Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI -Sehemu ya 31


Inaendelea.............


Kwa usiku huo kiukweli nilipata usingizi wa mang'amu ng'amu kwa ile taarifa ya mrembo Zainati maana nilikuwa nikimuhurumia sana.Asubuhi ya jumapili niliamka mapema na kuendelea na shughuli zangu kama kawaida,nilitoka kuelekea maeneo ya mjini,kuna mtu nilienda kuonana naye maana nilipanga kuanza ujenzi wa nyumba za biashara ya upangishaji.

Huyu jamaa kwasababu nilikuwa nimeongea naye kwa muda hivyo nilitaka anipatie ushauri wa namna ya kufanya,jamaa kwa kuwa alikuwa mjuzi wa ramani za nyumba aliniambia kama nataka kujenga nyumba za biashara basi maeneo ya Buhongwa yalikuwa yanafaa sana.Kiukweli ushauri wake niliuchukua na nilimwambia tutaanza na nyumba tatu ziwe katika apartment moja na ahakikishe ananipatia gharama za ujenzi na majumuisho yote.Tuliachana na jamaa ilibidi nielekee zangu nyumbani kwa mama kumsalimia,nilingia kwenye gari na kuondoka,ilipofika nida ya saa 7 mchana yule shemeji alinipigia simu nikiwa hapo kwa mama,sikuweza kuongea naye ilibidi nitoke kwanza nje ndiyo niongee naye ili asifahamu mtu yeyote hapo nyumbani.

"Hello vipi uko nyumbani?" lilikuwa swali lake mara baada tu ya kupokea simu.
Nilimwambia "nimetoka kidogo sipo nyumbani"

Aliendelea kuniuliza "Utakuwa umerudi muda gani?".

Nilimwambia kama nusu saa hivi nitakuwa nyumbani maana mtu niliyeenda kumuona sijamkuta.Basi sikutaka kupoteza muda kabisa,nilimwambia dereva tuondoke zetu.Kuna vitu nilinunua hapo mjini maana nilifahamu fika yule shemu akifika haitakuwa rahisi yeye kuondoka hivyo hayo mahitaji yangetusaidia kwa siku hiyo.Nilikuwa sipendi sana kununua vitu vikakaa tu,kwani vilikuwa vikiharibika na ukizingatia mimi sikuwa sana mlaji hapo nyumbani,chakula nilipenda sana kwenda kula kwa mama.

Baada ya saa 1 kupita toka nimeongea na shemeji nilimtumia sms nikamwambia "nishafika nyumbani".

Mara nyingi toka nimemuajiri yule dereva nilimwambia kama siku ambayo nilikuwa tu ndani sitoki basi yeye anaweza kuendelea na mambo yake ila ninapomuhitaji ahakìkishe anakuwepo.Muda si mrefu alinipigia simu akaniambia ndiyo anajiandaa kutoka kwake.Zilipita kama dakika 45 akawa amefika,nilisikia kengere ya geti ikigongwa na mlinzi alimfungulia geti.
Alipofika mlango wa kuingilia ndani aligonga nikaenda kuufungua.Kama nilivyosema hapo awali,huyu shemeji alikuwaga akivaa nguo za ajabu sana,kulingana na namna alivyokuwa na umbo zuri, kama ulikuwa mwanaume mwenye tamaa lazima udenda ungekumwagika hadharani bila kificho!.Nilimkaribisha ndani moja kwa moja akafikia kwenye friji.

Bila uwoga aliniambia "hapa ni kama kwangu lazima nijiachie shem" .

Nilimwambia "hakuna tatizo shemu wewe jiachie".

kwa namna alivyokuwa kavaa nilijisemea ya kwamba dhambi ambayo ningeenda kuifanya siku hìyo haikuwa na mfano!.Alikuja amevaa skini taiti ambayo ilipaswa avae akiwa na mumewe tena usiku,niliona kabisa ilikuwa ni makusudi ya kunitamanisha.Namna alivyokuwa amependeza kiukweli ilikuwa ni taabu tupu.Alianza kunywa wine kama kawaida na nilimwambia kuna chakula jikoni endapo angehisi njaa angeenda kuandaa ale.

Aliniambia "nimemaliza kula muda huu tu shem hata usijali".

Wakati akiwa pale sebuleni nilielekea zangu chumbani kuchukua ile dawa ambayo nilikuwa naichanganya na mafuta nikajipaka na kurudi sebuleni!,wakati huu sikutaka kupoteza muda kabisa nilimsogelea na kumshika kiuno na kumwambia kiukweli Mungu alikuwa kamtunuku zawadi ya pekee sana.

"Yaani shemu uliponigusa kiuno tayari ushanitia hamu" alisema huku akiyalegeza macho.

Nilimshika mkono nikamwambia "Njoo"

Nilimpeleka kwenye kile chumba ambacho Yusta nilimpigia bakora za kim-kakati,sikuwa na haraka nilimwambia "nakuja".

Nilienda nikaichukua ile wine yake aliyokuwa anakunywa nikampelekea mle chumbani halafu mimi nikatoka kwenda kuandaa ile dawa niliyopewa na mzee nchibaronda,nilipomaliza kuiandaa nikawa nakunywa kama chai.

