Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #4,801
Kocha Yanga aisifu mipango ya Simba Afrika Wednesday, 02 February 2011 20:38
Jessca Nangawe
KOCHA wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula amesema Simba ina nafasi kubwa ya kuvuka raundi ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na morali na juhudi walizoonyesha katika mchezo wao wa awali huku akidai Yanga inahitaji kuongeza juhudi na kushikamana zaidi kutokana na kutawaliwa na migogoro ndani ya klabu hiyo.
Simba na Yanga zote zinakabiliwa na michezo ya marudiano baada ya wote kutoka sare katika mechi zao za awali. Simba itakuwa nyumbani ikimenyana na Wacomoro wa Elan wakati Yanga wataifuata Dedebit ya Ethiopia mjini Addis Ababa wiki ijayo.
Mwaisabula alisema timu hizo zinakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha zinaiwakilisha vema Tanzania na kuvuka hatua ya pili hivyo zina kazi kubwa mbele yao katika kufanikisha hilo.
Kwa upande wake, alisema tofauti na Yanga, lakini Simba imeonekana kuwa na morali kubwa na kujituma zaidi hivyo kupewa nafasi ya kufika mbali ikilinganishwa na Yanga ambao walicheza chini ya kiwango na kusumbuliwa na migogoro inayoendelea kuikumba klabu hiyo.
Naye Kanakamfumo alisema kwa kiasi kikubwa, migogoro imesababisa kucheza chini ya kiwango tokea mchezo wa awali na endepo hawatajipanga na kucheza kwa ushindani ni wazi watayaaga mapema mashindano hayo.
Alisema kocha Msaidizi wa timu hiyo anatakiwa kuendelea na mfumo aliouacha Kosta Papic na kinyume na hapo atawachanganya wachezaji na kujikuta wakipoteza mchezo wa marudiano.
"Sisemi hivi ili kuwavunja moyo Yanga bali natoa kama hadhari kwao kuweza kujipanga mapema na kutambua makosa yao.
Yanga wanakabiliwa na migogoro inayoendelea ndani ya klabu hiyo na kwa kiasi kikubwa inaadhiri hata matokeo kuwa mabaya kwa timu hivyo ni vyema wakaangalia na ukubwa wa mashindano haya ili kutambua nini wanapaswa kufanya kwa sasa:alisema Kanakamfumo.