Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Siri ya Bitchuka kutoka Mlimani Park kwenda Safari Sound

Juma Kasesa

AHALAN wasahlan mpenzi msomaji wa Jamvi la Kulonga ikiwa ni Ijumaa nyingine tunapokutana Jamvini katika kujadili na kuchambua hili na lile yaliyojiri na yanayotarajiwa kutokea katika tasnia ya sanaa na burudani.
Katika Jamvi letu la leo ningependa kumzungumzia nguli mwingine wa muziki wa dansi ambaye ni mtunzi na mwimbaji wa bendi ya Mlimani Park Orchestra zamani ikijulikana DDC Mlimani Park Sikinde ‘Ngoma ya Ukae' naye si mwingine ni Hassan Rehani Bitchuka.
Kubwa ambalo Jamvi hili limepanga kukudadavulia kuhusu Bitchuka ni sababu ipi ilimfanya yeye na kundi la wanamuziki wenzake kuchukua uamuzi wa kuitosa DDC Mlimani Sikinde Ngoma ya Ukae na kwenda kuiasisi bendi ya Orchestra Safari Sound ‘Wanandekule'.
Huyu ni mwanamuziki ambaye alizaliwa katika Kijiji Kagunga kilichopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma na kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya muziki wa dansi Tanzania hakujatokea mwanamuziki aliyevunja rekodi yake ya kuimba sauti kali licha ya uwepo wa kina wa hayati Suleimani Mbwembwe, Nico Zengekala na wengineo.
Mchango wake ni mkubwa katika medani ya muziki wa dansi kutokana na kutunga nyimbo nyingi zenye kuelimisha na kuburudisha jamii, akiwa ameng'ara katika kila bendi ambayo amewahi kupitia.
Jamvi la Kulonga linapenda kukufahamisha kuwa nguli huyu wa muziki wa dansi alisoma katika Shule ya Msingi Kipampa Ujiji, mkoani Kigoma na kuishia darasa la sita kutokana na kujikita zaidi katika uhuni wa utotoni.
Uwezo wa sauti yake kali ya kuimba na yenye kuleta hisia kwa msikilizaji ni kipaji alichojaaliwa na Mungu kikiongezewa na mafunzo ya madrasa ambako alikuwa msomaji mzuri wa Kurani na kughani kaswida hali ambayo ndiyo chachu ya mafanikio ya kuwa na sauti kali hadi leo.
Bitchuka ambaye katika familia yao yeye ndiye mwanamuziki pekee alianza shughuli za muziki mwaka 1972 katika bendi ya Nationality iliyokuwa ikifanya maonyesho yake mkoani Arusha kabla ya bendi ya Jumuiya ya Wazazi Tanzanaia JUWATA Jazz kuja jijini humo na kumuona akiwa na bendi na kuvutiwa naye.
Jamvi hili linakujuza kuwa nguli huyu alijiunga na Juwata mwaka 1973 baada ya kufanyiwa majaribio ‘Ikiwa kama Hunitaki' na kuimba sauti kali iliyowasisimua wakongwe aliowakuta katika bendi hiyo Joseph Lusungu, Abel Baltazar, Kiza Husein, Ahmed Omary, Mabruk Khalfan, Saidi Mabera, Juma Kitambi na Muhidin Maalim Gurumo.
Baada ya kufuzu majaribio ya kuimba nyimbo yake ya kwanza kutunga ilikuwa ni ‘Msondo wa NUTA' ambako pia aliweza kutunga na kuimba nyimbo kadhaa ambazo ni ‘Mpenzi Zarina' ambalo ni jina la mkewe, ‘Dada Rehema', ‘Dada Asha' akishirikiana na wakongwe hao.
Kutokana na maudhi aliyokuwa akiyapata kutoka ndani ya bendi hiyo mwaka 1980 aliamua kujitoa na kwenda kuiasisi DDC Mlimani Park ambako alishirikiana na Abel Baltazar, Joseph Mulenga, Michael Enock ‘King Michael' na wengineo ambako wimbo wake wa kwanza kutunga ulikuwa ni ‘Duniani Kuna Mambo', ‘Wafanyakazi' na ‘Mume wangu Jerry'.
Jamvi la Kulonga linakujuza kuwa nyimbo hizo zilimng'arisha Bitchuka na kupata mafanikio katika medani ya muziki huo ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambako hadi leo nyimbo zake zinaendelea kupigwa kabla ya kutunga wimbo ‘Nawashukuru Wazazi Wangu' ambao ulimuongezea umaarufu zaidi.
Baada ya kukudadavulia kwa kifupi historia fupi ya nguli huyo turudi katika hoja ya Jamvi letu la leo ambayo nataka kukudadavulia kwanini Bitchuka licha kupata mafanikio akiwa na bendi hiyo aliamua kujitoa 1990 akiwa na wenzake na kwenda kuasisi Orchestra Safari Sound.
Aliamua kujitoa Mlimani Park akiwa na Abel Baltazar, Muhidin Maalim Gurumo, Charles Ngosha, Kassim Rashid ‘Kizunga', ‘Ally Makunguru' baada ya kiongozi mmoja wa bendi hiyo aliyekuwa akisimamia suala la nidhamu marehemu Mpoto kuwatusi kuwa kama wameshindwa kuimba na kutunga atawafukuza kazi, kauli ambayo iliwaudhi wanamuziki hao wakiongozwa na Bitchuka.
Jamvi la Kulonga linakujuza wakati huo Bitchuka alikuwa akilipwa mshahara wa shilingi 90,000 lakini kibaya zaidi Mpoto alitishia kushusha mishahara yao kwakile ilichoelezwa ni kubana matumizi ya bendi, hali ambayo ilimfanya yeye na wenzake kufanya uamuzi wa kwenda kuasisi Safari Sound na wimbo wake wa kwanza kutunga ulikuwa ni ‘Chatu Mkali' akafuatia na ‘Shukrani kwa Mjomba', ‘Pole Kaka Mudi' na ‘Wajifanya Wajua'.
Nyimbo hizo zilimpandisha chati zaidi kiasi cha DDC Mlimani Park kuamua kumshawishi kurejea kundini mwaka 1992 ambako alirejea na kutunga na kuimba nyingi zenye mafunzo na kuburudisha kwa jamii kabla ya viongozi wa JUWATA kumchukua tena mwaka 1994 hadi mwaka 2003 alipoamua kurudi Mlimani Park ambako yupo hadi sasa akiwa na kina Shabani Dede, Abdalah Hemba, Joseph Bernad na wengineo.
Huyu ndiye Hassan Bitchuka ambaye ni shabiki wa kutupwa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Wekundu wa Msimbazi (Simba) ambaye Jamvi la Kulonga lilitaka kukujuza nini hasa kilimfanya kujitoa Sikinde na wenzake na kwenda kuiasisi Orchestra Safari Sound.
Kwa leo nalikunja Jamvi hadi Ijumaa ijayo nikikutakia wikendi njema tukutane Jamvini kama ilivyo ada yetu.
 
