Mikasa gani umeipitia Jf ambayo hutoweza kuisahau kamwe

Babumawe

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2014
Posts
2,556
Reaction score
2,571
Kwenye jukwaa letu pendwa kila mtu amekumbana na mikasa majanga na vituko mbalimbali ambavyo haviwezi kumtoka kwenye mind yake, mi naanza na hivi:

1. Sitosahau siku najiunga jf niliambiwa na member mmoja humu kuwa eti mimi ndio mmiliki wa JF nilishangaa sana yani iweje mi mgeni ndo niwe mmiliki. Jamaa ikawa kila nikicomment ananijia kwenye comment huku akinipamba " sawaaa boss" aisee siwezi sahau lile jamaa sijui alikuwa na nia gani.

2.Sitasahau nilivyokutana na avatar moja hivi jamvini ina dada mmoja hivi wa kiarabu kipindi hiko mimi mgeni sasa mate yakawa yananidondoka nikaanza harakati za kumlia timing PM kumbe alikuwa wa kiume jamaa alivoona namsumbua sana aliniporomoshea mitusi balaa kuanzia siku hiyo alibadilisha avatar

3.Siwezi kusahau siku moja tuliongea mambo ya kibiashara na jamaa mmoja hivi humu jamvini sasa siku tumekutana tuweke sawa plan yetu daa jamaa akawa ananitazama kama haamini vile huku kapigwa na butwaa mpaka nikawa naona soo. jamaa akawa anauliza mara mbilimbili kwamba wewe ndo babumawe namjibu akawa haamini kabisa aisee tangu siku iyo nikaona kumbe wewe unaweza ukawa unapost vitu humu kuna watu wanakuzingatia na wanakujengea picha yao.

4. Sitasahau jamaa mmoja simkumbuki aliandika thread humu kuwa yeye katembea na mademu 500 kwahiyo anatafuta wa 501, aisee ile post ilinifurahisha sana kila siku ikinijia huwaga najiuliza jamaa alikuwa anawazaga nini mpaka akaposti vile.
 
Mimi nakubwa na tatizo moja..
Kuanzia kitaa hadi hunu JF yamenikuta..

Unakuta mtu katokea kukubali tu yani na anakuja hadi PM kwa mbinu zake, then unamsikiliza vizuri.

Baada ya hapo akiona huna habari nae sana.

Anageuka anakuja kwa Sura ya pili sasa.
Ni anakuchukia hadi unajiuliza umemkosea nini.

Ladies acheni hii kitu.
 
Hawapendi kukaushiwa mkuu jitahidi kuonesha ushirikiano nao
 
ISIS huyu member sitokaa kumsahau, alikua akiamka asubuhi mpaka usiku kazi yake ni kusifia CCM na kutafuta comment zangu ili aniamshie mzigo wa maneno ya kunitafutia ban kwa nguvu. Alikua anapenda kuniita mwehu/kichaa/mtopolo/chizi n.k (Walahi alexander wewe ni chizi na ni mwehu).

Halafu admini walikua wanamfumbia macho, anaweza akakutukana wanamuacha, sasa wewe thubutu kumjibu uone, unakula ban la nguvu halafu yeye anaendelea kupiga misele JF.
 
Wengine wanazaniaga watu wa humu tunatoka sayari ya peke yetu.😂😂
 
Au ni moderator kivuli
 
Itakuwa alikuwa anakulipoti we huoni hicho ki attach Cha report kweli ulikuwa chizi Kama si mwehu..😂
 
Sina la kukumbuka wala kujutia tokea niifahamu JF.
 
Tukio moja tu siwezi sahau JF ambalo lilipelekea nikapigwa ban ya mwezi mzima.. Mshana Jr Alifiwa na Mzazi wake Akaleta uzi wa msiba huo halafu Mimi kwenye ule uzi nikaleta utani wa mambo ya Kichawi nikihusianisha nyuzi zake na ule msiba.. Aiseee Ban ni mbaya Sana.. nilivyorudishwa Hadi leo Huwa niko makini Sana kujibu chochote.. mara nyingi nimekuwa msomaji mzuri kuliko kuanzisha uzi au kujibu chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…