Mmeku Tukulu
Member
- Feb 11, 2012
- 92
- 27
Kama tutakuwa wagombea wenye elimu na busara kama Slaa as opposed to Kiwete type hili ni jambo bora. Kikwete hakukimbia mdahalo. Jamani mlitegemea Kikwete aseme nini kwenye jambo kama hili linalotaka weledi na seriousness? Laiti ingekuwa kuandaa kutembelea misiba badala ya midahalo hapa CCM wangekuja kwa nguvu zote na Kikwete angeibuka mshindi. Je watakufa akina Kanumba wangapi ili Kikwete apate sehemu ya kuonyesha "ujuzi" wake?
Je? Tutaendelea kuwa na viongozi wanaogopa kuongea na kuhojiwa na wananchi wao hadi lini? Tutaendelea kusikiliza kampeni zenye ahadi hewa zisizo hojiwa hadi lini? Tutaendelea kupiga kura kwa kufuata propaganda na kauli mbiu za kiualinacha hadi lini?
Katika uchaguzi 2010 Tanzania
tulishuhudia CCM wakiikimbia midahalo
iliyokuwa inaendeshwa TBC na hata
kuwakataza wagombea wao kushiriki.
Midahalo hii ni fursa muhimu kwa
wananchi na upatikanaji wa viongozi bora.
Wana jamii mnaonaje swala hili lisiwe tena
la kihiyari bali la lazima na liwekwe
kwenye katiba?