Siri ya Bitchuka kutoka Mlimani Park kwenda Safari Sound

Juma Kasesa

AHALAN wasahlan mpenzi msomaji wa Jamvi la Kulonga ikiwa ni Ijumaa nyingine tunapokutana Jamvini katika kujadili na kuchambua hili na lile yaliyojiri na yanayotarajiwa kutokea katika tasnia ya sanaa na burudani.
Katika Jamvi letu la leo ningependa kumzungumzia nguli mwingine wa muziki wa dansi ambaye ni mtunzi na mwimbaji wa bendi ya Mlimani Park Orchestra zamani ikijulikana DDC Mlimani Park Sikinde ‘Ngoma ya Ukae’ naye si mwingine ni Hassan Rehani Bitchuka.
Kubwa ambalo Jamvi hili limepanga kukudadavulia kuhusu Bitchuka ni sababu ipi ilimfanya yeye na kundi la wanamuziki wenzake kuchukua uamuzi wa kuitosa DDC Mlimani Sikinde Ngoma ya Ukae na kwenda kuiasisi bendi ya Orchestra Safari Sound ‘Wanandekule’.
Huyu ni mwanamuziki ambaye alizaliwa katika Kijiji Kagunga kilichopo pembezoni mwa Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma na kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya muziki wa dansi Tanzania hakujatokea mwanamuziki aliyevunja rekodi yake ya kuimba sauti kali licha ya uwepo wa kina wa hayati Suleimani Mbwembwe, Nico Zengekala na wengineo.
Mchango wake ni mkubwa katika medani ya muziki wa dansi kutokana na kutunga nyimbo nyingi zenye kuelimisha na kuburudisha jamii, akiwa ameng’ara katika kila bendi ambayo amewahi kupitia.
Jamvi la Kulonga linapenda kukufahamisha kuwa nguli huyu wa muziki wa dansi alisoma katika Shule ya Msingi Kipampa Ujiji, mkoani Kigoma na kuishia darasa la sita kutokana na kujikita zaidi katika uhuni wa utotoni.
Uwezo wa sauti yake kali ya kuimba na yenye kuleta hisia kwa msikilizaji ni kipaji alichojaaliwa na Mungu kikiongezewa na mafunzo ya madrasa ambako alikuwa msomaji mzuri wa Kurani na kughani kaswida hali ambayo ndiyo chachu ya mafanikio ya kuwa na sauti kali hadi leo.
Bitchuka ambaye katika familia yao yeye ndiye mwanamuziki pekee alianza shughuli za muziki mwaka 1972 katika bendi ya Nationality iliyokuwa ikifanya maonyesho yake mkoani Arusha kabla ya bendi ya Jumuiya ya Wazazi Tanzanaia JUWATA Jazz kuja jijini humo na kumuona akiwa na bendi na kuvutiwa naye.
Jamvi hili linakujuza kuwa nguli huyu alijiunga na Juwata mwaka 1973 baada ya kufanyiwa majaribio ‘Ikiwa kama Hunitaki’ na kuimba sauti kali iliyowasisimua wakongwe aliowakuta katika bendi hiyo Joseph Lusungu, Abel Baltazar, Kiza Husein, Ahmed Omary, Mabruk Khalfan, Saidi Mabera, Juma Kitambi na Muhidin Maalim Gurumo.
Baada ya kufuzu majaribio ya kuimba nyimbo yake ya kwanza kutunga ilikuwa ni ‘Msondo wa NUTA’ ambako pia aliweza kutunga na kuimba nyimbo kadhaa ambazo ni ‘Mpenzi Zarina’ ambalo ni jina la mkewe, ‘Dada Rehema’, ‘Dada Asha’ akishirikiana na wakongwe hao.
Kutokana na maudhi aliyokuwa akiyapata kutoka ndani ya bendi hiyo mwaka 1980 aliamua kujitoa na kwenda kuiasisi DDC Mlimani Park ambako alishirikiana na Abel Baltazar, Joseph Mulenga, Michael Enock ‘King Michael’ na wengineo ambako wimbo wake wa kwanza kutunga ulikuwa ni ‘Duniani Kuna Mambo’, ‘Wafanyakazi’ na ‘Mume wangu Jerry’.
Jamvi la Kulonga linakujuza kuwa nyimbo hizo zilimng’arisha Bitchuka na kupata mafanikio katika medani ya muziki huo ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambako hadi leo nyimbo zake zinaendelea kupigwa kabla ya kutunga wimbo ‘Nawashukuru Wazazi Wangu’ ambao ulimuongezea umaarufu zaidi.
Baada ya kukudadavulia kwa kifupi historia fupi ya nguli huyo turudi katika hoja ya Jamvi letu la leo ambayo nataka kukudadavulia kwanini Bitchuka licha kupata mafanikio akiwa na bendi hiyo aliamua kujitoa 1990 akiwa na wenzake na kwenda kuasisi Orchestra Safari Sound.
Aliamua kujitoa Mlimani Park akiwa na Abel Baltazar, Muhidin Maalim Gurumo, Charles Ngosha, Kassim Rashid ‘Kizunga’, ‘Ally Makunguru’ baada ya kiongozi mmoja wa bendi hiyo aliyekuwa akisimamia suala la nidhamu marehemu Mpoto kuwatusi kuwa kama wameshindwa kuimba na kutunga atawafukuza kazi, kauli ambayo iliwaudhi wanamuziki hao wakiongozwa na Bitchuka.
Jamvi la Kulonga linakujuza wakati huo Bitchuka alikuwa akilipwa mshahara wa shilingi 90,000 lakini kibaya zaidi Mpoto alitishia kushusha mishahara yao kwakile ilichoelezwa ni kubana matumizi ya bendi, hali ambayo ilimfanya yeye na wenzake kufanya uamuzi wa kwenda kuasisi Safari Sound na wimbo wake wa kwanza kutunga ulikuwa ni ‘Chatu Mkali’ akafuatia na ‘Shukrani kwa Mjomba’, ‘Pole Kaka Mudi’ na ‘Wajifanya Wajua’.
Nyimbo hizo zilimpandisha chati zaidi kiasi cha DDC Mlimani Park kuamua kumshawishi kurejea kundini mwaka 1992 ambako alirejea na kutunga na kuimba nyingi zenye mafunzo na kuburudisha kwa jamii kabla ya viongozi wa JUWATA kumchukua tena mwaka 1994 hadi mwaka 2003 alipoamua kurudi Mlimani Park ambako yupo hadi sasa akiwa na kina Shabani Dede, Abdalah Hemba, Joseph Bernad na wengineo.
Huyu ndiye Hassan Bitchuka ambaye ni shabiki wa kutupwa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Wekundu wa Msimbazi (Simba) ambaye Jamvi la Kulonga lilitaka kukujuza nini hasa kilimfanya kujitoa Sikinde na wenzake na kwenda kuiasisi Orchestra Safari Sound.
Kwa leo nalikunja Jamvi hadi Ijumaa ijayo nikikutakia wikendi njema tukutane Jamvini kama ilivyo ada yetu.
 
