SoC04 Mikakati madhubuti inahitajika kuendeleza maeneo ya kandokando ya barabara kibiashara

SoC04 Mikakati madhubuti inahitajika kuendeleza maeneo ya kandokando ya barabara kibiashara

Tanzania Tuitakayo competition threads

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Maeneo ya kando ya barabara ni fursa nzuri ya kibiashara inayoweza kutumiwa na kuleta tija nzuri kwa wakaazi na mamlaka za miji, hata hivyo, kuna umuhimu mkubwa wa kuweka mipango maalumu inayoweza kuleta namna nzuri ya kuyaendeleza maeneo hayo.

uzoefu unatuonesha kuwa katika maeneo mbalimbali ya pembezoni mwa barabara za miji na majiji, yanapendelewa kibiashara hususani na wafanyabiashara ndogondogo kwa kuweka bidhaa zao ambazo ni wepesi kuhamishika, kwa mfano ; magenge, mabanda ya maduka, na wanaouza kwa mtindo wa kutandaza bidhaa zao sakafuni, na wengine.

Uchunguzi wangu wa awali kabla ya kuandika Makala haya, umebaini kuwa maeneo ya kando ya barabara yanapendelewa kibiashara kwa sababu ya “kuchangamka”, ikimaisha kuwepo kwa abiria na watumiaji wengine wa barabara kutokana na shughuli za usafiri inapelekea maeneo kuonekana yana mvuto kwa kuwa na wateja wengi.

Hali hiyo inajionesha katika barabara nyingi za mijini, au hata zile barabara kuu zinazounganisha Wilaya au Mikoa, utaona utitiri wa fremu za maduka, vibanda vya chips, matangazo ya mawakala wa huduma za kifedha, na mengine.

Kutokana na hayo, changamoto inaibuka kwa sababu ya kukosa utaratibu maaalumu, mathalan, msongamano wa vibanda na na wafanyabiashara inapelekea wengine kuingia ndani ya eneo la hifadhi ya barabara, jambo hili si sawa kisheria na kwa usalama wa wafanyabiashara na watumiaji wa barabara.

Udadisi wangu umebaini kukosekana kwa utaratibu maalumu wa kuendeleza maeneo hayo imechangia pia tatizo la ujenzi holela, ujenzi wa nyumba za kuishi, baa, na nyumba za wageni katika eneo ambalo si rafiki kuweka uwekezaji wa muda mrefu na wa namna hiyo.

Mfano kuna maeneo mengi hususani jijini Dar es Salaam unakuta kabisa flemu za biashara, barabara zinapita pembezoni yaani hatua moja kutoka fremu ilipo, hali ambayo ni hatari kwa usalama wa wahusika.

Vilevile, baadhi ya maeneo mengine ambayo yangeweza kutumika kibiashara hayaendelezwi kwa muda mrefu, utaona kwa mfano zuio la fensi, ukuta, na mengine, jambo ambalo linakosesha faida za kibiashara kwa wakaazi ukilinganisha kama ingekua linatumika kwa shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Nini kifanyike kuongeza tija?

Mamlaka za miji na majiji kwa mfano halmashauri waweke mipango makhususi kuhusu kuendeleza maeneo ya pembezoni ya barabara za miji ambayo yanaruhusiwa kisheria kutumika, mathalan, kwa kufanya ujenzi wa fremu za maduka, vizimba, na huduma nyengine kwa kuweka miundombinu bora na mizuri.

Jambo hilo linaweza kuleta faida kadhaa, kwanza, itasaidia kuwa na mpango mji mzuri na kuvutia zaidi ufanyaji biashara, Pili, ni fursa ya kujiendeleza kwa wafanyabiashara wadogo watakaotumia sehemu hiyo kufanya shughuli zao za kibiashara, na tatu, inaweza kuwa chanzo kizuri kuongeza kiasi cha mapato ya ndani kwa mamlaka ya mji na kusadia katika kutatua changamoto nyingine mbalimbali.
Vilevile, kuwepo mwongozo wa kisheria unaotoa ulazima maeneo hayo kuendelezwa, wamiliki wa maeneo yaliyo katika mazingira hayo wapewe muda maalumu wa kuyaendeleza maeneo yao badala ya kuyatelekeza.

Marekebisho ya Sheria ya Ardhi ya Kijiji ya Mwaka 1999 na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 yanaweza kutumika kama nyenzo kuweka msisitizo huo na kueleza namna bora ya kufanikisha hilo.

Hali kadhalika, mamlaka za miji zinaweza kuja na mpango maalumu kuelendeza maeneo hayo kwa makubaliano ya pande mbili, mamlaka na wamiliki wa maeneo hayo wanaweza kuweka mtindo mzuri namna gani kila upande unaweza kufaidika na mradi utakaofanyika. Tathmini ni kitaalamu inaweza kufanyika kubaini na kuanisha maeneo yanayoweza kutumika kufanya uwekezaji huo, faida na hasara, kabla utekezaji wa mpango huo.

Miongozo hiyo inaweza kuwekwa katika maeneo yote miji na majiji, itaisadia maendeleo ya mipango miji, kuongezeka shughuli za kibiashara na ajira, kuondoa uholela wa ujenzi, na kusaidia kuleta usalama wa wakaazi wa mji na watumiaji wa barabara.

Utaratibu huo wa 'mipango miji' ukiratibiwa vizuri na kusimamiwa kwa uweledi tutakuwa na miji ya kisasa inayovutia na kuibua fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zinaweza kuchochea ongezeko la mapato pia kuepusha usumbufu na gharama nyingine inapotokea Serikali inataka kuboresha zaidi miundombinu ya barabara.
 
Upvote 1
Vilevile, kuwepo mwongozo wa kisheria unaotoa ulazima maeneo hayo kuendelezwa, wamiliki wa maeneo yaliyo katika mazingira hayo wapewe muda maalumu wa kuyaendeleza maeneo yao badala ya kuyatelekeza.
Kwamba pamoja na msururu wa fremu nchini kwetu bado tunahitaji zijengwe zaidi au sijaelewa?

Utaratibu huo wa 'mipango miji' ukiratibiwa vizuri na kusimamiwa kwa uweledi tutakuwa na miji ya kisasa inayovutia na kuibua fursa mbalimbali za kibiashara
Hata hivyo nakubaliana kwamba miji inapaswa kupangiliwa vema ivutie
 
Kwamba pamoja na msururu wa fremu nchini kwetu bado tunahitaji zijengwe zaidi au sijaelewa
Fremu zipo msururu lakini maeneo mengi hazina hadhi kulingana, lazima tuepuke ujenzi wa fremu zisizo na hadhi hususani kwenye maeneo maalumu ya kimkakati
 
Back
Top Bottom