Mifumo yote ya TEHAMA Nchini iliyochini ya serikali haina mtandao na inasumbua; sekta binafsi hakuna changamoto. Serikali ipo salama?

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Hakuna mfumo wa serikali mtandao unaotoa huduma kwa wakati. Mifumo yote inasumbua na ipo slow sana.

Kwa wataalam wa TEHAMA mtakubaliana na mimi kwamba kadri mifumo ya serikali ya TEHAMA inavyohujumiwa ndivyo wanasiasa na watoa maamuzi wanavyosukumwa kutafuta suluhu mpya

Maana yake hapa tulipo wapo watu wanataka kuua mifumo iliyopo aliyosimika JPM ili wapige pesa. Watu hawataka kulipa kwa mtandao wanawaza kulipa manual.

Natabiri soon zitaanza kutangazwa tenda za kutengeneza mifumo ; soon tutaanza kuambiwa mikataba aliyoingia JPM imeisha na hatuna wataalam wa ndani walioandaliwa hivyo tunaanza kuwapa tenda wageni.

Hizi mentality zakuua mifumo na miundombinu ya serikali kwa ajili ya biashara zinarudisha sana nchi nyuma lakini pia zinakwamisha maendeleo ya watanzania.
 
Km jina pako vile, ni resilience tu tunadumu nayo
 
BWANA ROSTAM AZIZI ATAKUWA ANAPAKUA FEDHA KWENYE HIYO MIFUMO KAMA KAWAIDA YAKE
 
Hakuna mfumo wa serikali mtandao unaotoa huduma kwa wakati. Mifumo yote inasumbua na ipo slow sana.

Kwa wataalam wa TEHAMA mtakubaliana na mimi kwamba kadri mifumo ya serikali ya TEHAMA inavyohujumiwa ndivyo wanasiasa na watoa maamuzi wanavyosukumwa kutafuta suluhu mpya

Maana yake hapa tulipo wapo watu wanataka kuua mifumo iliyopo aliyosimika JPM ili wapige pesa. Watu hawataka kulipa kwa mtandao wanawaza kulipa manual.

Natabiri soon zitaanza kutangazwa tenda za kutengeneza mifumo ; soon tutaanza kuambiwa mikataba aliyoingia JPM imeisha na hatuna wataalam wa ndani walioandaliwa hivyo tunaanza kuwapa tenda wageni.

Hizi mentality zakuua mifumo na miundombinu ya serikali kwa ajili ya biashara zinarudisha sana nchi nyuma lakini pia zinakwamisha maendeleo ya watanzania.
Mifumo yote ya serikali ya hovyo sana naunga hoja mkono
 
Hata kuangalia namba yako ya NIDA mtandaoni ni changamoto.
 
Kama mfumo wa mapato ya nchi TRA nao ni tatizo unadhani wapo wapo serious kwa jambo gani ?kila ukienda kufuata huduma unakutana na kadada kwanza kamebinua mdomo utasikia kanakwambia mtandao upo down subiri hadi urudi! Hapo utasubiri hadi keshokutwa yake

Na hapo umejipeleka mwenyewe kwa uzalendo wako ukakadiriwe kodi ili ulipe
 
Natabiri soon zitaanza kutangazwa tenda za kutengeneza mifumo ; soon tutaanza kuambiwa mikataba aliyoingia JPM imeisha na hatuna wataalam wa ndani walioandaliwa hivyo tunaanza kuwapa tenda wageni.
Tender kwa kampuni binafsi ndio ufisadi??
Mimi nikadhani kuhujumiwa ni pale mfumo unakwamishwa ili watu waibe kimtandao kumbe ufisadi ni kampuni binafsi kupewa tender?

Kama hii ndio hoja yako basi niseme tu tusahau maendeleo maana tuna mawazo ya ujamaa sana kudhani mtu binafsi kupewa kazi ni ufisadi ilihali ndio inachochea uchumi.
 
Nchi hii inaongozwa na mbinu zile zile za kuongoza na kusimamia vilabu vya Simba na Yanga.! Watumishi na watendaji ngazi zote kuanzia juu mpaka chini wanawaza kujinufaisha na kuhujumu mali za umma kwa mtindo wa CCM...Chukua Chako Mapema.
Juzi nilibahatika kuongea na kijana mmoja aliyechaguliwa kuhudhuria kozi fupi ya kuhudumu kwenye miundombinu ya mwendokasi....nimeshangazwa sana na uelewa wake kuhusu kile anachosomea na matarajio yake makubwa ni kuwa atapata ajira ili mkono uende kinywani. Matarajio au mafanikio ya kampuni kufanya vizuri au vibaya hiyo haitamhusu....Aibu!.
 
Mifumo ya malipo ya serikali na mifumo ya huduma mwezi sasa imecollapse......serikali inapataje mapato kwa mazingira haya?

Lakini kibaya zaidi wapo watu wanafahamu mifumo mibovu lakini bado wanatoza faini kwa kuchelewa kuomba na kupata huduma

Mfano mifumo ya uhamiaji haifanyi kazi ila wageni wanalipishwa dola mia sita kwa nguvu wanapozidisha muda

Ukiomba visa hakuna huduma mpaka upige simu au itafute kishoka.....system zimecollapse na hakuna appology inatolewa.

Wageni wanalalamika bora waingie Kenya tu maana tumeshindwa kujisimamia.......watendaji wa serikali mnafahamu tunalipa kodi kwa kazi hizi? Bushit
 
Tuanzishe mchakato wa kuwa Jimbo la USA tu na senator awe mzungu.
 
Kama mfumo wa mapato ya nchi TRA nao ni tatizo unadhani wapo wapo serious kwa jambo gani ?kila ukienda kufuata huduma unakutana na kadada kwanza kamebinua mdomo utasikia kanakwambia mtandao upo down subiri hadi urudi! Hapo utasubiri hadi keshokutwa yake

Na hapo umejipeleka mwenyewe kwa uzalendo wako ukakadiriwe kodi ili ulipe
😂😂😂😂 Kiukweli wanaboa sana kwa huduma zao mbovu.
 
Back
Top Bottom