Mola akusamee wewe unayekosoa uumbaji wake.! ni ajabu sana binadamu unashindwa kujikubali vile muumba alivyofanya kazi yake kukuandaa kabla ya wewe kuwepo hapa duniani, fikiria ndg yangu siku utakarudi kwa mola wako unaanza kuvishwa sanda mpaka unawekwa kaburini, kisha utakutana na maswali kama kwa nini ulinikosoa mie muumba wako kwa kujibadilisha vioungo nilivyokujaalia nawe ukaona havistahili kuwa vile nilivyoviumba? jiulize kwa makini, ogopa sana kukutana na mola wako hali ya kuwa umekasirikiwa naye. hebu jiulize huu usiku na mchana kwa jinsi unavyokuwa nawe pia usingizi unaolala usiku hivi kweli unashindwa kuikubali hali ya kuumbwa kwako.
mi nakuombea sana kwa mungu akutolee mawazo hayo nawe uwe muongofu usije ukaidhulumu nafsi yako kwa kutenda vile ambavyo Mungu hataki vifanywe.