Simpi pole Mzee Yussuf ‘Mfalme'

Abdallah Menssah

NI kama natania vile katika hili, lakini acha niseme bayana kuwa niko ‘siriaz', potelea mbali hata kama nitasomeka isivyotarajiwa na kuduwaza wengi.
Leo nimeanza na spidi kidogo, ni kutokana na mwenyewe kujibaini wazi kuwa niko nyuma ya wakati yaani kwa lugha nyepesi inayoweza kueleweka zaidi, nimechelewa.
"Kuchelewa katika lipi?" Nafikiri ndilo swali ambalo hivi sasa unajiuliza kichwani mwako, basi nami bila hiyana, kinyongo wala choyo, nitakuwekea wazi.
Ni kwamba nimechelewa kutoa kauli hii kwa msanii huyu swahiba wa wengi na kipenzi cha umma, ambaye ni kati ya wasanii wenye mashabiki lukuki hapa nchini, Mzee Yussuf Mwinyi ‘Mfalme'.
Kiukweli, hapo awali nilipanga kuzitoa pole zangu za dhati kwa nguli huyu wa mipasho, mwenye vibao vinavyowakuna mashabiki wengi hadi wa ‘Umangani'.
Lakini, kwa sababu najua kuna watu wangechonga na kusema sana tu wakidai nampendelea na kumfagilia bure Mzee anayependa zaidi kujiita ‘Mzanzibar Halisi', acha niseme kuwa simpi pole.
Unajua, wengi wamesahau kuwa hata yeye Mzee pia anawapendelea na kuwafagilia mashabiki wake, ndiyo maana huonyesha kuwajali kwa kuwatungia vibao vinavyotufurahisha.
Bila shaka, hili la mashabiki wengi kusahau kuwa, mzee naye anatupendelea na kutufagilia ni kati ya sababu zinazotufanya wengi waone si lazima kumuenzi kwa kumpa pole.
Hebu ngoja nikwambie kitu, unajua nimebaini kuwa, tumekuwa tukiwapenda wasanii wetu wakiwa jukwaani tu na si wanapopatwa na matatizo.
Hii ndiyo maana hata katika misiba yao, mara kadhaa tumeshuhudia kukikosekana kwa misaada ya kutosheleza katika shughuli za mazishi licha ya umaarufu wao.
Mfano hai si ndo kama hivi, unafikiri kama leo anapougua hatuendi kumtazama, simuombei mabaya, kesho atakapokufa tutakwenda kweli kumzika?
Si wote tutaamua kuuchuna tu, tena basi ikizingatiwa kuwa wakati huo atakuwa amefumba macho na hajui nani kahudhuria maziko yake na nani kampotezea.
Manake, hebu twende mbele na kurudi nyuma, msanii kama Mzee ni wa kukosa kwenda kujuliwa hali hata na mbunge wake kweli, ambaye binafsi alishiriki kikamilifu kumpa ulaji!
Hivi sasa, Mzee yuko mapumzikoni nyumbani kwa wazazi wake, Michenzani, Zanzibar akijiuguza polepole baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti la kulia.
Lakini, kwa mujibu wa ndugu yake wa karibu, ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, idadi ya mashabiki waliopiga mguu kwenda kumpa pole inahesabika.
Inamaana mashabiki na wapenzi wake wote hapa nchini wako bize kiasi cha kushindwa kupanda boti na kufika Zanzibar kumjulia hali mara moja na kurudi?
Binafsi niko pamoja na wale wote waliojitokeza kumpa pole hata za ‘meseji' kwenye simu kutokana na labda kutingwa na majukumu ama kukambwa na tatizo la pesa.
Aidha, nami pia nitakuwa mmoja wa wale watakaohudhuria katika shoo zake kubwa mbili za kwanza kama alivyoahidi mheshimiwa mbunge wa Kinondoni, Idd Azan.
Si nasikia Mzee ataanza kuibuka kwenye onyesho la Jahazi Modern Taarabu la mkesha wa siku ya Wapendanao ‘Valentine's Day' Februari 13, pale Travertine Hotel, Magomeni Mikumi.
Kisha kesho yake, siku yenyewe ya Wapendanao kwenye ukumbi wa Buliyaga, Temeke jijini Dar es Salaam pia tutakuwa sote tukijirusha kwa kucheza ‘Alambaa!'.
Nafanya hivyo katika kuonyesha msisitizo wangu kuwa, nikiwa mdau niliye mstari wa mbele katika sanaa ya muziki nchini, nawajali wasanii kwa raha na shida.
Japokuwa bado nasisitiza kuwa simpi pole Mzee, lakini si kwa bifu kati yangu naye, ila ni kukwepa kelele za watu kuwa nampendelea na kumfagikia mno.
Kwa leo naomba niishie hapa na kuwaomba tukutane wiki ijayo panapo majaliwa, huku nikiwaacha wadau wangu kwa kaulimbiu isemayo ‘Bendera ya chuma haifuati upepo'.
Wadau wangu wa ukweli ni Hawa, Asiatu Damumbaya, Matilda Isaca wa Tukuyu, Geofrey Kabelege wa Kyela, Chikawe Juma wa Vigozi Charambe na Ben Mtwanga wa Mgeni Nani, Mbagala Kuu.
Wengine ni Dogo Baraka ‘Jembe', Asha Salum Msumi, Rehema Idd, Hassan na Hussein, Wastara Makumbato, Mariam Said, Mustapha Sopa ‘Inda' na Bilsan Hemed ‘Sharobaro'.
Bila kuwasahau muuza magazeti maarufu wa Mtoni Mtongani, Yahya Rajab ‘Westi', Said Makorokoto, Mohammed Mtwale wa Mkuranga Pwani, Ikota Mhamila, pamoja na Super D Mnyamwezi.
 
