Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Sakata la Samatta lachukua sura mpya


Na Zahoro Mlanzi

ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Klabu ya African Lyon, Jamal Kisongo ameanika ukweli kuhusu sakata la mshambuliaji Mbwana Samatta kwa kusema aliyekuwa Katibu
wake, Jeshi Zakaria ndiye anayekuza mjadala huo wakati ukweli wa mambo anaujua.

Mbali na hilo, Kisongo alisema bado kuna mambo matatu ya msingi hawajamalizana na TP Mazembe ambayo yatamalizwa baada ya mchezo kati ya timu ya taifa ya vijana na Uganda 'The Kobs', ambapo watakwenda Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kisongo alisema anashangazwa na Zakaria ambaye jambo hilo analijua kwa undani na alikuwepo wakati, Samatta akisaini mkataba wa kwenda Simba.

"Mimi nashangaa kila kukicha suala la Samatta katika vyombo vya habari, naomba mmuulize vizuri Jeshi Zakaria kwa kuwa suala hili analijua kwa undani na siku ya kusaini mkataba tulikuwa naye pale Magomeni pamoja na Makamu wa Simba, Geofrey Nyange 'Kaburu," alisema Kisongo.

Alisema mchezaji huyo kuendelea kuandikwa kila kukicha, kutamfanya achanganyikiwe na kiwango chake kushuka wakati kuna mtu anajua kila kitu kuhusu hilo.

"Mimi nilitegemea kuona African Lyon wakidai fedha, lakini kukanusha kwamba Samatta si mchezaji wa Simba hapo wanakosea, huyo ni mchezaji halali, ninachowaomba wafuate taratibu za malipo yao kwa Simba," alisema Kisongo.

Wakati huo huo, Kisongo alisema mchezaji huyo ataondoka kwenda Lubumbashi hivi karibuni kwani kuna mambo ya msingi hayajamalizwa kati ya Simba, TP Mzembe na wakala wa mchezaji huyo, Damas Ndumbaro.

"Mimi ni mtu wa karibu sana wa Samatta na ndiye ninayempa ushauri kwa kila kitu, hata TP Mazembe walipokuja nchini kumsainisha nilikuwepo na nikawa shahidi wa makubaliano hayo, hivyo najua kila kitu kuhusu Samatta," alisema Kisongo.

Alisema Simba bado hawajamalizana na TP Mazembe, kuhusu muda atakaocheza soka huko ambapo mabingwa hao wa Afrika wao wanataka asaini miaka mitano na hawajaafikiana nani atakuwa na haki ya kuzungumzia suala lake itakapotokea ameuzwa klabu nyingine na pia suala la malipo ya bonus.

Kisongo alisema maandalizi ya safari ya mchezaji huyo kwenda Lubumbashi, yameshakamilika na Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni ametoa baraka lakini mpaka amalize mechi ya Jumamosi kutokana na umuhimu wake katika kikosi hicho cha vijana.
 
‘Mapro' wajipeleka Yanga SC
• Wanatoka Cameroon, Ghana na Nigeria

na Dina Ismail


WAKATI timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara zikiwa katika mchakato wa kusaka wachezaji zitakaowatumia katika msimu mpya wa ligi, wachezaji kutoka nchini Cameroon, Ivory Coast, Ghana, Nigeria na Zambia wamejitokeza kuwania kujaribiwa ili wasajiliwe na mabingwa wa ligi hiyo nchini, klabu ya Yanga.
Akithibitisha taarifa hizo, Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema jana kwamba wachezaji hao wameshatuma maombi yao, huku wale wa kutoka nchini Nigeria wakiwa tayari wameshatua jijini kwa ajili ya majaribio.
Alisema mpaka sasa wamepokea maombi ya Wacameroon wawili, Wanigeria wawili, Wazambia wawili, Waghana wawili na Muivory Coast mmoja ambapo alisema huenda idadi ya wachezaji kutoka nje wanaotaka kujaribiwa katika timu yao msimu huu ikaongezeka.
Hata hivyo, Sendeu alisema wachezaji hao hawana budi kusubiri hadi Juni ambapo Kocha Mkuu wa wakali hao wa Jangawani, Sam Timbe, atarejea kutoka nchini Uganda alikokwenda kwa mapumziko, kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ili kuangalia nani anafaa kusajiliwa.
"Kweli tumepata maombi ya wachezaji kutoka nje na wengine wameshawasili nchini…hata hivyo ni vigumu kuwasajili moja kwa moja, tumewataka wasubiri hadi kocha atakaporejea mwezi Juni ili wafanyiwe majaribio," alisema Sendeu.
Hadi sasa, Yanga ina nafasi za kusajili wachezaji watatu tu wa kigeni ambao wataziba nafasi za wenzao waliotupiwa virago kutokana na viwango vyao kushuka, huku ikibaki na wachezaji wawili tu wa kigeni ambao ni mshambuliaji Davies Mwape kutoka Zambia na Kipa Yaw Berko kutoka Ghana.
Hata hivyo, uwezekano wa nyota hao wanaojileta kusajiliwa ni mdogo sana kutokana na Yanga kufanya wenyewe mchakato wa kusaka wachezaji wa kulipwa, ambapo kwa sasa ipo katika mazungumzo na kiungo wa APR ya Rwanda, Haruna Niyonzima ‘Fabregas wa Rwanda' , Mshambuliaji wa S.K Jagodina ya Serbia, Kenneth Assamoh huku pia Kocha Timbe akiahidi kuja na wachezaji wawili, mmoja kutoka Kenya na mwingine Uganda.
Aidha, tayari Yanga imeshasajili wachezaji watatu kutoka hapa nchini, wakiwemo kipa Said Mohammed (Majimaji ya Songea), Godfrey Taita (Kagera Sugar) na Pius Kisambale (JKT Ruvu), huku ikiwa katika mazungumzo na nyota kama kiungo wa Simba, Mohammed Banka na kipa wa Mtibwa Sugar, Shaban Kado.
 
