Michuano ya Ubingwa wa Africa: Yanga yapangiwa Timu kutoka Mauritius

Observer

JF HQ
Joined
Oct 18, 2006
Posts
189
Reaction score
299
Mabingwa wa soka wa Tanzania Dar Young Africans wamepangiwa kucheza na timu ya Cerce De Joachim ya Mauritius katika mechi ya kwanza itakochezwa nchini Mauritius

Mshindi wa pambano la yanga atacheza na mshindi wa mechi kati ya Mbambane Swallows ya Swaziland dhidi ya ARP ya Rwanda

Wakati Yanga imepangiwa timu ya Mauritius, timu ya Mafunzo ya Zanzibar itaanza kampeni kwa kumenyana na AFC Vita ya Congo {RDC}. Mechi ya kwanza itaanza Zanzibar

Kwenye kombe la Confederation, timu ya Azam itacheza na mshindi wa mechi ya kati ya timu kutoka Seychelles dhidi ya Bidvest Wits kutoka South Africa.

Azam mechi ya kwanza itaanzia ugenini

JKU ya Zanzibar itacheza na timu kutoka Botswana . JKU itaanzia mechi ya kwanza nyumbani.

*** Jina la timu kutoka Seychelles itakayocheza na Bidvest Wits na Jina la timu kutoka Botswana sikuwa nimeyapata mpaka sasa... yatawekwa yakishapatikana
 
Aisee wana Jangwani mwaka huu tushindwe wenyewe.
 
Mwanzoni mnaanza na vibonde. Baada ya hapo ni Exprance, Raja Casablanca etc hapo ndo Yanga itagota
 
Tena wasidhani hao waliopangwa nao ni vibonde.Mpira umebadilika sana kama mgambo kawavuta.Huko maurtius ndio watapigwa kamoja.Huku watashinda na kuendelea.Yanga bado sana kwa level za kimataifa.
 
YANGA KUANZA NA VIBONDE LIGI YA MABINGWA, WAKIWATOA WANAPEWA NA AL AHLY, AZAM WAPITA BILA JASHO RAUNDI YA AWALI

MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Cercle de Joachim ya Mauritius katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, wakati Azam FC itaanzia Raundi ya Kwanza.
Azam FC itakutana na mshindi kati Bidvest Wits ya Afrika Kusini na wawakilishi wa Shelisheli amabo hawajapatikana.
Yanga itaanzia nyumbani kati Februari 12, 13 na 14 mwakani huku ikimalizia ugenini kati ya Februari 26, 27 na 28 na ikivuka hatua hiyo,
itakutana na mshindi kati ya APR ya Rwanda na Mbabane Swallows ya Swaziland.


Na kama ikivuka tena hatua hiyo, itakutana na Al Ahly ya Misri, au mshindi kati ya Recreativo de Libolo ya Angola na Racing Micomiseng ya Equatorial Guinea.
Azam FC itaanzia kucheza ugenini kati ya Machi 11, 12 na 13 kabla ya kumalizia nyumbani kati ya Machi 18, 19 na 20 na ikivuka mtihani huo, itakutana na ama Esperance ya Tunisia, wawakilishi wa Chad au News Stars de Douala ya Cameroon.
Mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo wataanzia Raundi ya awali na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati JKU itacheza na Gaborone ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.
 
Kwa siasa zetu za mpira sidhani kama tutatobo tena, otherwise ni kawaida yetu kukatwa tukiwa round za chini.
 
Mpira wetu, kabumbu, soccer la Tanzania linachungulia kaburi kwa sababu zifuatazo

1. Kwa muda mrefu tumeshauriwa kuendesha vilabu vyetu hasa vikubwa vya Simba na Yanga kibiashara tumekuwa wagumu kweli kukubali ushauri huo, bado vilabu vyetu vinategemea wafadhili kidogo AZAM wamejikongoja kuendesha soccer la kibiashara.

2. Utawala wa Magufuli umewabana hao wafadhili walipe kodi kumbe walikuwa wanakwepa kodi kwa kisingizio cha kufadhili timu, sina imani imani kama Yusuf Manji, Zakaria Hans Pope na Bakresa wataweza kufadhili timu na kulipa kodi.

3 . Waziri aliyeteuliwa kusimamia michezo ni kimeo hafai kabisa kuwa waziri wa wizara yoyote

Changanya hizo sababu utaona kwamba matumaini ya Soccar letu kukua ni hakuna kabisa, tutaendelea kuangalia nchi za wenzetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…