Miss Afrika Mzanzibari apewa changamoto


na Mauwa Mohammed, Zanzibar


MREMBO wa Afrika kutoka Zanzibar nchini Australia Zaituni Mohammed Hunt ametakiwa kuwa balozi mzuri katika kuvitangaza visiwa hivyo kiutalii kutokana na nafasi aliyonayo nchini.
Changomoto hiyo ilitolewa juzi mjini hapa na Mwenyekiti wa Jumuiya inayotoa huduma kwa watalii (ZATO), Omar Said, alipokuwa akizungumza na mrembo huyo katika Hoteli ya Grand Palace iliyoko Malindi.
Mwenyekiti huyo aliwataka Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi kutumia fursa walizonazo katika kuikuza na kuitangaza Zanzibar katika sekta ya utalii.
Hata hivyo, alishauri serikali kuitangaza Zanzibar katika matamasha mbalimbali yanayotokea nchini sambamba na kumtumia vizuri mrembo huyo, kuweza kuitangaza nchi kupitia nyanja ya urembo.
Kwa upande wake, mrembo huyo alisema, Zanzibar ni nchi yenye historia ya kipekee, kutokana na mila zilizopo pamoja na ustarabu wa watu wake.
Alifahamisha kuwa, ushindi alioupata utasaidia kuitangaza kimataifa hasa katika nyanja za utalii na utamaduni.
Aidha Hunt alisema, anatarajia kuanzisha kituo kitakachobuni mavazi yatakayoingia kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa, ambayo rasilimali zitakazotumika zitatoka visiwani Zanzibar.
Mrembo huyo wa Afrika nchini Australia ambaye ni mzaliwa wa Zanzibar, alisema ana nia ya kusaidia wanawake pamoja na watoto yatima.
Hunt mwenye miaka 20 ni Mzanzibari aliyefanikiwa kupata ushindi wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Desemba 20 mwaka jana, ambayo yalishirikisha warembo 450 wenye asili ya Afrila.
 
Tamasha la Mwalimu Nyerere Feb. 14


na Samia Mussa


TAMASHA la filamu la Mwalimu Nyerere linatarajiwa kuanza kurindima kuanzia Februari 14 hadi 19 kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, alisema ni mara ya kwanza kufanyika kwa tamasha hilo, ambalo litahusisha wageni kutoka Nollywood Nigeria, Afrika Kusini na Hollywood Marekani.
Alisema, siku hiyo ya ufunguzi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete atazindua rasmi TAFF sambamba na tamasha hilo, ambalo zaidi ya filamu 20 zilizofanya vizuri za ndani na nje zitaonyeshwa.
Aidha, Mwakifwamba alisema, mbali ya kuwepo kwa filamu hizo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali likiwamo kundi la The African Stars ‘Twanga Pepeta', FM Academia, Ambwene Yesaya ‘Ay', Diamond, Khalid Mohamed ‘TID', Mzee Yusuph, Lawrence Malima ‘Marlaw', Albert Mangwea, Farid Kubanda ‘Fid Q', Joh Makini na wengineo.
Aliongeza kuwa, katika siku za tamasha hilo kabla ya maonyesho ya siku husika, kutatunguliwa na mafunzo ya mada mbalimbali zinazohusiana na shughuli za filamu na maigizo kutoka kwa wakufunzi waliobobea.
Alisema, siku ya kufungwa kwa tamasha hilo, mgeni rasmi atatoa zawadi na tuzo kwa waasisi wa taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Rashid Kawawa ‘Simba wa Vita' kwa mchango wao katika maendeleo ya taifa na tasnia ya filamu nchini.
 
Azan kubariki uzinduzi wa ‘Shoga' leo


na Nasra Abdallah


MBUNGE wa Kinondoni, Idd Azan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu ya shoga, katika hafla itakayofanyika leo ukumbi wa Hoteli ya Travetine Magomeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Muandaaji na mtunzi wa filamu hiyo, Hissani Muya, alisema katika uzinduzi huo pia kutakuwepo na burudani kutoka kwa Mapacha Watatu, Kalala Junior, Khalid Chokoraa na Jose Mara.
Kwa mujibu wa Muya, mashabiki wategemee kuona mambo mazuri katika uzinduzi huo, ambako siku hiyo ndio filamu ya Shoga itaanza kuuzwa rasmi.
"Mie nachoomba mashabiki wajitokeze katika uzinduzi huu, ambao nauita ni wa aina yake, kwani mbali na burudani watakazoziona pia watakuwa wa kwanza kuiona filamu hiyo, isiyokuwa na upinzani hapa nchini," alisema.
Filamu ya Shoga, inaelezea kuhusu mwanamume mwenye tabia za kike, ambazo hazipendezi machoni mwa jamii.
Hata hivyo, msanii huyu alisema, amesukumwa kutunga filamu hiyo kutokana na ukweli kwamba filamu zimekuwa nyingi lakini jambo hilo halijawahi kuigizwa wakati ni mambo yanayotendeka kwenye jamii.
Aidha, aliwataka wananchi wasimchukulie kama ndiyo tabia yake, kwani yeye kama msanii anatakiwa kuweza kuigiza jambo lolote ili mradi tu afikishe ujumbe uliokusudiwa kwa jamii.
 
