Huyu mama anaitwa mama Tairo afisa mtendaji kata ya Tabata , alitoka kituo cha kuhesabia kura za Segerea, Arnatoglo hall, mama huyo alijidai anaenda nje kununua msosi, na aloprudi watu walimwomba wamsachi ana nini watu baada ya kumsachi wakakuta anamakarasi ya majumuisho wa matokeo ambayo yalikuwa hayajapigwa muhuri wa tume, wananchi wenyehasira kali wakataka kumpa kichapo, bahati nzuri polis walikuwa karibu wakamchua yeye pamoja na hayo makaratasi wakaendae central police, Mpendazoe nae akaingia kwenye mchuma na wadau wachache na wenyewe wakaelekea central Police.
Vile vile kuna bwana mdogo muuza mihogo amekamatwa na mihuri na wino vyote mali ya Tume ya Uchaguzi, lakini baada ya mahojiano kidogo na polis katika kituo cha central walimwachia na bila aibu wala nini alirudi tena arnatoglo kucheck mambo yanaendaje.
Bado niponipo