Mifumo ya DP World kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato

Mifumo ya DP World kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Kutokana na madai ya kuwepo changamoto za mifumo madhubuti na kusababisha baadhi ya watu wasio na uadilifu kujihusisha na vitendo vya udanganyifu na kupoteza mapato ya Serikali katika Bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine nchini, Kampuni ya DP World (DPW) inayotarajiwa kuwekeza kwenye bandari hiyo itadhibiti vitendo hivyo kwa kusimika mifumo madhubuti ya TEHAMA.

DP World wamejenga bandari kavu Kigali, Rwanda yenye uwezo wa kuhifadhi makontena 50,000 na sasa wanaipanua na kutokea hapo ndio wanaihudumia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hivyo serikali imeona vyema ikafanya kazi na kampuni hii kwa kuwa tayari ina mtandao wa kutosha kibiashara.

Bandari ya Dar es Salaam inakosa fursa nyingi zinazofanya kushindwa kubadilisha uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa.
 
Back
Top Bottom