SoC03 Migogoro baina ya wanyamapori na binadamu

SoC03 Migogoro baina ya wanyamapori na binadamu

Stories of Change - 2023 Competition

Finley

New Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
2
Reaction score
2
UTANGULIZI

Jamhuri ya muungano wa Tanzania (URT) chini ya wizara ya maliasili na utalii (MNRT) yenye dhamana ya kutunga sera, sheria na kanuni za uhifadhi wa rasilimali za asili hasa wanyamapori ili kusimamia na kuleta maendeleo katika sekta ya wanyamapori Tanzania. Miongoni mwa dira ya sekta hiyo ya wanyamapori kwa miaka ishirini (20) ijayo ni kuendana na dira ya maendeleo ya mwaka 2025 ya Tanzania inayolenga uendelezwaji wa mazingira na mabadiliko ya kijamii Pamoja na kiuchumi. Miongoni mwa malengo katika dira ya uhifadhi wa Wanyamapori ni Pamoja na kuchangia katika kuukataa umasikini na kuboresha ubora wa Maisha ya wananchi wake; ambayo ndiyo kitovu cha andiko hili.

Miongoni mwa matatizo yaliyobainishwa na sera ya wanyamapori ya mwaka 1998 ni Pamoja na:

  • Kupotea na kupungua kwa makazi ya wanyamapori kutokana na shughuli za kibinadamu hasa uanzishwaji wa makazi, kilimo, maeneo ya ufugaji, uchimbaji wa madini na ukataji miti kwajiri ya mbao; haya yote yanasababishwa na ongezeko la idadi ya watu.
  • Ufinyu wa haki ya matumizi ya mazao yatokanayo na maliasili hasa kwa jamii za watu waishio vijijini.
  • Ufinyu wa uwezo wa kupambana na kuzuia madhara yatokanayo na Wanyama hatari na waharibifu.
Pia sera ya wanyamapori ya mwaka 1998 ilijidhatiti katika kushughulikia na kutatua changamoto changamoto zinazoikumba sekta ya wanyamapori; ikiwemo Pamoja na :

  • Kuihusisha jamii iishiyo jirani na maeneo ya uhifadhi katika uhifadhi wa wanyamapori.
  • Kuhusisha uhifadhi wa wanyamapori na maendeleo ya vijijini.
  • Kuwezesha utambuzi wa thamani itokanayo na uhifadhi wa wanyamapori kwa watu waishio Jirani na maeneo ya uhifadhi (vijijini).
  • Zaidi; ni katika kupunguza na kutatua migogoro baina ya wanyamapori na binadamu, pindi itokeapo.
Katika kutambua umuhimu wa uhifadhi wa wanyamapori katika kuleta tija kiuchumi nchini, sera ya taifa ya wanyamapori yam waka 1998 iliweka malengo yake; baadhi ya malengo hayo (hasa yale yanayoigusa jamii iishiyo Jirani na maeneo ya uhifadhi ni Pamoja na:

  • Kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori kwa kuanzisha jamii za uhifadhi wa wanyamapori (WMAs); ikiwemo pamoja na kutoa mafunzo kwa askari wa wanyamapori wa vijiji (VGS) ili kulinda rasilimali za wanyamapori.
  • Kukabidhisha usimamizi wa maeneo ya uhifadhi (WMAs) kwa jamii ili kuwapa nguvu ya kulinda mapito ya wanyamapori (corridors), njia zitumikazo na wanyamapori wakati wa kuhama (migratory routes) Pamoja na maeneo yote yatumikayo kulinda maeneo nyeti ya uhifadhi (buffer zones); ili kuhakikisha jamii hizo zinanufaika moja kwa moja kutokana na faida za uhifadhi.
  • Kuongeza uelewa kwa jamii kutambua masuala yanayohusu uhifadhi wa wanyamapori.
  • Kubwa Zaidi, ni kutatua migogoro baina ya wanyamapori na binadamu ambayo hupelekea madhara kwa binadamu na mali zake. Miongoni mwa njia zitumikazo ni Pamoja na:
  • Kuhakikisha wale watu ambao ni waathirika wakubwa wa Wanyama hatarishi/waharibifu wanakua ni wanufaika wakuu wa mapato yatokanayo na wanyamapori.
  • Kutumia njia ambazo sio hatarishi kutatua na kuzuia athari zitokanazo na Wanyama hatarishi/waharibifu; kama kuwakamata au kuwafukuza kuelekea maeneo yao asilia.
  • Kutunga sheria, kanuni na miongozo ya uhifadhi wa wanyamapori hasa ule mwongozo wa kupambana na Wanyama hatarishi/waharibifu ya mwaka 2011 ambayo inatoa miongozo katika utoaji wa fidia kwa waathirika wa uharibifu au madhara yatokanayo na Wanyama waharibifu/hatarishi.
Mapungufu katika utekelezwaji wa sera hii:

