingine ni Samatta na Ally Shibori walikuwa wakicheza kwa zamu kujaribu kufunga kwa krosi.

Katika zoezi hilo Mgosi na Okwi walipoteza nafasi nyingi na kuonekana kukosa umakini tofauti na ilivyokuwa kwa Samata na Shibori. Shibori alionyesha uwezo wa kukimbia wakati Samatta alikuwa makini kwenye kufunga.

Jambo ambalo Phiri hakuliona Jumamosi aliwaanzisha Mgosi na Okwi ambao walipoteza zaidi ya nafasi 10 kwa pamoja na mara moja tu mpira wa kichwa wa Mgosi uligonga mwamba.

Mbaya zaidi, ni uchezaji wa ubinafsi uliojaribu kuonyeshwa na Okwi na Mgosi kwani muda wote hakuwa tayari kutengenezea nafasi na hata kama moja amekaa sehemu nzuri hakupewa pasi bila ya sababu ya msingi jambo liloigharimu Simba.

Hata uamuzi wa kumtoa Mgosi na kumwingiza Shibori haukuwa sahihi sana kwa sababu Simba walihitaji mtu mwenye uwezo wa kumiliki mpira.

Kwa upande mwingine Phiri mapema alishakuwa na taarifa kwamba Elan ni wazuri kwa kushambulia kupitia winga na wanacheza kwa kasi muda wote lakini alijaza viungo wake wasiokuwa na kasi na wasiojua kukaba na kuruhusu kupigwa krosi nyingi.

Phiri aliwaanzisha Jerry Santo, Hillary Echessa, Patrick Ochan katikati huku Gumbo akicheza winga wa kulia na Mgosi kushoto.

Aliamua kumpeleka Mgosi ili kuondoa umakini wa mabeki wa Elan walioonyesha kumpania zaidi mshambuliaji huyo, lakini alisahau kuwaelekeza, Echessa au Ochan kucheza zaidi pembeni ili kuongeza ulinzi.

Kwa kuwa Mgosi na Gumbo wao ni wachezaji wa kati kwa asili walishindwa kutoa msaada wa kutosha kwa Haruna Shamte na Juma Jabu ambao walionekana kuzidiwa na kasi ya mawinga wa Elan, Moustakima Mmadi na Abdoulkarim Sandjema 'Beckham' waliopitisha krosi na hata kumfikia kirahisi kipa, Mustapha.

Haya ni makosa makubwa aliyoyafanya Phiri kwenye mchezo huo wa kwanza wa kutafuta kutimiza ndoto yake ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwenye mkutano wake na wanahabari wa hapa alikiri kuwa timu yake haikucheza kwenye kiwango stahiki na kuahidi kurekebisha hali hiyo kabla ya mechi ya marudiano.

Naye nahodha wa Simba, Nico Nyagawa alisema: "Kweli hatukucheza vizuri tumepoteza nafasi nyingi za kufunga na pia tulikaribisha mashambulizi mengi...tutajipanga mechi ya marudiano."
 
Minziro: Wiki mbili zitanitosha kujenga timu
Sunday, 30 January 2011 21:00

Clara Alphonce
KOCHA mteule wa Yanga, Fred Felix Minziro 'Majeshi' amesema Yanga itasonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho, kwani atatumia wiki mbili kuiandaa timu yake kabla ya mchezo wa marudiano.

Akizungumza baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Dedebit ya Ethiopia, Minziro alisema kuwa amepewa timu siku tatu kabla ya mechi hiyo kubwa na hakuwa anafahamu cha kufanya ispokuwa kutumia mfumo wa kocha Kosta Papic kwa mchezo huo.

"Nilihofia kuleta mfumo mwingine, huwezi kubadilisha timu haraka kiasi hicho, muda wa wiki mbili nikiwa na timu nitajipanga vizuri na naamini ushindi utapatikana...," alisema Minziro.

Minziro sasa anahesabika kama kocha wa timu hiyo baada ya Papic kutema kibarua na anatarajiwa kuondoka leo baada ya kutokubaliana na baadhi ya vitu alivyokuwa anavitaka Yanga na Mdhamini wao, Yusuf Manji.

Mgogoro wa Kocha huyo na Yanga uliibuka baada ya uongozi kumuajiri Minziro kuwa msaidizi wake (Papic), huku Papic akipinga kwa kile alichodai kutoshirikishwa akiwa mkuu wa benchi la ufundi.

