Michezo(Tetesi & Usajili).

Michezo(Tetesi & Usajili).

The Boldly

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,377
Reaction score
5,147
Wachezaji, wakufunzi na wafanyakazi wengine wa Manchester United wanaamini Jose Mourinho atafutwa kazi iwapo atashindwa mechi nyingine moja. (Daily Mail)

Maafisa wakuu wa klabu hiyo hata hivyo bado wana imani kwamba Mourinho, 55, anaweza kubadilisha mambo katika klabu hiyo hata baada ya United kushindwa mechi mbili kati ya tatu za kwanza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza tangu 1992-93.

Real Madrid wanamtaka mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambapo klabu hiyo ya La Liga inatarajiwa kumfuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa England uwanjani Wembley akicheza mechi ya Ligi ya Mataifa ya Uefa mnamo 8 Septemba. (Sky Sports)

AlfaPii
 
Mshambuliaji wa Ufaransa kutoka Arsenal Alexandre Lacazette, 27, ameanza kufikiria kuhusu mustakabali wake katika klabu hiyo ya Emirates. (le10sport)

AlfaPii
 
Winga wa Liverpool Sheyi Ojo, 21, anakaribia kujiunga na klabu ya Stade de Reims ya Ufaransa kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia msimu huu. Hii ni baada ya raia huyo wa England kueleza nia ya kutaka kuhamia ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1. (Mirror)

AlfaPii
 
Winga wa Liverpool Sheyi Ojo, 21, anakaribia kujiunga na klabu ya Stade de Reims ya Ufaransa kwa mkopo kwa kipindi kilichosalia msimu huu. Hii ni baada ya raia huyo wa England kueleza nia ya kutaka kuhamia ligi kuu ya Ufaransa, Ligue 1. (Mirror)

AlfaPii
 
Real Sociedad wanataka kumchukua mshambuliaji wa Everton raia wa Uhispania Sandro Ramirez. Mchezaji huyo wa miaka 23 alihamia Goodison Park majira ya joto yaliyopita lakini akatumwa Sevilla kwa mkopo. (Marca)

AlfaPii
 
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City Yaya Toure, 35, anakaribia kujiunga na klabu moja ya London. Hii ni baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Ivory Coast kupitia vipimo vya kiafya, wakala wake amesema. (Twitter)

AlfaPii
 
Fenerbahce wamekanusha taarifa kwamba wanajaribu kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Ufaransa Moussa Sissoko, 29. (Sky Sports)

AlfaPii
 
Winga Lucas Moura, 26, amesifiwa sana kama mmoja wa wachezaji muhimu zaidi Tottenham kwa sasa baada ya Mbrazil huyo kukaa Paris St-Germain kwa mkopo. Moura alifunga mabao mawili dhidi ya Manchester United Jumatatu wiki hii. (Sports Illustrated)

AlfaPii
 
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alitaka kumnunua mchezaji huyo wa Spurs kwa mujibu wa wakala wa Moura. (Manchester Evening News)

AlfaPii
 
Mkabaji wa Barcelona Gerard Pique, 31, amesema hawezi kamwe kurejea Manchester United. Mhispania huyo aliondoka Old Trafford na kuhamia Nou Camp mwaka 2008. (Star)

AlfaPii
 
Beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 29, anafahamu ni wapi Blues wanahitaji kujiimarisha licha ya klabu hiyo kushinda mechi zao tatu za kwanza msimu huu. (Football.London)

AlfaPii
 
Kipa wa England Jordan Pickford, 24, anasema wachezaji wa Everton wameanza kukumbatia na kuuamini mtindo wa uchezaji wa meneja wao Marco Silva. (101 Great Goals)

AlfaPii
 
Meneja wa Roma Eusebio Di Francesco anahitaji kufanyiwa upasuaji kwenye mkono wake wa kushoto baada yake akiumia akisherehekea bao la kusawazisha dhidi ya Atalanta siku ya Jumatatu. (Daily Mail)

AlfaPii
 
Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez anasema hajazozana kwa vyovyote vile na beki wa klabu hiyo raia wa England Jamaal Lascelles, 24, ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo inayochezea St James' Park. (Goal)

AlfaPii
 


Taarifa za andani ya klabu ya Manchester United zinaeleza kuwa wachezaji wa timu hiyo pamoja na wafanyakazi wanaamini meneja wao Jose Mourinho huwenda akatimuliwa kazi endapo atapoteza katika mchezo wao wa Jumapili ya terehe 01/09/ 2018 dhidi ya Burnley.

Kiongozi wa United, Ed Woodward amefanya mazungumzo na Mourinho juma hili kufuatia timu yao kupata matokeo mabaya mfululizo dhidi ya Brighton na Tottenham.

Wachambuzi wa mambo wanaamini kikao hicho kinafanana na kile alichofanyiwa meneja, Louis van Gaal katika siku zake za mwisho mwaka 2016 na nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho ambaye kwa sasa kunauwezekano mkubwa wa Zinedine Zidane kurithi mikoba hiyo.

