SoC04 Mikakati 5 ya kutunza vyanzo vya maji itakayo isaidia tanzania miaka 10 ijayo katika upatikani wa maji mijini na vijijini

SoC04 Mikakati 5 ya kutunza vyanzo vya maji itakayo isaidia tanzania miaka 10 ijayo katika upatikani wa maji mijini na vijijini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jaytz

New Member
Joined
Jun 13, 2023
Posts
2
Reaction score
3
Changamoto ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya mijini ina vijijini inachochewa na uharibifu wa vyanzo vya maji na hivyo kufanya kiwango cha maji kinacho patikana kiwe kichache ukilinganisha na mahitaji ya watu wa Tanzania, Hivyo ili kutunza vyanzo vya maji, Mikakati hii mitano itasaidia kuleta suluhu nchini.

1. MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UFUATILIAJI VYANZO VYA MAJI; Kama tutatumia vizuri Teknolojia ya kisasa ambayo itasaidia kuoanisha maeneo yote yenye vyanzo vya maji nchini, kisha kuifuatilia juu ya uhalibifu wake kutokana na matumizi na shuguli za kibinadam itasaidia sana kuokoa vyanzo hivyo.

2. ELIM JUU YA FAIDA ZA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI ITOLEWE KUANZIA NGAZI YA FAMILIA; Itengwe bajeti kuwawezesha watoa elim kwa umma kuwafikia wananchi walio karibu na maeneo ya vyanzo vya maji na kuwapa elim pana juu ya athari za uharibifu wa vyanzo vya maji na namna ya kuvitunza.

3. KUWATENGEA MAENEO MAALUM YA MARISHO KWA JAMII ZA WAFUGAJI; Kwa jamii za wafugaji ambao wanategemea mifugo kuendesha maisha yao ni kazi kuwaambia waache kutumia poli fulani, bali tunaweza kuwatengea maeneo mengine ya marisho ambayo hatakua na athari za uharibifu wa vyanzo vya maji

4.SHERIA NDOGONDOGO KUANZIA NGAZI YA KIJIJI ZITUNGWE ILI KUDHIBITI UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI; Kama sheria kali zitawekwa kuanzia ngazi ya kijiji juu ya udhibiti na uhifadhi wa maeneo ya vyanzo vya maji basi itasaidia kwa kiasi kikubwa juu ya janga hili ambalo kila siku serikali imekua ikitoa matanko lakini ufuatiliaji wa sheria juu ya watu wanao hatarisha vyanzo vya maji unakua mdogo.

5. BAJETI KUWEZESHA VYANZO VYA MAJI VITOE HUDUMA KWA JAMII IONGEZWE; Ni kazi sana kumshawishi mwananchi atunze chanzo cha maji hali ha kuwa haoni faida yake wala manufaa juu yake, ili mwananchi ahamasike lazima aone anapata maji safi ya kunywa kutokana na chanzo cha maji anacho kilinda, hivyo hapa serikali inatakiwa kuongeza bajeti katika wizara ya maji ili bajeti hio ikageuze vyanzo vya maji vilivyopo kutoa huduma ya maji kwa wanachi mjini na vijinini.

Hivyo tukiweka mikakati hio naimani vyanzo vya maji vitatoa maji ya kutosha kukidhi matumizi ya wanachi wa Tanzania Kwa miaka 5 hadi 10 ijayo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom