Michezo magazetini leo...
- Status
-
Not open for further replies.
Bashe kuipiga tafu Nkomanile sanaa
na Datus Boniface
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe, amejitosa kusaidia kundi la Sanaa za maonyesho la Nkomanile la jijini Dar es Salaam.
Bashe aliitoa ahadi ya kuisaidia Nkomanile jijini Dar es Salaam jana, katika semina ya kundi hilo juu ya namna ya kujiendesha katika sekta hiyo ya Sanaa.
Baadhi ya ahadi alizozitoa Bashe kwa kundi hilo ni pamoja na kuwapatia vitendea kazi kama vile Ngoma, Marimba na Mavazi ili litoe burudani ipasavyo sehemu mbalimbali.
"Nimesikia kilio chenu cha muda mrefu, hivyo nitamtuma mlezi wenu aeleze vitendea kazi mnavyovihitaji zaidi, vinagharimu kiasi gani ili niweze kuwasaidia," alisema Bashe.
Aidha, Bashe alisema kuwa, pamoja na kuhitaji kuwezeshwa na kusaidiwa, bado suala la mshikamano na ushirikiano ni muhimu kwao ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Aliwataka wasanii katika kundi hilo, kutokata tamaa katika kutoa burudani kutokana na uchanga wao, huku akiwahimiza kufanya kazi kwa bidii ili kufanikiwa kwa urahisi.
Kundi la Nkomanile lilianza mwaka jana likiwa na wasanii saba, ambako sasa idadi hiyo imeongezeka na kufikia 25 ikiwa ni pamoja na viongozi wake.
Simba yametimia
*Sasa kukutana na TP Mazembe
Na Zahoro Mlanzi
HATIMAYE sasa yametimia, unaweza kusema hivyo, baada ya mabingwa wa soka Tanzania Bara, timu ya
Simba, kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Elan de Mitsoudje ya Comoro, katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, jana.
Kwa ushindi huo, Simba sasa itaumana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo, TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), katika hatua inayofuata.
Tangu ratiba ya michuano hiyo ilivyotolewa kwa mara ya kwanza na kuonesha Simba ikivuka hatua ya awali itaumana na Mazembe, mashabiki na wanachama wa timu hiyo, walikuwa wakiomba kwa udi na uvumba wakutane nayo, na jambo hilo limetimia.
Katika mchezo huo wa jana ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi, huku wengine kubaki nje ya uwanja kutokana na uwanja huo kujaa, ulianza kwa kasi huku kila timu ikicheza kwa tahadhari zaidi.
Ilikuwa ni Simba iliyokuwa ya kwanza kubisha hodi langoni mwa Mitsoudje, baada ya Ali Ahmed 'Shiboli' kumzidi ujanja Othouman Ibrahim na kupiga krosi iliyokosa mmaliziaji na mpira kutoka nje.
Simba iliendeleza mashabulizi langoni mwa Mitsoudje na dakika ya 12, Shiboli nusura aifungie Simba bao la kwanza, baada ya kuunganisha vibaya krosi iliyopigwa na Rashid Gumbo na mpira kutoka pembeni ya goli.
Mitsoudje ilitulia na kupanga mashambulizi, ambapo dakika ya 30, Madaha Mohamed alitoa pasi fyongo kwa Mousteckima Mohamed, baada ya kubaki na beki Kelvin Yondani, lakini kipa Juma Kaseja aliuwahi na kuudaka.
Mitsoudje iliongeza mashambulizi kwa Simba na dakika ya 43, Madaha aliifungia timu yake bao la kwanza kwa shuti lililotinga moja kwa moja wavuni, baada ya mabeki wa Simba kudhani ameotea.
Mbwana Samatta wa Simba aliisawazishia timu yake, ikiwa imebaki dakika moja kabla ya kipyenga cha mapumziko kupulizwa, kwa shuti lililombabatiza Youssouf Mohamed na kutinga wavuni.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, dakika ya pili tangu kipindi hicho kianze, Patrick Ochan, aliifungia Simba bao la pili, baada ya kuugonga mpira uliopigwa na Samatta na kutinga wavuni.
Baada ya kufunga bao hilo, Simba iliongeza lingine dakika ya 56, lililofungwa na Samatta, baada ya kuanziwa mpira wa adhabu na Juma Jabu, na kupiga shuti nje ya eneo la hatari lililoshindwa kudakwa na kipa Youssouf Ahamada.
Mitsoudje ambayo inacheza soka la chini chini na kupiga pasi nyingi, dakika ya 63, ilifunga bao la pili kupitia kwa Abdulhouda Abdoleafor kwa shuti, baada ya wachezaji wenzake kuonana vizuri na kumpasia mfungaji.
Timu hizo ziliendelea kuonesha kandanda safi kwa kushambuliana kwa zamu, dakika ya 72, Amri Kiemba wa Simba aliyeingia badala ya Shiboli, aliifungia timu yake bao la mwisho akimalizia krosi iliyopigwa na Haruna Shamte kutokana na mabeki kudhani ameotea.
Simba: Juma Kaseja, Haruna Shamte, Juma Jabu, Juma Nyosso, Kelvin Yondani, Mohamed Banka/Jerry Santo, Rashidy Gumbo/Shija Mkina, Patrick Ochan, Mbwana Samatta, Ali Ahmed/Kiemba, Mussa Hassan 'Mgosi'.