  • Kukosekana kwa uhalisia kiutendaji na utekelezaji wa sera ya wanyamapori; hii inatokana na muingiliano baina ya wataalamu wa uhifadhi na wanasiasa (kuanzia ngazi ya wabunge, mawaziri wa wizara husika Pamoja na marais ambao kila awamu inakuja na vipaumbele tofauti kutokana na utashi wao wa kibinadamu pasipo kufuata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wahifadhi wa wanyamapori. Hii hupelekea kutokea migogoro baina ya wanyamapori na binadamu kutokana na kutokea kwa ongezeko la wanyamapori kwa kuzaliana kwa wingi bila kuwepo njia mbadala za kupunguza idadi yao kulingana na uwezo halisi wa maeneo tengwa kwa uhifadhi; pia kutokana na ukweli kwamba idadi ya watu inaongezeka miaka hadi miaka kwa kuzaliana na hvyo kuongezeka kwa uhitaji wa maeneo kwajiri ya shughuli za kiuchumi kama makazi na kilimo.
  • Kukosekana kwa ushirikiano wa kiutendaji baina ya sekta ya wanyamapori na sekta zingine ambazo zina uhusiano wa karibu katika matumizi ya ardhi ikiwemo sekta kilimo na ufugaji. Mfano, migogoro mingi baina ya wanyamapori na binadamu hutokea kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa matumizi ya ardhi katika kilimo na ugugaji; jambo ambalo linapelekea wakulima kulima maeneo Jirani na hifadhi au wafugaji kulisha mifugo yao ndani au Jirani na hifadhi. Hii hupelekea wanyamapori kuhama kutoka hifadhini kuja maeneo ya vijijni kufuata mazao au mifugo na kusababisha madhara ikiwemo vifo vya binadamu na mifugo, majeruhi, ulemavu wa kudumu na hata uharibifu wa mazao.
  • Watu hasa wanakijiji waishio Jirani na hifadhi kukosa faida na manufaa ya moja kwa moja kutokana na shughuli za uhifadhi ikiwemo nyamapori na hata miundombinu na huduma za kijamii (barabara, vituo vya afya, maji safi na salama) Pamoja na kuimarika kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja.


Nini kifanyike?


  • Utekelezaji wa sera ya wanyamapori kwa kuwapa nguvu mamlaka zote zinazohusika na uhifadhi wa wanyamapori bila kuingiliwa na siasa.
  • Kuwe na ushirikiano wa karibu baina ya sekta zote ambazo zina uhusiano wa karibu na sekta ya wanyamapori katika matumizi ya ardhi hasa sekta ya kilimo na ufugaji.
  • Marekebisho ya sera Pamoja na sheria na kanuni zinazosimamia uhifadhi wa wanyamapori ili kuendana na uhalisia wa nyakati za sasa; hii ni Pamoja na kuangalia upya mipaka ya vijiji na maeneo ya uhifadhi ili kuendana na kasi ya ongezeko la idadi ya wanyamapori na binadamu.
  • Kuzingatia utolewaji wa fidia kwa wakati.
  • Kufanyike mabadiliko ya baadhi ya vipengele/vifungu vya sheria hiyo ambavyo vinaleta mkanganyiko kama ilivyoainishwa, Pamoja na kuongeza vipengele ambavyo havikuwekwa kulingana na wakati ambao sheria ilitungwa ili utekelezaji wa sheria hii uendane na wakati wa sasa. Hii ni Pamoja na:
  • Kuongeza kiasi cha fidia ili kuendana na hali halisi ya Maisha ya sasa tofauti na kipindi ambacho sheria ilitungwa (mwaka 2011).
  • Kutambua utofauti wa thamani ya mazao; hasa kati ya mazao ya chakula na mazao ya biashara.


Uhifadhi kwa ustawi wetu!
 
Upvote 2
Back
Top Bottom