Michuano ya Ndondo cup 2017: Timu ya Misosi Fc Yaibuka mabingwa

Michuano ya Ndondo cup 2017: Timu ya Misosi Fc Yaibuka mabingwa

Thread Starter

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2017
Posts
1,378
Reaction score
1,045
Michuano ya Ndondo Cup msimu wa nne imehitimishwa leo Jumapili August 13, 2017 kwa mchezo wa fainali kati ya Goms United dhidi ya Misosi FC mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Kinesi.


Misosi FC wameibuka mabingwa wapya wa Ndondo baada kuifunga Goms kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya kufungana 1-1 katika dakika 90 za kawaida.


Misosi walianza kupata goli la kuongoza ambalo lilidumu kwa dakika zaidi ya 70 za mchezo lakini Misosi wakasawazisha kwa kutumia makosa ya golikipa wa Goms.


Katika hatua ya changamoto ya penati Misosi wakaichapa Goms kwa jumla ya penati 5-4 na kubeba ndoo ya Ndondo ikiwa ni mara yao ya kwanza.


Mechi ya fainali imeshuhudiwa na Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Tulia Ackson, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi, Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na wadau mbalimbali wa soka.

Misosi wamevuna kitita cha shilingi milioni 10 kwa kuwa mabingwa wa Ndondo Cup huku Goms wakijichukulia shilingi milioni tano baada ya kuwa washindi wa pili wa mashindano.


Habari hii kwa hisani ya Shaffih Dauda

Sent from my Android phone
25b18d9fae356a3b5bbd645a34888fae.jpg

409e24becc82e256c3c02f4738b46a7b.jpg

fe301f83d18697ab4b72f1a94043309f.jpg

5fdc1e7ed675cf1a2f8588a414f61c44.jpg

a9d0e1a7d0cbf926d02abddf642a788d.jpg
 
Yule golikipa mi ningekuwa ni mchezaji wake hakika nisingemvumilia,yani ningeanza kutwangana nae mangumi tu muda huohuo,na sijui yupo ktk hali gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali wandugu.
Misosi fc ni timu inayotoka mtaa gani hapa DSM ?
 
kibada one waliibuka washindi wa 3 kwa kuwafunga keko furniture 3_1

Sent from my Android phone
 
Back
Top Bottom