Hivi sasa kuna tabaka la vijana wanaosoma wakiwa na nia ya kuja kupata ajira za serikali waendeleze wizi wa baba zao,kuna program ambazo ndo zina hela,kwa maana ya nafasi ya kukwapua na kujilimbikizia mali,hili Taifa halitategemea wasomi tena,kwa sababu ndio walioliangusha,ndio waliotufikisha hapa tulipo,kuna kizazi cha wafanyabiashara kinaibuka,hiko ndicho kitakomboa Taifa letu,kwa kuwekeza hapa nchini wakati wasomi tunaowaamini na kuwapa vitengo nyeti wakiiba mali ya umma na kwenda kuficha kwenye akaunti zao za nje ya nchi badala ya kuwekeza nchini,nakerwa na wasomi wa aina hii.