Kaseja, Ngasa, Fuso wagongana Taswa
• Hashim Thabit, Nizar, Mtagwa ndani

na Dina Ismail


MFUNGAJI bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2010/2011, Mrisho Ngasa, pamoja na kipa wa timu ya Simba, Juma Kaseja, ni miongoni mwa wanamichezo walioteuliwa kuwania tuzo ya mwanamichezo bora wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa).
Ngasa anayekipiga Azam FC ya jijini Dar es Salaam, Kaseja, beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa ‘Fuso', pamoja na mchezaji kutoka Visiwani Zanzibar akikipiga katika klabu ya Zanzibar Ocean View, Khamis Mcha, watawania tuzo hizo ambazo hafla yake imepangwa kufanyika Mei 6, katika Hoteli ya Movenpick, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando, aliwataja wanamichezo wengine kuwa ni pamoja na Asha Rashid ‘Mwalala', Mwanahamisi Omary ‘Gaucho' (Mburahati Queens) na Fatuma Omary (Sayari Queens) ambao watawania tuzo ya mwanasoka bora kwa upande wa wanawake.
Alisema tuzo nyingine itakayowaniwa ni ile ya Watanzania wanaocheza nje ambapo walioteuliwa ni pamoja na Hasheem Thabeet (kikapu), Henry Joseph, Nizar Khalfan (soka), Rogers Mtagwa (ngumi), ile ya wachezaji wa nje wanaocheza Tanzania itawaniwa na Emmanuel Okwi-soka (Simba), Yaw Berko-soka (Yanga) na Kanda Kabongo (kickboxing).
Kwa upande wa riadha (wanaume) wanaowania ni Samson Ramadhan,Marco Joseph na John Bazil huku kwa wanawake ni Zakia Mrisho, Mary Naali na Magdalena Mushi, katika wavu wanaowania kwa upande wa wanaume ni pamoja na Kevin Peter (Magereza Wanaume), Mbwana Ally (Mzinga Morogoro) na Ibrahim Cristopher ( Nyuki Zanzibar), huku kwa wanawake ni Hellen Richard Mwegoha (Magereza Wanawake), Yasinta Remmy na Zainabu Thabit (Jeshi Stars).
Wakati katika netiboli ni Lilian Sylidion (Filbert Bayi), Mwanaid Hassan na Sekela Dominick (JKT Mbweni ), huku katika karate kwa upande wa wanaume ni Sempai Steven Bella na Sempai Ayub Seleman, wakati kwa upande wa wanawake kuna jina moja ambalo haliwezi kutangazwa.
Walioteuliwa katika mpira wa kikapu kwa upande wa wanaume ni George Otto Tarimo (Savio-Dsm), Lusajo Samwel Mwakipunda (Oilers-Dsm) na Gilbert Batungi, huku kwa upande wa wanawake ni Faraja Malaki (Jeshi Stars-DSM), Zakhia Kondo (Lady Lioness-Dsm) na Doritha Mbunda ( JKT Stars).
" Karama Nyilawila, Mbwana Matumla na Francis Cheka watawania katika ngumi za kulipwa, huku katika ngumi za ridhaa watakaowania ni Revocatus Shomari (uzito wa Bantam), Selemani Kidunda (uzito wa Middle) na Said Dume (uzito wa Fly )", alisema Mhando.
Gofu (wanawake) ni Hawa Wanyeche, Madina Iddi na Vailet Peter, huku kwa upande wa wanaume ni Frank Roman, Adam Abbas na Isaac Anania.Katika Baiskeli inawaniwa na Hamis Clement, Richard Laizer na Said Jumanne kwa waunaume huku kwa upande wa wanawake ni Sophia Anderson, Martha Anthony na Ndashimba Kulia.
Katika mchezo wa kriketi (wanaume) wanaowania ni Kassim Nassor, Seif Khalifa na Benson Mwita huku kwa wanawake ni Hawa Salum, Mariam Said na Sophia Hemed. Tuzo ya mpira wa mikono kwa upande wa wanaume itawaniwa na Kazadi Monga (Magereza), Hemed Saleh na Abineri Kusena (JKT) na wanawake ni Happiness Mahinya, Zena Mohammed (JKT) na Teresia Kifukwe (Magereza).
Aidha, Mhando aliwataja watakaowania tuzo ya mwanamichezo chipukizi ni pamoja na John Bazil (riadha), Magdalena Cristian (riadha), Lilian Sylidion (netiboli) na Vailet Peter (gofu), wakati Khamis Azan Hussein, Abeid Omar Dola na Masoud Amour Kombo (Zanzibar) watawania tuzo katika mchezo wa judo huku tuzo ya heshima itatangazwa siku ya hafla.
Mshindi wa jumla katika tuzo hizo ambazo zimedhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) pamoja na Hoteli ya Movenipick atazawadiwa gari aina ya GX 100, lenye thamani ya shilingi mil. 13, pamoja na kulala usiku mmoja katika Hoteli ya Movenpick. Pia mshindi wa kila kipengele atazawadiwa shilingi mil. moja kila mmoja.
 