Nilipomaliza nilielekea kule chumbani alipokuwa,nilipoingia ndani nilikuta nguo zipo kitandani alikuwa kaelekea bafuni kuoga.Baada ya muda kidogo alitoka bafuni akiwa ndani ya taulo,sasa kwasababu alikuwa na shepu kubwa ile taulo japo ilikuwa kubwa lakini haikufunga vizuri.Nilivuta lile taulo na kulitupa chini akabaki kama alivyozaliwa,kiukweli yule shemeji alikuwa kafunga kisawasawa na alikuwa mzuri pia.Nilianza kumtembezea bakora, mara ya kwanza akawa kama mtu mwenye dharau,labda alidhani mimi mtu wa kawaida tu ambaye aliwahi kukutana nao.Bakora za kim-kakati zilipokuwa zikimtembelea ndipo nilianza kuona akianza kuhangaika.Kwa namna ambavyo nilikuwa nina usongo naye,sikutaka kabisa kumuonea huruma hata kidogo,nilitaka nimshikishe adabu kisawa sawa,huyu shemeji nilikuwa ninausongo naye sana kwasababu nilikuwa nina lengo la kumkomoa kwa sababu ya nyodo na dharau zake.Baada ya bakora kumkolea alikuwa akitamka maneno ambayo mengine hata nilikuwa sielewi anasema nini!.

Baada ya kuwa amepumzika kitandani aliniambia "Kwanini hukunitongoza mapema shem maana kumbe hizi raha zote nilizokosa kwa muda mrefu!".

Nilimwambia kwasababu ilikuwa inaelekea saa 1 usiku aondoke maana watoto wako peke yao.

Alinijibu kwamba "siwezi ondoka leo nikaziacha hizi raha".

Nilimuuliza "watoto kule nyumbani wako na nani".

Akanijibu "wako na dada yao wa kazi hivyo haina shida!".



Itaendelea......................
 
Mkuu please naomba unielekeze kwa Babu huko congo na pia Kama una namba yke ya simu ,nishachoka maisha yakibwege
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 32

Inaendelea.............


Usiku huo kwa upande wangu ulikuwa mzuri sana na nilijiona mtu mwenye bahati sana kuliko binadamu wengine wote.Asubuhi ilibidi nimwamshe ili awahi kazini alikuwa amechoka sana lakini hakuwa na namna ilipaswa aende kazini hivyo hivyo.Aliondoka akawahi kwake ili akajiandae aende kazini.

Wakati anaondoka aliniambia "Wewe utanivunjia ndoa yangu ujue".


Nilimuuliza "kwanini unasema hivyo?"

Aliniuliza " Kwani hujui?".

Nilimwambia kamwe siwezi kumuachisha kwenye ndoa yake,mimi kiukweli nilitaka yeye ndiye awe mke wangu.Baada ya siku hiyo kuachana na shemeji niliendelea na shughuli zangu nyingine.Kumbuka kwamba mle kwenye kile chumba nilikuwa naingia mara mbili kila mwezi,labda itokee vinginevyo!.Kila tarehe 15 ya kila mwezi niliingia kuchukua pesa na kila mwisho wa mwezi niliingia kupeleka kibuyu chenye damu ya kafara!,kile kibuyu nilisema toka mwanzo kwamba kilikuwa ni kidogo lakini kilikuwa na mambo makubwa sana!.

Endapo ungeambiwa ukibebe bila kuwa na dawa maalumu usingeweza hata kukinyanyua,kilikuwa na uwezo wa kubeba damu lita 200 kwa wakati mmoja!.Ulipofika mwisho wa mwezi nilipanga kwenda kwenye mawindo ya kafara kama kawaida.Mawindo ya kafara nilikuwa natoa eidha kwa kuagizwa na Malikia kwa watu aliyowahitaji yeye au bila kuagizwa!,alimradi ikifika mwisho wa mwezi damu isikauke ndani ya kile chumba!.

Basi siku moja usiku nakumbuka nilijiandaa vyema na nilikuwa nimepanga kwamba usiku huo tukio ningeenda kupiga maeneo ya Bugando,nilifanikiwa kuondoka mle ndani kama kawaida,niliushika mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na irizi nikatamka ya kwamba "nataka niwe maeneo ya Bugando"(Si hospitali),Pale bugando kwa wenyeji wa Mwanza ukiwa unapanda kuelekea hospitali,kunakuwaga na mwinuko mkali sana na kwa wanaoshuka huwa ni mteremko mkali,hapo ndipo nilipoenda kutega usiku huo,nilijua gari zote zitakazo kuwa zinashuka lazima nichague moja ili waipate freshi!.

Kuna gari niliiona inakuja kwa mbali ikiwa inatokea maeneo ya hospitali,nilijaribu kuingalia kimazingara nikaona kabisa waliomo ndani ni weupe kama karatasi hivyo wasingenizuia mimi kufanya nililokusudia kwa wakati ule.Basi nilifanya haraka nikaenda nikaweka lile tego halafu kisha nikarudi zangu pembeni kuangalia matokeo.Lakini kabla lile gari halijafika pale kwenye tego lilisimama,kuna mwanamke mmoja alishuka,alikuwa kavaa nguo za vitenge,alikuwa akitazama yale maeneo niliyotega tego na alipomaliza alikuwa akinitazama sana!,mwanzo nilidhani hanioni,nilipomwangalia tena na kugonganisha macho niliona tu ghafla mwanga mweupe kama mwali wa moto na sikufahamu kiliendelea nini!.Nilikuja kushituka niko chini,nilikuwa nina maumivu kidogo,nilikuwa nimerushwa pembeni ya barabara nilipokuwa nimesimama,nilijaribu kuangalia kama kuna mtu yeyote ambaye ameniona lakini nikakuta hakuna aliyeniona maana ilikuwa usiku mida ya saa 5,niliamka nilipokuwa nimelala na kushika mkono wangu wa kushoto na kutamka kama ambavyo nilikuwa nikifanya nikajikuta nimo ndani ya kile chumba cha siri.

