VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Chimbuko la mikataba mitatu iliyosainiwa jana ni mkataba-tata kati ya Tanzania na DP World. Mkataba huu ulipangwa kuchakatwa; kujadiliwa na kusainiwa sirini. Ulipovujishwa na 'mzalendo', ukaibua mjadala mkali. Wengi waliupinga na kuupiga.
Serikali ikaiteka hoja kwa kudai kuwa inaruhusu maoni ya wananchi. Mbona waliuficha mkataba kama walitaka maoni ya wananchi, in the first place? Bila yule 'mzalendo' kutoka ndani ya mfumo kuuanika mkataba ule maoni ya wananchi wangeyapataje? Hadi hapo, imani ya wananchi kwa serikali ilitetereka.
Jana halikuzungumzwa. Jambo la utatuzi la migogoro. Kwenye mikataba ya jana, migogoro itatatuliwa wapi na kwa kutumia sheria zipi? Mamlaka ipi au zipi zitahusika kwenye utatuzi huo wa migogoro? Jambo hili halikugusiwa kabisa jana. Ni muhimu mliseme pia.
Kama maoni ya wananchi yamezingatiwa kwenye mikataba ya jana, tuonesheni hiyo mikataba husika!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Mpwapwa, Dodoma)