Michuano ya Ndondo Cup kufanyika Arusha mwishoni mwa wiki

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Mkoani Arusha mwishoni mwa juma hili kunataraji kufanyika michuano ya NDONDO CUP itakayoshirikisha jumla ya timu nane kutoka mkoani hapa.

Lengo la michuano hiyo ni kuwakutanisha wapenda soka mkoa wa Arusha pamoja na kuwapa nafasi wa mashabiki wa mchezo huo Mkoani hapa kukutana sehemu moja.

Michuano hii itaanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa ya tarehe 24/04/2015 na kufika tamati siku ya jumapili.
Mshindi wa kwanza katika michuano hii atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano (500,000) pamoja na kikombe, mshindi wa pili atajipatia fedha taslimu shilingi laki tatu (300,000).

Timu zitakazoshiriki katika michuano ya NDONDO CUP 2015 ni FFU OLJORO, TANZANITE SPORTS FOUNDATION, RED STAR, TANZANITE VETERAN, LEMARA BOYS, NJIRO SPORTS, SMALL NYOTA na UMBRELA GARDEN.

Ratiba katika michuano hiyo ni kama ifuatavyo

FFU OLJORO VS TANZANITE SPORTS CLUB, TANZANITE VETERAN VS RED STAR, LEMARA BOYS VS UMBRELA GARDEN,
NJIRO SPORTS VS SMALL NYOTA.

Michezo yote itapigwa siku ya ijumaa kwa mfumo wa bonanza na nusu fainali itakuwa siku ya jumamosi wakati mchezo ya fainali utapigwa siku ya jumapili.

Michuano hii itafanyika katika uwanja wa AICC uliopo karibu na round about ya KIJENGE. muda ni kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 12 jioni.

Katika michuano hii kutakuwa pia na burudani toka kwa bingwa wa kucheza na baiskeli dunia (BMX CHAMPION) VICK GOMEZ, pamoja na wasanii wa Bongo flava akiwemo G NAKO, CHABA, KINGS, na mchekeshaji KATARINA.

Imetolewa na Akida Kilango – Mratibu wa Mashindano
 
Pamoja sana mkuu.
Fainali hiyo Jumapili itakua saa ngapi?
 
Simba itaanza na ffu oljoro mechi ya ufunguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…