1 Maoni:
Anonymous said... TP Mazembe ni mabingwa watetezi wa vilabu Barani Afrika na makamu bingwa wa Dunia ngazi ya vilabu,Simba wanapaswa kuanza maandalizi ya uhakika kiufundi,kisaikolojia na kiuongozi.
February 14, 2011 5:04 AM
Mapacha watatu kupagawisha Mtoni
na Abdallah Menssah
KUNDI la Mapacha Watatu limejinasibu kukonga nyoyo za mashabiki watakaohudhuria onyesho lao pamoja na Five Stars Modern Taarab, litakalofanyika kesho kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa Mapacha Watatu, Hamis Dakota alisema kuwa, onyesho hilo ni maalum kwa ajili ya wakazi wote wa Wilaya ya Temeke
Dakota alisema kuwa, wakati umefika kwa mashabiki wa maeneo ya Mtoni na Wilaya nzima ya Temeke kwa ujumla, waliowaomba muda mrefu wawapelekee uhondo wao, kuburudika kwa vibao vyao motomoto.
Aidha Dakota aliwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika onyesho hilo ambalo kiingilio chake kimepangwa kuwa ni sh. 5,000, ili kushuhudia laivu sebene za nguvu pamoja na shoo kali kutoka kwa Khalid Chokoraa, Kalala Junior na Jese Mara.
"Katika onyesho hilo, kwa kuwa tutakuwa pamoja na wenzetu wa Five Stars, tutatumbuiza kwa zamu wa nyimbo tatu tatu, lakini ni katika mtindo wa bandika bandua, yaani bila kupumzika," alisema Dakota.
Simba sasa uso kwa uso na TP Mazembe
• Yawararua Wacomoro 4-2
na Mwandishi wetu
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam jana iliwatoa kimasomaso Watanzania baada ya kuirarua na kuiondosha kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Elan de Mitsoudje ya Comoro kwa mabao 4-2 kwenye Uwanja wa Uhuru ‘Shamba la Bibi' jijini.
Kwa ushindi huo, Simba imefanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ambako itakutana uso kwa uso na mabingwa soka barani Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kati ya Machi 18 hadi 20 na kisha kurejeana Aprili Moso hadi 3 mwaka huu. Mtanange huo wa jana, ulikumbwa na kadhia ya kuchelewa kuanza kwa takriban dakika 10, kutokana na Wacomoro kugoma kuingia uwanjani hadi wenyeji wao Simba waonyeshe pasi za kusafiria za wachezaji wake, ambao hadi sasa leseni zao hazijawasili kutoka Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kabla ya Kamisaa wa mchezo huo Christian Welly kutoa ufafanuzi ndipo walipokubali.
Mchezo huo ulianza kwa kasi ya wastani huku Simba wakitengeneza nafasi kadhaa za kupachika mabao, lakini washambuliaji wake walishindwa kutikisa nyavu za wapinzani wao ambao nao walionekana kukamia mechi hiyo.
Simba walipata nafasi ya wazi mapema dakika ya 9, baada ya Ally Ahmed Shiboli kumtoka beki Yousouf Ali Mohammed na kupiga krosi safi kwenye eneo la hatari, lakini mpira uliwapita Musa Hassan Mgosi na Mbwana Samatta ‘Popa'. Shiboli tena alipata nafasi nzuri ya kufunga akiwa karibu na goli baada ya kupewa pande safi na Rashid Gumbo.
Simba walitawala mchezo dakika za mwanzo na kutengeneza kona kadhaa sambamba na kosa kosa za mara kwa mara na kuwalazimisha Elan kufanya mabadiliko na kumtoa Saidi Mchamboulou Mpezi na kuingia Abdoulhouda Abdouleafor dakika ya 32.
Elan ilibadilika na kufanikiwa kujipatia bao la kuongoza dakika ya 42 mfungaji akiwa Madha Mohammed na kuwashtua Simba ambao waliamka na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 44 mfungaji akiwa Samatta, ambaye aliambaa na wingi na kupiga krosi langoni ambako kipa Youssouf Ahamada akaisindika wavuni katika harakati za kuokoa. Hivyo hadi mapumziko timu zote zilikuwa sare ya 1-1.
Katika kipindi cha pili, Simba walianza kwa kasi na kufanikiwa kuongeza la pili dakika 47 mfungaji akiwa Patrick Ochan baada ya krosi ya Samatta iliyounganishwa na Mgosi na kuokolewa na mabeki kumbabatiza mfungaji na mpira kutumbukia kimiani.
Alikuwa ni Samatta tena, alipocheka na nyavu na kuiandikia Simba bao la tatu dakika 56 kwa shuti kali la mbali, baada ya Juma Jabu ‘JJ' kumuanzishia mpira wa adhabu; adhabu aliyofanyiwa na beki Ali Ahmed Ali.
Simba waliendelea kumiliki mchezo, lakini Wacomoro walijitutumua na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 63 mfungaji akiwa Abdouleafor.
Baada ya mabao hayo, makocha wa timu zote walifanya mabadiliko ambapo Zaidou Soilihi aliingia akichukua nafasi ya Madaha Mohamed na Simba walimpumzisha Shiboli na kuingia Amri Kiemba, ambaye dakika ya 71 aliiandikia Simba bao la nne akiunganisha vema krosi ya Haruna Shamte aliyepanda kusaidia mashambulizi na kupigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Wacomoro hao.
AFC yazidi kuzinduka Ligi Kuu
na David Frank, Arusha
LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara jana iliendelea kwenye viwanja vitatu tofauti ambapo jijini Arusha ilishuhudiwa ‘vibonde' AFC wakizidi kuzinduka baada ya kuizamisha Majimaji ya Songea kwa bao 1-0 kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid.
Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa aina yake, bao pekee la washindi lilifungwa na Bakari Kigodeko.
Akizungumzia matokeo hayo, Kocha wa Majimaji, Nkoma, alisema kuwa kufungwa kwao kulisababishwa na uchovu wa safari ya kutoka Songea hadi Arusha.
Ushindi huo wa AFC ni wa pili mfululizo baada ya mechi iliyopita kuwatoa nishai maafande wa Ruvu Shooting kwa bao 1-0.
Katika mchezo mwingine uliopigwa Manungu Turiani Morogoro, wenyeji Mtibwa Sugar walishindwa kuutumia vizuri uwanja wao wa nyumbani kwa kulazimishwa sare ya bila ya kufungana na maafande wa JKT Ruvu.
Akizungumza kwa kujiamini, Msemaji ya Mtibwa Sugar, Tobias Kifaru Ligalambwike, alisema kuwa mchezo huo ulikuwa ni wa ushindani kwa timu zote kucheza kwa kujiamini kiasi cha kuonyesha kandanda safi.
Mjini Dodoma, Ruvu Shooting iligawana pointi kwa sare ya 1-1 na maafande wenzao wa polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri ya Dodoma, kwa kutoka 1-1.
Bao la Ruvu lilifungwa na Paul Ndauka huku la Polisi likisawazishwa na Maige.
Villa yaifanyia mauaji TMK
na Safari Chuwa, Tanga
TIMU ya soka ya Villa Squad jana iliwashushia kichapo kibaya ndugu zao wa TMK United cha mabao 5-1 katika mfululizo wa Ligi Daraja la Kwanza Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa.
Mabao ya washindi yalifungwa na Jafari Gonga dakika ya 19, Mecky Michael dakika ya 46, Roshwa Rashid dakika ya 74 na 77, kabla ya Yahya Daruweshi kukandamiza la tano dakika ya 85.
Bao pekee la kufutia machozi la TMK lilifungwa na Kenan Mwandusi dakika ya 12.
Katika mchezo mwingine, maafande wa Tanzania Prisons wa Mbeya walijisafishia njia ya kurejea Ligi Kuu baada ya kuichapa Morani FC kwama bao 2-0.
Wawakilishi ZFA kupatikana ligi ndogo
na Mohamed Said Abdullah, Zanzibar
KWA mara ya kwanza katika historia ya soka visiwani hapa, wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya kimatiafa 2012, watapatikana kupitia ligi ndogo inayotarajiwa kuanza Februari 28, ikiwa ni siku chache tangu Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), kilipobadilisha kalenda yake ya mwaka.
Hatua hiyo ya kufanyika kwa ligi ndogo Zanzibar, inatokana na maazimio ya Kamati ya Utendaji Taifa ya ZFA iliyoamua kubadilisha kalenda ya chama hicho, baada ya mfumo uliokuwa ukitumika kuleta athari kwa wachezeji kukaa muda mrefu bila ya kushiriki mashindano.
Mfumo wa zamani uliokuwa ukitumika kuendesha ligi hiyo ulikuwa ukiwadumaza wachezaji kutokana na ligi hiyo kuanza Januari na kumalizika Septemba kila mwaka.
Kuanzishwa kwa ligi ndogo, ni ukombozi kwa klabu zinazoshiriki ligi hiyo, kwa vile vitakuwa na muda mfupi wa mapumziko, kwa vile mfumo uliobadilishwa na ZFA unafanana na mfumo unaotumiwa na vyama vya soka ambavyo ni wanachama wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wa kuanza mashindano ya ligi kuu kila ifikapo mwezi wa Agosti.
Katibu Msaidizi ambaye cheo chake hakimo kwenye katiba ya ZFA, Masoud Attai, alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari vya Zanzibar, akielezea klabu zitakazoshiriki ligi hiyo, sambamba na ratiba yake inayotarajiwa kutolewa Febuari 14 mwaka huu, katika viwanja vitatu ambavyo ni Amaan, Mao Tse Tung na Ngerengere kilichoko kisiwani Pemba.
Miongoni mwa timu zilizotajwa kushiriki katika ligi hiyo ndogo ni pamoja na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu, Zanzibar Ocean View, ambao wameazna mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika kwa kuchechemea na wenzao KMKM ambao wamevunja rekodi ya kufungwa mabao mengi katika mashindano ya kimataifa ya mwaka huu.
Timu nyingine ni pamoja na Malindi, Polisi, Duma, Mafunzo, Mundu, Jamhuri, Chipukizi, Miembeni, Madungu United na Chuoni zilizopanda daraja msimu uliopita, ambapo kwa mujibu wa Attai, klabu hizo tayari zimepewa taarifa kuhusiana na ligi hiyo mpya iliyopachikwa jina la ligi ndogo, huku ZFA ikiwapatia matumaini makubwa wadau wa soka na vilabu vyote kuwa kiko katika hatua za mazungumzo na makampuni mbalimbali ili yaweze kudhamini ligi hiyo, inayojikongoja kila mwaka na kukosa msisimko kama miaka ya tisini.
Hata hivyo, Attai hakueleza suala hilo la udhamini limefikia hatua gani, hasa kwa kuzingatia kuwa wadau wengi wa soka, wamekatishwa tamaa na uendeshaji wa ligi hiyo, kutokana na ukosefu wa ufadhili, hatua ambayo imesababisha macho na msikio ya wapenda soka wengi wa visiwani Zanzibar kuelekeza katika ligi kuu za Ulaya ambazo zimekuwa zikivutia hisia za mashabiki wengi katika maeneo mbalimbali ya starehe pamoja na majumbani.
