Michezo programu za mazoezi mahala pa kazi iwe lazima

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Kwa sababu kumekuwa na ongezeko la magonjwa yanayotokana na kunenepeana na ulaji mbovu huku wafanyakazi wakiwa hawana muda wa mazoezi.
Sasa iwe lazima:-

○ Kila ofisi iweke programu za michezo mahala pa kazi.

○ Ofisi mpya zikiwemo zile za serikali Dodoma ziwe na facilities za kuoga ili wafanyakazi wanaotaka kuja kwa jogging kazini wapate mahala pa kujiswafi kabla ya kuendelea na kazi.

○ Canteen za maofisi hasa zile kubwa ziwekewe utaratibu wa chakula Chao kuwekewa viwango kwa kadri inavyofaa.

○ Ikiwezekana ofisi ziweke utaratibu wa kulipia mazoezi ktk gym parlors kwa ajili ya wafanyakazi wao kama baadhi ya ofisi binafsi zinavyofanya.

Kusema kweli wafanyakazi hasa wa ofisi za umma mostly wana vitambi (obesity) kutokana na ulaji mbovu...suala linaloongeza idadi ya magonjwa k.v. kisukari,kiharusi,nk.
 
Ni swala zuri ila mambo ya mazoezi inabidi uanze ww binafsi sisi kazini tulikuwa kila jumamosi tunakutana asubuhi tunafanya jogging tukifika tunafanya ya viungo ila watu walianza kusingizia kuumwa kila mara tukaona kuachana na iyo program
 
Mazoezi ni suala binafsi mtu akiona kuna umuhimu wa mazoezi kwa afya yake afanye..Sisi wengine maisha yetu ni zaidi ya mazoezi
 
Mazoezi ni suala binafsi mtu akiona kuna umuhimu wa mazoezi kwa afya yake afanye..Sisi wengine maisha yetu ni zaidi ya mazoezi
Ni kweli ni suala binafsi lakini katika taaluma ya Usimamizi wa rasilimali watu na taasisi moja ya vitu vinavyofundishwa na kusisitizwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya kijamii ya wafanyikazi.
 
Saa 12 asubuh napishana nao barabarani wananipigia honi tunapungiana mikono[emoji112], mimi niko busy na tizi, saa 1 narudi zangu home ku-relax na kunywa maji ya kawaida (sio baridi) saa 3 naamsha zangu mishe, jioni nikisharud najiandaa nakwenda zangu gym kwa lisaa limoja, njian nakutana na wale washkaj wamepaki mandinga wapo zao bar wanakula bia na nyama choma mixa michemsho safi, wananipungia tena[emoji112]............ITAENDELEA

KIKUBWA TUFANYENI MAZOEZI JAMAN, UKIWA UNAFANYA MAZOEZI HAUTAWEKEWA MASHARTI YA CHAKULA CHOCHOTE! TUSIPENDE KULA KULA HOVYO HALAFU MAZOEZI HATUFANYI, TUSISUBIRI MARADHI YATUPATE NDIO TUANZE KUFANYA MAZOEZI NA MUDA HUO USHAWEKEWA MASHARTI YA KULA, HAUNA RAHA TENA! SIO MBAYA UKIWA NA KIJITAMBI CHA KUCHOMEKEA SHATI LKN TUSIJIACHIE SAAANA, UKIWA UNAFANYA MAZOEZI UTAKULA NA KUNYWA KWA KUJIAMINI MNO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…