joanesbiitajohn
New Member
- Jun 7, 2024
- 1
- 0
1.Tausi -Portal Tausi -core
2. RITA
3. EGA
4. BIMA
5. KULAZA WAGONJWA HOSPITALI -Private - Goverment
6. UHAMIHAJI -Passport Visa
7. NIDA
8. MIFUMO YA KUHAMISHA WATUMISHI
9. MIFUMO YA MAHAKAMA
10. MAOMBI YA MIKOPO HESLB
Maana ya mfumo
Mfumo ni utaratibu wa ukusanyaji na uchakataji wa taarifa ili kuweza kuzifikisha mahali sahihi.
Ifuatayo ni mifumo kumi muhimu Tanzania ambayo inakuwa changamoto na kutesa raia
1. (a)Tausi portal- Huu ni mfumo ambao mteja usajiliwa na kuweza kuomba mwenyewe control namba za malipo ya serikali ya vitu mbalimbali mfano malipo ya Kodi za vibanda,ardhi,nyumbani n.k.
Mfumo huu umekumbwa na changamoto zifuatazo:-
Mtandao kusuasua mara kwa mara
Watumiaji wengi kutokupewa elimu ya kutosha juu ya mfumo huu
Utatuzi wa changamoto nashauri uwe hivi
Wataalamu wa TEHAMA watoe mafunzo kwa raia na watumiaji wake.
Serikali izidi kuboresha huduma za internet kwani vijijini bado ni shida.
(b) Tausi core-Huu ni mfumo ambao hutumiwa na serikali katika kutoa,kukagua,kuandaa malipo yaliyofanyika kwa control namba, zikiwa bili zote za serikali hasa serikali za mitaa(local government)

Baadhi ya malipo kujirudia mara mbili au control namba kujidouble..
Mfumo kuwa chini mara kwa mara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji
Mara nyingi mfumo huu unategemea umeme na siku zote umeme hautegemeki hukatika mara kwa mara, mteja huweza kusubiri hadi wiki ili ahudumiwe
Utatuzi wa changamoto hizo uwe kama ifuatavyo
Serikali iongeze wataalamu wa TEHAMA ili kuweza kusaidia mtandao kukaa sawa.
Miundombinu ya umeme na mitambo mingine ya mitandao iboreshwe.
2. Ajira portal -Huu ni mfumo wa kuomba kazi tamisemi mfumo huu hubagua baadhi ya data au maombi ya watumiaji lakini pia haupokei taarifa zote muhimu huchukua taarifa chache zilizosetiwa.