Kiukweli nilikuwa nina mawazo sana na sikuelewa ni nini kilichoendelea maana nilikuwa kama nimepigwa na shoti ya umeme!,nilifunga kile chumba nilaelekea zangu chumbani kulala nisijue la kufanya,kumbuka hiyo ilikuwa mwisho wa mwezi na siku ambayo ilikuwa inafuata ilikuwa tunauanza mwezi mpya!.Asubuhi kama kawaida nikiwaa bado nimelala ikiwa mida ya saa 1 asubuhi nilisikia ile sauti ya yule Malikia ikiita chumbani,ilibidi niamke niende bila kupenda,nilipofika nilimkuta yule Malikia akiwa anatoka machozi ya damu,akaanza kuniambia "Kwanini unanitesa?".

Kiukweli sikuwa na majibu zaidi ya kuangalia chini nikiwa natetemeka kwa uoga!.

Aliendelea kuniuliza"Kwanini unanitesa?"

Nilimwambia "tafadhali nisamehe na nakuomba naigize chochote nifanye ila usiniue"

Basi akaniambia "Namtaka huyu,hakikisha ndani ya masaa 24 niwe nimempata huyu"

Pale aliposema anamtaka huyu niliangalia vizuri ukutani mle ndani ya kile chumba ndipo nikaona alikuwa ni mtoto wa kike wa dada yangu mkubwa aliyekuwa akisoma,wakati huo alikuwa akikaa kule nyumbani nyegezi kwa mama.

Basi nilimjibu "sawa Malikia umempata!"

Baada ya hayo maagizo akatoweka!,kiukweli mpaka wakati huo sikuelewa ni nini kilitokea lakini kwasababu nilikuwa nikiyaelewa mambo hayo sikupata shida sana.Sasa labda hapa niseme kitu,ni kwamba yule mwanamke aliyeshuka kwenye gari na waliyokuwa kwenye ile gari pale Bugando,walikuwa wakilindwa na nguvu ya Mungu,maana wangekuwa washirikina kuna namna ambayo tungejibishana,siku zote mshirikina akiwa anataka kufanya tukio la kishirikina ni lazima kwanza aangalie rada zake kama zinasoma na mimi ndivyo nilivyofanya,mara nyingi ukikuta hata watu wanalindwa na Mungu unakuta rada zako zinasoma na kukwambia kwamba hao ni wepesi kama karatasi lakini cha moto hatimaye hukipata!.Mimi nilipima ile gari kwenye rada zangu zikasoma kumbe haikuwa kama nilivyodhani maana ilikuwa ni hatari na namshukuru Mungu akuniua maana huwa ni matukio machache yanayohusu mkono wa Mungu na ukatoka salama labda kama Mungu ana makusudi na wewe ndiyo utatoka salama lakini pia bado unaweza poteza viuongo vya mwili kabisa!.

Basi niliendelea kuwaza namna ya kumtoa kafara yule mtoto wa dada kwasababu nilipewa masaa 24,sikutaka kupoteza muda kabisa!.Nilijiandaa kikamilifu kimazingara na nilihakikisha hatochukua raundi maana nilikuwa nina hasira sana kwa kuwakosa wale watu ule usiku pale Bugando,sikuwa na namna ilipaswa nitekeleze ile amri.Basi nilipomaliza kujiandaa kikamilifu nilimpigia simu dereva nikamwambia aje twende anipeleke nyegezi kwa mama,hiyo ilikuwa mida ya saa 7 mchana,nilitegea mida ya kutoka shule ili nimalize kazi maisha mengine yaendelee.Nilipofika hapo nyumbani nilimkuta mama nikamsalimia lakini aliniambia "mbona kama unawasiwasi mwanangu unashida gani?"

Nilimwambia "ni uchovu tu mama siunajua tena ubize"

Basi mama alinipakulia chakula mimi na dereva tukaanza kula,wakati tukiwa tunakula,mama alianza kuniambia habari kuhusu yule ndugu yangu mwingine ambaye hapo mwanzo nilisema kwamba kwetu tulizaliwa watoto 4,wawili tulikuwa wa kiume,sasa huyo ndugu yangu ambaye yeye alikuwa akiishi kwa shangazi wakati sisi tukiwa Tarime,mama anasema alipata habari zake kwamba jamaa kazamia Afrika kusini!.Mimi na huyo ndugu yangu tulikuwa hatupatani toka mwanzo maana kuna wakati alikuwa akitoka kuvuta bangi na kunywa pombe anamtuhumu mama kwamba ni mchawi anamroga ili mambo yake yawe magumu,kitu ambacho kilikuwa si kweli,hivyo niliapa mimi na yeye ni mbalimbali!.

Huyo kaka yangu alipenda sana kukimbia kimbia,yaani alikuwa hakai akatulia sehemu moja,hivyo na mimi sikuwa na habari naye maana kila mtu na maisha yake.Basi wakati tukiwa tunaendelea kula yule mtoto wa dada alikuwa katoka shule akawa anatusalimia pale,nilimuita nikaanza kumshika kichwa nikiwa kama namsihi asome kwa bidii,nikawa namwambia akiwa na shida asisite kuniambia wakati wowote nitamsaidia maana ninapo muona yeye nikama nimemuona mama yake!.

Aliondoka kuelekea chumbani kubadili nguo na mimi nikajua tayari nishamaliza mchezo.Mara ghafla alitoka ndani akiwa anavuja damu puani na alikuwa akimuita mama "Bibiii.....bibiii...bibiii".

Nilipomuona nilimwambia "Umekuwaje wewe?".

