Migori: Afisa Mkuu wa polisi ajipiga risasi wakati akimpa silaha mwenzake

Migori: Afisa Mkuu wa polisi ajipiga risasi wakati akimpa silaha mwenzake

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Afisa mkuu wa polisi aliye stationed katika Kituo cha Polisi cha Kegonga huko Migori alijipiga risasi kimakosa alipokuwa akimpa silaha mwenzake ndani ya kituo siku ya Jumatatu.

Kulingana na ripoti ya polisi iliyopatikana na Citizen Digital, Koplo Caudence Nyangenya, ambaye alikuwa anasimamia mistari na silaha, alipewa jukumu la kumkabidhi bunduki aina ya Barreta kwa James Mugo Kabachia, Kamanda wa Polisi wa Sub-County ya Kuria Mashariki.

Baada ya tukio hilo, afisa huyo alikimbizwa Hospitali ya Kegonga Sub County na baadaye akahamishiwa Hospitali ya Migori County kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuzorota.

Akiwasili, alitangazwa kufariki kutokana na kupoteza damu nyingi.

Mwili wake ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo huku uchunguzi wa mwili baada ya kifo ukitarajiwa kufanyika.

CITIZEN TV
 
Back
Top Bottom