Akizungumza na Mwananchi jana Papic alisema kuwa anaondoka kesho (leo) kama alivyopanga baada ya kutofikia muafaka katika maongezi yao na Manji.

''Kweli nilikuwa na kikao na Manji lakini hatukumaliza maongezi yetu na pia nikiwapigia simu viongozi hasa Mwenyekiti, Lloyd Nchunga nashangaa hapokei simu yangu,'' alisema Papic ambaye hakufika kabisa katika mechi ya juzi.

Hata hivyo, habari zilizopatikana jana, zilidai kuwa Manji alikuwa afanye mazungumzo ya mwisho na kocha huyo kumshawishi abaki Yanga, lakini ni wazi kuwa inawezekana yasifikie suluhu kwa kuwa Mserbia huyo alikwishaamua kutaka kuondoka.

Katika hatua nyingine, uongozi wa Hoteli ya Tamar iliyopo Mwenge Jijini Dar es Salaam, umelizuia basi la viongozi wa Yanga kwa kuwa wanaidai klabu hiyo zaidi ya sh9milioni.

Mwananchi iliyokuwa hotelini hapo, ilifahamishwa na mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo kuwa basi hilo dogo limezuiwa hadi hapo watakapolipa fedha hizo.

"Unajua Yanga walikuwa wanakaa hapa, sasa baada ya kuona wachezaji wanatoka kwenda kwenye mechi Jumamosi, wakiwa na mabegi yao, ilitustua na uongozi ukaamuru gari hilo lizuiwe," alisema kwa masharti ya kutotajwa jina.

Afisa mmoja wa Yanga (jina tunalo) alikiri kuwepo kwa hali hiyo pamoja na deni. Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga mara kadhaa alipopigiwa simu kuzungumzia hali hiyo, ilikuwa ikiita bila majibu.

Hata hivyo, afisa huyo alisema kuwa viongozi wa klabu hiyo wameahidi kulipa deni hilo leo na Mwananchi ilipotaka kukutana na meneja wa Hotel hiyo kwa ajili ya kupata ufafanuzi zaidi, ilielezwa kuwa yuko kwenye kikao.

Wakati huo huo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Davis Mosha na Makamu Mwenyekiti wa kuratibu Matawi ya klabu hiyo, Mbwana Matokeo jana walizikunja hadharani kwa sababu mbalimbali.

Mosha alisema kuwa aliamua kumpiga Mbwana jana kwenye mgahawa wa Rose Garden baada ya kiongozi huyo kwenda kuwatukana wachezaji na kudai kuwa walicheza chini ya kiwango katika mechi yao ya juzi dhidi ya Dedebit huku akidai walipewa hela na Mosha ili wahujumu.

Alisema kuwa kiongozi huyo amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha yeye anatoka Yanga baada ya kuambiwa na mdhamini wao Manji wafanye linalowezekana kuakikisha anaondoka madarakani.

Lakini kwa upande wake Kibwana alisema kuwa tuhuma anazopewa na Mosha si za kweli kwani hakuwahi hata siku moja kwenda katika vyumba vya wachezaji na kumtukana pamoja na kuwashutumu wachezaji.

Hata hivyo, alisema kuwa baada ya kitendo hicho, Kibwana alikwenda kumfungulia kesi Mosha ya shambulio la mwili katika Kituo cha Polisi Oysterbay.
 
TMK, Rhino droo ngoma Sunday, 30 January 2011 21:01

Calvin Kiwia
TIMU za TMK United ya jijini Dar es Salaam na Rhino Rangers Tabora zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa ufunguzi wa Fainali za Ligi Daraja la Kwanza 9Bora uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Kocha wa timu ya TMK Utd ya jijini Dar es Salaam, John William 'Del Piero' aliliambia Mwananchi jana kwa simu kuwa mchezo huo umemalizika kwa timu zote kushindwa kufungana na kusifu uwezo mkubwa ulioonyeshwa na safu za ulinzi za timu zote mbili.

"Kikwazo kikubwa ambacho kimechangia kuwanyima mashabiki na wapenzi wa timu hizi ni uwezo mkubwa ulioonyeshwa na walinda milango pamoja na mabeki kwa timu zote mbili," alisema Del Piero.

"Mchezo ulikuwa mzuri na waushindani vijana walijitahidi kila wawezavyo lakini hawakufanikiwa kupata bao, kwasasa tunajipanga zaidi kwa mchezo wetu wa pili kesho dhidi Polisi Moro," alisisitiza.

