Washawasha
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 16,717
- 13,176
Mitoto ya siku hizi hata haijui hii michezo!Ha ha ha KOMBOLELA, kuna Signature ya mdau mmoja inasema "Butua uwakomboe wenzio" so funny. ila sasahivi sidhani kama hii michezo bado ipo.
kuna mchezo ulikuwa unaitwa malede(kwa wanawake) na nilikuwa napenda sana ule mchezo wa baba na mama au mnachanga hela ikifika ijumaa mnafanya harusi,mnamchagua mmoja wa kike kama bi harusi na wakiume bwana harusi,mnapika pilau mnaimba. hadi raha.
makida makida, au kujipikilisha, kuruka kamba,manakumbuka ule mchezo wa kuzungusha tairi la gari, ukifika msimu wa matairi utakuta kila mtoto anatairi la gari,ukitoka shule huyo unatairi lako,mnafanya mashindano ya kukimbia huku mnazungusha tairi mpaka apatikane mshindi.
au mchezo mwengine wa ringi, unakuwa na ringi la baiskeli,unalifunga kamba, halafu kila unapokwenda unaringi lako,hata ukitumwa dukani.
na unakumbuka ikifika jioni kila mtu kwenda kwao kuna kuwa na kidalo poo, ukalale nacho.
watoto wa uswahilini tulifaidi sana.
asante kwa hii thread, umenikumbusha mbali sana, sana kuna mtu alikuwa anaishi mitaa ya Uwanja wa Taifa humu ndani miaka ya 88-1996 nipe shout.
Mdau hapa ulivyotamka uwanja wa taifa nakumbuka mwaka 1992,Nilitoka Ubungo msewe na mdundiko mpaka uwanja wa taifa ilikuwa balaa hiyo cku sintoisahau kamwe
KULA M'BAKISHIE BABA.........ole wako kijiti kiangukie upande wako hayo magumi utakayopata.
na KIDALI CHA KWENYE MITI;;;;;;;;;watu mnaruka km nyani sasa kimbembe ni pale unaporukia tawi lililokauka:clap2::clap2::clap2:
kuna nn tena zaidi ya hilo?uswahilini raha mkuukombolela mnajificha halafu hamtokei kumbe mnamaliza majambozi mmmh:clap2:
pia kulikuwa na Kisikio poonilikuwa ninapenda KOMBOLELA na KIDALI poo baba yake yan freeesh