Twanga yajiimarisha zaidi


na Mwandishi wetu


BENDI ya muziki wa dansi ya The African Stars ‘Twanga International’, imetangaza kuongeza nyota wapya watatu ili kuzidi kuimarisha makali ya bendi hiyo inayotesa kwa sasa katika medani ya muziki wa dansi.
Wasanii hao wapya walioongezwa ndani ya Twanga ni rapa mahiri Jua Kali ambaye anatokea Tanzania One Theatre (TOT), Haji Ramadhani ambaye ni zao la Bongo Star Search (BSS), na Venas Joseph kutoka Bwagamoyo Sound kadhalika gwiji la unenguaji ambaye pia ni mkongwe katika bendi hiyo, Lilian Tungaraza, ambaye ametangazwa kuanza rasmi kazi baada ya likizo ndefu ya uzazi.
Kadhalika, mnenguaji mwingine aliyetajwa kwa jina moja la Sabrina ambaye alikuwa nchini Oman kikazi, naye amerudi kundini baada ya kumaliza kazi kwa mkataba maalumu.
Akizungumza katika onyesho lililofanyika mwishoni mwa wiki, kiongozi wa bendi hiyo Luiza Mbutu alisema, wasanii wote hao watarekodi katika albamu ya 11 ya bendi hiyo itakayozinduliwa baadaye mwaka huu.
Hivi sasa Twanga wanatamba na vibao vyao kama ‘Mapenzi Hayana Kiapo’ na ‘Kauli’ uliotungwa na Roggert Hegga.



 
Mashabiki kuamua Five Stars vs Manchester Musica


na Abdallah Menssah


MASHABIKI wa burudani wa Wilaya ya Temeke, leo wanatarajiwa kuwa majaji pale wakali wa mipasho, Five Stars Modern Taarab watakapopambana na wakali wa dansi, Manchester Musica kwenye ukumbi wa Manchester Pub, Mbagala Kilungule jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi, Kiongozi wa Manchester Musica, Adam Hassan na Kiongozi wa Five Stars, Ally Juma ‘Ally J', kila mmoja amejinasibu kuibuka kidedea katika pambano hilo.
"Kikosi changu kimejipanga vilivyo kwa kufanya mazoezi ya nguvu, ambapo ninaamini tutaibuka na ushindi katika pambano hilo," alisema Ally J ambaye ni Kiongozi wa Five Stars.
Naye, Kiongozi wa Manchester Musica, Adam Hassan, alitamba kukonga zaidi nyoyo za wapenzi, pamoja na mashabiki, hasa ikizingatiwa kuwa ukumbi huo wa Manchester Pub ni uwanja wao wa nyumbani.
 
Katibu Yanga adai ligwaride gumu


na Samia Mussa


KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga ya jijini Dar es Salaam, Mwesigwa John Selestine, amesema kuiongoza klabu hiyo ni kazi ngumu hivyo atajipanga ili kuhakikisha anatekeleza vema majukumu yake hayo mapya ikiwamo kuondokana na migogoro.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Selestine alisema kuwa, ili kujiepusha na kumaliza migogoro, yuko mbioni kujipanga ili kuhakikisha klabu hiyo inaondokana na matatizo hayo.
Alisema kuwa, ili kutimiza malengo waliojiwekea, atashirikiana na viongozi waliopo klabuni hapo kuhakikisha kila jambo linakwenda kama lilivyopangwa kwa maendeleo ya klabu hiyo.
Aidha, Mwesigwa alipoulizwa kuhusu uzoefu wake katika soka akiwa kama kiongozi, alisema hana mashaka juu ya mchezo huo kwani anaufahamu vizuri toka alipokuwa na umri mdogo na kwamba, hilo halitokuwa shida kwake katika kutoa ushirikiano kwa timu hiyo.
Mwesigwa alitangazwa juzi na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Wakili Lloyd Nchunga kukaimu nafasi hiyo baada ya Lawrence Mwalusako kutangaza kujiuzulu hivi karibuni, sambamba na aliyekuwa Meneja, Emmanuel Mpangala na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Juma Seif.




 
Olaba: Wana kazi ngumu kuitoa Dedebit


na Makuburi Ally


KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mkenya, Tom Olaba, ameipa somo Yanga kabla ya mchezo wake wa marudiano na Dedebit ya Ethiopia kati ya Februari 11 na 13 kuwa watambue wana kazi ngumu.
Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya mchezo kati yake na Yanga uliochezwa uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Olaba alisema, wanatakiwa wajue kwamba, wana kazi ngumu dhidi ya Dedebit ugenini licha kuwa na stamina ya kucheza, lakini tatizo linalowasumbua hawajui kuuchezea mpira, jambo ambalo litawagharimu.
Olaba alisema, Yanga sio timu mbaya ila inabidi wajiandae vilivyo kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Aidha Olaba alisema, Yanga wana kazi ngumu katika mchezo wa marudiano kwani wanatakiwa kushinda kutokana na Dedebit kuwa na bao moja la ugenini.
 
Simba yaipumulia Yanga


na Mwandishi wetu


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba jana waliiadhibu African Lyon kwa mabao 3-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, jana.
Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 30 ndani ya michezo 13 hivyo kuipumulia Yanga ambayo iko kileleni kwa pointi 31 na mchezo mmoja mbele.
Simba waliouanza mchezo huo kwa kasi ya aina yake, walifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya tano lililofungwa na Amri Kiemba kutokana na kona ya Haruna Shamte.
Kabla ya bao hilo, kipa wa African Lyon Noel Lucas aliumia katika harakati za kuokoa hatari langoni mwake, hali ambayo ilifanya mchezo huo kusimama kwa dakika 15.
Simba waliendelea kufanya mashambulizi langoni mwa Lyon, ambako dakika ya 18 Mussa Mgosi alipiga shuti karibu na lango la Lyon lakini mpira ulipaa.
Lyon ilijibu mapigo dakika ya 29, baada ya shuti la Mohamed Samata kupaa juu ya lango la Simba.
Katika dakika ya 39, Rashid Gumbo alipiga shuti kali langoni mwa Lyon, lakini kipa Lucas alipangua na kuwa kona.
Hadi mwamuzi wa mchezo huo, Oden Mbaga, anapuliza filimbi ya mapumziko, Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili, Simba walirejea uwanjani kwa nguvu na kufanikiwa kufunga bao la pili dakika ya 46 na mfungaji akiwa Mbwana Samata aliyeambaa na mpira kutoka katikati ya uwanja na kufumua shuti kali lililojaa wavuni.
Baada ya bao hilo, Simba waliendelea kulisakama lango la Lyon ambapo wapinzani wao kila walipojaribu kusaka namna ya kuliona lango la wana Msimbazi mabeki wa timu hiyo walikuwa makini.
Samata alifunga bao la tatu katika dakika ya 82 baada ya kazi nzuri ya Haruna Shamte.
Katika dakika ya 83, mshambuliaji wa Simba Ahmed Shiboli alipiga shuti kali karibu na lango la Lyon baada ya pasi safi ya Mohamed Banka, lakini likapaa juu ya lango.
Dakika ya 85, Mohamed Banka alikosa bao la wazi baada ya kazi nzuri ya Juma Jabu aliyeambaa na mpira kutoka upande wa kaskazini mwa uwanja wa Uhuru. Hivyo hadi mwisho wa mchezo Simba iliibuka kidedea kwa mabao 3-0.
Simba iliwakilishwa na Ally Mustafa, Haruna Shamte, Juma Jabu, Meshack Abel, Kelvin Abel, Jerry Santo, Rashid Gumbo/Aziz Gilla, Patrick Ochan, Mussa Mgosi/Ahmed Shiboli, Mbwana Samata na Amri Kiemba/Mohamed Banka.
African Lyon iliwakilishwa na Noel Lucas, Rajab Zahir/Stephano Nkomola, Hamis Shengo/Haji Dudu, Zubery Ubwa, Bakari Omar, Hamis Yusuf, Hamis Thabit/Samuel Ngassa, Mohamed Samata, Adam Kingwande, Idrissa Rashid na Sunday Bakari.