Kiukweli nilikuwa ninaumia sana ila sikuwa na namna maana nisingefanya hivyo mimi ndiye nilikuwa naondoka.

Nilikuwa namuuliza "Hili tatizo huwa linakutokeaga?"

Yule binti akawa anasema "Ni leo tu mjomba maana baada ya kuingia ndani ndiyo kichwa kimeniuma na kuanza kutoka damu!"

Nilimwambia dereva wangu amchukue amkimbize hospitali,mama alijianda wakawa wametoka wote!.Basi walipotoka mimi nilijifanya nampigia simu dada yangu na nikamweleza kwamba nilikuwa nimekuja kwa mama kumsalimia ila binti yake ghafla aliporudi kutoka shule alianza kutoka damu puani.Yule dada yangu alikuwaga mpole sana na kiukweli nilimuhurumia sana lakini sikuwa na namna!.

Aliniambia "Sawa kaka ngoja nimpigie mama simu"

Baadae alinipigia simu akaniambia "Nimempigia mama simu analia tu kaka,kwani kuna nini?".

Nilijua fika mambo yalikuwa yameshaharibika.Nilimwambia akate simu yake nimpigie mama,nilipomaliza kuongea naye,yule dereva wangu akawa ananipigia simu!.



Itaendelea..............
 

Endelea mkuu story imenoga [emoji4]
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 33


Inaendelea.............


Baada ya dereva wangu kunipigia simu alianza kuniambia "Boss huyu dogo katufia hata kabla hatujafika hospitalini".

Nilimwambia dereva waipeleke ile maiti ya yule mtoto wa dada hospitali ya mkoa pale Sekou Toure.Kiukweli niliumia sana,nilikuwa nikimuhurumia dada yangu na ukizingatia yule mtoto ndiyo alikuwa binti yake mkubwa.Nilipokuwa nikiua au kutoa kafara watu wengine niliona kawaida na nilikuwa siumii sana,ila ndugu zangu na watu wangu wa karibu waliniuma sana lakini sikuwa na namna,mimi nilitaka hela tu kwa wakati huo.

Baada ya muda dada yangu alikuja nyumbani Nyegezi,kwakuwa alikuwa keshampigia mama na kumweleza kilichotokea alianza kulia sana,nilijaribu kumtuliza lakini haikuwa kazi rahisi kunyamaza,majirani walianza kujaa pale nyumbani na muda si mrefu dereva na mama walirudi wakasema mwili wameuhifadhi hospitali ya mkoa.Nilimwambia dereva kwakuwa yeye ni mtoto wa mjini,ajaribu kutafuta watu waliyokuwa wanatoa huduma za maandalizi ya misiba kama vyakula,maturabai pamoja na viti.Ule msiba niliugharamikia kila kitu na hatimaye yule binti alizikwa!,kabla ya mazishi ya yule mtoto wa dada nilienda nyumbani kutengeneza dawa ambayo hata kama wangekuwa na wazo la kwenda kwa mganga kuangalia kuhusiana na kile kifo,basi hilo wazo liwatoke mara moja.

Baada ya ule msiba kupita namshukuru Mungu hakuna ndugu au majirani walionihisi vibaya,Kweli!,ndani ya zile siku 15 za pesa kutoka,nilielekea mle chumbani na kukuta pesa zikiwa zimejaa kile kibegi kama kawaida,nilizitoa na kuzipeleka kwenye lile begi kubwa ambalo nalo lilikuwa humo humo kwenye hicho chumba.Wazo nililokuwa nalo sasa ni kumnunulia dada yangu gari.

Nilimpigia simu nikamwambia "Dada bila shaka utakuwa umepoa sasa,mdogo wako nataka nikununulie gari niambie unataka gari gani?"

Dada aliniuliza"mdogo wangu umesha-make money kwenye biashara uliyoniambia?".

Nikamjibu "ndiyo".

Basi akaniambia nimpe muda ashauriane na mumewe angenijulisha.Zilipita kama siku mbili alinipigia simu yule jamaa ambaye nilimpa kazi ya kunithaminishia nyumba tatu kuwa kwenye eneo moja ingegharimu kiasi gani.

Yule mtaalamu aliniambia "Mkuu gharama za hizo nyumba zote kwa matilio uliyo taka wewe zitagharimu kiasi cha milioni 150".

Nilimjibu nikamwambia "sawa,ngoja mwezi huu uishe ili tuanze kazi".

Lengo langu ilikuwa ni mpaka ifike mwisho wa mwezi nikipiga tukio la kafara ndiyo tuanze ujenzi maana ningekuwa na pesa ya kutosha.Nakumbuka usiku wa siku hiyo nilipotoka kuongea na huyo mtaalamu nilipata ndoto ambayo nilisikia kabisa kwa sauti ikisema "wewe unataka ujenge kwa pesa zetu siyo?,naona unataka kutujaribu".

Ile ndoto ilifanya nikashituka usiku kama mwendawazimu,nilihamaki sana ile ndoto ilikuwa na maana gani!.Basi asubuhi na mapema nikawahi mle chumbani, kuna maneno nilikuwaga nayatamka endapo kama kulikuwa na jambo baya nililolihisi,kama nilijibiwa kwa sauti humo ndani basi nilijua halita nipata lakini kama ilikuwa kimya nilikuwa najiepusha nalo mapema maana niliogopa nisije tolewa kafara mimi.Kiukweli lile jambo la kutaka kwenda kujenga nyumba lilikuwa ni kosa kubwa maana nilipokuwa nikitamka yale maneno,humo ndani kulikuwa kimya sana,nilishindwa kuelewa kwanini iwe vile!.Nilikuwa najisemea "yaani kafara nitoe mimi na bado pesa wanipangie matumizi?".

