Wazaramo wasomi wanasemaga “When an apprentice graduates, the master will show up”
Hizi hekaheka sio bure, kuna mkubwa wao bado hajajitokeza, haiwezekani hawana hata Cognitive dissonance, tena kipindi ambacho Mtunzakiti wao anasota rumande na kesi ya uhaini.
Hawa
Wahamachama hawana jeuri ya kufanya hivyo kipindi kama hiki ambacho usaliti wa chama unahesabika kama usaliti kwa taifa, lazima kuna aliye na kiti mwengine anayewaongoza, na mwenye hicho kiti ni mtu mwenye ushawishi sana ndani ya chama kiasi kwamba amewapa huu uthubutu wa kusaliti upinzani wa kweli kwa hivyo vipande Shekeli bila ya nafsi kuwasuta hata kidogo.
Mtoto akiona baba anafanya jambo baya, na yeye hatoona ubaya wa jambo hilo… Narudia tena
Mwanafunzi akihitimu mkufunzi hujitokeza
Kuna aliyekuwa na kiti na sasa anakitunza kiti hiko kama mtunzaji kivuli bado hajajitokeza, na hili dili la kwenda Ubwabwa kuna kila uwezekano yeye ndiye amelidalalia. Zipo za chini kabisa Wanyetishaji wanadai
Mkingamwili wa Mtunzakiti kivuli alikuwepo huko Ubwabwani
😎
Yani mmekubali kiurahisi kabisa kwamba kwenye orodha ile ya
Wahamachama, kuna mwenye uwezo wa kukaa mezani na
Wauza mchicha kisha awashawishi kiasi cha kufikia hatua ya kutoa nyama? Narudia tena bado Mkufunzi hajajitokeza yupo pahala anaangalia hali ya hewa, ikiruhusu atatokea.
Angalizo tu kwa Wahamachama, wauza Wauza mchicha wananjaa kiasi kwamba. wameaza Ukanibali, huko kwao Watoto hawachezi mbali na nyumbani,
Watu wa Mumiani wamehamia kwao, sasahivi hadi wenyewe kwa wenyewe wanaogopana…
Wauza mchicha wamezoea udhulmati hata wenyewe kwa wenyewe, sembuse nyie watu baki? Eti Wanadhani wanaweza kupewa nyama na Wauza mchicha. Niwaambie tu, sisi bana tumepewa subra, tupo paleee tunasubiri mdunde mindundo yenu tuwacheke mwishoni.