Kwa upande wa Rhino Rangers Tabora kupitia kocha wake David Mwamaja alikisifu kikosi chake kwa kucheza kwa uelewano zaidi lakini akatupa lawama kwa safu yake ya ushambuliaji kukosa mabao ya wazi.

"Matatizo nimeyaona nitayafanyia kazi ili mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons niweze kupata pointi tatu na kujiweka katika nafasi nzuri," alisema Mwamaja.

Fainali hiyo inaendelea tena leo kwa michezo yake miwili ambapo wenyeji Coastal Union watakuwa wakitupa karata yao ya kwanza dhidi ya Villa Squad ya jijini Dar es Salaam na kufuatiwa na mchezo kati ya Morani FC Manyara na Oljoro JKT ya Arusha.
 
Yanga Bomba, mashabiki nusura wazitwange Taifa Sunday, 30 January 2011 20:58

Calvin Kiwia
MASHABIKI wa Yanga juzi nusura watwangane wenyewe kwa wenyewe kutokana na kila upande kumshutumu mwenzake kuwa amesababisha timu kucheza chini ya kiwango.

Baada ya filimbi ya mwisho, mizozo iliibuka nje ya uwanja na zaidi ni kundi la wananchama wanaojiita 'Yanga Bomba' na pande mbalimbali walikuwa wakizozana kukaribia kutwangana.

Mbali na hali hiyo, wadau wa Yanga walikuwa hawaamini kama Yanga imetoka sare ya 4-4 huku makundi mbalimbali ya mashabiki yakiwa 'yameganda' majukwaani na nje ya uwanja wakitafakari nini kimetokea.

Hali hiyo ilisababisha polisi waliokuwa wakilinda usalama kuanza kuwatangazia mashabiki hao kuwa hawatakiwi kuweka vikundi na waondoke mara moja. "Mpira umekwisha, watu waondoke...watu waende majumbani kwao...," ilisikika sauti hiyo na watu kuanza kuondoka.

Ukiacha hayo, katika mchezo wa juzi wa Kombe la Shirikisho, Yanga walitoka nyuma na kusawazisha mabao manne dhidi ya Dedebit kutoka Ethiopia kuwa sare ya 4-4, mchezo huo iliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wahabeshi hao walimiliki mpira kwa asilimia 61 dhidi ya 39 za Yanga wakitawala zaidi sehemu ya kiungo ya wenyeji wao Yanga. Walicheza pasi 27 bila kuguswa na wachezaji wa Yanga waliokuwa wakiutafuta kwa tochi.

Kumiliki huko kuliwafanya Dedebit kuweza kulifikia lango la wenyeji wao Yanga mara 17 na kufanikiwa kupata mabao yao yote manne na kona nne wakati Yanga walifika mara 13 na kupata kona mbili.

Beki wa Yanga Nadir Haroub aliongoza kutoa mipira nje kwa nia ya kutibua mipango ya Wahabeshi hao waliokuwa wakionana vema, alitoa mara 19 kati ya 41 za Yanga kwenye mchezo huo.

Wakati nahodha wao Shadrack Nsajigwa aliongoza kwa kuwapiga viatu Wahabeshi hao akiwa amewapiga viatu sita dhidi ya 14 walivyocheza wenyeji Yanga.

Dedebit waliongoza kwa kuotea, mara nne wakati Yanga mara tatu. Omega Seme, Tegete na Nurdin Bakari waliongoza kupoteza pasi. Pasi16 kati ya 21 walizopewa na wachezaji wenzao akifuatiwa na Iddi Mbaga aliyepoteza pasi saba dhidi ya 15 alizopewa.

Safu ya ulinzi ya Yanga ilionekana kutoelewana na kufanya makosa mawili ya kizembe yaliyosababisha mabao mawili yakifungwa kwa upande wao, moja ni lile ambalo kipa wake Yaw Berko kumuanzishia mpira Omega Seme akiwa na adui na kumlazimu kutoa pasi mbovu kwa Isaac Boakye aliyepokonywa mpira huo na kuzaa bao la kwanza.

Uzembe huo ilijitokeza tena pale beki wake Haroub kujaribu kumlamba cheza mshambuliaji wa Dedebit Damit Tikabu na kuteleza na alipiga krosi iliyounganishwa kimiani na Birham Bogale.

