Migogoro ya Ardhi Dodoma: Jinsi viongozi wanavyohusika na udalali wa viwanja

Migogoro ya Ardhi Dodoma: Jinsi viongozi wanavyohusika na udalali wa viwanja

Kimwakaleli

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2018
Posts
7,755
Reaction score
11,737
Habari wanajamii,

Mimi ni mkazi wa Dodoma tangu mwaka 1998, na kwa miaka yote hii, nimeshuhudia migogoro mingi ya ardhi, ambayo mara nyingi inachochewa na viongozi tuliowapa dhamana.

Imekuwa kawaida kwa wengi kuwania nafasi za uenyekiti wa mtaa, udiwani, na nafasi nyingine za uongozi si kwa lengo la kuwatumikia wananchi, bali kwa maslahi binafsi. Wengi wao wanajihusisha na udalali wa mashamba, viwanja, na nyumba, jambo ambalo limekuwa chanzo chao kikuu cha kipato zaidi ya mishahara yao rasmi.

Kuna hata kisa cha mmoja wao aliyefikia hatua ya kuuza kiwanja cha Waziri Mkuu mstaafu kinyemela! Hili ni tatizo kubwa, na ni muhimu viongozi hawa wachunguzwe kabla hali haijazidi kuwa mbaya.

Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom