Mihula ya high school kubadilika tz.

wanguwangu

New Member
Joined
Jun 5, 2008
Posts
4
Reaction score
0
MIHULA YA HIGH SCHOOL KUBADILIKA TZ.

Wanafunzi ambao wapo Form VI sasa imekubalika kufanya mitihani February(next month) badala ya May 2013) well and good.
Wanafunzi walio Form V sasa eti kuja kufanya mitihani May 2014! Ivi kweli wanafunzi wakikaa bila kusoma kwa muda wa miezi mitatu watakuwaje! Ivi kweli serikali inabajeti wa kuweza kuwa weka wanafunzi hao mashuleni kwa kipindi cha ziada miezi mitatu?

Labda Wizara ilikosa kufikiria kuwa kubadili mihula kuna taratibu nzuri ni kwamba hawa ambao walisha anza waendelee na wale watakao anza ndio waende na mabadiliko hayo. Nadhani kubadili ghafla hivi kuna madhara ya kuongeza bajeti kwa shule za serikali au laa kiwango cha elimu kitazidi kudidimia.

Kwa shule za binafsi wazazi watabidi waongeze ada zaidi kwa kipindi hicho kinacho zidi. Watakao anza form V mwaka huu sawa watakaa nyumbani kwa muda mrefu zaidi lakini sio mbaya sana kuliko wale walioko mashuleni.

Kama swala hili wahusika hawalioni basi nadhani siasa:- ELIMU TZ KUSIMAMIWA NA WATU WASIOKUWA NA ELIMU.
 
Kama naibu waziri wa Elimu ni dizaini ya akina Philip Mulugo aka Amim wewe unategemea nini?

Lakini haya yote tunayataka wenyewe (Watanzania) maana hawa akina Amim hawakushuka toka mbinguni, tumewachagua wenyewe! Kuna waziri mwingine wa Elimu wa CCM yeye aliwahi kufuta baadhi ya masomi, wabunge wa CCM wakapitisha UJINGA huo kwa kishindo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…