Sasa kwakuwa sikuridhika siku hiyo,usiku tena nilirudi kule chumbani nikaanza kuita kwa kusifu kwa kumtukuza yule Malikia ambaye siku zote alikuwa akija humo chumbani.Baada ya muda kidogo nilisikia mwili unasisimka mpaka nywele zikawa zimesimama,nilipogeuka nyuma nilishitukia yule Malikia yuko nyuma yangu akiniangalia kwa hasira!.

Aliniuliza kwa ukali "Mbona unahangaika?".

Niliinama kifudifudi kwa kusujudu na nilimuuliza "ile ndoto niliyokuwa nimeiota usiku ilikuwa na maana gani?"

Aliniuliza "Kwanini unapenda kuhangaika na mali za wenzio?"

Nikamuuliza "Mbona mimi sijahangaika na mali za mtu Malikia?"

Ndipo aliniambia mali zote nilizokuwa ninamiliki zilikuwa si zangu bali hizo mali zilikuwa na wenyewe na wenyewe ndiyo hao walionipatia mimi!.

Aliendelea kuniambia kwamba "Mali zote ulizo nazo hata hilo gari ulilonalo ni mali yetu na ina nembo yetu,hii nyumba unayoishi ni mali yetu na ina nembo yetu,mikufu uliyomnunulia mwalimu wako kipenzi ilikuwa na nembo yetu na ni mali yetu,vitu vyote tunavyoruhusu ununue na umiliki ni ni mali zetu"

Baada ya kunieleza na mimi kuelewa aliniambia "Ninakupenda sana na ndiyo maana nilikupa irizi ambayo ilitoka kiunoni mwangu,hakuna mtu niliyewahi kumpa hiyo irizi hivyo naomba usije niudhi tena".

Baada ya hayo maelezo ghafla alipotea machoni kwangu!.Niliondoka humo chumbani nikafunga mlango,kiukweli hapa sasa ndiyo nikaanza kupata picha yote maana kumbe mali zote nilizokuwa namiliki walitaka wao nizimiliki na ilikuwa ni lazima ziwe na nembo ya kwao ambayo waliifahamu wao tu!.Ndiyo maana hata hiyo nyumba yangu wakati naenda kuinunua hakukuwa na vikwazo sana maana ilikuwa ni mali yao toka mwanzo hata kabla sijainunua,lile gari lilikuwa mali yao hata kabla ya kulinunua hivyo isingekuwa rahisi kupata kitu kipya kisicho kuwa na nembo yao!.Niliumia sana lakini sikuwa na namna,basi siku iliyofuata dada alinipigia simu akaniambia kwamba ameshauliana na mumewe wafungue biashara,niliposikia anasema biashara nilimuuliza biashara gani?.Dada aliendelea kuniambia kwamba anataka aanze biashara ya kutoa dagaa na samaki kutoka Mwanza kwenda kuwauza Dar es salaam.Nilikuwa nikikumbuka maneno ya Malikia usiku,kwamba hata biashara ni lazima iwe ya kwao,kiukweli nilimwambia dada aachane na ile biashara maana nilifahamu fika huko mbele ingemletea shida.Wazo langu ilikuwa ni kumnunulia gari maana nilijua gari angefaidi utamu wa kuendesha lakini biashara angeweza kula hasara huko mbeleni.

Aliniambia "Basi sawa kaka wewe ninunulie tu hata vitz itanitosha".

Nilimpigia yule jamaa ambaye aliniuzia gari langu nikamwambia anitafutie vitz mpya.

Jamaa aliniambia "Sawa boss umepata".

Nilijua mpaka ile vitz ingefika kwa dada yangu, ingekuwa na chapa ya wenye mali.Jamaa aliniambia nimwandalie milioni 11,nikamwambia dereva wangu ampelekee zile pesa na hiyo gari aichukue aipeleke kwa dada yangu.Pia kuna hela kama laki tatu nilimpa nikamwambia ampeleke dada kwa ajili ya kununua mafuta na matumizi yake mengine madogo.

Basi maisha yakasonga,nakumbuka mwisho wa mwezi ulipofika nilitakiwa kufanya kafara kama kawaida,safari hii nilielekezwa nielekee mkoani Singida tena.



Itaendelea...............
 
Hapo kwa mtoto wa dada yako kufariki nimejikuta natoa machozi
Jamani tutafute pesa kihalali, huyu jamaa nadhani kaja kutuonesha jinsi duni ilivyo na mambo ya ajabu, unakuta mtu anavmba kabsa kitaani kumbe mali anazomiliki za miujiza

R.I.P Kanumba ulikuwa na moyo wa ujasiri kutokumuua mama yako,
 
Magere upo wp njoo huku
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 34

Inaendelea.............


Nilijianda kikamilifu maana nilielewa nisingejiandaa vizuri,ingekuwa vigumu endapo ningekutana na vikwazo vya kichawi,nilingia kwenye kile chumba cha siri nikachukua zana za kazi na nilihakikisha kila kitu kipo sawa,niliapa safari hii sitaki kabisa mchezo!.Mpaka wakati ule nilikuwa nimejaa hasira sana kama nimelishwa sumu.Eneo ambalo niliambiwa nikafanye tukio la kafara ilikuwa ni Singida eneo moja linaitwa Kilimatinde na eneo lile lilikuwa katikati ya Dodoma na Singida,hapo ndipo nilipaswa kuwepo siku hiyo.