Ligi hiyo iliyopachikwa ‘Ligi Ndogo ya Zanzibar' inafanyika huku ZFA, ikiwa haina uongozi wa kikatiba, baada ya matokeo ya uchaguzi na uongozi mpya kufutwa wakati uongozi wa zamani ukiwa umemaliza muda wake kwa mujibu wa katiba ya chama hicho ya mwaka 2010.
Hata hivyo, uchaguzi huo umepangwa kufanyika tena mwezi ujao, baada ya Mrajisi wa Vyama vya Michezo kuingilia kati mgogoro uliokikumba chama hicho baada ya matokeo ya uchaguzi ya Desemba 31 mwaka jana, ambapo hata hivyo bado haijaweza kufahamika kama wagombea wa uchaguzi uliopita kama ndio watakaochukua fomu upya au kugombea kwa gharama walizotumia mwanzo.
Awadh Tamim kutua leo kumvaa Ashraf
na Shehe Semtawa
BONDIA Awadh Tamim ‘Big Brother' ambaye anaishi nchini Sweden kwa sasa anatarajia kuwasili nchini leo kwa ajili ya kutetea ubingwa wake wa uzito wa juu Afrika Mashariki dhidi ya Ashraf Suleiman wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Aurora, Shomari Kimbau, Tamim anarejea nchini baada ya kusikia kuwa Suleiman amekuwa mara kwa mara akidai aachie mkanda huo wa ubingwa ili aweze kugombania na mabondia wengine.
Kimbau alisema, baada ya Tamim kusikia jambo hilo, amepinga vikali na kuamua kutetea mkanda wake huo katika mechi ya marudiano na Suleiman ambapo mkanda huo aliupata kwa kumpiga KO bondia Thomas Ukusi kutoka Kenya.
"Sisi tunampongeza bondia Awadh Tamimu kwa kukubali kurejea nchini kuja kutetea mkanda wake, hivyo tunawaomba wadau na mashabiki wa mchezo wa ngumi tujitokeze kwa wingi kwenda kumpokea leo," alisema Kimbau.
"Ni kitendo cha kishujaa, inafaa wanamichezo wote nchini kuiga kitendo hiki, kwani ni mara nyingi wanamichezo wanapopata mikataba ya kimataifa huwa ni ngumu kurejea makwao kuwakilisha Taifa," alibainisha Kimbau.
Kimbau alijinasibu kuwa pambano hilo litakuwa na mvuto wa kimataifa Afrika nzima, kwa kuwa mabondia wote wawili wamewahi kucheza mechi za kimataifa barani Ulaya.
Aidha, Kimbau alisema mshindi wa pambano hilo atacheza na bingwa wa Afrika katika uzito huo Joseph Chingangu wa Zambia.
Pambano la wababe hao linatarajiwa kupigwa Machi 5, mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Phiri aivutia pumzi TP Mazembe
Na Zahoro Mlanzi
BAADA ya kuifunga Elan de Mitsoudje kutoka Comoro katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika, Kocha Mkuu wa wabingwa wa
soka Tanzania Bara, Simba, Patrick Phiri, ametamba kuwafunga mabingwa watetezi wa michuano hiyo, TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), nyumbani.
Kauli hiyo ya Phiri aliizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopigwa jana, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.
Phiri alisema michuano hiyo ndio kwanza inaingia katika hatua ya pili, hivyo ni mapema kuanza kuzungumzia hali ya baadaye, kwani kila timu ina nafasi ya kutwaa ubingwa.
"Naiheshimu TP Mazembe, ni timu bora Afrika na si Afrika hata kwa Dunia kwani ilifika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia, licha ya kuwa na ubora huo, nina imani hapa nyumbani tutaibuka na ushindi," alisema Phiri.
Alisema kikubwa kinachotakiwa ni kufanya maandalizi ya kutosha kwani mchezo huo dhidi ya Mazembe ni mchezo mgumu kwao.
Akizungumzia mchezo huo wa jana, Phiri alisema anawashukuru wadau, wanachama na wapenzi wa soka nchini kwa kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao.
Alisema soka la Comoro limepiga hatua kubwa, licha ya kuibuka na ushindi huo, mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kiasi kilichompa wakati mgumu kocha huyo.
Alisema kama si juhudi za wachezaji wake katika kuhakikisha wanawatuliza Wacomoro hao, ingekuwa ngumu kuvuka hatua hiyo.
NSSF yaisadia BFT sh. milioni 1.6
Na Zahoro Mlanzi
MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umetoa udhamini wa sh. milioni 1.6 ili kufanikisha mashindano ya Taifa ya ngumi za
ridhaa kutafuta Mabingwa wa Taifa, yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Februari 26 hadi Machi 5, mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Msemaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Eckland Mwaffisi, alisema udhamini huo umedhihirisha dhamira ya mfuko huo kuendeleza na kuibua vipaji vya mabondia wa ridhaa nchini.
Alisema hadi sasa, mashindano hayo yamepata udhamini wa NSSF pekee, mbali ya umuhimu wake kwa taifa, pia itasaidia kupata mabondia ambao wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
Mwaffisi alisema, si mara ya kwanza kwa NSSF kuona umuhimu wa kudhamini mashindano makubwa ya ngumi za ridhaa ambayo yanaandaliwa na BFT.
