Michongo Live

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Wakuu nisiwe mchoyo wa michongo mjini na vijijini.
Leo nimewafungulia Uzi huu wa Michongo Live uzi huu nitatoa michongo mjini na vijijini ili wadau wapate kufaidika.

Mchongo wa Leo
Je, pengine umesoma mambo ya biashara au stationery, au pengine una uzoefu na mambo hayo? Basi fanya hivi.

Fungua biashara ambayo itatoa huduma kama hizi.
~KUSajili kampuni au jina la biashara (Business name ) kupitia mfumo wa Brela online registration biashara yako/ofisi yako toa huduma zifuatazo:

1.kusajili kampuni kupitia Brela online registration kwa ada ya bei nafuu

2.kusajili jina la biashara/Business name

3.updating company na updating Business name/jina la biashara(kwa Kampuni /jina la biashara zilizosajiliwa mfumo wa zaman chini ya mwaka 2018 wanabidi wapate update ili Kampuni yao iingie kwenye mfumo mpya wa online

4.Kufile annual returns Brela kwa kampuni kwenye mfumo wa online

5.kufuatilia kibali cha benki kuu tanzania (bot) kwa kampuni za kukopesha (micro finance company) kulingana na sheria mpya ilitungwa na serikal kuwa huduma ndogo za kifedha kusimamiwa na bot(bank of Tanzania/benki kuu tanzania)

6.Saidia kupata leseni Kwa njia ya online

7.Kutengeneza company profile

8.Kuaandaa Tender document (vitabu vya tenda) kwa Kampuni ili iweze kupata tenda Mbalimbali

9.Kutoa huduma online passport na visa application

10.Kutoa huduma ya work and residence permit kwa foreigners

11.Kutoa huduma ya logo design na website design kwa Kampuni mbalimbali

12.Kutoa ushauri na elimu wa jinsi ya ulipaji kodi tra na elimu ya kampuni na uendeshwaji wake



-Weka njia za Mawasiliano
Kama vile eneo biashara ilipo, namba za simu (SMS, WhatsApp telegram or call), email na mawasiliano mengine.

Huo ni mchongo live siku ya leo, pia mdau unaweza kuweka mchongo wako.
 
Duh poa Sana mze.
Me nipo Moro. kwa mfanyabiashara yeyote wa mazao anaweza niicheki na nikutafutie mazao kutoka kwa Wakulima nk
 
Duh poa Sana mze.
Me nipo Moro. kwa mfanyabiashara yeyote wa mazao anaweza niicheki na nikutafutie mazao kutoka kwa Wakulima nk
πŸ™πŸ™πŸ™ Nazani Watu husika watawasiliana na wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…