MIF & Care International Tanzania Wazindua Young Women Leadership Program

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MIF & CARE INTERNATIONAL TANZANIA WAZINDUA YOUNG WOMEN LEADERSHIP PROGRAM

Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (Mb) kwa kushirikiana na Care International Tanzania wamezindua mradi maalum wa kuwawezesha wanawake vijana kwenye uongozi (Young Women Leadership Program).

Mradi wa Young Women Leadership Program unatumia mbinu mbalimbali za mafunzo ya ana kwa ana na mtandaoni, pamoja na programu ya ushauri wa karibu (mentorship program) ili kuwajengea ujuzi na kuimarisha uwezo wao wa kuongoza.

Uzinduzi huu umehudhuriwa na wageni mashuhuri akiwemo Mhe. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Tanzania, Mh. Riziki Pembe, Waziri wa Wanawake na Jinsia Zanzibar, Getrude Mongera kama Mgeni wa Heshima, na Mhe. Wanu Ameir Hafidh, Mwenyekiti wa MIF.

Mradi wa Young Women Leadership Program utawanufaisha wanawake vijana 50 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, ukilenga kuwapa fursa za kujifunza, kujiamini na kushika nafasi za uongozi.

Ikumbukwe, takwimu zinaonesha kuwa bado kuna changamoto kubwa katika ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi na maamuzi. Pamoja na uwakilishi wa wanawake bungeni kuwa ni kati ya 36% - 37%, lakini katika ngazi za serikali za mitaa, bado ni mdogo zaidi.

Katika sekta binafsi, ni 20% tu ya wanawake wanaoshikilia nafasi za juu za uongozi huku bado kuna misingi hasi ya kimila na kitamaduni inayoendelea kuwa kikwazo kikubwa kwa wanawake kushiriki kikamilifu katika vyombo vya kutoa maamuzi, siasa, na nafasi za uongozi maendeleo ya uchumi.
 

Attachments

  • Screenshot 2025-02-12 at 00-43-28 Instagram.png
    828.3 KB · Views: 1
  • Gjg49xgXoAA92Qk.jpg
    374.1 KB · Views: 1
  • Gjg491CXMAA33j3.jpg
    415 KB · Views: 1
  • Gjg495JWAAA1BlY.jpg
    384.9 KB · Views: 1
  • Gjg4_GwXQAAg8Vv.jpg
    468.9 KB · Views: 1
  • GjgysRsXwAAw10r.jpg
    281.4 KB · Views: 2
  • GjgysRqWUAAq78g.jpg
    476 KB · Views: 2
  • GjgysRpWgAAlpT2.jpg
    400.2 KB · Views: 1
  • GjgysVYXMAADvi7.jpg
    489.2 KB · Views: 2
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…