Hakuna wa kuning'oa Yanga – Nurdin


na Chile Kasoga


KIUNGO wa timu ya soka ya Yanga, Nurdin Bakari, ameapa kuendelea kuitumikia klabu yake ya Yanga kutokana na thamani kubwa ambayo amekuwa akiipata katika klabu hiyo tangu alipojiunga nayo akitokea klabu ya Simba.
Nurdin ambaye inadaiwa tayari ameshamalizana na klabu yake hiyo kwa mamilioni ya fedha, alieleza kuwa anafikiria kuendelea kuchezea timu ya Yanga mpaka hapo kiwango chake cha soka kitakapofikia kikomo.
"Unajua kuna timu nyingine unaweza kukimbilia kusajiliwa nazo na kuishia kukalia benchi, kitu ambacho kinaweza kurudisha nyuma kiwango chako cha soka," alisema Nurdin ambaye ni kiungo wa kutumainiwa wa timu hiyo na ile ya taifa ‘Taifa Stars'. "Na soka langu likifikia kikomo nitaenda kulimalizia AFC ya Arusha badala ya kujiunga na timu nyingine," alisema Nurdin Bakari kwa mzaha.
Hata hivyo mchezaji huyo hakuwa tayari kuthibitisha kama ameshamalizana na timu yake ya Yanga, licha ya kuwapo kwa taarifa kuwa mchezaji huyo alikuwa anatarajiwa kujiunga na timu ya Azam FC kwa dau la shilingi mil. 40, ambazo tayari inadaiwa alishapewa na uongozi wa timu hiyo.
 
Credo Mwaipopo ajinadi Ligi Kuu


na Chile Kasoga


KIUNGO wa zamani wa timu ya soka ya Yanga, Credo Mwaipopo, kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam akisaka timu ya kujiunga nayo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Credo aliyekuwa akicheza soka ya kulipwa nchini Sweden alisema kuwa mkataba wake wa kucheza soka nchini humo umeshamalizika, hivyo yupo tayari kujiunga na timu yoyote itakayomhitaji.
"Nina miezi minne tangu nitue hapa nchini, nipo katika kusaka timu yoyote ya kuichezea hapa nchini na hadi sasa sijapata timu yoyote, hivyo nipo tayari kujiunga na timu yoyote itakayonihitaji," alisema Credo.
Credo aliyeichezea Yanga kwa mafanikio miaka ya nyuma kabla ya kutimkia nchini Sweden, alieleza kuwa alishindwa kuendelea na klabu yake ya Pannelinois IF inayoshiriki ligi daraja la pili kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimwandama.
Alisema kuwa anaendelea na mazoezi katika viwanja mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuonyesha uwezo wake endapo atapata timu itakayomsajili kwa msimu ujao wa ligi.
 
Mbwana Matumla awachapa mabondia watatu


Na Mwali Ibrahim

BONDIA Mbwana Matumla, amefanya vyema katika mapambano yake ya majaribio baada ya kuwapiga mabondia Issa Sewe, Omari Bayi na Said Hofu lililofanyika
katika Ukumbi wa Panandipanandi, Dar es Salaam juzi.

Ushindi huo utakuwa umempa nguvu bondia huyo la kumpiga mpinzani wake kutoka Kenya, Gabriel Ochieng ambaye atapambana naye Mei Mosi mwaka huu katika Ukumbi wa PTA.

Akizungumza Dar es Salaam juzi mratibu wa pambano hilo, Rajab Mhamila 'Super D' alisema Mbwana ameweza kuonesha uwezo mkubwa katika mapambano dhidi ya mabondia hao, ambapo aliweza kumtwanga Omari Bayi katika raundi ya pili huku akioneshana ubabe na Issa Sewa na Said Hofu hadi raundi ya mwisho.