Mwisho
 
Ashraf, Tamim kurudiana Machi 3 Dar


na Samia Mussa


HATIMAYE Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), imekubaliana na maombi ya muda mrefu ya bondia Ashraf Suleiman kuomba pambano la marudiano la uzito wa juu raundi 10, kati yake na Awadh Tamim.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Aurora ambao ni waratibu wa pambano hilo, Shomari Kimbau, pambano hilo linatarajiwa kufanyika Machi 3 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Awali, Ashraf alimuomba Tamim kuachia mkanda huo ili uweze kuwaniwa na mabondia wengine, jambo ambalo lilikuwa gumu kwa Tamim anayeishi Sweden na kuridhia kurejea nchini kutetea mkanda wake huo.
Kimbau alisema kuwa, mshindi wa marejeano hayo ya pambano la awali lililochezwa Julai 18, 2009 na kuvurugika hivyo kukosa mshindi, atakuwa na nafasi kubwa ya kugombania ubingwa wa Afrika dhidi ya Joseph Chingangu wa Zambia.
Pambano la Machi 3 mwaka huu, linatarajiwa kusimamiwa na Katibu Mkuu wa TPBC, Shabani Ogora, huku mwamuzi akitokea nchini Kenya, aliyetajwa kwa jina la Wyclif Malende.
Alisema kuwa, kwa mara ya kwanza Tanzania, pambano hilo litahudhuriwa na watu maarufu katika fani mbalimbali hapa nchini wakiwemo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, Mkurugenzi wa Lino Agency, Hashimu Lundenga, Mkurugenzi wa Benchmark Production, Rita Poulsen, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa, (BMT), Kanali mstaafu, Idd Kipingu, waigizaji, Steven Kanumba, Vicent Kigosi ‘Ray' na wengineo wengi.
 
Soka Singida wampongeza Mo


na Jumbe Ismailly, Singida


CHAMA cha Soka Mkoa wa Singida (SIREFA), kimempongeza Mbunge wa Singida mjini, Mohamed Dewji ‘Mo' kwa kuchaguliwa tena kuwakilisha jimbo hilo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo. Kauli hiyo ilitolewa na mwakilishi wa klabu za Soka mkoani Singida,Omari Kinyeto alipokuwa akizungumza na Wandishi wa Habari mjini Singida hivi karibuni mjini hapa.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo, SIREFA wanatoa shukrani za dhati kwa Mohamed Dewji ‘Mo' kuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa kupata kura nyingi.
Hata hivyo Kinyeto ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alibainisha kwamba, SIREFA pia inamshukuru mbunge huyo kwa ahadi zake alizotoa wakati alipokuwa akijinadi kuomba kura.
Kiongozi huyo alibainisha pia kwamba, chama hicho kinamshukuru mbunge huyo kwa ahadi yake aliyotoa wakati akijinadi kuomba ubunge kwamba, atahakikisha uwanja wa michezo wa kumbukumbu ya Namfua anaukarabati, ikiwamo kuweka nyasi za bandia.
Hata hivyo, licha ya kumpongeza mbunge huyo, lakini Kinyeto hakusita kutoa angalizo kwamba, ahadi hizo zisiwe kwenye makaratasi na mdomoni tu, bali vitendo kinyume na ilivyokuwa kwa ahadi ya mwaka 2005.
 
Tamim, Ashraf kuzichapa tena Diamond
Thursday, 03 February 2011 22:06

Imani Makongoro

BAADA ya tambo za muda mrefu kati ya bondia bingwa wa Afrika Mashariki na Kati wa uzani wa juu, Awadh Tamim na mpinzani wake Ashraf Suleiman ubishi huo utafikia tamati Machi 3 watapopanda ulingoni kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Pambano hilo litakalokuwa la raundi 10 litasimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati chini ya Katibu Mkuu wake Shaban Ogola.

Ofisa Habari wa Kampuni ya Ulinzi ya Aurola ambao ndio waandaaji wa pambano hilo, Shomari Kimbau, alisema mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi.

"Kutokana na uzito wa pambano hili, tumewasiliana na Vyama vya Ngumi za Kulipwa vya Dunia kwa ajili ya kuliboresha.

"Pia, televisheni mbalimbali zitaonyesha pambano hili ikiwamo ile ya Super Sport na hii itakuwa ni moja ya njia ya kuitangaza Tanzania kimataifa katika mchezo huu wa ngumi sambamba na kuibua vipaji," alisema Kimbau.

Alisema kuwa ili kuondoa dhana iliyojengeka ya waamuzi kutoa upendeleo kwa mabondia, pambano hilo litachezeshwa na refa Wyclif Malende kutoka Kenya na baadhi ya waamuzi kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati.

"Maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yanaendelea vizuri, wakati wowote kuanzia sasa Tamim atawasili nchini pamoja na kocha wake wakitokea Sweden anakoishi.

"Ashraf anaendelea kujifua Visiwani Zanzibar tayari kwa pambano hilo kubwa la kimataifa," alisema.

