Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,703
- 1,724
Mheshimiwa Asharose Migilo katika ahadi zake za kutekeleza akiwa waziri wa sheria na katiba amesema atahakikisha katiba inapatikana kama ilivopendekezwa na wananchi wengi, hilo halina ubishi kwani hii ndio demokrasia lakini baadhi ya viongozi wenzako kwenye chama chako (hasa Zanzibar tena wachache) wanataka kuhakikisha maoni ya wengi hayapiti. Je huoni hii itakukwaza katika shughuli zako? Kumbuka hawa (ZNZ) ndio waliokuwa wakitaka kukwamisha maridhiano kati ya CCM na CUF lakini waheshimiwa Rais Karume na Kikwete waliwazibia masikio na leo tunaiona Zanzibar ipo shwari.