Nayo safu ya ushambuliaji ilikuwa ikicheza bila ya kushirikiana tunafiki ni hii ni kazi ya mwalimu kuyafanyia kazi yote hayo ili ikaweze kufanya vyema kwenye mchezao wao wa marudiano utakaopigwa Ethiopia majuma mawili yajayo.
 
Wanariadha mashuhuri kushiriki mbio za K'njaro Sunday, 30 January 2011 20:57

Na Mwandishi Wetu
WANARIADHA mashuhuri duniani, wako katika maandalizi ya kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon, zitakazofanyika Februari 27, mkoani Kilimanjaro

Rais wa Chama cha Riadha Tanzania, AT, Francis John alisema jana kwamba wanariadha mashuhuri kama vile Patrick Nyangero, Andrea Silvini, Daudi Joseph, Sarah Majah, Sarah Kavina na Banuelia Brighton wataungana na wanariadha wengine wa hapa nchini na wengine kutoka mataifa mbalimbali.

Patrick Nyangero alikuwa mshindi wa pili kwenye mbio hizo mwaka 2009 baada ya kumaliza mbio katika muda wa 02:15:35, Andrea Silvini alishika nafasi ya tatu kwenye mbio hizo mwaka 2008 baada ya kumaliza mbio katika muda wa 02:16:22.

Banuelia Brighton alishinda mbio hizo kwa upande wa wanawake akimaliza katika muda wa 02:48:37.

Wanariadha wengine waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Martin Sulle (mshindi wa nusu marathon mwaka 2006 katika muda wa saa 01:04:03, Peter Sulle, Samwel Shauri na Mary Naali ambaye hivi karibuni alishinda mbio ya Vienna Marathon nchini Austria.

John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, waandaaji wa mbio hizo alisema nchi zaidi ya 35 zinatarajiwa kushiriki huku washiriki kutoka nje ya nchi wakitarajia kuwa zaidi ya 600 ukilinganisha na 500 wa mwaka jana.

Washiriki wa kigeni wanatarajiwa kutoka Afrika Kusini, England, Zimbabwe, Kenya, New Zealand, China, Canada, Marekani, Australia, Ufaransa na Italia. Zaidi ya wakimbiaji 5,000 wanatarajiwa kushiriki mbio za hizo.

Mbio hizo zimedhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager na wadhamini shirikishi ambao ni Vodacom (5km Fun Run), CFAO DT Dobie, KK Security, TanzaniteOne, TPC Sugar, Precisionair, Kilimanjaro Water, Bodi ya Utalii Tanzania na Tanga Cement.



Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!
 
Japan mabingwa Asia Sunday, 30 January 2011 20:41

DOHA, Qatar
TIMU Japan imetwaa ubingwa wa kombe la Asia kwa mara ya nne baada ya kuichapa bao 1-0 Australia katika mechi ya fainalin iliyochezwa kwenye Uwanja wa Khalifa.

Alikuwa ni mshambuliaji Tadanari Lee ambaye alikuwa ametokea benchi aliyeipatia Japan bao hilo la ushindi katika dakika ya 109 baada ya kupiga shuti la kali la mguu wa kushoto akiwa umbali wa mita 10 kutoka goli la Australia.

Lee alipiga shuti hilo baada ya kupokea pasi kutoka kwa beki Yuto Nagatoma ambapo mpira ulikuta akiwa peke yake hivyo kupiga shuti hilo ambalo lilimshinda kipa wa Australia Mark Schwarzer.

"Tumecheza mashindano haya kwa kujituma sana na kujitoa kweli na siku zote tumekuwa tukilazimisha kuopata ushindi kwa kutandaza soka, timu yetu ina vijana wadogo,"alisema kocha Japan ambaye ni raia wa Italia, Alberto Zaccheroni.

"Wachezaji pia waliokuwa wakitokea benchi na wenyewe walifanya kazi kubwa akama alivyofanya Lee,"aliongeza Zaccheroni.

Mchezaji wa kiungo wa Japan Keisuke Honda alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa timu ya Australia kuingia fainali baada kuhama katika mashindano ya Oceania mwaka 2006, ambapo miaka minne iliyopita ilifungwa na Japan katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo ya Asia.

Mashindano hayo ya Kombe la Asia yalifanyika katika nchi ya Qatar ambayo imepewa nafasi ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia 2022, hivyo kuandaa mashindano ya kombe la Asia ilikuwa ni kama majaribio kwao.