òMwaka 2010, mfuko huu ulitoa udhamini wa sh. milioni moja ili kufanikisha mashindano ya kimataifa ya ngumi za ridhaa ya Afrika Masharik ya Bingwa wa Mabingwa.
òNatoa mwito kwa mifuko mingine ya jamii, taasisi, kampuni na wadau wengine wa michezo, kuiga mfano wa NSSF ili mashindano haya yaweze kufanikiwa kama yalivyopangwa ambapo mikoa 21, tayari imethibitidha kushiriki,¦ alisema Mwaffisi.
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya ngumi za ridhaa, Hurtado Pimenter kutoka nchini Cuba, atachagua mabondia ambao wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ikiwemo michezo ya Afrika, ambayo imepangwa kufanyikia mjini Maputo nchini Msumbiji, Septemba mwaka huu.
Alisema gharama za mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 25, ambapo hadi sasa, BFT imepata sh. milioni 1.6 kutoka NSSF .
Alisema mashindano hayo yana umuhimu mkubwa kwa Taifa kwani mchezo wa ngumi za ridhaa na riadha, ndiyo pekee iliyoweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na wachezaji wake, kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
òLeo, mchezo wa soka ndiyo unaopewa kipaumbele na wadhamini kuliko michezo mingine, ambayo kama itapata udhamini wa kutosha, Tanzania itafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na kuondoa dhana iliyojengeka kwa wachezaji wetu kuitwa watalii,¦ alisema.
Kiwango cha Man United chamfurahisha Ferguson
LONDON, Uingereza
KOCHA Alex Ferguson amefurahishwa na kiwango cha timu yake na kuweza kuwafunga mahasimu wao Manchester City mabao 2-1, Jumamosi na
kuzidi kujichimbia kileleni.
Ushindi huo umeiweka United katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England.
Kocha huyo amesifu wachezaji Wayne Rooney na winga wa kireno Luis Nani, baada ya wawili hao kufunga mabao yaliyoifanya United kupata ushindi, huku City ikipata bao lake pekee kupitia kwa David Silva.
Lakini, katika mabao ya juzi, Rooney alifunga bao la kusisimua la ufundi kwa kupiga tiktak, na kuifanya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku ikiwa na pointi 57, na kuwapita wapinzani wao kwa pointi nane.
Fergie alitamba: " Bao lile lilikuwa lakusisimua, huwezi kuamiani.
"Bao la Nani lilikuwa ni la kusisimua, lakini kila mmoja alilisahau, hakuna hata mtu aliyelizungumzi, kila mtu anazungumzia bao la Rooney.
"Lilinikumbusha bao la Denis Law. Ilikuwa ni bao ambalo huweza kuamini."
Pia, Kocha wa City, Roberto Mancini, alilisifu bao lilifungwa na Rooney akieleza kuwa, lilikuwa zuri sana na kueleza kuwa, ndilo liliiua timu yake dhidi ya Manchester United.
Mshambuliaji huyo wa England alifunga bao hilo dakila ya 78, wakati matokeo yakiwa bao 1-1, na kuifanya United kupata bao la pili na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
City imeondoka na masikitiko kwa kutopata angalau pointi moja, wakiwa ugenini katika Uwanja wa Old Trafford.
Prisons yaichapa Morani Sunday, 13 February 2011 21:14
Burhani Yakub, Tanga
TIMU ya Tanzania Prisons imeichapa Morani SC mabao 2-0 katika mechi ya Ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Katika mechi hiyo Prisons walitawala sehemu kubwa ya mchezo tokea kipindi cha kwanza mpaka mwisho wa mchezo.
Prisons walipata bao la kwanza katika dakika ya tano lililofungwa na Dominick Meshack.
Baada ya bao hilo kufungwa Morani walicharuka na kuanza kushambulia lango la Prisons bila mafanikio yoyote yale, lakini Prisons waliwabadilishia kibao na kuwashambulia mfululizo na kufanikiwa kufunga bao la pili katika dakika ya 44 kwa njia ya penati iliyofungwa na Mbega Dafa baada ya mchezaji wa Morani, Makungu Silima kumchezea rafu mchezaji wa Prisons.
Kwa matokeo hayo Prisons watakuwa na pointi 8 na Morani wataendelea kubaki na pointi 1.
Pia jana jioni kulikuwa na mechi kati ya Villa Squard dhidi ya Temeke United, ambapo Villa Squard iliichapa Temeke United bao 5-1.
Mabao ya Villa yalifungwa na Jafari Gonga dakika ya 19, Meck Michael dakika ya 46, Roshwa Rashid dakika ya 74 na Yahaya Darwesh katika dakika ya 85, wakati bao la Temeke lilifungwa katika dakika ya 12 na Kenan Mwandisi.
Mwananchi FC mabingwa Media Cup Sunday, 13 February 2011 21:12
Salome Milinga, DACICO
TIMU ya soka ya Mwananchi FC, imetwaa ubingwa wa michuano ya vyombo vya habari iliyofanyika kwenye Viwanja vya Chuo cha Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Bonanza hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya Airtel, lilishirikisha michezo mbalimbali na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari walishindana.
Katika soka, Mwananchi chini ya kocha wake, Allan Goshashy huku ikiwa 'imesheheni' nyota wake, Sweetbert Lukonge, Calvin Kiwia, Salum Jaba na Sosthenes Nyoni ilianza kwa kuikandamiza Habari Corporation mabao 4-0 kabla ya kuifunga Global Publishers 5-3.
