MIKAKATI BORA YENYE KUJALI MASLAHI YA WAAJIRIWA PAMOJA NA WASTAAFU.
Utangulizi
Tanzania, inakabiliwa na changamoto nyingi katika kuhakikisha maslahi bora kwa wafanyakazi na mikakati endelevu kwa wastaafu. Maslahi bora kwa wafanyakazi ni muhimu katika kujenga nguvu kazi yenye furaha na motisha, huku mikakati bora kwa wastaafu ikihakikisha maisha yenye heshima baada ya kustaafu.
Hali ya sasa ya maslahi ya wafanyakazi nchini Tanzania hairidhishi kwa baadhi ya kada nyingi, huku wanufaika wakubwa wakiwa ni viongozi wa kisiasa. Licha ya uwepo wa sheria mbalimbali zinazolinda maslahi ya wafanyakazi, kumekuwepo na ukiukwaji wa sheria hizi hali inayopelekea baadhi ya wafanyakazi kutokupanda madaraja na kukosa nyongeza ya Mishahara kwa wakati.
Tunashuhudia uwepo wa kisheria wa vyama vya wafanyakazi ambavyo badala ya kutetea maslahi ya wafanyakazi vimekua sehemu ya Siasa na kukandamiza wafanyakazi licha ya kupokea ada kutoka kwa wafanyakazi hao.
Ni vyema Serikali kujitathmini na kuchukua hatua stahiki zitakazomaliza tatizo hili angalao ndani ya miaka 5 ijayo ilikuongeza furaha na motisha kwa wafanyakazi jambo ambalo litaimarisha pia uchumi wa nchi yetu.
Mikakati yenye kuleta Maslahi bora kwa wafanyakazi.
Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini (Employment and Labour Relations Act) ni vyema utekelezaji uzingatie misingi ya sheria hii kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata haki zao za msingi kama vile kupata mshahara kwa wakati, Kupanda madaraja kwa wakati, Kufuata taratibu za kumuachisha mtu kazi na sio kutekeleza kulingana na kauli ya kiongozi au mwajiri haswa kwenye sekta binafsi.
Serikali kupitia Taasisi za Kifedha iongeze kiwango cha Mikopo kwa wafanyakazi yenye riba nafuu. Utaratibu wa taasisi za kifedha kwa sasa unatoa upendeleo zaidi kwa Wafanyakazi wenye mishahara mikubwa kupata kiasi kikubwa cha mikopo. Hivyo ni vyema Serikali iwatazame na wafanyakazi wenye kiwango kidogo cha mshahara utumike utaratibu maalumu utakaowawezesha kupata fedha za kutosha kwa ajili ya uwekezaji na kufanya shughuli za maendeleo.
Serikali iache kuingilia uhuru wa mishahara ya wafanyakazi, Hivi karibuni imesikika baadhi ya wafanyakazi katika halmashauri mbalimbali wakilalamikia kulazimishwa kutoa michango kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kupokea mwenge wa uhuru. Hii sio sawa kwani Serikali tayari inakua imetenga bajeti kwa ajili ya shughuli hiyo, Hivyo kuchangisha wafanyakazi ni unyanyasaji na kuzorotesha hali yao kiuchumi.
Vyama vya Wafanyakazi vianzishwe kwa misingi ya kisheria na kwa lengo la kusimamia haki na maslahi ya Wafanyakazi, Na si kwa lengo la kutumika kisiasa. Ada za wafanyakazi zikatumike kuwakwamua wafanyakazi kiuchumi na sio iwe fursa ya Wanasiasa au Serikali kujipatia fedha. Serikali iache kuingilia uhuru wa vyama vya Wafanyakazi kama vile chaguzi za chama. Pia mfanyakazi apewe uhuru kamili wa kuchagua chama anachokitaka endapo kuna chama zaidi ya kimoja. Mfano katika kada ya ualimu, wengi wamekua wakilalamikia kulazimishwa kujiungana CWT ilihali kuna CHAKUHAWATA.
