Mikakati ya kumaliza migogoro ya Wakulima na wafugaji Kilosa

Mikakati ya kumaliza migogoro ya Wakulima na wafugaji Kilosa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
"Tumejipanga na tunakuja na mkakati kabambe kumaliza Migogoro ya wakulima na wafugaji, nataka tuandike pamoja historia ya kumaliza kabisa changamoto ya migogoro hii Kilosa.

Namimi nikiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hii nitaanza na watendaji ndani ya serikali ambao ni sehemu ya ustawi au wanufaika wa migogoro hiyo, hivyo niwahahakishie kama kuna mtu yeyote miongoni mwetu, anafaidika na migogoro hii ama anahusika kwa namna moja ama nyingine kuistawisha atakutana na mkono mkali wa sheria kwenye hili hatutangaliana usoni"

Kauli ya DC Shaka Hamdu Shaka wakati akiweka msisitizo asubuhi Alkhamis 16 Februari 2023 alipokuwa akiongea na Madiwani katika kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya Kilosa ambapo wakati wa. Jioni alipata fursa kufika eneo la Magomeni ambako wananchi walifikisha malalamiko yao ofisini kwake jana.

#Kilosa2Fursa2
#Maendeleo endelevu

IMG-20230217-WA0004.jpg
 
Aise.....ngoja tuone

Huu moto alianza nao

Ila kwa sisi tunaoijua kindakindaki wilaya ya kilosa na sakata la matatizo ya wakulima na wafugaji huko,naona kama maneno tu ya wanasiasa haya.

Ova
 
Post ya February 2023 na leo ni June 2024.Kwa ujumla hali sio nzuri.Siwezi kumlaumu DC Shaka kwani tatizo hili ni la nchi nzima lakini angeonyesha uenyekiti wake wa Kamati ya Ulinzi kwa kudhibiti yale maeneo korofi ya kila wakati.Tatizo lipo kwenye matumizi ya ardhi ambapo wafugaji wanaweza kuhamia kwenye vijiji vy a wakulima bila udhibiti lakini wakulima hawawezi kuhamia vijiji vya wafugaji.Lingine ni bei nzuri ya mifugo na ukwasi walio nao wafugaji.
 
Back
Top Bottom