Alisema mapambano hayo yalikuwa ya raundi nne ambapo, Mbwana sambamba na kuyatumia kama maaandalizi yake ya mwisho ya pambano lake la ubingwa wa UBO dhidi ya Ochieng la uzito wa Kg. 55 la raundi 12, pia alikuwa akitoa hamasa kwa mabondia wa Ilala kuupenda mchezo huo.

Super D alisema kutokana na uwezo aliouonesha, bondia huyo ana nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa katika pambano lake la Mei mosi kwani ameonekana kuiva.

Kwa upande wake, Mbwana alisema anajiona yupo katika nafasi nzuri kiushindani na kuahidi kutetea vyema mkanda wake alioutwaa mwaka jana.

Pambano hilo litasindikizwa na mapambano mengine ya utangulizi kati ya bondia Ambukile Chusa atakayedundana na Emmanuel Kayala katika uzito wa kg. 69, Faraji Magia atazichapa na Issa Sewe uzito wa kg. 61 na Omari Zungu watazikunja na Fadhili Awadhi uzito wa kg. 59.

Mabondi wengine watakaosindikiza ni Said Momba ambaye atapigana na Jumanne Mapombe uzito wa kg. 57, wakati Fadhili Magia ataoneshana kazi na Kijepa Omari katika uzito wa kg. 52 na John Mbwana atambana na Ally Mahiyo katika uzito wa kg. 49 ambapo mapambano yote yatakuwa katika raundi nne.
 
Real Madrid kumgeuzia mgongo Adebayor


MADRID, Hispania

REAL Madria inatarajia kumgeuzia mgongo,Emmanuel Adebayor wakati mkataba wake wa mkopo kutoka Manchester City utakapoisha mwezi ujao.Adebayor mwenye
miaka 27, amefunga magoli manne, mawili kati ya hayo aliifunga Tottenham katika muda wake aliochezea Bernabeu.

Mshmabuliji huyo wa zamani wa Arsenal, alifurahi sana kupata kombe lake la kwanza tangu aanze kucheza soka ya kulipwa Ulaya, baada ya Real Madrid kutwaa Kombe la Mfalme kwa kuifunga Barcelona bao 1-0 katika fainali iliyopigwa wiki iliyopita.

Lakini kutokana na City kutaka dau la pauni milioni 12 kwa mchezaji huyo waliyemnunua kwa pauni milioni 25 kutoka Arsenal mwaka 2009, imefanya miamba hiyo kushindwa kufikiri kumsaini, pamoja na safu yake ya ushambuliaji kuanza kufunga magoli.

Karim Benzema ameendelea kufunga magoli wakati, Gonzalo Higuain amerejea uwanjani na kuanza kufunga mabao baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi minne kutokana na kuumia, Jumamosi katika mchezo dhidi ya Valencia alifunga magoli matatu.

Kocha wa City, Roberto Mancini ambaye anaweza kumkosa mfungaji wake Carlos Tevez, tayari anamkaribisha Adebayor kurejea.

Kocha huyo mtaliano alisema: "Mwishoni mwa msimu, tutaona kama Emmanuel atataka kubakia hapa."

Lakini Adebayor anataka kuondoka City moja kwa moja na angependa kubakia Real.

Mshambuliaji huyo anaweza akawa amesikitishwa sana na habari hizo lakini ana kitu kingine cha kuamua, huku Lazio nayo ikimtamani nyota huyo wa Togo.
 
Wanaocheza nje ya Tanzania kupata tuzo Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:11

Clara Alphonce
WANAMICHEZO wa Tanzania wanaocheza nje ni miongoni mwa wanamichezo 74 waliotajwa kuwania Tuzo za Mwanamichezo Bora wa Chama cha Waandishi wa Habari za michezo Tanzania ( TASWA) zitakaziofanyika Mei 6 kwenye Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando aliwataja wachezaji watakaopambanishwa kuwania tuzo hizo kuwa ni pamoja na Hasheem Thabeet anayecheza kikapu katika timu ya NBA ya Houston nchini Marekani na Henry Joseph Shindika anayekipiga katika klabu ya Kongsivinger ya Norway.

Wengine ni Rogers Mtagwa anayezipiga nchini Australia na Nizar Khalfan wa Vancouver Whitecaps ya Canada. Wachezaji hao wameingia katika kategoria za Taswa kwa ajili ya tuzo hizo za kwanza kushirikisha wachezaji wa nje.

Alisema mbali na tuzo hizo, pia kutakuwa na tuzo za wachezaji wa nje wanaocheza Tanzania ambao wamefanya vizuri mwaka jana akiwemo mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, kipa wa Yanga, Yaw Berko Yanga na Kanda Kabongo anayecheza kickboxing.

