Michongo ya kutishana na kuamini ukitokea kwenye umasikini ndio unakuwa kiongozi mzuri inatufelisha

Michongo ya kutishana na kuamini ukitokea kwenye umasikini ndio unakuwa kiongozi mzuri inatufelisha

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Japokuwa sina elimu au ufahamu mkubwa kuhusu ile ishu ya viongozi wa umma kuweka wazi mali zao kwenye mamlaka husika lakini nina uhakika kuna vitu havipo sawa.

Nawaza hivi kweli viongozi wetu wanaandika mali zao wanazomiliki za ukweli TAMISEMI au tunapigwa changa la macho?

Kama vipi tuwe kama Marekani tu, wale wanaowania nafasi za juu hasa Urais lazima uwe vizuri kiuchumi, siyo kama huku kwetu masikini anayewania uongozi ndio anaonekana mtu wa watu, matokeo yake wengi wakiingia kwenye madaraka wanakuwa wezi kuliko hata waliokuwa wezi wenyewe.

Mimi siyo kwamba naona poa kama wanadanganya kuhusu mali zao, lakini naamini jamii ikitengeneza mazingira ya kuwa ukweli ndio unaoheshimika basi hakutakuwa nah ii michongo ya viongozi kuficha mali zao.
 
Nani aliyekwambia kuwa Rais wa Marekani LAZIMA uwe vizuri kiuchumi?

Baada ya kushinda urais kwa awamu ya kwanza, Bill Clinton alisema ya kwamba sasa atakuwa ana uwezo wa kuihudumia familia kwani kabla ya hapo pesa yake ya ugavana haikuweza kukidhi na hivyo kumfanya mkewe Hillary Clinton aliyekuwa mwanasheria kuchangia kwa kiasi kikubwa pesa ya kuhudumja familia.

Unafikiri angelikuwa tajiri angelisema hivyo?
 
Kiongozi aliyetoka kwenye Ufukara huwa anakuwa na Roho mbaya sana na ulimbukeni wa kutisha.
 
Back
Top Bottom