Mikakati ya kudidimiza uchumi wa Chato

Mikakati ya kudidimiza uchumi wa Chato

Mudawote

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2013
Posts
10,771
Reaction score
14,129
GTs,

Nakuja kwenu na hisia.

Usalama barabarani barabara ya Kwenda Bukoba kupitia Chato kwa muda sasa imekua na maafisa usalama barabarani wenye nia ovu ya kuhakikisha mabasi yaendayo Bukoba kupitia Chato hayapiti ili kudidimiza uchumi wa Chato.

Kuna kipindi mabasi yote yalipita Chato kuelekea Bukoba ila vituo vilizidi vya mlungula kiasi kwamba wamiliki wa vyombo vya usafiri wakachoka. Vyombo vya ulinzi na usalama viwamulike traffic wenye nia ovu na Chato.

Nawasilisha.
 
kesho piteni hiyo njia,
hao traffic wakijua wewe kondakta ni mataga mtaruhusiwa kupita na njia itafunguliwa rasmi.
 
Wahujumu uchumi hao traffic.
Sijui huwa mnapata nini kusema uongo? Hata Kama Polisi siwapendi lakini huwa siwezi kumsingizia mtu. Kilichisababisha mabasi yasipite njia unayodai ni umbali na kukosa abiria. Mwanzoni traffic haohao walilazimisha Mabasi yapite Chato, lakini baada ya kujifanya mji umekuwa makao makuu ya nchi na kukawepo na mqbasi madogo yanayoanzia Chato wenye mabasi wakaacha. Nani aende kilomita zaidi ya 10 bure ili kufurahisha mtu?
 
huyu mataga ni msukuma wa chato ndiyo maana ameamua kuwachafua traffic bila sababu za msingi.
 
huyu mataga ni msukuma wa chato ndiyo maana ameamua kuwachafua traffic bila sababu za msingi.
Hawa watu baada ya kujua bosi wao anapenda majungu sasa wanapeleka chochote kujipendekeza. Mtu unakaa kutunga uongo ilimradi upate mkate hata kwa njia haramu. Narudia nawachukia Polisi na hata traffic najua wanakula rushwa lakini kuwasingizia kwa faida binafsi Mungu hapendi wanafiki.
 
Hakuna basi linajipangia route ya kupita. Uliona hivyo route haina ufanisi watu wanapita upande wa pili

Au mnasemaje mods
 
Hawa watu baada ya kujua bosi wao anapenda majungu sasa wanapeleka chochote kujipendekeza. Mtu unakaa kutunga uongo ilimradi upate mkate hata kwa njia haramu. Narudia nawachukia Polisi na hata traffic najua wanakula rushwa lakini kuwasingizia kwa faida binafsi Mungu hapendi wanafiki.
Wewe utakuwa traffic wa hiyo mitaa
 
Mudawote unaumwa na unahitaji tiba ya haraka.. Nakushauri wahi hospital.. Wanaopanga route sio traffic

Jr[emoji769]
 
Mudawote unaumwa na unahitaji tiba ya haraka.. Nakushauri wahi hospital.. Wanaopanga route sio traffic

Jr[emoji769]
Mshana Jr wanaochukua rushwa na kusumbua vyombo vya usafiri ni traffic. Route ikizidi rushwa wenye usafiri hubadili njia, that’s obvious.
 
Mtaga akili zenu huwa ni fupi sana.

Kipindi Magu yupo kwao kwa siku 50. Chato ilikuwa under curfew. Dola ilifanya jitihada kubwa sana kuhakikissha maambukizi ya covid 19 hayafiki mji uo.

Ndyo mabasi kutoruhusiwa kupita chato pale nyumbani kwa mweshimiwa. Hata zilizokuwa zikipita pale walikuwa hawaruhusiwi kushuka kula hotelini kama hapo awali.

Hii hali inaendelea maana ndyo "mbochi" la mkulu kujipiga lockdown. Anasikilizia tu sasa hivi. Kikinuka anakimbilia uko tena.

Sa lazima waweke jitihada nyingi kuhakikisha chato ipo free from covid 19.
 
Back
Top Bottom