Chanzo hicho kutoka ndani ya Manchester United kimesema kuwa ”Muda si mrefu, Jose atatimuliwa wengine wakiamini ataondoka endapo atapoteza mbele ya Burnley na wengine wakiamini hatokuwepo mwanzoni mwa mwezi wa tisa ,” kimesema chanzo hicho.

Inaelezwa kuwa wachezaji nane pekee ndiyo waliyoungana meneja wao, Mourinho kutoka kwenye viunga vya Carrington kwenda kwenye hoteli yao ya the Lowry baada ya kumalizika kwa mechi yao na Spurs wakati wengine wakiamua kuondoka binafsi huku Paul Pogba akitumia gari lake.

AlfaPii
 
ADVERTISEMENT
KAZI imeanza. Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars Emmanuel Amunike ameanza kazi yake kwa kuwachomoa nyota sita wa Simba katika kikosi chake kilichoingia kambini tangu juzi, huku Shomari Kapombe akishangaa.
Waliochomolewa kwenye kikosi hicho ni John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni,
Shomari Kapombe, Shiza Kichuya na Hassan Dilunga kwa kosa la kuchelewa kambini.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau, alisema Kocha Amunike, amefikia uamuzi huo baada ya kushangazwa na jinsi nyota wa Stars wanavyojivuta wanapoitwa timu ya taifa.
"Niliongea na Kocha jana baada ya kuona wachezaji wa Simba walivyoipotezea Stars huku kipa Aishi Manula pekee ndiye aliyefika huku wengine wakikausha, licha ya kambi kuwa hoteli wanayoitumia pia Simba," alisema Kidau.
"Niliongea na baadhi yao walieleza hawakuwa na taarifa mapema licha ya sisi kupeleka barua mapema, tunauunga mkono maamuzi ya Kocha kwa vile timu ya Taifa inahitaji maandalizi na hakuna mtu ambaye yupo juu ya timu ya Taifa."
Hata hivyo akisema kwamba nyota hao walisema walichelewa kupata taarifa, cha ajabu Manula anayecheza nao aliwahi mapema kambini, kitu kilichowaponza.
Kuhusu kambi kuanza mapema na kusimamisha baadhi ya mechi za Ligi, ilihali Stars itaenda kucheza na Uganda, Septemba 9 katika mechi ya kuwania fainali za Afcon 2019, Kidau alisema imetokana na Kocha kuwa mpya, hivyo alihitaji muda wa kutosha kukaa na wachezaji na kuwalisha mbinu zake.
KISIWA MATATANI
Kutokana na ishu ya wachezaji hao kushindwa kuripoti ilihali taarifa ilitolewa mapema, TFF imeamua kuwatia matatani viongozi wa timu ya Simba, Meneja Richard Robert na Kaimu Katibu Mkuu, Hamis Kisiwa kwani walipokea taarifa yao.
"Tumewaita katika Kamati ya Maadili ili kupata majibu, wao nduo waliopokea wito wa wachezaji hao na tuliwasisitizia wafike asubuhi ya leo (jana) Jumatano."
Alisema nafasi za kina Bocco zitazibwa na Salum Kimenya (Prisons), Paul Ngalema (Lipuli), Ally Abdukadir (Lipuli), David Mwantika, Frank Domayo (Azam), Kelvin Sabato na Salum Kihimbwa (Mtibwa).
KAPOMBE ASHANGAA
Mmoja ya nyota hao wa Simba aliyepigwa 'stop' Stars, Kapombe jana saa 7 alipoulizwa juu ya adhabu hiyo, alisema mbona yeye yupo kambini mapema tu.
"Mimi sijui lolote ila nakwambia nipo hapa kambini", alisema kwa kifupi.
Hata hivyo TFF ilisisitiza hakuna mchezaji atakayepokelewa kwani muda uliotangazwa ukishaisha.
Upande wa nyota wa Azam walishawasili kambini mapema, huku wale wa Yanga wakitarajiwa kuingia mara baada ya kurejea kutoka Rwanda na wale wanaocheza nje watajiunga na wenzao Septemba 4 wakimaliza majukumu ya klabu za
 
LIGI KUU TANZANIA BARA
Ijumaa
Singida United v Mbao (Saa 10:00 jioni)
 
Jumamosi, Sept 01, 2018
Stand United v Biashara United (Saa 10:00 jioni)
Coastal Union v KMC (Saa 10:00 jioni)
Mtibwa Sugar v Mbeya City (Saa 10:00 jioni)
Kagera Sugar v African Lyon (Saa 10:00 jioni)
Prisons v Alliance FC (Saa 10:00 jioni)
 
Jumapili, Sept 02, 2018
JKT Tanzania v Ndanda (Saa 10:00 jioni)
 
Back
Top Bottom