Basi kama kawaida niliushika mkono wangu uliyokuwa na irizi nikatamka tu ya kwamba,inapaswa niwe eneo la tukio,kilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua nikawa lile eneo la Kilimatinde.Nilipofika hapo haukupita muda nikaanza kuiona ile gari nilionyeswa kwa mbali ikiwa inakuja!.Ile gari ilikuwa Hiace fulani ndogo na nadhani ilikuwa inapiga ruti za huko vijijini,nilipoitazama ilikuwa imejaa sana watu,niliwatazana hao abiria waliokuwemo ndani,kiukweli hakukuwa na mwenye uwezo wa kunizuia kufanya kafara.Nilisogea mpaka katikati ya barabara,safari hii nilikaa mimi mwenyewe kwenye ile barabara maana sikutaka kabisa niweke tego halafu nikae pembeni,nilitaka hiyo gari na hao abiria niwashughulikie mimi mwenyewe kwa mkono wangu!.

Ilipozidi kunikaribia nilinyoosha ule mkono wa kushoto uliyokuwa na irizi,ndipo ikaongeza spidi mara mbili ya uwezo wake wa kawaida na nikailekeza kwenye korongo ambapo ilienda ikapiga kwenye mwamba mmoja ikawa ny'anga nyang'a,nilipoona mambo tayari nilianza kusogea kwa ajili ya kufanya kilichonipeleka,safari hii niliapa sitorudia makosa kama niliyoyafanya Bungu.Basi nikakuta kuna watu wengine wamekufa papo hapo na wengine waliendelea kuteseka kwa maumivu,nilikichukua kibuyu nikaanza kujaza damu kama kawaida,nilipoona damu zimefika kipimo nilichokitaka sikutaka kupoteza muda niliondoka zangu hilo enek kama upepo!.Hilo tukio halikuchukua hata nusu saa nikawa nishamaliza,nilipofika nyumbani kwenye kile chumba cha siri,niliweka kile kibuyu ambapo kilikuwa kinakaa kisha nikafunga kile chumba na kutoka kuelekea chumbani kwangu.Ile kazi ya utoaji wa kafara ilikuwa ngumu sana lakini sikuwa na namna maana tayari nilishafanya agano vinginevyo nisingetimiza wajibu basi mimi ndiye ningetolewa kafara,sikutaka kabisa iwe hivyo!,ule uoga wa mara ya kwanza wakati nainza kazi ya kutoa kafara ulikuwa umetoweka kabisa maana sasa nishakuwa mzoefu!.Ile Irizi niliyowekewa mkononi ilinifanya niwe nina kiburi cha ajabu maana watu wengine niliwaona si chochote wala lolote!.

Hivi ndugu zangu huwa mnaelewa ni kwanini ajali nyingi nchi hii ya Tanzania huwa zinatokea sana Singida,Mbeya na Morogoro,na kuna eneo moja pia liko kule Karatu?,Je ulishawahi kujiuliza hilo swali?.Ngoja niwaeleze leo mkae mkifahamu.

Ukiachilia mbali ajali za kawaida ambazo huwa zinasababishwa na matatizo ya chombo husika au uzembe wa madereva,lakini asilimia 90% za ajali zinazotokea hayo maeneo niliyoyataja huwa zinasababishwa na Ushirikina,wakati mimi bado sijaanza kuwa tajiri wa kutoa kafara,miaka ya nyuma pia nilikuwa nikijiuliza sana hayo maswali kwamba kwanini ajali nyingi kubwa huwa zinatokea sana hayo maeneo niliyoyataja lakini baada ya mimi mwenyewe kushiriki mara kadhaa ndiyo nilipokuja kuelewa ni nini chanzo!.Hayo maeneo niliyoyataja kitaalamu kwa kishirkina yanaitwa LANGO KUU au MNADANI,ikiwa na maana kwamba washirikina wote wa nchi hii(wachawi)wakitaka kwenda makao makuu ya wachawi ya hapa Tanzania ilikukwepa migongano ya kimaslahi huko angani basi hupitia hapo kwenye hiyo mikoa niliyoitaja,Kaa ukifahamu kwamba angani pia washirikina wanamiliki maeneo yao na kuna maeneo ambayo kama una nguvu ndogo hupaswi kupita kabisa maana unaweza jikuta unakufa na wanakula nyama,hivyo angani unakuta kuna maeneo yanamilikiwa na wachawi wakubwa na wenye nguvu kubwa hivyo wachawi wengi huwa wanachukua tahadhari mapema.Sasa kwakuwa hayo maeneo niliyoyataja ndiyo lango kuu,hivyo ishazoeleka kwa washirikina wakiwa wametumwa kafara wengi wao huwa wanatega maeneo yaliyo jirani na kuingia au kutoka huko makao makuu ili iwe rahisi kwao kuchukua hizo kafara,ndiyo maana hayo maeneo huwa ajali haziishi.

Bado sijajua nieleze vipi ili mnielewe lakini fahamu hivyo ndiyo huwa inakuwa,sasa kwasabu mimi sikuwa mchawi bali mshirikina hivyo ndiyo nilielewa,kama kutakuwa kuna mtu humu ndani aliwahi kuwa mchawi na akaacha na anasoma huu uzi tafadhali namuomba aje atoe ufafanuzi vizuri maana ndivyo ilivyokuwa inafanyika.Hata lile tukio lililotokea hapo Morogoro majuzi na kuua mamia ya watu kwa kuripukiwa na mafuta nilikuwa nasikia watu wanasema ile ni kwasababu kuna jamaa alichomoa betri ya gari,hivyo gari ikapiga shoti ikaripuka.Ndugu zangu ile ilikuwa ni kafara na hayo mambo ya kuchomoa betri ilikuwa ni kuwapumbaza wasiyo elewa,kwasababu mimi nilikuwa ninafahamu nilibaki tu nawahurumia watu waliyokuwa wanasema eti ni kwasababu betri ilichomolewa!.