Katika mechi ya fainali kati ya Japan na Australia, Raisi wa FIFA, Sepp Blater alikuwepo pamoja na raisi wa Shirikisho la soka Asia,Mohamed bin Hammam na raisi wa UEFA,Michael Platini.

Mashindano hayo ya Asia ambayo yalifanyika kwa muda wa wiki tatu na kuchezwa mechi 32 yalishuhudiwa yakifungwa katika uwanja wa Khalifa katika mechi ya fainali ambayo ilijaza watu 37,174.

Akizungumzia kuhusu pambano hilo kocha wa Australia,Holger Osieck alisema,"tumesikitishwa kushika nfasi ya pili, tulipata nafasi za kupata ushindi lakini tulishindwa kuzitumia, tunatakiwa kufanyia kazi sana suala la ufungaji kwenye timu yetu."

"Nawasikitikia vijana wangu hawakupata zawadi waliyokuwa awakistahili kutokana na kujituma kwao ambayo ni kutwaa ubingwa wa Asia,"alisema Osieck.

Alisema,"Kosa moja tu walilolifanya vijana wangu ndilo lililowangusha na hii ni baada ya kumuacha Lee afunge bao wakati wa muda wa nyongeza."

Japan pia ilihitaji muda wa nyongeza na penati kuweza kuifunga Korea Kusini katika mechi ya nusu fainali na ilikuwa ikicheza bila ya kiungo wake mahiri Shinji Kagawa.

Katika kipindi cha kwanza dhidi ya Australia, timu ya Japan iliipa Australia nafasi nyingi za kupata ushindi, lakini washambuliaji wa Australia hawakuwa makini kutumia nafasi hizo, lakini hata Japan katika kipindi cha pili walipata nafasi baada ya kutawala vizuri nafasi ya kiungo.

"Tulienda fainali tukiwa tumechoka sana, lakini tulikuwa na nia ya kupata ushindi,"alisema Zaccheroni.
 
Djokovic ashinda Australian Open http://www.mwananchi.co.tz/componen...rb3ZpYy1hc2hpbmRhLWF1c3RyYWxpYW4tb3Blbi5odG1s
Sunday, 30 January 2011 20:41

MELBOURNE, Australia

NOVAK Djokovic ametwaa ubingwa wa Mashindano ya Australia Open baada ya kumchapa Andy Murray 6-4, 6-2, 6-3 katika mechi ya fainali.

Katika mashindano ya mwaka jana ya Australia Open, Murray alitolea katika fainali na Roger Federer.

"Tunafahamiana sana mimi na Murray kwa hiyo mechi ya leo ilikuwa ngumu sana,"alisema Djokovic.

Murray alitarajiwa na Waingereza wengi kwamba atamaliza ukame wa Waingereza kutwaa ubingwa wa mataji makubwa katika mchezo wa tenisi ambapo mara ya mwisho Muingereza Fred Perry ndiye aliyetwaa US Open mwaka 1936.

"Nitajaribu kujipanga vizuri mwaka huu ili niweze kuwa nafasi ya kufanya vizuri siku za mbeleni, nimefanya vizuri kuliko mwaka jana , nafikiri Novak amecheza vizuri sana,"alisema Murray.

Murray na Djokovic wote wana miaka 23 ambapo wachezaji hao ni marafiki na mara nyingi hufanya mazoezi pamoja, hata baada ya mechi kumalizika wachezaji hao walikumbatiana.

Katika mechi ya wanawake iliyochezwa siku ya Jumamosi, mwanadada Ki Clijster alitwaa ubingwa baada ya kumchapa Li Na 3-6, 6-3, 6-3.
 
Papic azidi kuikoroga Yanga


*Asisitiza kuondoka nchini

Na Mwandishi Wetu

SIKU chache baada ya kudaiwa Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic kukubali kuendelea kuinoa timu hiyo, kocha huyo
sasa amezua jipya ambapo sasa amesema hataki kufanya kazi na aliyekuwa msaidizi wake, Salvatory Edward na kusisitiza kwamba ataondoka leo nchini.

Papic hivi karibuni alitangaza kujiuzulu kwa kile anachodai hataki kufanya kazi na kocha aliyeletewa na uongozi, Fredy Felix 'Minziro' kwa madai kwamba hataki kusaidiwa na kocha aliyewahi kuwa Kocha Mkuu wa timu inayocheza Ligi Kuu.

