Tetesi: Miguel Gamondi atajwa kutua Singida Big Stars kurithi mikoba ya Patrick Aussems aliyefurushwa

Tetesi: Miguel Gamondi atajwa kutua Singida Big Stars kurithi mikoba ya Patrick Aussems aliyefurushwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Klabu ya Singida Black Stars imewasimamisha makocha wake wawili, Patrick Aussems na msaidizi wake Dennis Kitambi kutokana na matokeo mabaya, huku ikidaiwa kumwania Miguel Gamondi aliyeachana na Yanga hivi karibuni.

Leo asubuhi Singida ilitoka sare ya mabao 2-2 na Tabora United kwenye Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulitarajiwa kupigwa jana lakini ukasogezwa mbele kutokana na uwanja kujaa maji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo, imesema kuwa imewasimamisha makocha hao kutokana na matokeo mabaya ya timu hiyo, ambayo imepoteza mchezo mmoja na kutoka sare miwili kati mechi 11 iliyocheza chini ya makocha hao.

"Tunapenda kuutarifu umma na mashabiki wetu kuwa Bodi ya Ukurugenzi ya Singida Black Stars imefikia uamuzi wa kuwasimamisha kazi makocha Patrick Aussems pamoja na Denis Kitambi kuanzia leo 25/11/2025.

"Uamuzi huo unatokana na mwenendo usioridhisha wa timu yetu katika mechi tatu mfululizo, licha ya jitihada zote kufanyika kuwapatia benchi la ufundi, katika kipindi chote ambacho makocha hao watakuwa nje, timu itakuwa chini ya Mkurugenzi wa Ufundi Ramadhani Nsanzurwimo kama Kocha Mkuu na Muhibu Kanu kama Kocha msaidizi ",imesema taarifa hiyo.

Hata hivyo, wakati Aussems na msaidizi wake wakiwekwa kando kuna taarifa kuwa aliyekuwa kocha wa Yanga Miguel Gamondi, amekuwa akitajwa kuwa anaweza kwenda kurithi mikoba ya Mfaransa huyo aliyeiongoza Singida katika michezo 10 ya Ligi Kuu Bara akiwa ameshinda saba, ametoka sare miwili na kupoteza mmoja tu dhidi ya Yanga. Timu hiyo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 24 sawa na Yanga na Azam, ikiwa imefunga mabao 15 na kuruhusu sita.

Hata hivyo, wakati Aussems na msaidizi wake wakiwekwa kando kuna taarifa kuwa aliyekuwa kocha wa Yanga Miguel Gamondi, amekuwa akitajwa kuwa anaweza kwenda kurithi mikoba ya Mfaransa huyo aliyeiongoza Singida katika michezo 10 ya Ligi Kuu Bara akiwa ameshinda saba, ametoka sare miwili na kupoteza mmoja tu dhidi ya Yanga.

Timu hiyo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 24 sawa na Yanga na Azam, ikiwa imefunga mabao 15 na kuruhusu sita.

"Wakati wa mechi dhidi ya Tabora jukwaani mashabiki walikuwa wanasema kuwa timu hiyo inamwania Gamondi endapo itaachana na Aussems, nafikiri ndiyo jambo labda ambalo linaweza kutokea baada ya taarifa hii," kilisema chanzo kutoka Singida.

Gamondi aliondolewa Yanga Novemba 15, 2024, baada ya uongozi wa timu hiyo kusema kuwa hairidhishwa na matokeo ya timu hiyo ambayo ilikuwa haijapata ushindi kwenye mechi tatu mfululizo akiwa aliipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.
IMG_0926.jpeg

PIA SOMA
- Tetesi: - Kocha Miguel Gamondi kwenda kurithi mikoba ya Benchika akifutwa kazi JS Kabylie
 
Hili bundi la kuvunja benchi za ufundi liko njiani hivi Sasa kuelekea Msimbazi. Tegeni sikio tu!
 
Litakuwa kosa kubwa sana kwa Singida na kama itakuwa hivyo Ausem achukuliwe yanga awe hata mshauri huku akipiga jaramba maana huyu Said sioni akienda mbali
 
Wanataka kumchukua gamondi akiwachomolea sijui itakuwaje? Sema mzee wa trouble na trat anampiga sana mama ana jeuri ya kufanya chochote kwa nguvu ya fedha wakali wa hizi kazi wanaita vijisenti in chenge's voice na mimi nasema ni vijisenti tu
 
Moto utawaka kwenye kuwania nafasi ya tatu na nne tu mkuu, tofauti na hapo ndio yatakuwa ni yale maajabu ya mpira
Pale singida pesa ipo wanaweza kusajili dirisha dogo likifunguliwa halafu moto ukawaka
 
Anachukua kabla ya kukutana na Simba wakikutana anawapiga maana wale wachezaji wa Singida sio poa
Jamaa wanafaa kubeba kombe kabisa msimu huu
 
Ausem achukue Namungo Juma arudi Tanga kupumzika kidogo huku akiandaa mazoezi ya team oyah oyah ya taifa
 
Back
Top Bottom