Migomo kuelekea uchaguzi inahitajika, watarudi wenye maarifa na hekima

Migomo kuelekea uchaguzi inahitajika, watarudi wenye maarifa na hekima

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Mpo salama bila shaka.

Inapotokea migomo ya nyakati hizi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ni muhimu kuiendea kwa umakini.

Wanasiasa wanaelewa nazungumzia nini.

Watatuzi wa migomo lazima wawe na ujuzi, uwezo na hekima za kuongea mbele za Watu.

Sio unachagua mtu asiye na ujuzi wa mambo hayo anaanza kuropoka ropoka na kutia chumvi kwenye kidonda.

Kizazi cha sasa sio kile kizazi cha wajinga ambao unaweza kutisha tisha Watu kama watoto ilhali Watu wanahitaji haki fulani. Uelewa na elimu ya kizazi hiki imeongezeka maradufu hivyo hata mbinu za kudili na wananchi lazima ziwe za kisomo na uelewano.

Kwenye ulimwengu huu wenye vitisho bila kutumia akili na maarifa hawadumu hata ungekuwa na cheo kikubwa kiasi gani.

Kwanza unatisha wanaume wenzako hiyo kama sio dharau ni nini? Mtu hafanyi uhalifu anahitaji marekebisho kuhusu jambo fulani wewe kwa akili zako za kizamani unakuja kutisha Watu. Unafikiri wewe ni nani hasa? Na hivyo unavyojifikiria unadhani kila mtu anakuona hivyo.

Heshimu Watu ili uheshimiwe.

Kuna Watu wanaushamba fulani wa kizamani. Hata raia wa kawaida unakuta mtazamo wake upo kizamani.

Hawa ndio wakipewa kinafasi na kicheo fulani wanaanza kuumiza Watu.

Elewa, hukohuko serikalini kuna Watu ni Open minded ambao mitazamo yao ipo kisasa na sio kizamani.
Elewa, wale unaodhani wanakulinda wapo mitazamo yao sio yakizamani.

Unapokuwa mtawala au kiongozi usiwe mjinga. Angalia nyakati ulizomo. Hiyo ipo hata katika ngazi ya familia. Baba ukiwa mpumbavu na mbabe mbabe elewa usaliti unaweza kufanywa hata na mtoto wako uliyemzaa. Sasa ikiwa mtoto au mkeo anaweza fanya hayo sembuse Watu back wanaokulinda kwa kisa cheo.

Viongozi wenye hekima hujua namna ya kuchagua maneno ya kuongea mbele za Watu.
Mihemko huiweka mbali. Ishu ya vitisho huweza kuwa indirect au field lakini mbele za Watu hutumia lugha ya hekima

Adui wa mbali ndio hutolewa mikwala na kufanyiwa ubabe. Lakini kuwapa mikwala wananchi na kuwafanyia ubabe Watu wako. Kimedani Umefeli.

Elewa, mtu mzima kumfanyia ubabe ni kumdhalilisha. Tena ubabe kwa haki yake. Alafu uchukulie itaisha au atasamehe utakuwa haufikirii vizuri.

Wanaokemewa ni wahalifu. Wanaokemewa ni waovu.

Hivyo ndivyo ilivyo.
Vijana wenye ndoto za kuwa viongozi ni hayo tuu.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Upo sawa mtalaam wa fasihi. Viongozi wasiotumia akili ni wengi sana hii nchi, mimi kuna kiongozi wangu nimeamua nimchukulie kama mtu asiyejitambua na mtoto mdogo ili nisigombane nae mara kwa mara. Viongozi hawa wanapotaka kuvuruga amani na umoja wanapaswa kukemewa mara moja
 
Upo sawa mtalaam wa fasihi. Viongozi wasiotumia akili ni wengi sana hii nchi, mimi kuna kiongozi wangu nimeamua nimchukulie kama mtu asiyejitambua na mtoto mdogo ili nisigombane nae mara kwa mara. Viongozi hawa wanapotaka kuvuruga amani na umoja wanapaswa kukemewa mara moja

Kitu kidogo unaanza kutisha Watu wazima na kuanza kufanya mambo kuwa makubwa
 
Ulichosema ni kwel kabisa
Nakumbuka km miaka 2 iliyopita nilitaka kupigana na maafisa wa TRA hivi hivi kisa ujinga wao na maneno ya kebehi na ubabe
Baba yangu kaanza biashara miaka ya 70/80’s na mm nineingia kwenye biashara baada yakumaliza chuo IAA MWAKA2013

Sasa kipindi cha magufuri jiwe maafisa weng wa TRA walijiona sana mungu mtu tena km wale walofanya interview uwanja wa mkapa
Bas bana vi afisa tra vinakuja kwenye maofisi na makampuni ya baba wanampiga mkwala wengne ad wanamtishia watampoteza mara watafunga biashara zake zote yan ni ubabe na lugha za mazarau wakat ukiwaangalia kazini hawana ata miaka 5 baba yangu kafanya biashara mwaka wa 40 afu ww fala unakuja kumpiga mkwala kisa ni afisa tra
 
Kitu ambacho serikal na tra hawajui ni kua wazee wetu walikua ni wastaarabu sana wapole na wavumilivu so walikua wanaweza vumilia vitisho na maneno ya kibehi na kibabe kutoka kwa maafisa wa serikal pamoja na tra
Sasa wazee wanaaza kuchoka na biashara wanakabizi vijana tena vijama waliosoma na kuelimika lakin pia saiv vijana weng wanaingia kwa biashara tena ni wafanya biashara wakubwa sasa tra na maafisa wa serikal inabidi wabadilike saiv wanafanya kaz na vijana sio wazee uwezi kuja nitukana au kunipiga mkwala mimi kijana tutagombana
 
Back
Top Bottom