Uchaguzi 2020 Mifuto ya kufutia wino imesambazwa ili mtu apige kura zaidi ya mara moja

Uchaguzi 2020 Mifuto ya kufutia wino imesambazwa ili mtu apige kura zaidi ya mara moja

Frustration

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,134
Reaction score
4,124
Habari za jioni hii, mimi frustration nimeapishwa kuwa wakala wa ACT Wazalendo katika Kata yangu.

Changamoto kubwa ilikuwa ni kutojipanga kwa chama cha CHADEMA na ACT Wazalendo. Kwenye Kata yangu vyama hivi vinashirikiana katika suala la wakala bila shaka sababu ni ukata wa pesa.

Siku ambayo tunaenda kuapishwa kwa mtendaji Kata, watu zaidi ya nusu waliojiandikisha walikuwa mashambani. Hivyo sisi na uchache wetu tulienda kuapishwa kwa imani kuwa bora ivujie kuliko inyeshee.

Haikuwa rahisi kuapishwa maana mtendaji Kata alikuwa design anazingua. Nishukuriwe mimi baada ya kumkamia mtendaji Kata kwa kumwambia tuonyeshe hitaji hilo lililoletwa na CCM.

Mfano alikomaa sana barua 2 za chama kitu ambacho wenzetu CCM hawakuambiwa. Ila Siku ya Siku tuliapishwa na katika Kata vituo vyote vina mawakala mmoja wa upinzani either CHADEMA au ACT Wazalendo.

KIJIJI CHENYE WATU CHINI YA ELFU MOJA NIMEKUTA WAPIGA KURA 1026.
Kijiji kina vitongoji vinne na wastani kila kitongoji watu Jumla chini ya 200. Mwaka 2015 Kilikuwa kituo kimoja ila safari hii kuna vituo vitatu. What a biriani goal planned by CCM?

USHAURI KWA UPINZANI.
Wapiga kura hewa ni wale walionjiandikisha kituo zaidi ya kimoja, sasa wahakakishe watu wanachovya kidole kwenye wino baada ya kupiga kura.

Najua CCM wana namna ya kufuta wino maana wana mifuto wameigawa kwa makatibu wa shina na tawi. Ila safari hii wameshindwa mapema kwa sababu miaka mitano wapo bize kuandaa NEC iwape kitonga cha ushindi.

Chagua Lissu kwa maendeleo ya wafanyakazi na wakulima
Ahsante.

Simu nimeazima maana yangu display wamevunja wanaccm kwenye kurupushani za hapa na pale.

NB: Kijijini wameikataa zaidi CCM Kuliko mijini. Mtego wa mbolea za bure umefeli mno vijijini na ugumu wa maisha umechangia, hata display ya laki na 50 Samsung S5 nimeshindwa.
 
Back
Top Bottom