Minziro awali kabla ya kuitwa Yanga kumsaidia, Papic alikuwa akiifunza Ruvu Shooting inayocheza Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lakini kabla ya siku moja kucheza Dedebit ya Ethiopia katika mechi ya Kombe la Shirikisho, vyombo vya habari viliripoti kuwa Papic ameamua kurejea Yanga baada ya kuzungumza na Mdhamini wa Yanga Yusuf Manji kwa kina.

Kocha huyo anadaiwa alikuwa akisubiri kauli ya Manji, ambaye awali walifanya naye mazungumzo kuhusu hatima yake lakini hadi jana alikuwa hajaonana naye tena.

Katika mechi hiyo ambayo timu hizo zilitoka sare ya mabao 4-4, Papic hakuwepo kwenye benchi la ufundi ambalo lilikuwa chini ya Minziro.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Yanga, Llody Nchunga alisema baada ya kusikia Papic amebadilisha uamuzi wake aliamua kukaa naye chini kujadili hatma yake.

"Nilizungumza na tukakubaliana amalizie mkataba wake, lakini hata hivyo aliendelea na msimamo wake wa kuondoka na pia si kung'ang'ania kuondoka tu hivi sasa hamtaki tena Salvatori (Edwrad) kufanya naye kazi," alisema Nchunga.

Alisema wanashindwa kumwelewa kocha huyo kwanini anakuwa na masharti mengi ambapo awali alikataa kufanya kazi na Minziro na sasa hataki kufanya kazi na Salvatory.

Nchunga alisema kutokana na hali hiyo amemwandikia barua ya kutaka kujua baadhi ya mambo kabla hajaondoka.




1 Maoni:


Anonymous said... Hi

Kwani kuna ulazima wa kumng'ang'ania? huyu mzungu?

January 31, 2011 3:46 AM
 
Simba SC kurejea nchini leo


Na Zahoro Mlanzi

WAWAKILISHI wa Tanzania Bara katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Simba inatarajia kutua nchini leo ikitokea Komoro huku wakijuta kuwadharau
wapinzani wao, Elan de Mitsoudje ya nchini humo.

Timu hizo zilikutana juzi kwenye mchezo wa awali wa michuano hiyo, ambapo zilitoka suluhu matokeo ambayo Simba hawakuyatarajia.

Akizungumza kwa simu jana kutoka Komoro Meneja wa timu hiyo, Innocent Njovu alisema wachezaji wake walicheza chini ya kiwango kutokana na kuonekana kuidharau timu hiyo, lakini walikuja kushtuka muda ulikuwa umekwenda.

"Inaonekana timu za Komoro zimebadilika sasa, hatukutarajia kama ingetoa upinzani ule na hilo nadhani wachezaji wetu watakuwa wamepata somo, ila nina uhakika kama wangejituma kama kawaida uwezo wa kushinda ulikuwepo," alisema Njovu.

Alisema walitarajia kurudi jana, lakini kwa ratiba za ndege hakukuwa na usafiri wa kurudi nchini, lakini kwa leo ipo hivyo hawana budi kurudi.

Njovu alisema mara baada kurudi wataendelea na programu yao ya mazoezi kama kawaida kwa ajili ya kujiandaa na michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba inatarajia kushuka uwanjani Februari 5, mwaka huu kuumana na Polisi Tanzania katika mfululizo wa michezo ya ligi hiyo.
 
Wanariadha kibao kushiriki Kili Martahon


Na Mwandishi Wetu

WANARIADHA nguli wa mbio za marathon kutoka nchi mbalimbali duniani, wako katika hatua za mwisho za maandalizi kabla ya kwenda Moshi kushiriki
awamu ya tisa ya mbio za Kilimanjaro Marathon, zitakazofanyika Februari 27, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Francis John alisema wanariadha mashuhuri kama vile Patrick Nyangero, Andrea Silvini, Daudi Joseph, Sarah Majah, Sarah Kavina na Banuelia Brighton wataungana na wanariadha na wengine kutoka mataifa mbalimbali.

Nyangero alikuwa mshindi wa pili kwenye mbio hizo mwaka 2009, baada ya kumaliza mbio katika muda wa 02:15:35 huku, Silvini alikuwa mshindi wa tatu mwaka 2008 baada ya kumaliza katika muda wa 02:16:22. Banuelia alishinda mbio hizo kwa upande wa wanawake akimaliza katika muda wa 02:48:37.

