Samwel Ngulinzira
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 1,829
- 1,972
Asalam aleykum!
Bila kupoteza muda naomba tujadili hili suala kama dharura.
Ninaomba TCRA, BoT na mitandao ya simu watengeneze haraka mfumo wa malipo kwa njia ya simu.
Huduma kama lipa kwa M-Pesa, Airtel Money, T-Pesa, Halo Pesa, Tigo Pesa na Ezzy Pesa ili tuepuke matumizi ya pesa taslimu inayoweza kupelekea kusambaa kwa ugonjwa wa corona.
Simu za wafanyabiashara wadogo na wakubwa ziwezeshwe kupokea malipo kwa njia ya simu kama ilivyo kwenye Master Card.
Jambo la pili napendekeza mifuko ya jamii iandae fao la dharura kwa waajiriwa na wanachama wa hiari.
Fao hili liwe maalum kwa wale ambao shughuli zao zitakwamishwa na ugonjwa wa Corona kwa namna moja au nyingine waweze kujikimu kama itatokea tukapewa tangazo la kutokutoka nje.
Kuna maeneo kama utalii, shule, mabenki, kumbi za mikutano, kumbi za sherehe, nyumba za ibada na supermarket zitapata madhara makubwa kwa kua ndiyo maeneo ambayo yanategemea uwepo wa watu ili kutengeneza vipato vya wafanyakazi na wamiliki.
Hivyo kama hali ya kufunga shule na nyumba za ibada itatokea ulipaji wa mishahara pia utakua mgumu hivyo itabidi mifuko ya jamii iwapatie wafanyakazi fao la kujikimu ili waweze kujikimu mpaka hali itakapokua sawa.
Kwa hayo machache naomba kuwasilisha.