Miguu yangu jamani

SHINYAKA

Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
74
Reaction score
39
Ma-Doctor wa JF, naja kwenu nachechemea, tafadhali nipeni fafanunuzi kinachonisibu ni nini?
Dalili zinisumbuazo ni hizi:-
1. ngozi ya Miguu inauma kwa mtindo wa kuwasha, kuanzia magotini hadi makanyagioni hasa ukivaa suluari ikawa inagusagusa unapotembea.

2. Wakati ukioga jioni, ukiimwagia maji hiyo miguu, huja hali ya kuwasha ndipo hamu ya kukuna inapokuja, utataka kukuna bila kuacha.

3. Usiku ukiwa kitandani hali ya maumivu ya kuwasha huzidi kidogo, utaendelea kujikuna baadae hutoa alama za uvimbe kutokana na kukuna.

TAFADHARI NISAIDIENI NATESEKA
 
Pole sana, ngoja wataalam waliotaalamikiwa wakujibu, then sisi akina yahe ndo tutakuja na vinyongeza vyetu.
 
Nenda tu hospitali. hizo symptoms hazieleweki, lazima daktari ajionee. inaweza kua kitu chochote kuanzia diabetes hadi varicose veins na vyote vina affect vitu vingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…