Mabondia hao waliwahi kupigana mwaka 2009, ingawa bingwa hakupatikana baada ya pambano lao lililokuwa la raundi 10 kuvunjika raundi ya 7 kufuatia mashabiki kufanya vurugu.
 
Polisi TMK wajitosa kwenye michezo Thursday, 03 February 2011 22:05

Elizabeth Suleyman

JESHI la polisi Kanda ya Mkoa wa Polisi Temeke, linajiandaa na mchakato wa kuanzisha michezo itakayowashirikisha vijana mbalimbali wanaokaa mitaani bila ya kuwa na kazi.

Kamanda wa Mkoa wa polisi Temeke, David Msiime aliliambia Mwananchi ofisini kwake jana kuwa, lengo la kuanzisha michezo hiyo, ni kuwaweka karibu na jeshi la polisi vijana mbalimbali wanaokaa mitaani bila ya kuwa na kazi, ili waweze kuwa tayari kutoa taarifa za uhalifu.

Msiime aliongeza pia kuwa hiyo ni njia ya kuwaondolea hali ya kukaa bure mtaani na kwenye vijiwe vinavyosababisha kujiingiza kwenye vitendo viovu kama wizi na uvutaji wa bangi.

"Nafikiri mchakato huu, utasaidia vijana hawa kujitambua na kuondokana na tabia za kukaa bure vijiweni bila ya kufanya kazi,"alisema Msiime.

"Kwa sababu kupitia michezo hii, itawasaidia kukuza vipaji vyao tofauti na kukaa bure na hatimaye kuja kuwa wachezaji wakutegemewa na Taifa," alisema.

Hata hivyo, Kamanda alifafanua mchakato huo utawashirikisha wadau mbalimbali wa michezo, kikiwemo Chama cha soka cha Wilaya ya Temeke(TEFA), ili kuongeza nguvu na kutoa mchango wao.

"Pekee Yetu, hatuwezi kwani ni lazima tuwashirikishe wadau wa soka ili waweze kutusaidia angalau vifaa vya michezo,"alisema.

Pia Kamanda huyo aliongeza, michezo hiyo itawahusisha vijana wa aina zote, lengo ni kuwaweka pamoja na jeshi la polisi pamoja na kuwaondolea hali ya kukaa bure bila kujishughulisha.
 
Katibu mpya Yanga FC alonga


Na Mwali Ibrahim

KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine amesema baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo, atahakikisha haipi nafasi migogoro inayoendelea na
badala yake ni kuangalia njia za kuindesha kisasa klabu hiyo kongwe nchini.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Selestine alisema matatizo yaliyopo Yanga si makubwa na tayari yameshapatiwa ufumbuzi na sasa kilichobaki ni yeye kufanya mambo ya utendaji.

"Uongozi uliopo kwa sasa madarakani umenihakikishia kwamba kuna hali nzuri ya kiutendaji, hivyo nitahakikisha kutumia nafasi hiyo vizuri kwa manufaa ya chama.

Alisema matatizo hayo si makubwa kiasi cha kuifanya klabu ishindwe kuendelea na taratibu nyingine za maendeleo na viongozi wamemhakikishia kwamba ufumbuzi utapatikana hivi karibuni.

Katibu huyo alisema, klabu hiyo ni kubwa na ina wapenzi wengi na pia ina mafanikio makubwa na hiyo ni moja ya changamoto atakazokabiliana nazo katika kipindi hiki.
 
RT yatangaza nchi zitakazoshiriki michuano


Na Amina Athumani

CHAMA Cha Riadha Tanzania (RT), kimetangaza nchi 10 zitakazoshiriki mashindano ya riadha ya Afrika Mashariki na Kati, yatakayofanyika Dar es Salaam
Juni 3 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nchi hizo ni Misri, Jubouti, Elitrea, Somalia, Ethiopia, Sudani, Kenya, Uganda, Zanzibar na Tanzania Bara.

AKizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alisema kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la riadha Afrika Mashariki na Kati amepewa jukumu la kuhakikisha mialiko yote inafika kwa mashirikisho ya riadha ya nchi hizo na kuhakikisha zinathibitisha ushiriki wao.

"Kikao cha Kamati ya Utendaji kimeandika barua za mialiko kwa nchi 10, ambazo ndizo zitakazoshiriki mashindano haya, ambayo yanafanyika Tanzania kwa miaka miwili mfululizo hivyo tayari RT, tumeshakutana na tunaanza maandalizi mapema," alisema Nyambui.

Alisema RT imepewa kibali cha kuandaa mashindano hayo kwa miaka miwili mfululizo, baada ya kuandaa mashindano kama hayo yaliyofanyika mwaka jana na kwamba Shirikisho la Riadha Afrika Mashariki na Kati, limeridhishwa na ubora wa Uwanja wa Taifa hivyo kuwataka RT kuwa tena wenyeji wa michuano hiyo.

Nyambui alisema mashindano hayo yatashirikisha wanariadha wakubwa na wakongwe tofauti na ya mwaka jana ambayo yalishirikisha vijana chini ya miaka 17 na Zanzibar, ikaibuka washindi wa jumla wa michuano hiyo.
 
Real Madrid, Barcelona kukutana fainali


MADRID, Hispania

TIMU ya soka ya Real Madrid itakutana na wapinzani wao wakubwa Barcelona katika mechi ya fainali ya Kombe la Mfalme Aprili mwaka huu.Miamba
hiyo ya Hispania inakutana, baada ya Real Madrid inayonolewa na kocha, Jose Mourinho kuwafunga mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Sevilla mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Ushindi huo unaifanya Real Madrid kutinga hatua hiyo ya fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.

Katika mechi hiyo ambayo ilifanyika usiku wa kuamkia jana, mshambuliaji mpya wa timu hiyo raia wa Togo, Emmanuel Adebayor ndiye aliyeifungia Real Madrid bao la kwanza na likiwa ni la kwanza kwake tangu ajiunge na timu hiyo katika muda wa nyongeza, huku bao hilo likiwa ni la pili baada ya Mesut Ozil, kuipatia bao dakika ya 81 na kuifanya timu hiyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-0.

Kocha huyo Mreno kwa sasa anakuwa na nafasi ya kutwaa taji lake la kwanza, akiwa na klabu hiyo na ambalo litakuwa ni Kombe la kwanza la Mfalme kunyakuliwa na timu hiyo, tangu mwaka 1993.

