I
Karatasi ya thamani ni pesa vyeti ni uchafu chochote utakacho pesa kwanza
Silali kitandani nakesha kuziseti chafu tatu popote niendapo pesa kwanza
“Babu hilo goma linanitia stimu yaani siku mimi nikija kubutua kudadekilazima nipitena wema ” Suma alikuwa anatoa maoni yake baada ya kuonekana kuguswa sana na wimbo uliokuwa ukichezwa kwenye redio ndogo inayotumia “flash disk” kuchezea nyimbo. “Mhh Wema tena hahaha babu hebu malizia kushi halafu kalale” Nguzo aliyekuwa akijishughulisha ‘kunyonga kushi’ akawa anamwambia Suma huku akicheka kicheko cha kivivu.
“Oya Mido ubao unaeleweka au ndo tia maji tia maji” Nguzo alimgeukia Mido akimuulizia mwenendo wa uchangiaji wa watu kwenye kampeni yao isiyo rasmi ya kuipa nguvu timu yao ya mtaa. Baada ya ‘kushi’ kufikia uelekeo wa Mido akaikamata sawia kabisa kama mtu aliyeingojea kwa kitambo kidogo akaielekeza moja kwa moja kwenye papi zake za midomo na kuvuta pafu kadhaa kisha naye akaipitisha kwa wengine.
Ndani ya sekunde kadhaa za kuisikilizia kushi Mido huku akiwa ameegemeza mikono yake kwenye magoti yake akamgeukia Nguzo , “Faza watu hapa kiskani wanaleta ugaigai mwingi, kuna watoto hao ukiwaachia kitengo yaani ni kama umempa ajira” akaweka kituo kisha akaendelea “Madogo wanashindwa kuelewa kuwa hili suala ni la kifamilia, wao wanajiangalia wao tu. Mtu unamwambia kibingwa tu oya kaba goli halafu yeye anageuza pale ndo kitega uchumi chake, yaani sisi tunamwamini mwana ila yeye anahamisha magoli anaenda kuhonga chura wake, oya wanangu tutazinguana” Nguzo akadakia mazungumzo ya Mido na kuuliza kwa hamaki “Oi Mido nani huyo analeta pigo za kishamba?” Mido alivyopokea lile swali la ghafla akakaza macho mbele yake akimwangalia kwa ghadhabu sana mmoja wa jamaa zake waliopo hapo “Huyu mtoto Maestro mshamba sana huyu.”
Watu wote wakaelekeza macho yao kwa kwa Maestro, Mido akamgeukia jamaa yake mwingine na kumuunganisha kwenye hiyo shutuma “We nawe unakodoa nini?, jana si niliwaacha wewe pamoja na Maestro mlinde goli pamoja mbona unajifanya huelewi wakati wote walewale tu?” Jamaa baada ya kuona ameunganishwa kwenye hiyo shutuma bila kutarajia akawa ametamaushwa ghafla sana “Daah kaka mkubwa sasa hapo unafeli, sasa mimi naingiaje hapo?” Nguzo akadakia “Janja tulia hivyo hivyo usomewe kesi, mikato yako naielewa vizuri yaani, mdogo wangu Sufi una tamaa sana nakujua kinoma kwahiyo mambo kama haya yakiongelewa wala sishangai”
Sufiani baada ya kuona shutuma zimehamia kwake kutoka kwa maestro akataka kujitetea ili ajinasue na huo mzigo wa lawama “Sema mabroo mnazingua ujue kusema vitu ambavyo havipo” Ni kama Maestro alikuwa anangojea kwa hamu sapoti ya utetezi ili naye ajitetee, akajiweka sawa ili naye aseme yaliyoandaliwa kwenye kichwa chake “Mi ndo nashangaa hapa wanangu wote hapa zigo la mavi mmeniangushia mimi, kwa sababu mimi sijachukua mbuni nyekundu na najua watu wananiona mimi kama nimechukua hela kwa sababu mzigo umeongezeka kidogo” Utetezi wa Maestro ni kama haukumridhisha Mido ndipo akazidi kushikilia hoja yake “Hapo mi ndo nashindwa kuelewa yaani kwanini ukikaa wewe golini mzigo hautembei ila tukikaa wengine chati inapanda?” Nguzo baada ya kuona mjadala umekuwa mkubwa ikabidi aingilie kati ili kuua mzozo, akapiga pafu kadhaa za kushi baada ya zamu yake kufika, halafu ikabidi sasa na yeye aseme kitu kuepusha shari “Sema nini mwanangu Mido huyu janja kweli mi namsoma pigo zake ila ‘sometime’ tunatofautiana ujue kwenye mitikasi kama hii, mimi na wewe kila mtu anaijua amshaamsha yako na yangu kwahiyo labda ndo maana chati ilikuwa inasoma sana na huyu janja na mwenzake hawana maajabu