Wachezaji wa ndani watakuwa na tuzo yao itakayowaniwa na Khamis Mcha (Zanzibar Ocean View), Mrisho Ngassa (Azam), Shadrack Nsajigwa (Yanga) na Juma Kaseja wa Simba. Kaseja alitajwa pia katika tuzo za mwaka juzi.

Katika riadha, waliotajwa ni Samson Ramadhan, Marco Joseph na John Bazil wakati kwa wanawake ni Zakia Mrisho, Mary Naali na Magdalena Mushi.

Alisema tuzo hizo zitashirikisha michezo yote bila kubagua na tayari wamekwisha pokea baadhi ya majina kutoka vyama mbalimbali pamoja na vigezi huku baadhi ya vyama vikiwa havijakamilisha baadhi ya vitu lakini wamewapa muda hadi leo kuwasilisha majina ya wanamichezo kwenye kamati ya maandalizi ya tuzo hizo.

Mhando alisema tuzo za mwaka huu ziko katika kategoria 17 na washindi wa kila kategoli wataunganishwa na kupigiwa kura kwa ajili ya kumpata mwakamichezo bora wa mwaka ambaye ataondoka na zawadi ya gari aina ya Toyota Cresta, GX100.
 
Waziri awapasha wachezaji U-23 Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:08

Kalunde Jamal
SERIKALI imeitaka timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23, kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa marudiano dhidi ya vijana ya Uganda ili kusonga mbele katika michezo hiyo ya kuwania kucheza Michezo ya Afrika.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara aliwatakia mchezo mwema wachezaji hao na kuwataka kufanya vizuri ili waweze kusongambele.

"Cha kwanza nataka washinde, pili nawaomba mashabiki kuja kwa wingi uwanjani kuwapa moyo vijana na kuwafanya wacheze kwa kujiamini wakijua Watanzania wapo nyuma yao.

"Kutokana na jitihada zilizofanywa na mwalimu wao na sisi kama serikali tulikuwa nyuma yao na tupo nyuma yao kuhakikisha wanafanya vizuri," alisema Mukangara.

"Walionyesha upinzani wa hali ya juu walipocheza na Cameroon, sasa nguvu ile tunataka kuiona na Uganda Jumamosi," alisema. Uganda wanawasili leo tayari kwa mchezo huo keshokutwa
 
Toto yapanga kufanya mabadiliko makubwa Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:06

Sweetbert Lukonge
UONGOZI wa timu ya soka ya Toto Afrika ya mjini Mwanza umesema unatarajia kukifanyia mabadiliko makubwa kikosi chake kwa ajili ya mikikimikiki ya Ligi Kuu msimu ujao.

Akizungumza na Mwanachi jana Mwenyekiti wa timu hiyo Omary Nofrin alisema wamefikia hatua hiyo ili kuhakikisha wanapata mafanikio kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

"Tunatarajia kukifanyia mabadiliko makubwa kikosi chetu kwa ajili ya kuhakikisha tunafanya vizuri msimu ujao kama ilivyokuwa miaka ya nyuma,"alisema Nofrin.

Alisema,"Tumechoka kila mwaka kumaliza ligi tukiwa katika nafasi za chini jambo ambalo pia haliwafurahishi mashabiki wetu pamoja na wananchi wa mkoa wa Mwanza."

Nofrin alisema tayari wameshanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji wa ndani na nje ya nchi ambao pia ni wachezaji wa timu za taifa katika nchi zao.

Hivi karibuni uongozi wa timu hiyo ulitangaza kuwa unatarajia kutumia zaidi ya sh 250 milioni kama bajeti yake ya msimu ujao, pia timu hiyo inatarajia kupata udhamini kutoka kwa baadhi ya makampuni ya hapa nchini pamoja na makampuni ya nje ya nchi ambayo yameonyesha nia ya kuisaidia timu hiyo kufanikisha ndoto zake.
 
Ferguson: Schalke wamshukuru kipa wao Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:01

MUNICH, Ujerumani
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amempongeza kipa wa Schalke kwa kuonyesha kiwango wakati wa mechi yao na kusema kuwa huenda akawa kikwazo zaidi mpambano wao wa marudiano utakaofanyika Old Trafford wiki mbili baadaye.

Ferguson alimpongeza, Manuel Neuer licha ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kusema alifanya kazi ya ziada kupungza mabao. Kipa huyo anajiunga na Bayern Munich baada ya msimu wa ligi kumalizika.

Neuer ameanza kuvumishwa kuja Old Trafford na kwamba kiwango chake kimemkuna kocha huyo wa United kabla ya Ryan Giggs kufunga katika dakika ya 67.

Akizungumza na Sky Sports baada ya mchezo, Fergie alisema kuwa alifanya kazi ya ziada katika mchezo huo uliofanyika Veltins-Arena.

ìNafikiri, tunafahamu [Neuer anakwenda Bayern Munich] lakini alicheza vizuri sana. Ni mojawapo ya makipa hodari niliowahi kuwaona nikiwa na Manchester United," alisema Ferguson.