Mfumo huu huumiza watanzania wengi na ni wachache wanaonufaika na mfumo huu.
Lakini pia hata ukiitwa kwenye usaili unaweza ambiwa taarifa ulizoleta sio sahihi
Utatuzi wa changamoto hizo uwe kama ifuatavyo:-
Mfumo huu urudiwe upya na wataalamu wetu ili uweze kuwa rafiki kwa watumiaji
Bado baadhi ya halmashauri nchini ziko na upendeleo hivyo maombi yatumwe moja kwa moja kwa katibu wa ajira utaratibu wote ukamilike Dodoma.
3. RITA
Huu nimfumo wa usajili wa vizazi na vifo Tanzania ambazo mteja ujisajili na kuweza kuomba vitu vifuatavyo cheti cha kuzaliwa,cha ndoa,cha kifo na wosia.
Changamoto za mfumo huu ni kama ifuatavyo:-
Asilimia ya wanaoomba kupitia mfumo huu hawajibiwi na sasa hivi ofisi nyingi Tanzania wanakuambia uombe kupitia mfumo wao, sasa mamlaka husika naomba zitujibu kwanini baadhi ya watumiaji hawapati wanachohotaji
Huduma muhimu hazipatikani kwani wanakuambia pitia RITA
(4) BIMA
BIMA ni dhamana ambayo huwekwa ili ije ikusaidie baadae.Bima nyingi Tanzania ikiwa ni ya afya magari au nyumba zinaonekana zinategemea sana taarifa za RITA au NIDA ambavyo navyo vina changamoto kubwa. ,hivyo mteja au mtumiaji hubaki njiani pale anapoambiwa nenda huku nenda kule ili aweze kuhudumiwa.
Utatuzi wake
Mamlaka za BIMA zote ziwe na uwezo wa kujiamulia wenyewe na kutoa huduma sahihi.
(5) MFUMO WA KULAZA WAGONJWA HOSPITALI ZIWE BINAFSI AU ZA SERIKALI
Katika mfumo huu naomba wizara ya afya ije na usaidizi mkubwa wa tatizo ilo kwani mgonjwa hulazwa peke yake hospitalini kuna faida gani wakati msaidizi wake yupo yamkini hata kama ni kulala macho yupo tayari mwishowe mgonjwa kukaa peke yake na wengine hudondoka na kupoteza maisha madaktari wengine ni mashuhuda wa hili. Na wengine ndugu uliona hilo na kukosa mahala pa kushtaki.
Utatuzi wa changamoto hii
Mamlaka husika kuangalia juu ya umuhimu wa kuwa wanamruhusu msaidizi wa mgonjwa ili kuweza kupunguza vifo visivyotarajiwa.
6. UHAMIHAJI
Hapa katika mamlaka hii mifumo ya kuomba passport,visa imejaa changamoto nyingi kwani bado taarifa zote ili uweze kuziingiza zinahitaji malipo kwa wataalamu wa TEHAMA. Mfumo wa uhamihaji nao hutegemea taarifa kutokea NIDA, RITA.
Bado kunakuwepo na tatizo la mamlaka Moja kutegemea mamlaka nyingine inakuwa usumbufu kwa watumiaji na wengi wao huishia kukosa huduma.
Wito wangu naomba mamlaka husika kuangalia upya mifumo ili kuweza kutoa huduma Bora.
(7) NIDA
Mfumo wa taifa wa utambuzi wa namba au uraia kwa watanzania bado umekumbwa na changamoto lukuki kwani mpaka sasa kuna watanzania wengi wanahangaika kupata namba ya utaifa lakini mfumo unawakataa ilihali ni watanzania wenzetu
-Wito wangu naziomba mamlaka husika kujitahidi kuwafikia hao watanzania walio wengi wanateseka.
(8) MAOMBI YA MIKOPO KWA WANAFUNZI
Katika mfumo huu kweli umeghubikwa na changamoto lukuki kwani walengwa wengi wapo nje na hawapati huduma hii muhimu na kusababisha wanafunzi wengi kukaa makwao na kushindwa kuendelea na masomo.Kuna tatizo la kinfumo au basi kutakuwepo na connection maana watoto wa vigogo wanapata mikopo lakini watoto wa maskini hukosa.
Naomba mamlaka husika kupitia wizara ya elimu kuliangalia upya na ikiwezekana watume wataalamu kubaini ukweli huu.
(9) MFUMO WA KUHAMISHA KITUO CHA KAZI KWENDA KINGINE
Ni haki ya mtumishi yeyote kuhama kutokea kituo kimoja kwenda kingine lakini kwa Tanzania imekuwa maumivu na kuacha donda kwa watumishi wengi kushindwa kuhama kwani hukutana na vikwazo vingi na wengine uhamisho hufanyika pasipo malipo.
Mwisho naitimisha na kutaarifu kuwa mifumo hii inachangamoto rukuki naomba mamlaka husika Kila kada, wizara na taasisi husika kutambua Bado mifumo hii haijaka sawa katika kukamilisha zoezi zima la ukusanyaji wa data. Wakae chini na wataalamu wa software zote na kuweza kuunganisha utaratibu uwe sawasawa.
Andiko langu Joanes Biita John ..... mdau wa maendeleo

Upvote
1