Pambano la Global ilibidi luiamuliwe kwa mikwaju ya penalti baada ya kumalizika matokeo yakiwa suluhu.
Sifa za pekee zimwendee kipa wa Mwananchi FC, Ibrahim Bakari aliyepangua penalti mbili huku Majuto Omari akihitimisha furaha ya Mwananchi kwa kufunga penalti ya mwisho iliyoihakikishia ushindi.
Katika nusu fainali, Mwananchi ilikuwa icheze na Sahara Media (Star TV) lakini wakaingia mitini na katika fainali ilicheza na Business Times na kuwabandua kwa bao 1-0 lililofungwa na Majuto baada ya kupata pande la Abdallah Masoud aliyefanya kazi nzuri kupangua ngome ya BTL.
"Mwananchi Limesheheni...Mwananchi Limesheheni" zilikuwa kelele za waandishi na wapenzi wa Mwananchi FC baada ya mchezo huo kumalizika.
Katika netiboli, Mwananchi Queens iliyocheza bila nyota wake wanne, ilifungwa kwa taabu mabao 18-3 na Global Queens na kutolewa katika michuano hiyo.
Ujumbe wa TFF kwenda Sudan Feb. 21 Sunday, 13 February 2011 21:11
Doris Maliyaga
UJUMBE wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, unatarajia kyuondoka nchini Februari 21 tayari kwa mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika, CAF, utakaofanyika kwenye mji wa Khartoum nchini Sudan.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah aliiambia Mwananchi hivi karibuni kuwa timu hiyo ya ujumbe wa Tanzania itaongozwa na Rais wa TFF, Leodegar Tenga na Katibu Mkuu.
Mkutano huo wa CAF unafanyika kwa lengo la kupitisha, kuangalia na kuzungumzia masuala mbalimbali ya maendekleo ya soka katika Afrika.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la taifa, Idd Kipingu atafungua semina ya FIFA kwa viongozi wa klabu za Ligi Kuu Bara inafunguliwa leo kwenye hoteli ya White Sands nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam hadi Februari 18.
Semina hiyo ina lengo la kutathmini semina iliyofanyika Desemba 2007 huko Bagamoyo na watakaoshiriki ni wenyekiti, makatibu na maafisa habari.
Afisa habari wa TFF Boniface Wambura ameliambia Mwananchi kuwa, semina hiyo itakuwa ya siku hizo na kwa wenyekiti ni siku ya kwanza ya ufunguzi.
''Watakaoendesha semina hiyo ni viongozi wa FIFA na baadhi yao ni kutoka nchi za Mauritius, Uswisi na Afrika Kusini,''aliongeza Wambura.
Wakati Katika hatua nyingine, wenyeji Sudan na Algeria zimeingia robo fainali ya Michuano ya CHAN, ya wachezaji wa ligi za ndani inayoendelea Sudan.
Sudan ilipata tiketi yake baada ya kuirarua Gabon wakati Uganda iliyotoka sare, imepata tiketi baada ya kujikusanyia pointi saba ikifuatiwa na Algeria yenye tano, Gabon nne na Uganda haina pointi.
Bao la Rooney lafunika England Sunday, 13 February 2011 21:09
LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa England, Wayne Rooney juzi alifunga bao la aina yake na kuiwezesha Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliokuwa mkali na kusisimua.
Akifuta ukame wa mabao, Rooney alifunga bao la staili ya sarakasi katika dakika ya 78 na kufuta ndoto za City katika mbio zake za kuwania ubingwa.
Arsenal iko nyuma ya United baada ya juzi kupata ushindi wa mabao ya Robin Van Persie na kuifanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wanaoshika mkia wa ligi hiyo, Wolverhampton Wanderers.
Bao la Rooney katika mchezo huo uliofanyika Old Trafford, limemfanya kocha wake, Alex Ferguson kuwa mwenye furaha wakati wote. "Sijawahi kuona bao kama lile, hiyo ni uhakika," Ferguson alikuwa akizungumza na Sky Sports.
"Lilikuwa bao kali sana, huwezi kuamini kama angefunga kwa staili ile. Tumekuwa tukifunga mabao ya aina yake na yenye mvuto."
United ilianza kuziona nyavu za wapinzani wao, baada ya Nani kufanya kazi ya ziada na kufunga kabla ya David Silva kusawazisha dakika chache kabla ya mapumziko.
Matokeo hayo yanaifanya United kufikisha pointi 57 kutokana na michezo 26 ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 53 kutokana na mechi 26. City wanaendelea na pointi zao 49 katika nafasi ya tatu.
Tottenham Hotspur imeipiku Chelsea katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 47 kutokana na mechi 26 baada ya mshambuliaji wa Croatia, Niko Kranjcar kufunga bao lililoipa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sunderland. Chelsea leo inacheza na Fulham.
Liverpool chini ya kocha wake, Kenny Dalglish ilipunguzwa kasi na kulazimishwa sare ya 1-1 na Wigan Athletic kwenye Uwanja wa Anfield.
Nayo West Ham United ikiwa nyuma kwa mabao 3-0 ilifufua matumaini yake na kulazimisha sare ya 3-3 na West Bromwich Albion, Blackpool ilitoka sare ya 1-1 na Aston Villa wakati Birmingham City ilipata ushindi jioni wa bao 1-0 dhidi ya Stoke City. Blackburn Rovers na Newcastle United zenyewe zilitoka suluhu.
