Mifugo ipo lakini ngozi hazipo

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Uwepo wa ng'ombe wengi ulinishawishi kutaka kujenga kiwanda cha viatu lakini nilipochunguza malighafi nikakuta kumbe ngozi zetu nyingi hazifai kwa kazi hiyo, labda kwa mikanda tu ya suruali. Wafugaji wetu wanazalisha ngozi zisizo na ubora unaotakiwa. Wanaweka alama na kuichapa viboko mifugo yao ovyo bila kuzingatia kazi za ngozi.

Ngozi zetu zina makovu mengi mno zinazofaa kwa kulalia tu na kuanikia tumbaku juani likauke vizuri.

Tunaongoza Kwa kuwa na ng'ombe wengi wasiokuwa na maziwa wala ngozi



Kazi bado ipo kuelekea Tanzania ya viwanda.
 
Sasa tufanyeje ili tuweze kutembea kifua mbepe??
 
Tatizo hili halitaisha mpaka iwekwe adhabu kali
Yaani hatuendi bila fimbo kama wanavyowachapa mifugo
 
So, nini kifanyike? Tufanyeje kuweza kuzalisha ngozi safi na zinazofaa kwa matumizi ya bidhaa mbalimbali za ngozi?
 
So, nini kifanyike? Tufanyeje kuweza kuzalisha ngozi safi na zinazofaa kwa matumizi ya bidhaa mbalimbali za ngozi?
Itangazwe bei kubwa ya ngozi bora. Wataalam wetu watoe elimu ya namna ya kuzalisha mifugo yenye hiyo ngozi bora.
 
Ethiopia kuna ng'ombe wengi na viatu vingi vya ngozi Yao vipo vingi Sana kila kona. Sisi tunashindwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…