pilipili kichaa
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 18,406
- 14,643
Laana waliypipata ni kuwasingizia wapinzani ndio waliowachelewesha hata wakaamua kuwadhulumu na kuwapora bila huruma.Majuzi nilisoma uzi wa ndugu yetu Mayala Pascal unaoelezea namna tulivyoingia mikataba ya hovyo kabisa ya Gas yetu ya Mtwara kwa wageni kijinga kabisa.
Nimejiuliza sana haya;
1. Nini kilitokea hadi wabunge wakapitisha mikataba ile kwa 'hati ya dharura'?
2. Kwanini wabunge wa upinzani walikataa hili na kutoka nje baada ya kushindwa kwa 'hoja hasi' za wabunge wa ccm?
Inauma sana, inasikitisha sana, kumbe akina 'Sultani Mang'ung'o' bado wapo Tz ya leo tena wenye dhamana kubwa hivi?
Laana waliyoipata ni kuwasingizia wapinzani ndio waliowachelewesha hata wakaamua kuwadhulumu na kuwapora bila huruma.
Hii nchi ina Mambo Sana tuliingia mikataba ya madini miaka ya nyuma tukaumizwa na kuachiwa mashimo sababu ya ujinga wetu CCM haikujifunza Kwa ujinga walioufanya maika Ile ya nyuma gesi ikaja tukaimbiwa ngonjera nyingi sana na mbwembwe zote na Sheria ikapitishwa Kwa Hati ya dharura watu wakala pesa Leo hii nchi iko kwenye kipindi cha mpito cha ukame ule umeme tulipokuwa tunautegemea kuwa utakuwa WA msaada kwetu umekuwa kilio kwetu kweli CCM ni tatizo kwenye hii nchiLaana waliypipata ni kuwasingizia wapinzani ndio waliowachelewesha hata wakaamua kuwadhulumu na kuwapora bila huruma.