Zesco United yafuzu Ligi ya Mabingwa Sunday, 13 February 2011 21:08
LUSAKA, Zambia
MABINGWA wa Zambia, Zesco United imefuzu kucheza raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kufungwa mabao 2-1 na Liga Muculmana ya Msumbiji.
Wazambia hao wamefuzu raundi hiyo kwa jumla ya mabao 4-2 na ni kutokana na ushindi mzuri walioupata katika mchezo wa kwanza, uliofanyika mjini Lusaka na wenyeji kushinda mabao 3-0 kabla ya kufungwa 2-1 mchezo wa marudiano.
Muculmana ilikuwa inatakiwa kushinda mabao zaidi lakini bahati haikuwa yao. Alikuwa, Manuel Mablango aliyefunga bao la kuongoza katika dakika ya 25 kabla ya Portipher Zulu kusawazisha dakika 12 baadaye.
Dario Monteiro alifumania nyavu dakika ya 74 kwa shuti la 'guu' la kulia lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Wakati huo huo, MC Algers ilifuzu raundi ya pili baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real de Bangui ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, mchezo uliopigwa Ijumaa.
Kiungo, Bouchema Nassim na mshambuliaji Mohamed Derrag walifunga katika kila kipindi na kufanya timu hiyo kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-1.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Bangui, timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Mabingwa hao wa Algeria sasa watakutana na mabingwa wa Zimbabwe, Dynamos.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Yanga ya Tanzania imeaga michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 2-0 na Dedebit ya Ethiopia katika mchezo wa marudiano ulichezwa mjini Addis Ababa.
Wawakilishi hao wa Ethiopia wamefuzu kwa jumla ya mabao 6-4 baada ya sare ya 4-4 katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam.
Nayo Tiko United ya Cameroon, imefuzu raundi ya pili kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Arrondissement ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mchezo wa kwanza wa timu hizo, ulimalizika kwa suluhu.
Wageni walianza kufunga katika dakika ya 32 wakati Gourrier Junior alipofunga penalti yake, kabla ya Alain Nkafu, Clovis Ngalame na Edwin Mbon Ayuk kuifungia Tiko mabao.
Foullah Edifice ya Chad imefuzu licha ya kufungwa bao 1-0 na Ela Nguema ya Guinea ya Ikweta kupitia kwa Gerard Douala Ellong katika dakika ya 58.
Nayo Victors ya Uganda imesonga mbele baada ya kuitoa Mbabane Highlanders ya Swaziland kwa jumla ya mabao 2-1. Mchezo wa marudiano ulimalizika kwa sare ya 1-1 na ule wa kwanza, Victors walishinda bao 1-0.
Timu hiyo ya Uganda sasa inajiandaa kucheza na wawakilishi wa DR Congo, DC Motema Pembe iliyoifunga KMKM mabao 4-0 mjini Zanzibar.
Nigeria yapeleka ujumbe mzito mkutano CAF Send to a friend Sunday, 13 February 2011 21:13
ABUJA, Nigeria
WAZIRI wa Michezo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Michezo, Nigeria, Profesa Taoheed Adedoja ataongoza ujumbe wa Nigeria kwenda Sudan kwa ajili ya kupiga ndogondogo kuhakikisha Mwenyekiti wa zamani Chama cha Soka Nigeria, (NFA), Alhaji Ibrahim Galadima anapata nafasi ya ujumbe katika Shirikisho la Soka Afrika, CAF.
Katika ujumbe huo pia yumo mwenyekiti wa (NFA), Aminu Maigari, balozi wa Nigeria nchini Sudan, kiongozi wa zamani wa NFA, Bigedia Generali, Dominic Oneya na makamu wa NFA, Mike Umeh na wengine.
Chanzo cha habari kilisema, uamuzi wa kupeleka ujumbe wa serikali Sudan ulifikiwa katika mkutano wa saa 10 uliofanyika kwenye hoteli ya Eko Hotel, Lagos katika mkutano uliowashirikisha viongozi wa NSC na NFA. Mkutano huo ulifanyika baada ya mechi kati ya Nigeria na Sierra Leone.
Sababu hasa iliyoelezwa ya kupeleka ujumbe wa serikali nchini Sudan, ni kwa ajili ya kutoa ushawishi katika mkutano wa CAF wa Februari 23, pamoja na kuzungumza na Rais wake, Issa Hayatou na kumpigia debe Galadima kwa kuwa ni chaguo la serikali.
Gareth Bale to miss Tottenham's Champions League trip to Milan
• Wales winger not fit to travel with Spurs to Milan
• Bale's back problem not recovered in time
- Guardian.co.uk, Monday 14 February 2011 10.33 GMT <li class="history">Article history
Gareth Bale will miss Tottenham Hotspur's trip to Milan in the Champions League. Photograph: Nick Potts/PA Wire/Press Association Images Gareth Bale will not travel to Italy for the first leg of Tottenham Hotspur's Champions League match with Milan. The Spurs manager, Harry Redknapp, had previously said he thought the Wales midfielder would be fit to play, but the 21-year-old will now not take part in the first leg of the last 16 tie.
Bale has a back injury and has not played since the 1-1 draw at Newcastle United on 22 January.
There are also injury doubts over two other players who have been instrumental in Tottenham's European success this season, Luka Modric, who has had his appendix removed, and Rafael van der Vaart, who has a calf strain.
"I have got to see how Rafa is," said Redknapp." The return to the first team of Nicko Kranjcar, who has scored the winning goals in Spurs' last two games, also gives Redknapp an attacking midfield option. "Niko deserves his place in the team," Redknapp said.