ìNafikiri jinsi gani tunacheza, kasi na mashambulizi yetu yalikuwa makali, lakini alitulia. alicheza sana, sana.

ìKwa mimi, wakati Chicharito anafunga alipokuwa ameotea, na kupiga kuonyeha kuwa anaweza kumfunga [Neuer] na ni karibu, alidaka lakini Ryan [Giggs] alimfunga kifundi."

Matokeo hayo yanaifanya Red Devils kujiweka katika mazingira mazuri ya kukutana na mshindi kati ya Real Madrid na Barcelona, na Sir Alex alisema kuwa ni wakati wake wa kufanya vizuri.

ìNikiangalia mechi kama hizi, zinanipa msingi mzuri, tunauzoefu na tuna wachezaji wazuri kama Nani na vilevile Valencia yuko katika kiwnago cha juu,î alifafanua.

ìTumekuwa katika utata wa kupanga kikosi, lakini kikubwa ninachotaka kusema ni kuona tunapiga hatua. Tutakuwa na timu nyingine dhidi ya Arsenal [Jumapili] na natumai tutapata matokeo mazuri.

ìHivyo ndivyo, ninavyoweza kusema, na Jumapili nakamilisha matokeo mazuri, tutashinda na kujitengenezea morari zaidi kwa mechi yetu.

ìKwa kutegemea matokeo ya Jumapili, naweza kufanya mabadiliko ya aina tatu [kwa mechi ya marudiano] kwa sababu Chelsea, tutakuwa nao baada ya Jumapili hii. Ni siku saba za mechi ngumu lakini ndivyo inavyotakiwa na tutashinda.î
 
Walcott atema cheche Arsenal Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:00

LONDON, England
KIUNGO Theo Walcott amesema huu si wakati wa Arsenal kutafuta mchawi na kinachotakiwa kuangalia nini kimesababisha timu kufanya vibaya katika mechi za Ligi Kuu ya England.

Mchezaji huyo wa Arsenal na England, alipingana na kauli ya Wenger, kuwa timu yake imefanya vibaya kutokana na kuwa na vijana wengi na kuwa hawana uzoefu.

Alisema kuwa timu imefanya vibaya kwa kiwango kikubwa lakini tatizo si umri wa wachezaji ama uchanga wao, kinachotakiwa ni kumsaidia kocha, Arsene Wenger.

The Gunners imekuwa ikishambuliwa kutokana na kushindwa kutwaa ubingwa wa aina yoyote katika miaka sita na Walcott alisema kuwa ni wakati wa klabu kuonyesha kuwa sasa wameimarika na kujituma.

Akizungumza kabla ya Arsenal kutandikwa 2-1 na Bolton, Walcott aliiambia Sunday Telegraph: ìKama tunataka kutwaa vikombe, lazima tujifunze. Tuondokane na kuangalia wachezaji vijana. Tuna uzoefu. Kuna haja ya sisi kusimama wenyewe na kuangalia majukumu yetu uwanjani, na nina uhakika wote tunaweza kufanya hivyo.î

"Kwa sasa tuko nyuma ya Manchester United kwa pointi tisa, na tumepoteza pointi 13 ikiwemo mechi waliyokuwa mbele kwa 3-1 ya White Hart Lane.

Alipoulizwa ni vipi Arsenal wanaweza kufufua matumaini ya ubingwa, Walcott alisema: ìLabda kusiwe na hofu zinapokuja mechi kubwa, tunakuwa mbele kwa mabao 2-0 na tukisema sasa tumemaliza mchezo, inakuwa tofauti.î

Hali hiyo iliyotokea karibuni, imezua maswali mengi Emirates huku wengine wakimtaja Wenger kama ni tatizo licha ya kuitumikia klabu kwa miaka 15 sasa.

Aliongeza: ìWatu wanamwangalia yeye, lakini wengine wanaangalia timu na lazima walaumu kwa kuwa hatufanyi mambo makubwa.î
 
Olaba: Kado fikiri kabla ya kuamua Send to a friend Tuesday, 26 April 2011 21:11

Calvin Kiwia
KOCHA wa timu ya Mtibwa Sugar, Mkenya Tom Olaba amemtaka kipa wake Shabaan Kado kujiuliza mara mbili kabla ya kuchukua uamuzi wake wa kujiunga na Simba inayomuwinda kwa udi na uvumba.

Olaba aliliambia Mwananchi jana kwa simu kuwa Kado anatakiwa kukaa chini na kutafakari kabla ya kuamua kuchukua uamuzi wake huo wa kujiunga na Simba.

"Sioni sababu za msingi kwa Kado kuondoka Mtibwa na kujiunga na Simba halafu matokeo yake akaishie kulikalia benchi na kushusha kiwango," alisema Olaba.

"Tunafahamu kila mmoja wetu anatafuta maisha bora na hali hiyo inakuja baada ya kupata maslahi bora, ila lazima tuangalie upande mwingine wa kukitunza kipaji na kiwango chako ili kiweze kudumu kwa muda mrefu," aliongeza.

