“Niliingia katika siasa kwa sababu, niliona masuala mengi ya wanawake hayaingii kwenye sera mipango na bajeti kwa kuwa, nafasi nyingi za maamuzi zimeshikiliwa na wanaume.
“Hiyo ni kwasababu ya kushamiri kwa “Mifumo Dume” katika vyama vya Siasa nchini, nilitamani kuingia kwenye uongozi kufanya jambo la ziada kwa kuhakikisha masuala yanayohusu Wanawake na makundi mengine, yanaingia kwenye sera, mipango na bajeti, binafsi niliamini kila mwanamke ni kiongozi, anahitaji tu uthubutu na kuamua kushika hatamu.”
Hizo ni kauli za Lucy John Mtembo mwenye umri wa Miaka 40, ni miongoni mwa Wanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja).
Kupata taarifa na matukio kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Alianza harakati za siasa Miaka ya 2010, ambapo enzi hizo nafasi za uongozi kama Udiwani, Uwakilishi na Ubunge ulikuwa unashikiliwa na Wanaume wengi huku Wanawake wakionekana kuwa ni wapiga debe tu katika kampeni.
Anasema “Nimejifunza kuwa tunapaswa kuwa na uthubutu na utayari kujifunza mambo mapya na kujiwekea mipango inayotekelezeka ili tuwe viongozi wazuri.”
Lucy anaeleza kuwa bado Wanawake wapo kidogo katika nafasi za uongozi na vyombo vya maamuzi.
Soma Pia kwa taarifa zaidi zinazowahusu wanawake kipindi hichi cha uchaguzi: Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?
“Sisi wanawake tuko wengi kuliko wanaume, lakini huu wingi wetu hauakisi katika nafasi za uongozi na vyombo vya maamuzi,” anasema.
Licha ya Tanzania Bara na Zanzibar kuridhia mikataba na matamko mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa, yenye wito wa usawa katika uwakilishi na ushiriki wa wanawake na wanaume katika siasa, anadai bado wanawake wana uwakilishi mdogo katika vyombo vya maamuzi na nafasi za uongozi.
Anadai baadhi ya sababu zinazochangia hali hii zimetajwa ni uwepo wa Mfumo Dume, mitazamo hasi ya kibaguzi na mgawanyo wa majukumu kijinsia.
Takwimu zinaonesha Zanzibar, hadi sasa kuna wanawake nane tu, waliowahi kugombania nafasi za uongozi majimboni, ambao walishinda uwakilishi, wanawake 18 walipata uwakilishi kupitia nafasi za viti maalum na hivyo, kufanya idadi ya wanawake katika Baraza la Wawakilishi kuwa 29 kati ya 77 waliyochaguliwa sawa na Asilimia 40.
Fatma Abdul Habib Ferej ni Katibu wa Ngome ya Wanawake wa Chama cha ACT Wazalendo, ambaye aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, amesema bado wanawake wako kidogo katika nafasi za uongozi jambo ambalo linahitaji kuangaliwa.
“Licha ya Serikali kukubali mikataba mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa, ya kuhamasisha usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi na vyombo vya maamuzi lakini bado ushiriki wa wanawake haujaridhisha,” anasema Mwenyekiti huyo wa ngome ya ACT Wazalendo.
Amesema katika chama chake, wana Mabaraza ya Wanawake na Kamati Kuu ya Chama, ambayo yana ushiriki wa wanawake kwa Asilimia 52 ya washiriki wote.
Anaeleza “Ushiriki sawa wa wanawake katika kufanya maamuzi hauhitaji haki au demokrasia tu, bali ni lazima uonekane kama sharti muhimu la msingi ili maslahi ya Wanawake yazingatiwe.”
Naye, Naibu Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Anna Athanas Paul anaeleza kuwa tathimini iliyofanywa na wizara hiyo, katika taasisi mbalimbali imeonesha wanawake bado wapo kidogo katika nafasi za Uongozi, ukilinganisha na wanaume jambo ambalo linahitaji kuangaliwa.
“Takwimu zilizokusanywa na wizara kutoka taasisi mbalimbali kwa mwezi Machi 2024, zinaonesha ni Asilimia 30 tu ya Wanawake ambao wako katika uongozi, ukilinganisha na wanaume ambao ni asilimia 70,” anasema Naibu Waziri Anna.
Anna ameongeza kuwa Serikali inaendelea na jitihada katika kufikia malengo yaliyowekwa kupitia Dira ya 2050 na Mpango wa Maendeleo (ZADEP) 2021/2026 ambapo lengo katika nafasi za uongozi ni kufikia 50/50.
“Serikali imejipanga kuhamasisha ushiriki wa Wanawake katika nafasi za uongozi na vyombo vya maamuzi na lengo ni kufikia 50/50,” amesema Anna.
Ripoti ya Sensa ya Watu na Makaazi ya Tanzania ya Mwaka 2022, inaonesha Zanzibar ina Wakaazi milioni 1.8 kati ya hao wanaume ni 915,492 na wanawake ni 974,281.hii ina maana kwamba wanawake ni Asilimia 51.6 ya Wakaazi wote wa Zanzibar, lakini wingi huo hauonekani katika nafasi za uongozi.
Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA ZNZ) ni Taasisi isiyo ya kiserikali, inayojishuhulisha na masuala ya utetezi wa haki za mtoto wa kike na kuhamasisha wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA ZNZ, Dk. Mzuri Issa amesema vyama vingi vya siasa nchini, vimetawaliwa na mfumo dume jambo ambalo linawarudisha nyuma wanawake kugombea nafasi za uongozi.
”Wanawake wenye nia ya kugombea wasivunyike moyo na wawe majasiri ili kuongeza wingi wao katika nafasi za uongozi mwaka 2025 ili kufikia ile 50/50 tunayoitaka ” Amesema Dkt Mzuri.
Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Tanzania, kwa upande wa Zanzibar Mohamed Ali Ahmed amesema kuongezwa kwa kifungu cha 10 C ndani ya Sheria ya Vyama vya Siasa nchini, kinatoa nafasi kwa wanawake kuongeza ushiriki wao.
“Kutokana na kuongezwa kwa kifungu hicho, vyama vya siasa vitawajibika kwa kuwa na sera ya jinsia kwa muda wote, na kitasaidia kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi,” amemaliza Naibu Msajili huyo.
NA MARYAM NASSOR