Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Ziara ya siku mbili ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, XI Jinping, ambaye aliwasili nchini juzi, siyo kitu kidogo hasa ikizingatiwa kwamba Tanzania imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kwa kiongozi huyo kutoka taifa kubwa linaloelekea kushika hatamu za kiuchumi duniani kuwasili na ikiwa ni nchi ya pili kuitembelea baada ya Russia tangu achaguliwe kushika madaraka hayo.
Ziara hii kama ambavyo imeelezwa na wengi, ina manufaa mengi kwa Tanzania na watu wake. China ni miongoni mwa mataifa makubwa ambayo yameonyesha nia ya dhati ya kufanya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi na mataifa ya Afrika ikiwa tayari kutoa ama mikopo au misaada mbalimbali ya kiuchumi kwa maana ya kusaidia nchi nyingi za bara hilo kujikwamua kiuchumi.
Tanzania kama taifa lina historia ndefu ya ushirikiano na China, ukiweka kando masuala ya kisiasa chini ya mifumo na sera za uchumi hodhi ukiasisiwa chini ya sera za kiuchumi za kijamaa, taifa hilo limeshirikiana na nchi yetu katika miradi mikubwa kama vile ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara),
kiwanda cha nguo cha Urafiki, kiwanda cha zana za Kilimo cha Ubungo (Ufi), ushirikiano katika nyanja za mafunzo ya ufundi na sayansi, kijeshi kutaja kwa uchache tu.
Kama ambavyo imekwisha kuelezwa kwamba Rais Jinping angesaini mikataba 17 ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili, ikilenga uboreshaji wa sekta ya viwanda, kilimo hasa cha tumbaku pamoja na wa kuboresha sekta ya utangazaji, ziara hii inakuwa na maana kubwa zaidi kwa Tanzania kwa sababu tunapozungumza mataifa yanaoongoza kwa kuwa na nguvu kubwa za kiuchumi duniani kwa sasa, hakika China ni namba mbili baada ya Marekani, lakini ikiwa na nafasi ya kipekee kwa maana ya kujiepusha sana kuingilia mambo ya ndani ya mataifa inayoshirikiana nayo.
Tunaamini kwamba China inasukumwa na sera yake ya kutokuingilia mambo ya ndani ya taifa lolote kama mojawapo ya sifa au vigezo ama vya kutoa mikopo, misaada au ushirikiano wa aina yoyote; jambo linalotoa uhuru kwa taifa lolote kujiamulia litakavyo juu ya kuendesha mambo yake bila kusukwasukwa kwa masharti ya mikopo au misaada kutoka China.
Pamoja na sera ya China ya kutokufungamanisha uhusiano wake na mataifa mengine na masharti ya kuingilia sera za maendeleo na masuala ya demokrasia na rekodi za haki za binadamu, yapo mambo ya kimsingi ambayo hata hivyo katika ziara hii ni lazima yatazamwe kwa mapana yake.
Miongoni mwake ni kwamba katika mikataba na hata uhusiano wowote utakaozaliwa au kuendelea kuenziwa kati ya mataifa haya mawili ni lazima yajikite kwenye kile kinachoitwa kwa kimombo win win situation yaani kila mmoja anufaike.
Tunaposema kunufaika tunakusudia kusema kuwa isije kuwa kinachosukuma China kuongeza ushirikiano na Tanzania na mataifa ya Afrika kwa ujumla ni kusaka mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyake, kwani uhusiano huo ndio uliifikisha Afrika hapo ilipo kuanzia biashara ya utumwa, mkutano wa Berlin wa 1884-85 wa kuigawa Afrika mapande mapande baina ya wakoloni na kuzaa makoloni na hata wakati huu wa ukoloni mambo leo ambao wengine wanauita utandawazi.
Tanzania ingependa kuona uwekezaji chanya, unaogusa viwanda, kukuza ajira na faida baina ya pande zote mbili; Tanzania ingependa kuona China ikiingilia kati suala zima la uzalishaji wa bidhaa feki na zilizo na viwango duni ambazo kimsingi zinachafua jina la taifa hilo; pia Watanzania wangependa kuona China ikisaidia mataifa ya Afrika kunufaika katika maendeleo ya tekinolojia kwa kusaidia kujenga uwezo wa Waafrika kwa kutoa fursa zaidi za elimu na kuwajengea watu wake uwezo wa kuwa magwiji katika fani mbalimbali kulingana na mahitaji ya kitekinolojia katika mataifa hayo.
Pia lipo suala la maombi ya viza kwa ajili ya watu kwenda China kwa shughuli mbalimbali, hakuna ubishi kwamba Wachina wamezagaa kila kona duniani, wako kila nchi, wanajihusisha na kila aina ya shughuli ya uzalishaji mali, kuanzia biashara kubwa kubwa za kimataifa, uwekezaji katika miradi mikubwa mikubwa hadi kwenye uchuuzi;
wanafanya hayo kwa kuwa wanapata fursa ya kuingia katika nchi nyingine kwa urahisi, ni vema na haki China nao wakaachia milango wazi kwa watu kuingia alimradi wamefuata utaratibu. Taratibu hizi zisiwe na lengo la kuwakwamisha watu kwenda China. Hii itasiadia kujenga kuaminiana na watu kutambua kwamba China ni wadau wa kweli katika maendeleo na siyo kujinufaisha wao tu.
CHANZO: NIPASHE