sana kwahiyo tusiwalamu au vipi mzee” Ni kama Nguzo alikuwa anangojea jibu au muitikio wowote kutoka kwa Mido lakini Mido akawa ametulia tuli. Nguzo alivyoona Mido hajamjibu akawageukia Maestro na Sufiani “Sema wadogo zangu kama kuna michezo mnaifanya tutawafanyia kitu kibaya mjue wakati mwingine, yaani hapa ni kama tume’assume’ hakuna kilichotokea” Sufiani akadakia akitaka hata kidogo wasihushwe na hizo shutuma “Sema mabroo hapo ndo mnazingua yaani kutusingizia mazima yaani…” Kabla hajamaliza sentensi yake Nguzo akamkatisha na kumfokea “Dogo halafu nikiwa natoa speech yangu sitaki unipinge, we tulia usomewe kesi kama umefanya acha kama hujafanya ndo usijaribu kabisa, haya.”
Karipio la Nguzo kwa Sufiani ni kama lilileta utulivu uliopotea kwa muda kidogo kwenye maeneo hayo na kila mtu akarudi katika hali yake ya kawaida ndipo Nguzo alipochukua nafasi hii na kuanza kuwashirikisha mkakati mpya ni kwa jinsi gani ‘Harambee’ yao ifanye kazi kama walivyotarajia. “Sikieni wanangu jumamosi ndo mbungi inagongwa halafu tulichopata ni jau, hebu tushauriane ndo tunafanyaje sasa maana tunahitaji maji, glukozi na kibati cha kuwaamsha wana hapo kitaa si unajua chura bila haya mambo hawaji” Nguzo akatoa mawazo yake huku akisikilizia na wengine kama kuna chochote cha kuongezea kwenye yale maoni aliyowasilisha.
Maestro alipoona Nguzo ametoa nafasi kwa wengine kusema chochote naye akachukua hiyo nafasi kusema chochote huku akichukua mkono wake wa kulia na kuupitisha chini ya vesti yake na kuanza kukuna mbavu za upande wake wa kushoto “Mi naona hapa ili kuepusha lawama wote tukae kitengo ili kila mtu ashuhudie kinachopatikana, maana hii ya kauchiana ndo inaleta magumashi kwa sababu kila mtu ana matarajio yake wakati hela zenyewe hizi za ku’force’ kingi watu ndo wanachukulia kama ndo ‘siriaz’ basi hapo ndo tumemaliza aah”
“Sasa mdogo wangu hayo mabango” Mido aling’aka maana alihisi ni kama alikuwa analengwa yeye. “Kwahiyo tusiseme sasa?, kwa sababu watu akili zao wamezaliza hapa kwenye donee tu” Sufiani naye akadakia akiunga mkono hoja ya Maestro. “Halafu we dogo una hamu sana nitakuvuruga muda siyo mrefu” Mido alihamaki na ghafla akasimama kuelekea upande aliopo Sufiani, na Sufiani alipoona ni kama anaenda kukabiliwa naye kwenye kujihami akasimama ghafla ili kikabiliana na Mido “Oya Mido mi nakuheshimu kama broo lakini usinitishe nakuambia,mi nakumudu vizuri tu” Kusikia kauli hiyo Mido kifua kikatokota ghafla sana na kwa haraka mno akataka kurusha ngumi lakini kabla haijafika popote Ngozi akamuwahi Mido na kumdhibiti kwa nyuma asifanye chochote “Oya acha mambo ya kitoto mwanangu, sasa hapo vitu vya kutaka kupigania viko wapi na huyo dogo?” huku akiwa kadhibitiwa vilevile Mido ni kama alikatiliwa kuonesha umwamba wake “Madogo wana dharau sana hawa acha nimkaribishe kiskani ili ajue nani ni wandewa hapa, fala sana huyu dogo” Sufiani akaamua kuwa mpole akishuuhudia jinsi ile hali ya Mido na Ngozi ikiendelea. “Tatizo mdogo wangu unachonga sana halafu kila mara mi nakwambia jiangalie” Sufiani akona ajitetee “Kosa langu liko wapi sasa hapo?” “Kula kobisi basi” Ngozi alimsistitiza Sufiani. Ukapita muda kidogo kila mtu akawa kimya
Suma aliyekuwa kimya muda mwingi akisikiliza jinsi wenzie wakizozana na kushutumiana hatimaye naye akavunja ukimya katikati ya mazungumzo yao “Oya wanangu nani ana karata tukate?” akauliza swali lililo na maoni ndani yake huku akimuangalia mmoja baada ya mwingine. Kila mtu baada ya kusikia Suma alichokisema akaanza kusonya na mmoja baada ya mwingine akachukua uelekeo wake wakimuacha peke yake kwenye hivyo viunga.