Basi baada ya lile tukio niliingia kulala mpaka ilipofika mida ya jioni nilipo shitushwa na simu ya yule jamaa aliyekuwa mtaalamu wa majengo alikuwa akiniuliza "bosi umefikia wapi?".

Nilimjibu kwamba "nimeahirisha,pesa nilizokuwa nazo nimezipeleka kwenye majukumu mengine,nikipata pesa nitakujulisha ili tuanze ujenzi".

Muda haukupita alinipigia simu shemeji na kuniambia angekuja nyumbani baadae!,kwakuwa akukuwa na vyakula kwa wakati huo nilimwambia dereva twende zetu mjini nikafanye manunuzi ya vitu ambavyo huyo mwanamke angefika aanze kuvitumia kwa siku hiyo!.Ilipofika jioni mida ya saa 11,shemeji alikuja akiwa ndani ya gari yake huku bado akiwa na sare za kazini kwake!.

Nilimuuliza "mbona leo mama umekuja umevaa sare za kazini?".

Akanijibu "leo nalala hapa ili ikifika asubuhi nisihangaike kwenda nyumbani kuvaa"

Ulikuwa umepita muda tangu nilipofanya ngono na yule shemeji hivyo kiukweli nilikuwa nina njaa sana ya ngono!.Basi nilimpeleka kule chumbani kwa siku zote ambako ni maalumu kwa ajili ya kuwakarabatia,alibadili nguo akavaa traki ambayo nilimpatia ya kwangu na shati,kama kawaida yake ilikuwa ni lazima anywe kwanza wine ndiyo mambo mengine yaendelee.

Alianza kuniambia "Yaani shemu lazima ndoa yangu ivunjike maana nishaanza kuchanganyikiwa na wewe".

Mimi nilimjibu kwamba "sitaki kuivunja ndoa yako mama,mimi nataka tu tuwe tunafanya halafu wewe unaendelea na mambo yako"

Alisema "Aisee siwezi kuendelea tena na yule mwanaume maana alikuwa hata hanipi raha kama nazo zipata kwako"

Sasa nikawa najisemea kimoyo moyo "Alikuwa hakupi raha vipi mpaka umemzalia watoto wawili?".

Any way nilijua ni yale madawa yamemkolea shemeji,kwasababu nilitaka iwe hivyo nilikuwa ninafurahi kimoyo moyo maana nilidhamiria toka mwanzo awe mke wangu ambaye atakuwa ananizalia watoto ili niwatoe kafara.



Itaendelea.................
 
Dah! Ushirikina siyo mzuri kwa kweli. Ona LwandaMagere anavyoteseka na pesa ya kishirikina,nje anaonekana mwenye furaha lakini ndani ya nafsi yake ana maumivu mazito sana.
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 35



Inaendelea.............




Alipomaliza kuandaa chakula tulianza kula huku tukipiga stori za hapa na pale.

Alianza kuniambia "Najuta sana kwanini sikukufahamu mapema shemu".

Nilimuuliza "kwanini shemu?"

Aliendelea kuniambia " Kama ningekufahamu mapema huyo mwanaume nisingezaa naye maana nimetokea kukupenda wewe shemu,naomba kuanzia leo jina la shemu life nataka uniite mke wako".

Mimi nilijua fika ni ile dawa ndiyo inafanya kazi,sikuwa na hiyana nikaanza kumuita mke wangu kuanzia siku hiyo.Sikujuta kamwe kufanya maamuzi ya kumpata yule shemeji maana niliona ulikuwa ni muda muafaka mimi kuwa naye,japo sikutaka kabisa ndugu zangu waelewe chochote.Baada ya bakora za kim-kakati usiku kucha,nilipitiwa na usingizi,alinishitua tena usiku na nilipoangalia simu ilikuwa mida ya saa 10 usiku!.

Alianza kujisemesha "Mwenzio usingizi umekata".

Nikamuuliza "kwanini mke wangu?".

Akaniambia "Nipe tena kidogo".

Sasa kwasababu ile dawa niliyopewa na mzee nchibaronda ilikuwa na nguvu za ajabu,sikwenda kuinywa tena,bali nilianzia pale nilipoishia!.Nilimshughulikia mpaka mida ya saa 12 asubuhi,ndipo nilipoamuachia maana alianza kulia mpaka nikawa namuhurumia.


Baada ya muda aliniambia "Siku ukiniacha nakunywa sumu".

Nilimwambia "Usijali mama hapa ndiyo umefika hakuachi mtu".

Basi asubuhi hiyo alijiandaa kuelekea kazini kwake,alipokuwa tayari nilimtoa nje akawa anasema "leo sijui kama nitafanya kazi maana nahisi kuchoka".

Alipoondoka nilirudi zangu ndani kulala maana nilihisi uchovu sana.Sasa yale maisha yakaanza kumkolea shemeji na kuna baadhi ya marafiki zake aliyokuwa akifanya nao kazi wakawa wananiita shemeji,nilikuwa nikimwambia bado mapema sana yeye kufanya hivyo lakini aligoma kabisa akawa anasema yeye ndiye kaamua iwe hivyo nisimpangie!.Basi mpaka wakati huo mama yangu na huyo shemeji walikuwa hawapatani kabisa maana ile kauli aliyowahi kuitamka kipindi cha nyuma ilimuudhi sana mama mpaka akawa analia!.