Kuwekwe utaratibu Maalumu utakao mwezesha Mfanyakazi kudai stahiki ambazo zitakiukwa kulingana na makubaliano ya mkataba au sheria, kama vile kupanda daraja na nyongeza ya mshahara. Mfanyakazi awezeshwe kudai haki zake ambazo alinyimwa kwa utaratibu uliokiuka sheria na kulipwa fidia ya usumbufu. Tulishuhudia mwaka 2016 Raisi alisitisha upandaji wa madaraja na vyeo bila kufuata utaratibu hivyo kupelekea Wafanyakazi kukosa stahiki zao.
Serikali iweke utaratibu Maalumu wa kuboresha maslahi ya Wafanyakazi kwa kutoa posho kulingana na mazingira ya kazi. Gharama za maisha zinatofautiana katika maeneo mbalimbali hapa nchini, Mfano Mfanyakazi aliyeko mazingira ya Mjini kama Dar es salaam, anakutana na gharama kubwa kuliko mfanyakazi aliyeko kijijini kama Sumbawanga. Hivyo ni vyema kuwepo na posho maalumu ilikupunguza ukali wa maisha na kuongeza ufanisi wa kazi.
Kuwepo na Utaratibu wa kutoa Semina kwa Waajiriwa wapya, wajulishwe haki zao za msingi kisheria na wajibu wao katika majukumu. Hili bado ni tatizo katika sekta binafsi pamoja na Serikali. Waajiriwa wengi wamekua wakinyanyasika kwa sababu ya kutokujua sheria na haki zao, Huku wanaopewa semina wakielezwa majukumu yao tu na sio haki zao.
Kwa upande wa Wastaafu, Utaratibu uliopo kwa sasa bado haumwandai Mfanyakazi kua mstaafu mwenye Amani na Furaha kwenye maisha baada ya ajira. Mifuko ya hifadhi ya jamii inaendeshwa kwa misingi mibovu ya sheria ambayo imewekwa kuwanufaisha Wastaafu wa Kisiasa.
Kuongeza Malipo ya Pensheni: Serikali ibadilishe utaratibu unaotumika kwa sasa, Mstaafu alipwe akiba yake yote kwa pamoja anapostaafu, Kisha malipo ya mwezi yafate kulingana na faida iliyozalishwa na akiba ya mfanyakazi kipindi chote alipokua kazini. Utaratibu wa sasa ni Kandamizi na wa Kibaguzi kwani unatoa upendeleo zaidi kwa Mstaafu wa kazi za Kisiasa na Kumbagua Mwajiriwa kulingana na Taaluma.
Kuongeza kiwango cha malipo ya pensheni kutamsaidia Mstaafu Kufanya uwekezaji, kumudu gharama za maisha na kukidhi mahitaji yao ya msingi.
Bima ya Afya ya Taifa iwe ya kudumu baada ya miaka 20 kazini. Napendekeza Mfanyakazi akifikisha Miaka 20 kazini basi Huduma ya Bima ya Afya iwe ya kudumu endapo hatokuwepo kazini kwa sababu yoyoye ile. Hii itasaidia kuleta matumaini na furaha kwenye Maisha baada ya ajira.
Hitimisho
Kuendesha Nchi kwa kutegemea kodi za ndani kama vile PAYE na TOZO kuna chochea kupanda kwa gharama za maisha kwa sababu makato haya yanachangia kushushaa kipato, Kupanda kwa Gharama za bidhaa kutokana na wafanyabiashara kuongeza gharama ilikufudia kodi hizo, Kuzuia uwekezaji na utunzaji wa Akiba katika ngazi ya familia, Kuchochea mfuno wa bei, Na kuua au Kuzorotesha biashara ndogo ndogo kwani hazina mtaji imara wa kuweza kumudu utitiri wa kodi.
Ingawa kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi na utekelezaji wa miradi ya umma, ni muhimu kuwe na uwiano mzuri ili kuepuka kuleta ugumu wa maisha kwa Wananchi. Tumeshuhudia ongezeko la kodi mbalimbali katika Mafuta na Miamala ya kifedha bila ongezeko la kutosha la Mishahara ambalo lingechangia kuleta uwiano wa Kipato na Kodi.
Serikali zinapaswa kufikiria athari za kodi kwa maisha ya kila siku ya watu na kuhakikisha kuwa mfumo wa kodi ni wa haki na endelevu.
Serikali ijikite katika shughuli za uzalishaji zitakazochangia kuinua pato la Taifa ili kupunguza utegemezi wa mapato kutoka kwa Wananchi.

Upvote
4