“Ankoli uko poa!?” Mido alitoa salamu kwa mwanaume mmoja mwembamba mwenye muonekano wa nusu kijana nusu mzee ambaye kwa wakati huo alikuwa ametingwa na shughuli kadhaa za hapa na pale, bila kusikia salamu aliyopewa aliendelea na shughuli zake kabla ya ghafla kushtuliwa na sauti moja iliyojaa fujo maeneo hayo “Oya ankoli eeh mpwa wako nakusalimia halafu unanichunia, dharau au” alivyogeuka akamuona Mido akiwa anaendelea kutabasamu huku akiwa anaangalia ueleko aliopo yeye “Aaah kunyangisi wewe mtoto, ujue umenishtua eeh” alihamaki huku akihoji katika hali ya taharuki ndogo.
Mido alivyoona vile akaangua kicheko cha dhihaka “Tatizo mzee kila siku nakwambia nenda kaliondoe hilo dude wewe unaling’ang’ania utadhani ni tambiko lako au ndo kizizi chako?” huyo mwanaume alivyosikia hivyo naye akatabasamu huku akionesha kusikikitika baada ya kusikia hayo maneno. “Muulize Shangazi yako nimelitoa au bado lipo?” Mido alitupiwa swali “Aaah weeh shangazi yangu utamfanya nini wewe nyuki wa mashineni” alijibu kwa kejeli, “Lofa kweli waulize vizuri shangazi zako nilikuwa nawafanyaje shule ya Msingi Rutihinda watakusimulia, unanichukulia poa eeh!? Mak*lio wewe” Mido akaangua kicheko kikali, “We jichekeshe tu kama Malaya kaona danga jipya”
”We ba mbiki hebu tufungie basi hizo nyanya chungu sisi tuondoke jamani, yaani nyie waluguru mkishakutana ni shida tupu kelele mtindo mmoja” mwanamke mmoja wa makamo aliyevalia kitenge tupu kilichopitishwa juu ya kifua chake akayaingilia yale mazungumzo ya wale wawili akihitaji kupewa alichokuwa anakitaka kwa haraka. “Si huyu mtoto anafanya hadi nasahau wateja wangu, nakufungia mama yangu” Ba mbiki alijitetea, huku akibetua mdomo wake Yule mama naye akazidi kusisitiza “Fanya haraka unatuchelewesha au mnataka tuachike?” Ba Mbiki huku akiweka bidhaa kwa mteja wake akazidi kunogesha yale mazungumzo “Hamna bwana huwezi kuachika, haya huu hapa mzigo wake” Yule mama akaishia zake
Mido alipoona yule bi mkubwa ameshatokomea akamkaribia Ba Mbiki na kupenyeza jambo lake, “Sasa ankoli mi sielewi leo mpwa wako hebu nifanyie mafekeche mwanao leo niishi maana nimevurugwa kweli.” Ba Mbiki alimuangalia kwa muda Mido halafu akacheka upande huku akitikisa kichwa chake “Mi nilijua tu mbwembwe zote zile kunioshea kwa akina mama hapa mwisho wake utavaa mtandio tu fala wee, haya unataka nini leo na sikukopeshi nakauhonga kabisa mbuzi maji we” Mido aliishia kutabasamu tu “Sema haraka we mwari” Ba Mbiki alizidi kumnanga Mido. Mido alitandaza mikono yake kwenye meza ya genge na kuanza kuchagua alichokuwa anahitaji alipojiridhisha akaweka weka pembeni “Mjomba ni hivi tu kwa leo” Mido alimuambia Ba Mbiki “Kwahiyo