Tetesi: Mifuko ya hifadhi ya jamii kwa Watumishi kubakizwa miwili

Nilimsikia akiongea na itapelekwa bungeni
 
Mimi binafsi nitafurahi sana ikiunganishwa, kuna watu wangu wa karibu nawajua wanateseka sana kwa manyanyaso ya mfuko mmoja siutaji ila ni jambo jema.
Katika mifuko hii pia imekuwa km kichaka cha kujificha....
Probably itakuwa ni ppf! Huu mfuko umekaa kihuni mno! Kuna kampuni moja kubwa huko arusha ambayo wafanyakazi wake wanalazimishwa kujiunga ppf tu! Halafu sasa fedha wanazokatwa zinatumika kuwakopesha kwa riba kubwa ya 30%! Dhamana ni akiba yako ya ppf, na unapoacha au kuachishwa kazi basi tajiri ana uwezo wa kukukata direct kutoka kwenye hifadhi yako maana pia yeye ndiye anayekulipa ppf yako! Yaani hadi penalties nyingine kama za low performance zinakatwa kwenye ppf yako! Sasa unashindwa kujua kama huo mfuko ni wa tajiri(mmiliki wa kampuni) au serikali?
 
Pale kemia ya maganda ya korosho inapogeuka sayansi ya uchumi[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Huo mpango wa kitambo sana na hii ni serikali kutaka kukontrol hizi pesa za mifuko ya hifadhi
 
Nawezaje kukopa pesa walau kidogo pspf, mimi ni daktari nina miezi 6 kazin
 
Hakuna haja ya kua na utitiri wa mifuko ya hifadhi ya jamii wakati yao kazi ni ile ile ya kutoa mafao mbali mbali na pensheni, hata hii mifuko ya afya ya jamii yote ijumuishwe kwenye huo mfuko mmoja mkubwa, tuokoe mishahara kwa kulipa utitiri wa wakurugenzi
 
kwa mawazo yangu naona ni sawa ili kupunguza gharama nyingi za uendeshaji bora kuwe na mifuko michache yenye tija
 
Ushindani ni muhimu sana, sasa serikali itakusanya pesa vizuri ila huduma kwa wafanyakazi na vile vibonus sijui mafao ya uzazi na mikopo ya kuanzia maisha wasahau.
Hivi uliwaza nini hadi ukachagua hiyo avatar, thought shapes reality, hiyo avatar inaakisi jinsi ubongo wako unavyofanya kazi
 
Twafaaa hao staff watawapeleka wapi
Walikuwa wanakula mishahara ya bure tu, walikuwa wanafanya duplicate jobs, kazi ya kufanywa na mfuko mmoja inafanywa na mifuko 10, that is a wastage of resources!
 
Itaua ufanisi pamoja na uendeshaji wa mifuko kwa ubora kuunganusha mifuko kuwa mmoja ni ishara ya kuifanya kuwa kama wizara kitu ambacho kitatufanya turud tulikotoka! Last suala la kuunganisha linahitaji critical negotiations especially kwa maeneo na mikataba ilivyoingia!
 
Walikuwa wanakula mishahara ya bure tu, walikuwa wanafanya duplicate jobs, kazi ya kufanywa na mfuko mmoja inafanywa na mifuko 10, that is a wastage of resources!
ila ni njia ya ku create emplyment mkuu tuangalie wana familia
 
Itaongeza ufanisi na punguza garama.Tuangalie mashirika mengine pia yaunganishwe kupunguza dublication na garama.
 
ila ni njia ya ku create emplyment mkuu tuangalie wana familia
Watu hawajui tu. Kuajiri watu wengi kunafanya mzunguko wa pesa uwe mkubwa na kukuza uchumi. Serikali ikiiajiri watu wachache ni mbaya kwa uchumi tofauti na shirika binafsi.
 
Itaongeza ufanisi na punguza garama.Tuangalie mashirika mengine pia yaunganishwe kupunguza dublication na garama.

Serikali sio Profit oriented ni Service oriented
 
Hizo tetesi ni za kweli kabisa.
Ni suala la muda tu, kuna mswaada wa dharula wa marekebisho sheria ya mifuko ya jamii utapekwa bungeni wakati wowote ili kukidhi hilo takwa la rais.

Hatua hiyo itakuwa ni nafuu kwa serikali ili kupunguza gharama za uendeshaji LAKINI ni hasara kubwa kwa wafanyakazi na ni janga kwa taifa.
 
Umbea wa kiwango cha makinikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…