Wanariadha wengine waliothibitisha kushiriki ni pamoja na Martin Sulle, Peter Sulle, Samwel Shauri na Mary Naali ambaye hivi karibuni alishinda mbio ya Vienna Marathon nchini Austria.

John Addison, Mkurugenzi Mkuu wa Wild Frontiers, ambao ndiyo waandaaji wa mbio hizo alisema nchi zaidi ya 35 zinatarajiwa kushiriki huku washiriki kutoka nje ya nchi wakitarajia kuwa zaidi ya 600 ukilinganisha na 500 wa mwaka jana.

Washiriki wa kigeni wanatarajiwa kutoka nchi za Afrika Kusini, Uingereza, Zimbabwe, Kenya, New Zealand, China, Canada, Marekani, Australia, Ufaransa na Italia. Kwa ujumla, zaidi ya wanariadha 5,000 wanatarajiwa kushiriki mbio hizo.

Naye Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Kili Marathon George Kaviseha alisema mashindano hayo yameendelea kuwa kivutio na ni mashindano makubwa ya kimataifa ikiwa na zaidi ya chi 35 yanayoshiriki.

"Mbio hizi huvutia wanariadha mashuhuri wa kimataifa na kuwapa fursa wanariadha wa Tanzania kujipima na kupata uzoefu katika mbio ndefu," alisema Kavishe.

Wadhamini wengine washirikishi katika mbio hizo ni Vodacom ambao wanadhamini mbio za kujifurahisha za kilometa, CFAO DT Dobie, KK Security, TanzaniteOne, TPC Sugar, Precisionair, Kilimanjaro Water, Bodi ya Utalii Tanzania na Tanga Cement.
 
Barcelona yazidi kuchanja mbuga


ALICANTE, Hispania

TIMU ya Barcelona, imeshinda mechi yake ya 15 ya ligi hivyo kufikisha historia ya miaka 50 katika ligi ya Hispania iliyowahi kuwekwa na Real Madrid.Barcelona
iliweka rekodi hiyo usiku wa kuamkia jana, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Hercules huku nyota wake, Lionel Messi akipachika mabao mawili ndani ya dakika tatu.

Mchezaji huyo bora wa FIFA, mara mbili alipachika mabao hayo dakika ya 87 na 89 na kuongeza idadi yake ya mabao msimu huu na kufikia 37 yakiwemo 21 aliyofunga kwenye ligi huku, Pedro Rodriguez akiongeza bao jingine moja.

Kwa ushindi huo Barcelona itakuwa imeongeza pengo la pointi saba, mbele ya timu inayoshika nafasi ya pili, Real Madrid, ambayo usiku wa kuamkia leo ilikuwa ikiumana na Osasuna.

Real Madrid wamewahi kushinda mechi 15 mfululizo katika msimu wa 1960-61 na huenda, Barcelona ikaweka rekodi nyingine itakapokuwa ikiikaribisha Atletico Madrid Februari 6 mwaka huu.




1 Maoni:


Anonymous said... Hongera zao wako juu, maana na jana Real Madrid
wamefungwa 1 bila na hao Osasuma kwa hiyo gape 7 points clear

January 30, 2011 10:36 PM
 
Defensive boost for United


RivalsDM



PRINT
RSS




Updated Jan 30, 2011 11:47 AM ET
Manchester United manager Sir Alex Ferguson is expecting Rio Ferdinand and Nemanja Vidic to face Aston Villa on Tuesday night.
Both men have been carrying knocks of late and have been given time to rest their respective ailments.

TRANSFER SPECIAL

Keep up with all the biggest moves around the globe with our 2011 January transfer gallery.

Ferguson opted to shuffle his entire defensive pack in the FA Cup on Saturday, with a new-look back five fielded in the win at Southampton.
He is, however, expected to revert back to his tried and tested performers in midweek, with Vidic and Ferdinand set to take up their regular roles.
Rafael and Patrice Evra should also be returned to the side, with Edwin van der Sar reclaiming the number one jersey from Anders Lindegaard.
"Vidic should be alright," Ferguson told United's official website.
"Rio started running on Thursday and hopefully will be okay by Tuesday.
"Rafa should also be okay, he got the all-clear on Friday [after suffering concussion at Blackpool] and Patrice Evra had a family bereavement so we left him out at Southampton.
"We should have our back four back against Villa."
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…