Bale has been outstanding for Spurs in Europe this season and has already scored a hat-trick in San Siro, against Milan's rivals Internazionale in the Champions League group stage in October.
Gareth Bale to miss Tottenham's Champions League trip to Milan
Wales winger not fit to travel with Spurs to Milan
Bale's back problem not recovered in time
- Guardian.co.uk, Monday 14 February 2011 10.33 GMT <li class="history">Article history
Gareth Bale will miss Tottenham Hotspur's trip to Milan in the Champions League. Photograph: Nick Potts/PA Wire/Press Association Images Gareth Bale will not travel to Italy for the first leg of Tottenham Hotspur's Champions League match with Milan. The Spurs manager, Harry Redknapp, had previously said he thought the Wales midfielder would be fit to play, but the 21-year-old will now not take part in the first leg of the last 16 tie.
Bale has a back injury and has not played since the 1-1 draw at Newcastle United on 22 January.
There are also injury doubts over two other players who have been instrumental in Tottenham's European success this season, Luka Modric, who has had his appendix removed, and Rafael van der Vaart, who has a calf strain.
"I have got to see how Rafa is," said Redknapp." The return to the first team of Nicko Kranjcar, who has scored the winning goals in Spurs' last two games, also gives Redknapp an attacking midfield option. "Niko deserves his place in the team," Redknapp said.
Bale has been outstanding for Spurs in Europe this season and has already scored a hat-trick in San Siro, against Milan's rivals Internazionale in the Champions League group stage in October.
Arsenal will give Barcelona a tough test this time, says Jack Wilshere
• Gunners need to 'get in their faces' in first leg of last-16 tie
• Samir Nasri recovered from hamstring injury and could start
- Dominic Fifield
- guardian.co.uk, Sunday 13 February 2011 22.30 GMT <li class="history">Article history
Arsenal's Jack Wilshere, left, impressed again in his side's 2-0 win over Wolves and will be in the side to face Barcelona on Wednesday. Photograph: Sang Tan/AP Jack Wilshere believes Arsenal have learned the lessons from their chastening Champions League elimination by Barcelona last season and has called on his team-mates to "be a bit nasty" by "getting in the faces" of the Spanish team during a daunting tie, which begins at the Emirates Stadium on Wednesday.
Arsène Wenger's side are set to be boosted by the unexpected availability of Samir Nasri, arguably their most consistently impressive player this season, with the France international having recovered from hamstring damage sustained in the FA Cup fourth-round win over Huddersfield. His return would add to Arsenal's attacking options, though Wilshere and his team-mates will be just as intent on nullifying a Barça team who have scored 71 times in La Liga already this campaign and won 6-3 on aggregate in last year's quarter-final.
"I was at the Emirates Stadium for the first game against Barcelona last season and they were brilliant, especially in that first half," said Wilshere. "I was in Bolton [on loan] for the second match and watched on television but I remember we basically played our game, passing it around. This year we have to get in their faces and show them what we're all about. When we have the ball, we've got to keep it as well as they can. We've got to change our game a bit to play against Barcelona – we'll learn from last year, but we need to get in their faces and, if you like, be a bit nasty, in a footballing sense, to get the ball back.
"We have to press them as a team – there's no point just one of us going after them, so we have to close them down as a team and get the ball back from them. But we'll go into the game on Wednesday looking for the win still. It's important we get that to take to their place for the return match."
Although the teenage midfielder acknowledged a need to tweak the team's approach, Wenger retains faith that his players can unsettle Barcelona by tapping into their own strengths, albeit if they can secure possession for themselves. Arsenal claimed an unlikely 2-2 draw against these opponents in last season's first leg despite being without key players, and with Cesc Fábregas's domestic season ended by the injury picked up converting the hosts' equaliser from the penalty spot. Yet there is strength in depth this time around, with Nasri's potential return particularly timely.
The French midfielder has excelled, scoring 14 times, and had been expected to miss the first leg at the Emirates Stadium. He will have further tests on his hamstring tomorrow and Tuesday before a decision is made, though there is optimism that he will be able to feature against the Spanish champions.
"I will not take a crazy gamble, but physically he is ready," said Wenger. "There is just a risk of him suffering a setback, so we will test him medically and physically. There are other important games coming up – we have Leyton Orient in the FA Cup, and the Carling Cup final, and the return game in Barcelona in three weeks. So it is important not to be stupid.
"I personally believe we go into the Barcelona game in better shape than last year. We had so many uncertainties last season – Robin [van Persie] was injured, William Gallas went off in the first game, Andrey Arshavin went off after 27 minutes, we had no Alex Song or Fábregas in the second game … The team, for me, had less confidence and we have matured since then. We can certainly compete technically better with them. It will be interesting to see whether we play with belief.
"You can wonder whether we need to change the way we play at the Nou Camp but, at home, we will try to play to our strengths. We will try to attack the other team. If we just play in the final third defensively, that would not be our natural game and we would not be happy – we'd come out of the match thinking we hadn't played. But if we can escape their pressure, then we can be dangerous. We will create chances if we can put them under pressure. We have to think about how we do that."
The size of the task awaiting Arsenal was put into perspective by Fábregas who acknowledged the Catalans are "the best team in the world" at present. "We have a young team but one with a lot of quality and energy," he said. "We are very motivated. They are such a good team that, even if you know everything [about them], they have so many quality players that they can make the difference. We don't have to worry too much about them. We have to play with no fear. Last season in the first half [of the first leg] especially we respected them too much. We just have to play our game and that is it."
- Status
-
Not open for further replies.