Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Bashungwa akiwa ameambata na Waziri Wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede kutoa pole kwa Wananchi wa Nankanga, ameeleza kuwa kufuatia upepo mkali uliotokea mnamo tarehe 23 Januari 2025 na kuwakuta Wavuvi 550 wakiwa katika shughuli zao ambapo jitiada za awali zilifanikiwa kuwaokoa Wavuvi 540 wakiwa salama.
“Kwa taarifa tulizozipata sasa, pamoja na jitihada nzuri za mafanikio tuliyopata ya kuokoa ndugu zetu 540 ambao tumewaokoa kutoa ziwani kutokana na takwimu tulizokuwa nazo jana, lakini bahati mbaya kwa taarifa nilizo nazo sasa kutoka kwa wanaonendelea ukoaji ziwani tumewapoteza ndugu zetu saba” ameeleza Bashungwa saa sita mchana.
Bashungwa ameeleza zoezi za ukoaji linaendelea likiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji CGF John Masunga ambae anatumia helkopta kuwasiliana Vikosi maalum vya uokoaji ambao wanashirikiana na Wananchi ambao wana jumla ya vyombo 19.
Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea kuimarisha Jeshi la zimamoto na Uokoaji ili kuteleleza majukumu yake kwa ufanisi ambapo ameliwezesha Jeshi hilo linanunuq helikopta moja ya kuokoa na kuzima moto, magari 150 ya kuzima moto, magari 40 ya kubebea wagonjwa na boti 23 za kuzima moto na uokoaji.
Kwq upande wake, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF John Masunga ameeleza kuwa Oparesheni ya Ukoaji itaendelea vizuri kwa kuhakikisha wavuvi wote waliokuwa ziwani wanapatikana wakiwa hai au kupata miili yao.
GGF Masunga amesema Kikosi Maalum cha Askari cha Uokoaji kutoka Dar es salaam kitafika hapo Nankanga kuongeza nguvu ya uokozi kwa kushirikiana Kikosi na Wananchi wanaoendelea na shughuli hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Sumbwanga Nyakia Chirukile amesema Zoezi la Wananchi kuitambua miili ya ndugu zao linafanyika katika Zahanata ya kijiji Nankanga ili kuwezesha taratibu za mazishi kufanyika.
Awali, Diwani kata ya Nankanga, Anyisile Kayuni ametoa shukrani kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa faraja na upendo mkubwa kwa Wananchi kwa kuwaagiza Mawaziri kuja na vikosi maalum kuweka kambi na kuhakikisha ukoaji unafanyika pamoja na shughuli nyingine.