Mihemko imeamua tukio

mrdocumentor

Member
Joined
Nov 27, 2021
Posts
45
Reaction score
56
Kuwa kiongozi ni dhima na ni jambo ambalo linakuongezea mzigo wa kufikiri ziada ya wanavyofikiri watu wako unaowaongoza, kwa sababu kumbuka unawaongoza watu tofauti, waliozaliwa na kulelewa mazingira tofauti lakini pia wana itikadi tofauti.

Mnamo Tarehe 24/06/2023 Ulichezwa mchezo wa marudiano wa playoff kati ya Mashujaa Fc kutoka mkoani Kigoma dhidi ya Mbeya city ambao walikuwa wenyeji katika mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa mashujaa kushinda Bao 1 kwa Nunge na kufanikiwa kufuza NBC premier league kwa aggregate ya mabao manne kwa moja.

Ishu hapo sio matokeo, ninachotaka kuzungumzia mimi ni tukio lililotokea baada ya Mashujaa kufunga bao la kwanza, wakati wanashangilia video ya mwanzo ilimuonesha Kocha wa walinda mlango wa Mashujaa Fc aliyetambulika kwa jina la Shomari Ndizi akirusha ngumi kuelekea kwa kocha mkuu wa Mbeye city Bwana Abdallah Mubiru, Lakini baada ya maamuzi ya TFF kuamuru Bwana Ndizi kufungiwa msimu mmoja kujihusisha na soka na Faini ya 2,000,000 Ikapatikana video nyingine ikimuonesha Bwana Mubiru akirusha teke kwa Bwana Ndizi.

kwanini hii video imesambaa wakati huu ambao maamuzi yalishatolewa lakini Je, ni kweli watoa maamuzi tukio hili la kwanza ambalo kimsingi ndio kisababishi cha tukio la pili hawakuliona? Cha kuchekesha Zaidi Mubiru kupitia Wasafi fm anasema Ndizi alijikwaa tu hakumpiga, Hivi kwa ile video ni kweli Bwana Ndizi alijikwaa?

Mimi sina majibu ya hayo maswali yote bali natoa mtazamo wangu, Kwenye hili Mihemko ya mitandao ya kijamii ndio imefanya maamuzi na sio kamati ya maamuzi ya TFF,
NDIO hauna haja ya kushangaa, kwa sababu baada ya mchezo habari kubwa mtandaoni haikuwa Mashujaa kupanda bali ni "Kocha wa Mashujaa hajafanya kitendo cha kiungwana".

Mtu akiwa na mihemko huwa haangalii sababu ya kufanya kitu huwa anaangalia matokeo pekee ndicho ambacho waandishi wengi kiliwakuta kikawaingia hadi kamati ya maamuzi na kufanya maamuzi kwa mihemko na si kwa weledi.

Sasa hivi upepo umegeuka na TFF na Mubiru ndio wanaonekana wakosefu unajua kwanini?
Ni kwa sababu sasa wamepata mda wa kutulia na kutafakari sababu ya kufanya vile ni nini? na wakajiuliza kuwa Bwana Ndizi hana tatizo la akili hawezi kufanya vile bila sababu. Na huo ndio weledi ambao huwezi kuupata ukiwa na mihemko.
 
Ngoja nikazitafute hizi video zenye hayo matukio.
 
Mashujaa ya Dodoma?
 
Una hoja ila title yako haivutii watu kusoma thread hii, ungeweka title iliyo wazi na kueleweka
 
Hizo video zote za hayo matukio sijayaona ila naungana na wewe kuhusu bandari yetu, Serikali inachofanya sio sahihi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…