"Siwezi kumzuia Kado kujiunga na Simba isipokuwa nampa nasaha zangu kama kocha wake ili hali hiyo itakapokuja kumtokea asije kujuta kwa uamuzi aliouchukua," alisisitiza kocha huyo.

Alisema Kado bado ni kijana mdogo hivyo anatakiwa kukitunza kipaji chake na kuendeleza kwa malengo ya kutimiza ndoto zake za kuwa mchezaji wa kimataifa na sio kuishia tu kucheza soka la nchini Tanzania pekee.

Hata hivyo kocha huyo alisema kuwa kipa wao huyo bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo ya Manungu.

Olaba alimuuliza kipa huyo kwa kutoa mfano wa msitu wenye Simba wengi halafu hauna chakula na msitu wenye simba wachache na wenye chakula yeye atachagua kuishi katika msitu upi kati ya hiyo miwili?.

Mfano huo ni sawa na Kado atapojiunga na Simba itamlazimu kupigania namba na Juma Kaseja wakati Mtibwa Kado ndiye mfalme.

Naye Kado aliliambia Mwananchi kuwa endapo Simba watakaa meza moja na Mtibwa kwa nia ya kuvunja mkataba wake huo yuko tayari kujiunga na Wekundu hao, lakini kwa masharti ya kupangwa kikosi cha kwanza.

"Malengo yangu katika soka ni kuwa na maisha bora kwa hapo baadae na maisha bora hayo yanakuja baada ya kuwa na maslahi mazuri," alisema Kado.

Alisema kwa sasa anaona kama ndoto zake za kucheza soka la kulipwa na kuwa na maisha bora zinatimia hivyo hayuko tayari kuona timu ama kocha kumshinikiza kushusha kiwango chake.

Hata hivyo; Simba tayari inadaiwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Mtibwa naTaifa Stars, Salum Machaku kwa mkataba wa miaka mitatu huku wakiendelea kumwinda beki Obadia Mungusa wa timu hiyo.
 
Yanga yataja vigezo vyake vya usajili Send to a friend Wednesday, 27 April 2011 21:07

Sosthenes Nyoni
KLABU ya Yanga imetaja baadhi ya vigezo vyake vikuu inavyozingatia katika kufanya usajili wa wachezaji watakaoitumikia timu hiyo katika msimu ujao, ambapo suala la umri mdogo na nidhamu nzuri likitajwa kupewa kipaumbele.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Seif Ahmed alisema ili kuhakikisha hilo linatekelezeka ndio maana wamekuwa wakifanya taratibu zoezi la usajili .

Alisema wameamua kutilia mkazo suala la umri na nidhamu katika usajili wao kwa lengo la kupata wachezaji watakaoitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu na kuipa klabu mafanikio.

Ahmed alisema wamejifunza umuhimu wa kuzingatia vigezo hivyo kupitia usajili wa misimu iliyopita ambapo baadhi ya wachezaji hawakucheza kwa muda mrefu kutokana na kuwa na umri mkubwa sambamba na majeruhi ya mara kwa mara.

"Kitu kikubwa katika usajili wetu wa msimu huu tunataka kikosi kiwe na vijana wengi wenye uwezo uwanjani na umri mdogo pia,hatutaki kukurupuka safari hii tumeona athari zake huko nyuma tuliposajili wachezaji na matokeo yake wakashindwa kucheza kwa muda wote,"alisema Ahmed.

Alisema,"Lakini sio umri tu hata nidhamu, lazima tuangalie historia ya mchezaji huko alipokuwa kabla ya kuamua kumsajili, hatutaki usumbufu,"alisema Ahmed.

Baadhi ya wachezaji ambao tayari imedaiwa wamesaini fomu za usajili wa Yanga kwa ajili ya msimu ujao ni pamoja na aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Majimaji, Said Mohamed, mlinzi wa Kagera Sugar, Godfey Taita na mwenzake David Lwende pamoja na mshambuliaji wa JKT Ruvu, Pius Kisambale.
 
Comments




0 #2 juma 2011-04-28 08:39 Ndugu yangu seif suala kubwa ni kuangalia nidhamu endelea na kamati yako ya usajili
Quote









0 #1 a 2011-04-28 04:44 Ewe Sefu wee. Kashindwa Manji utayaweza wewe mtoto wa watu. Kama una vijipesa vyako ni heri kuvitunza kuwawekea akiba watoto wako. Vijipesa vyako hivyo vitaliwa na pale utapotaka kuuliza kuhusu matumizi ya pesa ndipo utavotimuliwa kama Manji la ikiwa una tamaa nyenginezo sijui lakini tunakwambia tahadhari jiti na macho yako.
Quote