hapa na hivi vya leo utakuwa unanidai shilingi ngapi?” akasindikizia na swali “We kama umejisahaulisha mi nakulipia tu” ba Mbiki akamjibu kwa dhihaka “Halafu mjomba unajikuta mende sana wewe, we subiria tu siku nikipiga mshindo hapa lazima nikuaibishe” mi naenda. Ba Mbiki akamuangalia Mido halafu akawa anacheka “We fala leo nimekuweza hahaha” huku akainza kupga hatua kadhaa Mido akamjibu kwa kisirani Ba Mbiki “Kwenda zako huko halafu we mzee kavu sana”
Akiwa anarudi ghetoni kwake taratibu lundo la mawazo likawa linapita kichwani mwake akitafakari ni kwa namna gani anaweza kupambana ili akabiliane na changamoto kadhaa alizonazo. Bila kutarajia akawa ameufikia uwanja wa maeneo ya hapo anapoishi. Akwasalimia watoto waliopo hapo nao kwa bashasha wakamuitikia huku wakimfata alipo na kuanza kumzingira, “Anko Mido naomba zawadi yangu” mtoto mmoja akimshtukiza Mido kwa hilo hitaji la ghafla, “Kwanza mtu mwenyewe hujui kusoma unataka zawadi ya nini?”
“Anko mi najua sasa hivi kusoma” Yule mtoto alijitetea. Kabla hajaendelea zaidi kujitetea mtoto mwingine akaingilia yale maongezi “Muongo! huyo hata hajui kusoma anko hadi mdogo wangu anampita hahaha!, anko nipe mimi tu zawadi” Mido akatasamu kichovu halafu akamwambia huyu mtoto wa pili “Na wewe nilikuambia ukiacha tu tabia yako ya kubana (utoro) basi lazima nikupe zawadi” yule mtoto akajibu kwa shauku “Mi anko mbona sikuhizi ‘sibani’ kila siku ‘naendaga’ shule” Naye mtoto wa kwanza akadakia “Anko huyu muongo kila siku wanashindaga michumvini kuogelea na wenzake, mi ‘namwambiaga, anakataa”
“Kaaaaaaaahhhhh! Unanisingiziaa” mtoto wa pili alijitetea kinyonge “Anko kweli tena mi sidanganyi hata juzi alisemelewa na monita akachapwa na mwalimu wa mwandiko” Mido aliyafurahia yale mabishano kati ya watoto wale wawiil halafu akawaambia “Haya halafu wote siwapi maana hapa mmoja ni mzembe hajui kusoma na mwingine ni mbanaji wa shule” wale watoto walivyosikia hivyo wakanyong’onyea na Mido akajisukuma mdogo mdogo hadi ndani kwake akaliangalia geto lake kwa sekunde kadhaa lilivyokosa mpangilio. Pembeni ya ukuta wa moja ya kuta za chumba kulia mwa mlangoni wakati anaingia vyombo kadhaa vilivyokosa kuoshwa baada ya kutumika vikawa vinamzomea, akahisi ana kibarua tena cha kuvisafisha uvivu ukamvaa akaelekea kwenye moja ya kona ya karibu yake ya chumba chake na kuvibwaga vitu alivyotoka navyo gengeni kisha akajitupa kwenye godoro jembamba lililochoka na kuhitaji kustaafishwa baada ya huduma ya malazi iliyotoa muda kidogo. Katikati ya tafakari akapitiwa na usingizi.
“Mbona Mido na Suma siwaoni? Na Godi, Fure nao wako wapi?”
ITAENDELEA....
Like yako muhimu,
Maoni yako muhimu