Siku moja dada yangu alinipigia simu akaniomba kama nitaweza kwenda kwake basi nifanye hivyo maana alikuwa na mazungumzo na mimi.Sikuchukua muda sana ilibidi niende,nilipofika wakati tunapiga stori za hapa na pale alianza kuniuliza "Mdogo wangu kwani unatembea na........(shemeji)?".

Nilimwambia "Hapana,kwani kuna nini?".

Dada aliendelea "naomba unieleze ukweli mimi nafahamu kila kitu maana mpaka kukuita hapa naelewa kila kitu".

Niliendelea kumkatalia,lakini ilibidi aniambie kwamba "wifi alinipigia simu toka juzi akanieleza wewe na yeye ni wapenzi na akasema mnakaribia kufunga ndoa".

Dada yangu alikuwa akimuita wifi kwasababu kaka yake alikuwa amemuoa yule dada yetu mwingine ambaye mimi nilikuwa nikimfuatia.Ukiachilia uzuri aliyokuwa nao yule shemeji lakini pia alikuwa na machepere sana,hakuweza kukaa na ile siri ilibidi aimwage hadharani!.Sasa kwasababu alikuwa ameshamwambia dada,sikuwa na namna ilibidi nimwambie dada yangu kwamba,kila alichoambiwa ilikuwa kweli!.

Dada aliniambia "Mbona unatutia aibu?,ina maana kweli umekosa wanawake mpaka ukatembee na shemeji yako? kibaya zaidi ana mume wake,mume wake akijua unadhani itakuwaje?".

Aliendelea kuniambia "Shauri yako maana ushakuwa mtu mzima na kila mtu ana maamuzi yake hofu yangu mdogo wangu ni huyo mumewe akijua unadhani atalichukuliaje?".

Sikuweza kumjibu kitu chochote dada yangu maana niliona aibu mbele yake lakini rohoni mwangu mimi ilikuwa ni safi tu maana nililipanga hili toka zamani!.Sasa kama mjuavyo maneno ambavyo huwa yanasambaa kama moto wa nyika,yale maneno yalimfikia mam na haikuchukua hata wiki dada alinipigia simu akasema "mama yako anakuita anamazungumzo na wewe".

Nilifahamu tayari maneno yalishamfikia mama,nilijua dada yangu asingeweza kumwambia maana alikuwaga mpole sana na hakuwa na maneno ya umbea umbea!.Dereva alinichukua kuelekea kwa mama,sasa wakati tukiwa njiani nilikuwa nikipiga stori na dereva wangu naye akawa ananipa mtazamo wake kuhusu hilo suala.

Dereva alikuwa akiniambia "Bosi wewe miliki ile mashine,kama kakupenda mwenyewe na hujamwibia huyo mume wake,wewe miliki".

Kwakuwa mimi nilikuwa naielewa picha nzima hivyo sikupata taabu sana.Muda si mrefu nilifika Nyegezi kwa mama,nilimkuta pale sebuleni akiwa na dada yangu mkubwa pamoja na yule Shangazi yangu!.Nilipowaona tu nilijua lazima kungekuwa shughuli nzito!.

Baada ya salamu mama aliniuliza"Mwanangu ina maana wanawake wote hapa Mwanza hujawaona mpaka ukatembee na Shemeji yako?".

Mama aliendelea kuniambia "Sasa nimekuita hapa ili uniambie hayo aliyonieleza huyo shemeji yako ni kweli au naota?".

Mama yangu aliendelea kuniambia huku akitetemeka "Alikuja juzi hapa nyumbani akaanza kuniambia kwamba mnapendana na nyie tayari niwapenzi".

Mpaka hapo nikaelewa kwamba yule shemeji ndiye alimwambia mama,kwasababu nilikuwa nikimpenda sana mama yangu ilibidi nimwambie ukweli.


Nilimwambia "Ndiyo mama ni kweli!".

Mama aliniambia "Sasa mwanangu unawezaje kwenda kutembea na shemeji yako na unajua kabisa kaolewa?,basi bora hata angekuwa hajaolewa,pia unaelewa kabisa ambavyo simpendi yule mwanamke kwa namna alivyo tudharirisha".

Shangazi yangu ikabidi aingilie kati "Huyu hana kosa lolote yule ndiye mwenye makosa maana kama unajua umeolewa na una mume wako kwanini usitulie?".

Mama aliendelea kuongea kwa huzuni "Sawa wifi mimi sikupingi ila hii aibu ya mume wake tutaificha wapi?maana sasa hivi si ndugu wala marafiki zake wanafahamu kabisa hawa ni wapenzi".

Basi baada ya mazungumzo ya muda mrefu pale nyumbani shangazi yangu akaaga akaondoka,mimi pia sikumaliza muda mwingi niliwaaga nikaondoka zangu.Niliwaza sana namna nilivyomkosea mama lakini sikuwa na namna maana mimi nilikuwa ninataka mwanamke wa kuzaa naye ili watoto wale wawe kafara,niliyeona angenifaa ni yule shemeji,ukiacha uzuri aliyokuwa nao,pia nilitaka nimkomoe maana alikuwa na dharau sana.

Wakati nipo njiani naelekea nyumbani,dada yangu alinipigia simu akaniambia "Rudi nyumbani haraka mama kaanguka na hawezi hata kufumbua mdomo".

Nilimwambia dereva ageuze gari maana hali ya mama haikuwa nzuri,nilipofika nyumbani nilishuka kwenye gari kama nimechanganyikiwa huku nikikimbilia ndani!.



Itaendelea...............
 

Tuendelee mkuu shusha episodes za kutosha ili tupunguze arosto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…