Refresh comments list

Add comment
 
Champions League semi-final, first leg

José Mourinho rages at 'plot' to put Barcelona in the final

• Real Madrid coach livid at red cards in 2-0 home defeat



  • Sid Lowe at the Bernabéu
  • The Guardian, Thursday 28 April 2011 <li class="history">Article history José Mourinho, Real Madrid's coach, watches from the stand after being sent off in the Champions League defeat by Barcelona. Photograph: Alex Livesey/Getty Images

    José Mourinho effectively accused Uefa of fixing it for Barcelona to reach the Champions League final after his Real Madrid team were beaten 2-0 at home by their fiercest rivals in an ugly and controversy-filled first leg of their semi-final.
    Mourinho claimed it was "impossible" for Madrid to defeat the dark forces lined up against them after a night on which he and his defender Pepe were sent off. Two goals by Lionel Messi followed those dismissals to leave Barça on the verge of the final, where they look certain to meet Manchester United.
    Madrid's coach accused Barcelona of wielding untouchable power in European football and said their coach, Pep Guardiola, should feel "ashamed" if he wins a competition that "yet again" is engulfed in "scandal". Barcelona also had a man sent off, their substitute goalkeeper, José Pinto, for his role in a mass brawl as the teams left the field at half-time. The incident was one of numerous flashpoints.
    "One day," Mourinho said, pointedly using the Barcelona coach's full name, "I would like Josep Guardiola to win this competition properly." That was a reference to the controversial semi-final victory of Guardiola's team over Chelsea en route to their triumph in 2009.
    Mourinho, who has had a player sent off in all four meetings with Barcelona this season and with Internazionale in last season's semi-final, said that he did not want to say what he "really thinks" because he feared a life ban but he did insist he felt "disgusted" to be working in football. In the end there was little holding back. The accusation was hardly a veiled one.
    Mourinho claimed his red card and that handed to Pepe were unjustified and that this was not the first time Barcelona's opponents have been singled out for unfair punishment. He reeled off a list of referees whom he said had "favoured" the Catalan side, pointing an accusing finger at those who he sees as engaged in a pro&#8209;Barça conspiracy. He insisted that the evidence is unavoidable and asked: "Why?"
    "If I tell Uefa what I really think and feel, my career would end now," Mourinho said. "Instead I will just ask a question to which I hope one day to get a response: Why? Why? Why Ovrebo? Why Busacca? Why De Bleeckere? Why Stark? Why? Because every semi-final the same things happen. We are talking about an absolutely fantastic football team, so why do they need that? Why? Why does a team as good as they are need something [extra] that is so obvious that everyone sees it?
    "Why Ovrebo [two] years ago [when the Norwegian referee did not give Chelsea a series of penalties against Barcelona]? Why couldn't Chelsea go to the final? Last year it was a miracle that Inter got there playing with 10 men for so long. A miracle. Why weren't there four penalties against Chelsea [in 2009]? Why send off [Arsenal's Robin] Van Persie [in the last 16]? Where does their power come from?
    "It could have been 0-0 tonight, but then suddenly we are down to 10 men and they have a free path to find solutions that they could not find before then: we could have played for three hours and they would not have scored. But today we have seen that it is not difficult &#8211; it is impossible.
    "The question," Mourinho continued, "is why? I don't know if it is the Unicef sponsorship or if it is because they are nice guys. I don't understand. Congratulations to Barcelona on being a great team and congratulations for all the other stuff you have which must be very hard to achieve. They have power and we have no chance. Chelsea had bans for Drogba and Bosingwa; Wenger and Nasri were banned for Arsenal; me today. I don't know why. All I can do is leave that question here in the air and hope that one day I will get the response. They have to get to the final, and they'll get there, full stop."
    Asked if Madrid, trailing 2-0, were now out, Mourinho replied simply: "Yes, yes." There was a pause and then he added: "We will go there with pride and respect for football. It is a world that sometimes disgusts me to live in and earn a living from, but it is my world. We have to go there without Pepe, who didn't do anything, without [the suspended] Ramos who did nothing, without a coach who can't be on the bench. It is impossible. And if we score a goal and open up the tie a little, they will just kill it again. Tonight we have seen that we do not have any chance."
    Mourinho sought to discredit Barcelona's 2009 Champions League success and any victory they may have this season.
    "Josep Guardiola is a fantastic coach," he said, "but I have won two Champions Leagues. He has won [only] one Champions League and that is one that would embarrass me. I would be ashamed to have won it with the scandal of Stamford Bridge and, if he wins it this year, it will be with the scandal of the Bernabéu. I hope that one day he can win a proper Champions League. Deep down, if they are good people, it cannot taste right for them. I hope one day Guardiola has the chance of winning a brilliant, clean championship with no scandal."
    On their website, Barcelona responded to the Portuguese's comments by threatening to report him to Uefa. "Barcelona's legal department will study the declarations made by José Mourinho to determine whether to refer them to Uefa," a club statement read.
    "In the post match press conference, Jose Mourinho severely criticised the referee (Wolfgang) Stark and insinuated that Uefa treated Barcelona favourably."

 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…