Matokeo hayo yanavifanya vigogo hivyo vya soka nchini Hispania, kukutana katika hatua hiyo ya fainali huku kocha Mourinho, akiwa na matumaini ya kufanya vizuri tofauti na ilivyokuwa kwenye mechi ya ligi ambapo timu yake ilifungwa mabao 5-0 na Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Kwa upande wake Barcelona, wao wamefanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuilaza Almeria mabao 3-0, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 8-0.

Miamba hiyo ya soka inatarajia kukutana Aprili 20 mwaka huu zikiwa ni siku nne baada ya kukutana kwenye michuano ya ligi.

 
Liverpool yaichapa Stoke Thursday, 03 February 2011 22:03

LIVERPOOL, England
TIMU ya Liverpool imeshinda mechi yake ya tatu mfululizo baada ya kuichapa Stoke 2-0 huku mchezaji wao mpya raia wa Uruguay, Luis Suarez akifunga bao katika mechi yake ya kwanza kwenye Uwanja .

Alikuwa ni Raul Meireles wa Liverpool aliyekuwa wa kwanza kuifungia timu yake bao katika dakika ya 47 baada ya kupata mpira uliokuwa ukizagaa katika lango la Stoke na kupiga shuti ambalo lilimshinda kipa wa Stoke, Asmir Begovic.

Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Luis Suarez aliingia katika kipindi cha pili katika dakika ya 63 akichukua nafasi ya Aurelio, ambapo dakika 16 baadaye alipiga shuti kali la mguu wa kushoto ambalo lilikwenda moja kwa moja nyavuni ingawa beki wa Stoke, Andy Wilkinson alijitahidi kuzuia mpira huo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Liverpool chini ya kocha wake mpya Kenny Daglish kushinda mechi tatu mfululizo katika msimu huu baada ya Liverpool kuzifunga Wolverhampton Wanderers,Fulham na hivi sasa Stoke.

"Suarez amefunga bao katika mechi yake ya kwanza kuichezea Liverpool, hilo ni jambo zuri kwake na pia kwa mashabiki, nafahamu atafanya vizuri, tutajitahidi kufanya vizuri katika kila mechi, hivyo tunajitahidi kutengeneza nafasi na kuzitumia,"alisema Dalglish.

Baada ya Suarez kufunga bao mashabiki wa Liverpool waliripuka kwa furaha kwa sababu pia Liverpool ilikuwa imetawala mchezo huo.

Kikosi cha Stoke kinachofundishwa na kocha Tony Pulis kilionekana kilikuwa kikitafuta sare katika mechi hiyo kwa sababu ni mara chache kilionekana kikitaka kuleta madhara katika lango la Liverpool huku wakimtumia zaidi mshambuliaji wao John Carew.

Katika kipindi cha kwanza Liverpool itabidi wenyewe wajilaumu kwa kushindwa kupata bao la kuongoza mapema, kwa sababu katika kipindi hicho Stoke hawakutoa ushindani mkubwa.

Hata Liverpool walipata bao la kuongoza baada ya Steven Gerrard kupiga faulo ambayo ilimkuta Meireles na kufunga akiwa umabli wa mita nane kutoka katika lango la Stoke.

"Nilimuona wakati akiichezea Ajax pia nilimuona wakati wa Fainali za Kombe la Dunia, vijana wangu walijitahidi kucheza sana katika mechi hii, lakini Liverpool ni timu nzuri na ina wachezaji wazuri, lazima tuelewe klabu ya Liverpool imetumia pauni milioni 70 kwa ajili ya kununua wachezaji wawili,"alisema kocha wa Stoke, Pulis.

"Tulifanya vizuri katika kipindi cha kwanza na kipa wangu Asmir aliokoa mipira mingi ya hatari, pia tuliweza kudhibiti vizuri Liverpool, hata walipotufunga bao la pili bado tulikuwa mchezoni, lakini Liverpool waliweza kutumia nafasi walizopata kupata ushindi,"alisema Pulis.
 
Ronaldinho aanza kazi Brazil
Thursday, 03 February 2011 22:01

RIO DE JANEIRO,

ZAIDI ya mashabiki 40,000 walijazana katika Uwanja wa Enganhao kwa ajili ya kumshuhudia mchezaji nyota Ronaldinho wakiwa na picha zilizoandikwa karibu R10.

Akiichezea mechi yake ya kwanza timu ya Brazili baada ya miaka 10, Ronaldinho aliweza kuiongoza timu yake mpya ya Flamengo akiwa kama nahodha katika mechi dhidi ya Nova Iguacu katika mechi ya kuwania ubingwa wa Mji wa Rio de Janeiro na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ronaldinho ambaye mara mbili ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa duniaaliweza kuonyesha makali yake katika mechi hiyo ambapo upo wakati alipiga faulo ambayo ilipanguliwa na kipa wa timu pinzania Diogo Silva.

Katika mechi hiyo timu ya Nova Iguacu ilitoa upinzani mkali dhidi ya Flamemengo, lakini ilijikuta ikifanya makosa na kufungwa bao na mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Wanderley zikiwa zimebaki dakika nne kabla ya mpira kumalizika.

"Sijacheza soka kwa muda mrefu sasa, nahitaji kurudi mchezoni taratibu na pi aili niweze kuzoean na wachezaji wenzangu katika timu, sina cha kusema ila nawapongeza wachezaji wenzangu ambao wamenipokea kwa mikono miwili pia nawapongeza na mashabiki wetu,"alisema Ronaldinho.

Alisema,"Hii ni siku ya furaha katika maisha yangu."

Ronaldinho ni mchezaji wa zamani wa klabu za Barcelona na AC Milan, ambapo alisaini kuichezea Flamengo mwezi uliopita akiwa na lengo la kutaka kurudisha kiwango chake cha kutandaza soka na kumvutia kocha wa timu ya Taifa ya Brazil, Mano Menezes ili aweze kumuita katika kikosi cha Brazil kitakachoshiriki Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil 2014.

Ronaldinho ambaye kipaji chake cha kusakata kabumbu kilianzia huko kusini mwa Brazil akiwa anachezea klabu ya Gremio kabla hajaenda kuichezea klabu ya Ulaya ya Paris St Germain, alishinda na timu ya Taifa ya Brazili ubingwa wa dunia mwaka 2002, pia alicheza fainali za kombe la dunia mwaka 2006, lakini alichwa katika kikosi kilichoshiriki fainali za kombe la dunia nchini Afrika Kusini 2010.

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…